Baada ya jana shirkisho la soka la Tanzania (TFF) kupitia kamati yake Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji, kufikia uamuzi wa kumruhusu Kelvin Yondan kuichezea klabu ya Yanga kwenye mashindano ya Kagame tu, na mustakabali wake wa mbele kuhusu kuendelea kuichezea Yanga utajulikana baadae.
Kutokana na suala hili kumetojitokeza maswali mengi ambayo TFF na CECAFA itabidi watupe majibu wadau wa soka nchini.
Kwanza kabisa mojawapo ya kanuni ya mashindano ya CECAFA - ili mchezaji fulani aweze kuwa halali kuichezea timu fulani kwenye mashindano haya ni lazima awe pia halali kuichezea klabu yake kwenye mashindano ya ligi kuu ya nchini husika inapotoka klabu yake. Kwa maana hiyo kifungu hiki kinamuhukumu Yondani kuruhusiwa kucheza Kagame Cup, kwa kuwa bado hajathibitishwa kuwa na uhalali wa kuitumikia Yanga kwenye ligi kuu ya Tanzania bara.
Emmanuel Gabriel |
Sasa linakuja swali iweje kanuni hii ibadilike kwa Kelvin Yondani tu, ama imebadilishwa na kwa bahati mbaya wadau hatuna taarifa?
Kama kuna mwenye jibu au ufafanuzi juu hili naomba atoe hapa kwenye maoni.
Ni mtazamo tu - nawasilisha.
TUACHE UNAZI KWA YONDANI! KWANZA TUJIULIZE HIVI WACHEZAJI WOTE AMBAO NI WAPYA KWA SIMBA NA YANGA AMBAO WANASHIRIKI KAGAME MSIMU JE WAMEHALALISHWA KUSHIRIKI LIGI KUU YA BARA?
ReplyDeleteSHAFII MIMI NAONA UNACHANGANYA MAMBO HAPO UMEONA MKATABA WA YONDANI UANISHA LINI...?
ReplyDeleteTFF WANASEMA KATIKA KALABRASHA ZAO NI KUWA YONDANI NI MCHEZAJI HURU TANGU TAREHE MOJA JUNE 2012.....HALAFU NAJUA WEWE NI MNAZI WA SIMBA UNAWAAMBIAJE VIONGOZI WAKO KUHUSU KUTOKUWA MAKINI KATIKA UANDIKAJI WA TAREHE KATIKA MIKATABA..?
Shaff huna jipya wewe, huna mvuto hata kidogo siku hizi blog ya michezo ya kuaminika bongo ni Bin Zubery na Straika. Wewe fanya blog yako iwe ya Simba Fans....nawakilisha.
ReplyDeleteMdau
Washington
Shaffih acha usimba wako, pitia vipengele vyo vya hao watatu afu pia angalia dosar zilizopo. Mwisho wa siku watu km nyie wa media ndo mnaleta matatizo kwenye michezo nchini.
ReplyDeletendugu yangu shaffih wala usijisumbue. hivi mpaka leo bado haujafahamu kama tff ipo kwa ajili ya yanga? mambo mangapi ambayo yameshazua utata mpaka hivi leo? je uchunguzi kuhusu kelvin yondan kutoroshwa kambini na kiongozi wa tff ili akasaini yanga umefikia wapi? kumbuka kipindi kile ndolanga alipowatorosha kambini wachezaji wa pamba kule arusha ili wakasini yanga na wote wakasaini kasoro nteze john ambae alikataa. umesahau kampeni za uchaguzi watu walivyokua wanahaha kuhakikisha hakuna mtu wa friends of simba anashinda japo ujumbe sababu anaweza kuvuruga mipango yao ya kuibeba yanga? ila ipo siku kitaeleweka tu.
ReplyDeleteMie sijui sheria za Cecafa, lakini kama mwafunzi wa sheria, naweza kusema Yondani yupo huru. Mkataba niliuona kwenye magazeti kama ni kweli, huyu mchezaji ni huru. Kama Simba wanasema wameingia naye mkataba mpya utakaonza Dec 2012 kwa sasa huyu ni mchezaji huru. Hii ni introduction course ya sheria course 101.
ReplyDeleteNachoweza kusema sisi Simba tubadilike, tuache ubabaishaji na kungangania wachezaji. Nadhani timu hizi zifuate mfano wa Azam, hawa jamaa hawana malumbano...wanafuata sheria ya mikataba. Simba walitaka kumchukua kijana mmoja toka kwao, wenyewe walikuwa kimya wakisubiri haki yao, sasa huyo kijana amerudi zake Azam. Tuache mambo ya kiuni,tufuate sheria.
JP
Mlimani
LIGI KUU BADO HAIJAANZA HATA USAJILI KWA AJILI YA LIGI KUU PIA BADO UNAENDELEA HIVYO BASI HAKUNA HATA TIMU MOJA ITAKAYOSHIRIKI LIGI AMBAYO IMEWASILISHA MAJINA YA WACHEZAJI ILIOWASAJILI KWA AJILI YA KUHAKIKIWA NA TFF KWA MAANA HIYO BASI WACHEZAJI WOTE WAPYA WA SIMBA NA YANGA WANAOSHIRIKI KAGAME HAWANA UHALALI WA KUSHIRIKI LIGI KUU YA BARA
ReplyDeleteNI MAWAZO YANGU TU
Jibu mwenyekiti wacecafa na viongozi wa juu wa tff wote ni yanga
ReplyDeleteShaffih acha ushabiki,kumbuka kelvin ni mchezaji huru,mkataba wa simba na yondan ulikwisha may na mkataba mpya unaanza december 2012,ukifika huo muda yondani atarudi kwenu kwa sasa yupo huru,ili haulioni kwa sababu ya kupotosha umma
ReplyDeletepole kwa majukumu ya kufuatilia soka la bogo na kuhakikisha lina piga hatua.Mimi naomba kufahamu mazingira ya uhamisho wa yondani na hao jamaa wawili ulio wataja hapo juu yana fanana?
ReplyDeleteshaffih unashusha imani yako kwa kwa wanamichezo
ReplyDeletehilo swali ni la kiufundi wewe na sisi hatujui nini kinaendelea wala hatuna elimu tosha ya kuweka hoja
NILIKUA NATAFUTA CHANZO CHA KWANN SOKA LETU HALIENDELEI!SASA ISHAJUA KUMBE WAANDISHI WA HABARI NA VYOMBO VYA HABARI NDIO VINAHARIBU MPIRA WETU HAPA NCHINI NA BLOG NYINGI ZIMEJAA UNAZI NA USHABIKI WA SIMBA NA YANGA!KWA KANUNI UNAYOSEMEA SHAFFIH HATA AKINA KANU MBIYAVANGA MUSSA MUDDE KINJE KWA UPANDE WA SIMBA WOTE NI BATILI KUCHEZA MASHINDANO HAYA NA UPANDE WA YANGA LUHENDE,BAHANUZI,SAID NA BATHEZI NI BATILI KWA MASHINDANO HAYA NA AZAM AKINA DIDA,NA BLACKBERRY NAO HAWARUHUSIWI KUCHEZA KAGAME!NAOMBA NIKUKUMBUSHE SHAFFIH ISHU YA YONDANI SIO ITC NI MKATABA WA SIMBA NA YONDAN THEN YONDAN NA YANGA SHERIA INGEFUATWA KIUFASAHA KABISA MANAGEMENT YA SIMBA INGEWAJIBIKA KWA KUIDANGANYA TFF KWA KUUOVERLOOK MKATABA WA YONDANI WAKATI MDA BADO HAUJAFIKA MKATABA UNAANDALIAWA NA CLUNB NA LAZMA UPITIWE NA MWANASHERIA WA CLUB LEO HII UNAKUJA KUNIAMBIA TYPING ERROR ARE SERIOUS?ANDIKENI VITU VYA MSINGI KWENYE BLOG YENU KWA MAAENDELEO YA MPIRA WA MIGUU TZ!YANGA SIMBA NA TFF UOZO MTUPU HATA WW SHSFFIH NA BIN ZUBEIRY MMEJAA UNAZI KWENYE BLOG ZENU HATUTAFIKA KWA STYLE HII KUWENI NA FIKRA ENDELEVU JAMANI MNAPELEKA WAPI MPIRA WA TZ?
ReplyDeleteKk na wac wac na elimu yako,yaani unafananisha vitu vi2 tofauti kabisa, hebu fuatilia vizuri mkataba wa Yondani na Simba vizuri then uje hapa ucomment, punguza ushabiki maandazi.
ReplyDeleteinaonyesha jinsi gn wenzetu wa jangwani tff ilivyokuwa ya kwaoo huu sio mpira na co haki inakuwaje watu mnakuwa upane wa team moja.. jitaiini kuwabeba mpk kiama yanga aiatofanya vizuri maisha simba sc iatabaki kuwa taifa kubwa
ReplyDeleteJamani tusimuhukumu Shaffih hiyo hoja hapo kwn hajaandika yy ni mdahu km cc ndio kaandika kawasilisha kwa hiyo vibaya yy kuiweka?
ReplyDeleteninataka kwambia kwamba tarehe kwenye mambo ya kisheria ina maana kubwa sana kama wewe unaona kuwa yondani usajili wake una utata ni wewe lakini mimi ninayejua sheria sioni huo utata kwani ata mkataba wake wa kwanza umekwisha kwa sababu ya tarehe ,na pia kanuni za tff zinasema renewal ya mkataba inabidi ifanyike kabla ya mkataba wa mwanzo haujakwisha na kusajiliwa tff je simba na yondani wamefanya hivyo ,swala linalotakiwa kujadiliwa ni yondani kusaini mikataba miwili na wakati bado kwani mkataba wa yondani na simba utaanza tarehe tajwa mwezi wa dece kwahiyo kwa sasa yondani ana mkataba moja tu na yanga na si vinginevyo.
ReplyDeleteNYIE WAPUUZI MNAODAI HII BLOG NI KISHABIKI ZAIDI MNAFUATA NINI? SOMENI BLOG AMBAZO ZITAWAFUHAISHA NYIE NA MUME WENU MANJI, SIO KUTUPOTEZEA MUDA HAPA NA COMMENTS ZENU ZA KIPUUZI, NYIE WA WAPI? HEBU KWENDENI HUKO.
ReplyDeleteMdau umeshatoka milembe?
DeleteMatusi ya nini? sio bure utakuwa unaugua kichaa wewe
DeleteSHAFFIH ACHA KUPOTOSHA UMA,....SOMA HAPA
ReplyDeleteArticle 9 International Transfer Certifi cate
1. Players registered at one association may only be registered at a new
association once the latter has received an International Transfer
Certifi cate (hereinafter: ITC) from the former association. The ITC shall
be issued free of charge without any conditions or time limit. Any
provisions to the contrary shall be null and void. The association
issuing the ITC shall lodge a copy with FIFA. The administrative
procedures for issuing the ITC are contained in Annexe 3 of these
regulations.
IV. MAINTENANCE OF CONTRACTUAL STABILITY
BETWEEN PROFESSIONALS AND CLUBS
Article 13 Respect of contract
A contract between a professional and a club may only be terminated
upon expiry of the term of the contract or by mutual agreement
LINK: www.fifa.com/mm/document/.../01/.../statusinhalt_en_122007.pdf
naitwa ATANASI.
Kwa mtizamo wangu ninyi mnaomshutumu Shaffih mna matatizo na ninyi ndio wanazi wa Yanga so kilichoandikwa kimewaudhi. Mimi hua nasikiliza sana na kusoma uchambuzi wa Shaffih kwakwel mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, uyu jamaa ni kati ya wachambuzi wachache wa soka ambao wapo very subjective, simba wakiharibu anasema wazi yanga wakiharibu hali kadhalika. Ni tofauti sana na wachambuzi wengi na waandishi wa habari za michezo wengi ambao wanasifia tu siku zote. Kwa suala la Yondani tuache usimba uyanga, hapa kuna utata mkubwa si kweli kbs kwamba ni mchezaji huru. Lkn ukwel ni kwamba viongozi wetu wa soka Tz ni either simba au Yanga so hata kama hili suala lingehusu simba maamuzi yangekua haya haya hasa ukuzingatia alikua ashacheza match moja tayari. Shaffih nakutia moyo endelea ivyo ivyo achana na wapuuzi wachache wanaokutuhumu maana huwezi kubaliwa na kila mtu hata Mungu alieumba kila kitu bado hapendwi na wote sembuse weyw binadamu. Hawa wanaosema hii blog yako haina maana wanafuata nn huku? mimi nadhani huu ni ukichaa maana mm hua kuna blog nyingi sna ambazo siangalii kwakua sizikubali, so ukiingia humu hata ukitoa matusi basi wewe ni fan wa Shaffih. MWISHO TUKUBALI TUKATAE, SIMBA NA YANGA NDO ZINAHARIBU SOKA YA TZ NADHANI ZINGEKUFA NDO SOKA LA BONGO LITAKUA..OTHERWISE WE ARE NOT GOING ANY WHERE...
ReplyDeleteSio kweli shaffih amepoteza muelekeo sana kipindi chake kimepoteza mvuto,huku arusha inaitwa simba radio,imefikia wakati sasa watu wanamsubiri mbwiga tu wa commedy na sio habari za michezo,kwa mfano juzi yanga imeifunga APR alisema sio kipimo sahihi kwa sababu APR walishafuvu jana kwa simba anasema ilikuwa kipimo sahihi,turudi kwenye sakata la yondan hakuna anapowazungumzia viongozi wa simba kwa uozo,kama mkataba ulisahiniwa december 2011 walikaa nao wa nn hadi ule wa Tff umaliize muda wake,hakuna anapozungumzia tarehe na umuhi wake akaishia kuwaita yanga wahuni simba mashujaa
DeleteHabari yako naona hata ww unashindwa kuelewa issue inayozungumziwa hapa, achana na habari za unazi soma vizuri story hii then uone Shaffih anashutumiwa kwa nn, Yondani alikuwa ni mchezaji huru na hao wengine wamenunuliwa wakiwa na mikataba kutoka nchi zingine ndio maana zikatakiwa ITC, huoni utofauti huo we unasema tu mambo ya unazi tu na wewe ukiitwa mnazi wa Shaffih nitakuwa sawa, fuatilia issue vizuri uielewe na na ndiyo utoe comments za kueleweka acha kukurupuka.
DeleteTatizo hata wewe inaonekana ni mnazi wa simba ndo maana unashindwa kuona msingi wa shutuma za watu kwa shaffii mimi binafsi Nilikuwa namheshimu sana Huyu bwana ili reputation yake inaporomoka kutakana na mapenzi yake kwa chama lake simba. yupo so bias kiasi cha kupoteza sifa za kuwa mchambuzi mahiri.
Deletehicho kipengele hakimbani yondani pekee bali hata wachezaji wote wenye mikataba mipya, je? SHAFFIH kunauhalali gani kwa mbiyavanga,kigi,bahanuzi,kinje,nizar,blackbery nk? kwanini yondani tu? je tff imeshathibitisha mikataba ya wachezaji wapya? ni vizuri kufikiri mara mbili kabla hujaweka habari kwenye blog yako kaka, heshima yako kwa wapenzi wa soka unaishusha kutokana na hoja zako zisizo na mashiko, piga kazi kaka wacha habari za unazi zitakudharaulisha,simba na yanga zenyewe hazina muamana leo watakusapoti kwa kuwa wanataka kukutumia kesho watakugeuka,watakushambulia,watakushinda na kukucheka.
ReplyDeletekaka shaffih umechanganya habari mifano ya wachezaji uliyotoa walikuwa na mikataba na timu nyingine ndiyo maana ikatakiwa ITC(hati ya uhamisho wa kimataifa) yondan ni mchezaji huru yeye kasema hivyo mkataba uliouweka kwenye blog yako unasema hivyo.kama ni makosa ya kibinadamu ya kukosea tarehe hilo nalikubali lakini imekula kwao kwani na mbaya zaidi makosa yapo sehemu waliposaini viongozi kabla ya kuwahukumu viongozi wa tff washauli viongozi wa simba wawe makini ndiyo maana wamesajiri midfield tupu na foward wawili tu huo ni ukilaza
ReplyDeleteTATIZO MOJA LINAWASUMBUA MASHABIKI WA SIMBA NI MKWAMBA WANASHIKIWA AKILI NA VIONGOZI WAO,SIO MARA YA KWANZA VIONGOZI WA SIMBA WANASHINDWA KUTAFSIRI SHERIA ZA MIKATABA YA WACHEZAJI WAO,REJEA SAKATA LA CHUJI,ILIFIKIA KIPINDI DALALI ALIAPA KUWA CHUJI HATOICHEZEA YANGA YEYE AKIWA KIONGOZI.HII INAONYESHA AINA YA VIONGOZI WASIO NA UFAHAMU NA MASUALA YA SHERIA.LEO KANUNI ZA TFF ZINASEMA MKATABA BAINA YA MCHEZAJI HAUKAMILIKI HADI USAJILIWE NA CHOMBO HICHO,MKATABA WA YONDANI ULIOSAJILIWA TFF UMEMALIZIKA MEI 23 SASA HUO WA EXTENSION UMESAJILIWA NA CHOMBO GANI WAKATI MWISHO WA KUWASILISHA NI JULAI 30...HAPA WATANI ZANGU MNAHITAJI ELIMU YA URAIA HUSUSAN SHERIA ZA MIKATABA BILA HIVYO KILA MWAKA TUTAWALIZA SANA..BAHATI NZURI NDANI YA KAMATI ZA YANGA KUNA WANASHERIA WA KUTOSHA NA HATA VIONGOZI WA JUU WALIOPITA NI WANASHERIA,NCHUNGA NA MADEGA...NAOMBA KUWASILIOSHA
ReplyDeleteHUO WA MKATABA WA YONDANI NA YANGA UMESAJILIWA LINI? AU KWA SABABU ANGETILE OSIAH YUPO PALE NDO WENYEWE UNATAMBULIKA?? MBONA SIMBA WALIPELEKA MKATABA WAKAAMBIWA MUDA BADO WA KUSAJILI MIKATABA?? NA KAMA WAKATI HUO YANGA WALIKUWA WAMESHAMSAJILI YONDANI KIHALALI, IWEJE WAMTOROSHE KAMBINI ILI AKASAINI? KUTOROSHA WATU NDO KUJUA SHERIA?? YANGA NI WATU WA VURUGU, UTEMI NA MAGUMASHI TU, NDO MAANA HATA UWANJANI MNAPIGANA NGUMI. NA SASA HIVI MNAMTUMIA ANGETILE NA NGUVU YA HELA YA MANJI. NUNUENI YOYOTE HATA MESSI KAMA HAMNA UTARATIBU MZURI MTAFUNGWA TU NA SIMBA.
DeleteKikubwa ni kuwa uongozi mzima wa TFF umetawaliwa na uyanga kuanzia m/kiti katibu mpaka huyo Mgongolwa unategemea nini hapo? Musonye alisha sema mchezaji atakaye shiriki mashindano ya CECAFA ni lazima awe na usajili uliokamilika sasa iweje Yondani ambaye majina yake yamejitokeza pande zote aruhusiwe kucheza upande mmoja hiyo ni kanuni ya wapi ?
ReplyDeleteWEWE NI MWEHU KABISA, UNAJISIFIA VIONGOZI WA YANGA NI WANASHERIA, BASI ITAKUA WALICHAKACHUA VYETI, MAANA MADEGA ALIINGIZA YANGA KATIKA MATATIZO NA CECAFA KWA KUGOMA KUPELEKA TIMU UWANJANI, AU ALIKUA BADO HAJAHITIMU? NCHUNGA ALILAZIMISHA CANAVARO ACHEZE HTA PALE ALIPOSHAURIWA NA WATU WENGINE KUHUSU SHERIA ALIGOMA NA MATOKEO YAKE AKAIGHARIMU YANGA. TATIZO LENU MASHABIKI WA YANGA WENGI NI SHEHE KASEMA, UWEZO WENU WA KUCHANGANUA MAMBO NI VINYU KULIKO KITU CHOCHOTE. KUKAA NA MSHABIKI WA YANGA NYUMBA MOJA NI AFADHALI KUKAA NA PAKA ANAWEZA KUKUSAIDIA KUKAMATA PANYA, YAANI KWA KIFUPI NI WEHU.
ReplyDeleteShaffih s'times una-bore kwa unazi usokuwa na tija. Nakumbuka mwanzo wa hili sokomoko ulishadidia sana kwamba Kelvin Patrick Yondani aliyesajiliwa Yanga ni KINDA na wala si yule wa SIMBA. As the days were numbered, ukaja kivingine kwamba yanga wamenunua mbuzi kwenye gunia! Mwisho wa siku Kelvin Patrick Yondani katua Yanga na macho yakakutoka na sasa unashindwa kujinasua. Mi nafikiri ka uko kazini fanya kazi na unazi weka pembeni!
ReplyDeleteMbunge-Dodoma.
Ni kweli walikosea mkataba wa mwanzo. Yanga walipoona simba wamewasilisha ule wa extension, na wakagundua makosa yao kwenye ule wa kwanza (ikiwemo kukosea mwaka wa kuzaliwa) ndipo wakamtorosha Yondani kambini. Simba ndo walipeleka mkataba kwanza wakaambiwa muda bado. Hiyo ni nini sasa. Mbona TFF wakakaa kimya kwenye hili pia. Anzeni kumsema huyo Angetile Osiah kwanza anayeleta unazi wa wazi ndo mje kwa Shaffih
DeleteUkisoma mkataba wa Calvin Yondan na Simba unaonesha wazi kua Calvin alisaini mkataba mwezi December 2011, na sehemu nyingine zote za mkataba zinaonesha kua ulisainiwa kipindi icho, ukija kwenye shemu ya viongozi wa simba ndo inaoneka december 2012 badala ya december 2011. Ofkoz iyo inaonesha kua tayari mkataba wenyewe una utata, ila tafsiri ya namna yoyote ile lazm itaonesha kua kulikua na typig era ambalo ni kosa la kibinadamu..Wewe unaejidai unajua sheria usidhani kua ww pekeee ndo unaejus sheria...Sasa kisheria mkataba unapokua na tarehe mbili tofauti inakuaje? mkataba huo unatakiwa utafsiriwe kwa kuangalia nn kama sio intention of parties? nyie mnazungumzia sehem walosain viongozi wa simba vp kuhusu seheme alosain Yondan ambayo inaonesha ni december 2011? lets be subjective, tuache kutoa shutuma zisizo na msingi, hapa hata kisheria tayari lazima interpretation ifanyike ili kujua mkatana usomeke vp kwani tayari kuna utata...So, the best option isingekua kumruhusu Yondani achezee timu yoyote, angetakiwa awekwe pembeni asbr mpaka muafaka ufikiwe..Sasa tumesikia Simba wanasema hawajaridhika wanaenda mbele vp kama wakishinda huko ikaamuliwa kua Calvin ni mali ya simba? itakuaje? Hata ivyo watu kama nyie mnaosapoti huu upuzi ndo mnaharibu soka koz alichofanya Yondani ni uhuni, ambao inabidi ukemewe kwa nguvu zote, ni sawa na kile alichofanyaga Victor Costa, wote ni uhuni, ktk karne hii mtu ansainije timu mbili? tuache kuunga mkoni mambo ya kijinga..Anyways tuassume kwamba Yondani mkataba wake na Simba utakua unaanza December 2012 kama ambavyo wengi mnaonekana kuamini, tuangalie upande wa pili makataba wake na Yanga ni wa miaka miwili which means ikifika december bado atakua na mkataba na Yanga sasa huo wa simba nao utaanzaje wakati bado wa Yanga haujaisha? ndo maana tunasema hapa kuna utata, mkubali mkatae, mambo hayapo clear kabisa lots of ambiguities...hapa lzm kuna uhuni umefanya na either simba, Yanga au Yondani mwenyewe...tuache kuunga mkono ujinga..
ReplyDeleteBaada ya maelezo yako mengi at least umesema kuwa kuna uhuni umefanywa na either simba, Yanga au Yondani mwenyewe. hapo uko sawa coz hatujui nani mhuni kati yao. Tatizo huyu shafii unaemtetea hata hilo halioni ama hataki kulikubali badala yake anajaribu kuwaaminisha watu kuwa simba wapo sahihi katika hili kitu ambacho sio sahihi na ndio maana watu wanamlaumu kwa kuweka unazi mbele
Deleteameuliza iweje aruhusiwe kucheza Yanga? Unazi uko wapi hapo. Yondani amesaini timu mbili, kumruhusu achezee Yanga ikiwa suala bado lina utata hivi ndio Unazi wenyewe. Nani asiyejua unazi wa Angetile Osiah kwa Yanga, si alikuwa mjumbe kabisa!! Kuna masuala kadhaa yalikosewa hapa likiwemo la kumtorosha Yondani kambini ili asaini mkataba mpya na Yanga.
Deletejamani sisi sote tuliochangia post hii ya shaffih hatujailelewa wala Shaffih mwenyewe hajaelewa alikuwa na intention gani ya kupost that article, nimepitia comments zote za wachangiaji na nimegundua kuwa uelewa miongoni mwa wapenda soka hapa TZ ni mdogo mno hususani ktk mambo ya sheria na taratibu zinazoongoza soka, suala la Yongani limejawa na uzushi mtupu na i think KABURU atakuwa na siri nzito sana na wala hataki kuadmit makosa yake, kwenye mkataba WOWOTE TAREHE ni kitu muhimu sana kwasababu tarehe ndio inayotaja kuanza na kukoma kwa mkataba na unapozungumzia maslai ya CLUB na MCHEZAJI, vitu kama intention of Parties na maslai binafsi ya mchezaji ni ndio vitu vya ha msingi sana. na inawezekana KABURU alisaini sehemu ya SIMBA baada ya kusikia YONDANI kasajiliwa yanga thats why alikuwa na mchecheto wa kusaini na ndio akajikuta amekosea,Pia inaonesha SIMBA SC walipanga kumchinjilia mbali na kumtupa YONDANI ndio maana hawakuhangaika kuupeleka Mkataba wa kuongeza muda na YONDANI ili waupeleke TFF ukasajiliwe na unapozungumzia HUMAN ERROR nani anabeba lawama hizo je ni TFF, SIMBA SC AU YONDANI? na je SIMBA SC club hawana mwanasheria wa Club anayesimamia suala zima la kusaini mikataba, i think angekuwepo wala HUMAN ERROR isingetokea, KABURU NA VIONGOZI WA SIMBA ni budi wakawaambia ukweli tu wanachama na wapenzi wa SIMBA kuwa walikosea, kwani KUKIRI KOSA SIO DHAMBI NA WALA SIO UDHAIFU NI NAMNA TU YA KUSAHIHISHA MAKOSA.
ReplyDeleteSimba walipeleka mkataba wakaambiwa muda bado wa kusajili mikataba mipya. Kama ni suala la kukosea mikataba, wa Yondani na Yanga ule wa mwanzo ulionyesha Yondani kazaliwa 1992 kabla ya kumtorosha kambini akasaini mpya. Na mbona TFF wamekaa kimya kuhusu Yondani kutoroshwa ili akasaini mkataba na Yanga??
DeleteShaffih acha wivu wa kike!!!Mzee Akilimali anakutafuta kwenu apeleke Posa!!
ReplyDeleteSasa wewe naona umevuka mipaka unaposema Mzee Akilimali anamposa Shaffih unamaanisha Mzee Akilimali ni Basha sio?? Au unamaanisha Mzee Akilimali anajihusisha na ndoa za jinsia moja?? Hivi hujui Kama huyu Mzee ni mwislamu safi mwenye kufata dini na ni Hamsa salawati??
ReplyDeletesasa Kama umeelewa kosa lako mwombe radhi Mzee wetu
KAKA SHAFII HIVI KWELI ULIKUWA HUJUI KUWA
ReplyDelete1) UHALALI WA MKATABA WA KUONGEZA MUDA LAZIMA UFANYIKE NDANI YA MIEZI SITA
2) NA LAZIMA UWASILISHWE TFF KWA USAJILI
ACHA UNAZI WAKO UNASHUSHA GOODWILL YAKO KTK MEDALI YA UCHAMBUZI WA SOKAIGA MFANO WA AKINA EDO KUMWEMBE AMBAO WANATULIA SANA KATIKA KUWASILISHA HOJA MBALIMBALI.
Hivi Yondani anafanana na naini vile kiuchezaji??? inaokekana huyu jamaa anauweza sana mpira, siwa kawaida huyu. Tangu nimeliona suala hili ni zamani na mengi yanaongewa hadi matusi ya hadharani. inaonekana Yanga wamepata bonge la mchezaji. inaonekana Yanga hawatafungwa mwaka huu. au kuna nini. hebu tuambieni. huyu mtu anaonekana super sana????!!!!!!
ReplyDelete