Baada ya jana kukuletea mahojiano mafupi na kocha wa APR, leo hii nakuletea interview yangu niliyofanya na kocha wa klabu ya Atletico ya Burundi ambayo leo hii imeifunga Wau Salaam goli 5-0.
Atletico - Kaze Cedric
Swali: Nini malengo yako katika mashindano haya?
Jibu: Malengo ni kuonyesha ushindani na tukifanikiwa tufike
hatua ya fainali na kubeba kombe, na naamini hilo ndio lengo kuu la kila timu kwenye mashindano.
Swali: Baada ya mechi ulizoziona, unazungumziaje viwango vya
timu nyingine?
Jibu: Viwango vya timu zote zina ufanano hazizidiani sana.
Swali: Timu gani unakuumiza kichwa na kwanini?
Jibu: Nafiki ni ile ya Uganda (URA) kwa sababu ina wachezaji
wazuri pia wanaonekana wamezoeana sana kiasi cha kwamba wanacheza mpira mzuri sana tena wa ushindani.
Swali: Wewe ni kocha mzalendo na timu yako ni moja ya
zilizoonyesha ushindani hata kuzizidi zile zinazofundishwa na wazungu kutoka nje, nini
siri ya mafanikio yako?
Jibu: Mafanikio yangu ni wachezaji wenyewe kusikiliza
ninachowaagiza kwa kucheza kwa mujibu wa mbinu zetu. Tunafanikiwa kwa sababu ni timu ambayo niko nao kwa kipindi
kirefu sasa ni mwaka wa nne tuko pamoja na kadri siku zinavyozidi kwenda kunakuwa na
mabadiliko kimaendeleo. Ujuzi wa kocha ni kuaminiwa tu atakapoaminiwa atafanya kazi
nzuri, tatizo la klabu
hizo zinazochukua makocha kutoka nje ya nchi tatizo lao
hawawaamini wazalendo wakati si sawa, waamini tu kocha mzalendo anaweza kufanya mambo
makubwa zaidi wageni.
Kosa lingine wageni hawawajulii wachezaji wetu vitu
wanavyohitaji.
Swali: Fomesheni gani unapenda kutumia?
Jibu: Napenda kutumia 4-4-2 na mara nyingine ni 4-3-3.