AZAM FC leo (Ijumaa) inashuka kwenye uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga kuvaana na wenyeji wao Coastal Union katika mchezo wa ligi soka Tanzania Bara.
Wawakilishi hao pekee wa nchi katika Kombe la CAF iwapo wataibuka na ushindi kwenye mchezo huo watakuwa wamekata tiketi kwa mara nyingine kushiriki michuano hiyo mwakani.
Pia, iwapo Azam itashikwa na kulazimishwa sare ya aina yoyote na Coastal, Yanga itakuwa imetwaa rasmi ubingwa wa ligi hiyo.
Yanga ambayo inaongoza ligi na point 56 huku ikiwa na mechi mbili mkononi dhidi ya Coastal Union na Simba, inahitaji pointi moja tu kutawazwa mabingwa wapya wa ligi.
Azam ambayo inashika nafasi ya pili kwenye ligi ndiyo timu pekee ambayo inaweza kufikisha
pointi 56 iwapo itashinda mechi zake zote tatu zilizobaki dhidi ya Coastal, Oljoro JKT na Mgambo
JKT.
Kocha wa Azam, Mwingereza Stewart Hall amesema kikosi chake kitapigana hadi tone la mwisho kwavile katika soka lolote linawezekana.
"Kazi yangu ni kuhakikisha tunapata matokeo mazuri bila kujali matokeo ya wengine, tupo vizuri kuikabili Coastal Union na kunyakua pointi tatu,"alisema Hall.
Katika mtanange huo Hall atawakosa mabeki wake Jockins Atudo na Haji Nuhu ambao ni majeruhi ingawa nafasi ya Atudo inatarajiwa kuzibwa na beki Aggrey Morris aliyekuwa amesimamishwa kwa tuhuma za rushwa.
No comments:
Post a Comment