Search This Blog

Saturday, February 8, 2014

PHOTOZ: YANGA WALIPOWANYOOSHA WACOMORO TAIFA LEO


 Kiungo wa Komorozine Sports, Moidjie Ali akimdhibiti mshambuliaji wa Yanga, David Luhenda katika mchezo wa Ligi ya klabu Bingwa Afrika uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga imeshinda 7-0 


 Wacheaji wa Yanga wakishangilia baada ya kuifunga timu ya Komorozine Sports katika mchezo wa Ligi ya Klabu Bingwa Afrika uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 
 Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva akitafuta mbinu za kuwatoka wachezaji wa timu ya Komorozine Sports.
 Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa akimtoka mchezaji wa wa Komorozine Sports, Attouumane Omar katika mchezo wa Ligi ya Klabu Bingwa Afrika uliofanyika kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

LIVE SCORE: YANGA SC 7-0 KOMOROZIE DE DEMONI - FULLTIME


Mpira umemalizika Yanga 7-0 Wacomoro

  Dakika ya 81, Didier Kavumbagu anaipatia Young Africans bao la saba

Dakika ya 75, Young Africans 6 - 0 Komorozine de Domoni

Dakika ya 68, Mrisho Ngasa anaipatia Young Africans bao la tano

Dakika ya 65, Mrisho Ngasa anaipatia Young Africans bao la tano

59' Hamisi Kiiza anapigilia bao la nne...pasi nzuri ya Kavumbagu.

57' Didier Kavumbagu anaipa Yanga bao la tatu.

54' Komorozine wanapata mkwaju wa adhabu, Simba wanashangilia, Yanga wanazomea...bado mpira umesinzia.

Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza, Young Africans inafanya mabadiliko anaingia Didier Kavumbagu kuchukua nafasi ya David Luhende

HT: Yanga 2-0 Komorozine ( Ngassa, Nadir Haroub ) #CAFChampionsleague

42' Yanga 2-0 Komorozine

39' Hamisi Kiiza ana uchu mno wa kufunga, mpaka sasa offside mara nne,

32' Komorozine wanapata kona ya kwanza. Kwa mara ya kwanza Simba wanapiga makofi.

Dakika ya 30, Young Africans 2 - 0 Komorozine de Domoni

23' Timu nzima ya Komorozine imegeuka kwa mabeki. Hawavuki mstari wao.

20' Nadir Haroub anamalizia kwa kichwa adhabu ndogo iliyopigwa na Msuva na kuaindikia Yanga bao la pili.

 13' Bao! Ngassa anachupa vizuri na kuiandikia Yanga bao la kwanza.

7' Kisigino cha Hamisi Kiiza kinatua mikononi mwa kipa wa Komorozine.

2'  Kona tasa. Shuti la Ngassa lililokuwa likielekea nyavuni limepanguliwa na beki na kuwa kona. Krosi ya Msuva.

1' Mpira umeanza...Yanga ndani ya jezi za kijani ilhali Komorozine wamevaa jezi za njano na bukta nyeusi.

LISTI YA VILABU VYA EPL VINAVYOONGOZA KWA MATUMIZI MAKUBWA YA FEDHA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MITANO ILIYOPITA


Hii ni listi ya vilabu vinavyoongoza kwa matumizi makubwa ya fedha katika kipindi cha miaka mitabno iliyopita ndani ya English Premier League.
Mchanganuo inaonyesha fedha zilizotumika katika kununua, fedha zilizoingia kutokana na mauzo.

*Vilabu vya Arsenal, Everton na Newcastle ndio vimetengeneza faida katika biashara ya manunuzi na mauzo ya wachezaji. Arsenal kwa upande wao kwa muda wote huo wametumia kiasi cha £188m, wameuza kiasi cha £192, hivyo wamepata faida ya £4m
Everton wametumia kiasi cha £63, na kuuza kiasi cha £75m, faida kiasi cha £12m.
Klabu ya Newcastle ndio klabu iliyoingiza fedha nyingi zaidi - wamepata faida ya £45m, walitumia kiasi cha £93m na kuuza kiasi cha £138m.

Friday, February 7, 2014

TAKWIMU MBALI MBALI KUELEKEA MICHEZO MBALI MBALI JUMA HILI.







MJADALA: NANI ANAFAA KUWA NAHODHA WA MAN UNITED BAADA YA NEMANJA VIDIC KUONDOKA? PIGA KURA


Nani kati hawa anastahili kurithi unahidha wa Nemanja Vidic msimu ujao ndani ya Manchester United?

1: Robin Van Persie 
2: Wayne Rooney
3: Johnny Evans
4: Micheal Carrick
5: Phil Jones
6: Micheal Carrick
6: David De Gea

KUTOKA TWITTER: MRISHO NGASSA AKIRI AMISI TAMBWE NI HATARI, AZUNGUMZIA KUFIKIRIA KUACHA KUCHEZA SOKA NA MECHI YA MBEYA CITY

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga ametumia akaunti ya mtandao wake wa Twitter kutoa sifa nzuri kwa mshambuliaji wa klabu ya Simba Amisi Tambwe. Ngassa pia ametumia akaunti hiyo kuzungumzia changamoto alizokutana nazo kwenye soka kiasi cha kufikiria kuachana na mchezo huo, huku akisema mechi ya Yanga dhidi ya Mbeya City ni mechi kubwa sana kwenye kumbukumbu zake za soka na alifurahia mno kushinda.


BREAKING NEWS: NEMANJA VIDIC ATANGAZA RASMI KUONDOKA MANCHESTER UNITED

Thursday, February 6, 2014

LIVERPOOL VS ARSENAL: LUIS SUAREZ NA REKODI MBOVU YA UFUNGAJI DHIDI YA TIMU ZA TOP 4 - WIKIENDI KUIENDELEZA AU ATAIADHIBU GUNNERS?

Kiwango cha Luis Suarez msimu kimekuwa katika hali ya juu mno, waandishi kibao wa habari wamekuwa wakiandika makala za kumsifia huku thamani yake katika soko la usajili ikipanda maradufu. 
Lakini pamoja na kuwa rekodi nzuri za upachikaji wa mabao msimu huu - ila kuna kuna sehemu mshambuliaji huyu wa Uruguay anapata zero - hii namba ya mabao aliyoyafunga dhidi ya vilabu vikubwa kabisa vya ligi kuu ya England. 

Katika mabao yote 23 aliyoyafunga msimu huu, hakuna hata moja kati ya hayo lilotinga katika nyavu za vilabu vya Manchester United, Manchester City, Chelsea au Arsenal – vilabu vilivyoshika nafasi nne za juu msimu uliopita.

Kiundani zaidi, kati ya mabao hayo ni manne tu amezifunga timu 10 za juu katika msimamo wa ligi.

Je Suarez anavionea vilabu dhaifu tu? Hata ukiangalia rekodi za 

REKODI YA UFUNGAJI YA SUAREZ

Timu ambazo Suarez amezifunga msimu huu...
Sunderland (14th kwenye ligi)  mabao 2
Crystal Palace (17th) bao 1
West Brom (16th) mabao 3
Fulham (20th) mabao 2
Everton (5th) mabao 2
Norwich (15th)mabao 4
West Ham (18th)mabao 2
Tottenham (6th) mabao 2
Cardiff (19th) mabao2
Hull (13th) bao 1
Stoke (11th)mabao 2

REKODI DHIDI YA TOP 4
(Man Utd, Man City, Chelsea, Arsenal)
2013-14 – 23 goals, 0 against top four. (MECHI 4).
2012-13 – 30 goals, 4 against top four. (Mechi 8).
2011-12 – 17 goals, 2 against top four. (Mechi 8).
2010-11 – 4 goals, 0 against top four. (Mechi 3).
nyuma ya msimu huu, takwimu zinaonyesha hivyo. 
Ni mara 74 mshambuliaji huyo wa Uruguay ameweza kubusu mishipa ya kiganja chake akishangilia mabao anayoyafunga tangu ajiunge na Liverpool, lakini mabao 6 tu kati ya hayo amezifunga timu za TOP 4, na hayo yamepatikana baada ya mechi 23.

Wakati huo huo, amefunga mabao 11 dhidi ya timu ya Norwich. Pia katika miaka yote hii ameifunga Manchester United goli moja tu miaka miwili iliyopita katika dimba la Old Trafford.

Msimu huu, Suarez alifunga mabao 10 katika mechi nne tu mapema mwezi Desemba kabla ya Liverpool haijangia katika wakati muafaka wa kuamua hatma yao ya ubingwa msimu huu waliposafiri kwenda kucheza na Manchester City na Chelsea, katika michezo hiyo muhimu, Suarez alitoka kapa, huku Liverpool akifungwa mechi zote - pia alishindwa kufanya chochote katika mchezo dhidi ya Arsenal na hata dhidi ya Manchester United katika kombe la ligi - pia mechi hizo zote Liverpool walifungwa. 

Jumamosi hii, wanakutana na viongozi wa ligi Arsenal katika dimba la Anfield. Ndio kwa ukali wa Suarez kuzifumania nyavu dhidi ya timu za chini umeipa nafasi Liverpool ya kuweza kusogolea Top 3.
Ingawa kwa hilo ili liweze kutokea inabidi Liverpool ianze kushinda dhidi ya vilabu hivyo vikubwa, mabao na uchezaji mzuri wa Suarez unahitajika kufanikisha hilo.

Wapinzani wao wa Jumamosi, Arsenal, ndio timu ile ile iliyojaribu kumnyakua Suarez kutoka Merseyside kwenda London ya kaskazini wakati kiangazi walipotuma ofa ya £40m-plus-£1. 
Kwa kuwa na Suarez, iliaminika wangeweza kushindania ubingwa, lakini hata baada ya kumkosa wanaonekana kuwa vizuri mno katika harakati zao za kumaliza ukame wa miaka 9 bila kombe.  

Arsenal nao, wameshindwa kufnya vizuri dhidi ya kubwa kama United, City na Chelsea, kama ilivyo kwa Suarez.

Wikiendi hii Suarez ana nafasi ya kuwafunga midomo wachambuzi wa soka walio na mashaka juu ya uwezo wake dhidi ya vilabu vikubwa na kuiwezesha timu yake kuisogelea top 3 ya EPL. Je ataweza kuisimamisha Arsenal iliyo on fire???? Muda utatoa majibu. 



BARCELONA YAFIKISHA MABAO 100.

 Kwa msimu wa tisa mfululizo klabu ya FC Barcelona hapo jana usiku ilifikisha jumla ya mabao 100 ya kufunga baada ya kuifunga Real Sociadad mabao 2-0 kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya kombe la mfalme.

wachezaji 15 tofauti wa timu hiyo wameshirikiana kufunga jumla ya hayo mabao huku,wachezaji 5 kati yao wakiwa tayari wameshafunga zaidi ya mabao 10.
 Leo Messi 19, Pedro 16, Alexis 15, Cesc 12 and Neymar Jr 11.


SOKA KWENYE NAMBA: WESLEY SNEIJDER AFUNGA HAT TRICK YA PILI TANGU AANZE KUCHEZA SOKA LA KULIPWA



25
 Rekodi ya ushindi mfululizo wakiongoza ligi, iliyowekwa na FC Barcelona ilifikia tamati baada ya kupokea kipigo kutoka kwa Valencia na kuporwa uongozi wa Ligi na Atletico Madrid. Ushindi wa Valencia ulikatiza rekodi ya kushinda mara 25 mfululizo kwenye la liga zilizochezwa kwenye dimba la Nou Camp. Valencia imeweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kushinda nyumbani kwa Barca tangu Real Madrid walipofanya hivyo mnamo April 2012. Siku iliyofuatia Atletico Madrid wakashinda 4-0 dhidi ya Real Sociedad, wakaenda kushika usukani mwa ligi kwa mara ya kwanza tangu waliposhinda makombe mawili msimu wa 1995/96.
3
 Mabao matatu yaliyofungwa na Wesley Sneijder katika ushindi wa Galatasaray wa 6-0 dhidi ya Bursaspor jumapili iliyopita - ilikuwa ndio hat trick ya pili ya Sneijder tangu alipoanza kucheza soka la kulipwa. Pia ilikuwa hat trick ya kwanza katika kipindi cha miaka saba, mara ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa kwenye mchezo wa ushindi wa 4-1 wa Ajax dhidi ya Feyenoord mnamo 4 February 2007. Ushindi huo wa Gala ulikuwa mkubwa zaidi katika miaka ya hivi karibuni, mara ya mwisho walishinda ushindi mkubwa ilikuwa walipoifunga Manisaspor 6-3 February 2008.
3
 Miaka mitatu, miezi mitatu ya mechi 61 za matokeo chanya - huo ndio muda kamili tangu mara ya mwisho Manchester City waliposhindwa kufunga goli katika mchezo wa ligi kuu ya England uliochezwa nyumbani kwao, lakini kikosi cha Jose Mourinho kikavunja rekodi hiyo usiku wa Jumatatu, Lakini pia kikosi cha Jose Mourinho hakikuvunja rekodi hiyo tu bali pia walivunja rekodi ya City ya kushinda kwenye mechi ya ligi ya nane mfululizo pia kipigo cha pili katika mechi 22 walizocheza Etihad. 

SAMATTA; TUZO YA MASHABIKI NI KITU KIKUBWA


Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta amefunguka na kusema kuwa anajivunia tuzo aliyopewa ya mchezaji bora wa mwaka wa klabu yake ya TP Mazembe. Samatta alichaguliwa na mashabiki wa klabu kama mchezaji bora wa klabu kwa mwaka 2013. Mfungaji huyo bora wa michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika amesema hayo wakati akizungumza na mtandao huu siku ya leo.

"Nafurahi tu kwa kupata tuzo hiyo,  maana wapo wachezaji wengi pia ambao walistahili. Inaleta maana kubwa kama tuzo hiyo inatoka kwa mashabiki wa timu yako."
 
Samatta ametokea kuwa mchezaji muhimu sana wa klabu hiyo ambayo aliisaidia kufika hatua ya fainali ya michuano ya vilabu barani Afrika mwaka uliopita. Endelea kufuatia mtandao huu ambao kwa sasa upo katika jitihada za kufanya mahojiano na mshambuliaji huyo wa timu ya Taifa ya Tanzania.

KUELEKEA KOMBE LA DUNIA - KUNDI A; BRAZIL YA SCORALI v CROATIA YA NIKO NA ROBERT KOVAC



 Na Baraka Mbolembole
Brazil iliifunga Croatia katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi, Juni 13, mjini Berlin kwa bao 1-0. Timu hizo zitakutana tena baada ya kupita kwa miaka nane katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya ijayo ya kombe la dunia, Juni 12, mwaka huu katika uwanja wa Arena de Sao Paulo.

Mambo mengi yamebadilika tangu wakati ule kiungo mshambuliaji, Ricardo Kaka' alipoifungia, Selecao pekee katika mchezo wa mwisho kati ya timu hizo mbili. Croatia, chini ya kocha Niko Kovac, na wasaidizi wake, Robert Kovac ( mdogo wake Niko), Goran Lackovic na Vatroslav Miliacic, inasotea ushindi wake wa kwanza katika michuano tangu walipoifunga
Italia mabao 2-1, juni 8, 2002.
 
CROATIA
 Croatia ilishindwa kufuzu katika fainali zilizopita nchini Afrika
Kusini, washindi hao wa tatu wa mwaka 1998, wanarekodi ya kushinda michezo saba kati ya 13 waliyocheza katika fainali tatu walizofuzu miaka ya nyuma, huku ushindi wao mkubwa ni ule dhidi ya Ujerumani, Julai 4, 1998 walipoifunga kwa mabao 3-0 katika mchezo wa robo fainali. Mechi yao ya kukata utepe dhidi ya Brazil inatarajiwa kuwa kali kwa kuwa nchi hiyo inao wachezaji wa viwango vya juu kwa sasa barani Ulaya. 

CAMEROON INAWEZA KUVUKA KUNDI HILI
Katika mchezo mwingine wa kundi A, timu za Mexico na Cameroon, zitapambana juni 13, katika uwanja wa . Pengine ni timu iliyofuzu kwa utata mkubwa kuliko nchini nyingine yoyote. Cameroon ilimaliza nyuma ya Libya katika harakati za kufuzu kwa hatua ya mtoano katika kundi,' Simba wasiofugika' walipata nafasi ya kuikabili Tunisia na kuitupa nje na kufuzu kwa fainali za Brazil.

Ingawa hawana matokeo mazuri tangu mwaka 90, Cameroon si  timu ya kudharauliwa kwa namna yoyote. Kwa upande wa Mexico, timu hiyo ya Amerika ya Kati, iliishia katika hatua ya mtoano mwaka 2010 walipoondolewa na Argentina.  Mafanikio yao makubwa katika michuano hiyo ni yale ya miaka ya 1970, na 1986 walipoishia hatua ya robo fainali. Watacheza na Brazil, juni 17 na kumaliza na Croatia, Juni 23 ikiwa ni marudiano ya mpambano wao wa mwaka 2002 katika fainali za Korea kusini na Japan. Mexico ilishinda 2-1.

NYEPESI NYEPESI
Brazil inashikilia rekodi ya kucheza fainali mara tatu mfululizo. Walifanya hivyo katika miaka ya 1994, walipoifunga Italia kwa changamoto ya mikwaju ya penati, katika fainali za Marekani. Wakapoteza kwa mabao 3-0, dhidi ya waliokuwa wenyeji Ufaransa, 1998, na wakatwaa tena taji mbele ya Ujerumani, 2002, kwa ushindi wa mabao 2-0 katika fainali za Korea Kusini na Japan.

UJERUMANI
ndiyo timu iliyopoteza michezo mingi ya fainali za kombe la dunia. Imepoteza mara nne, 1966 dhidi ya waliokuwa wenyeji England, 1982 dhidi ya Italia, katika michuano ilipigwa nchini Hispania, wakalala tena mbele ya Argentina katika fainali za Mexico, 1986, na mara ya mwisho walilala dhidi ya Brazil, 2002.

Roger Millar aliisaidia timu ya Cameroon kufika robo fainali mwaka 1990 na kutolewa na England kwa kufungwa mabao 3-2 katika muda wa ziada. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Cameroon alikuwa na miaka 42 na siku 39 wakati alipoiwakilisha Cameroon dhidi ya Urusi, Juni 28, 1994 katika fainali zilizofanyika nchini Marekani.

WAAMUZI WANAKOSEA KATIKA MECHI ZA TIMU KUBWA TU ?


Baraka Mbolembole

WAAMUZI, hivi sasa wamekuwa kero kubwa kwa wapenzi wa soka nchini kutokana na kuboronga kwao katika michezo mbalimbali ya ligi kuu inayoendelea nchini. Abdallah Kambuzi, mwamuzi huyu alichezesha mchezo kati ya Yanga SC na Mbeya City, jumamosi iliyopita alionekana kushindwa kufanya maamuzi sahihi. Si yeye tu kumeibuka malalamiko zaidi kutoka kwa timu nyingine kuhusu uchezeshaji mbaya wa waamuzi wengi nchi.

Nao ni binadamu, hivyo kufanya makosa ni jambo la kawaida. Kama mchezaji hufanya makosa na kuadhibiwa, hivyo mwamuzi nae anaweza kufanya makosa. Ila pamoja na adhabu mbalimbali ambazo wamekuwa wakipata bado hali si nzuri. Wamekuwa wakifanya makosa  kwenye mechi za Yanga, Simba na Azam FC, tena ni makosa ya makusudi kabisa. Mfano, ni kadi nyekundu ambayo alipewa kiungo wa City, Steven Mazanda wiki iliyopita katika mchezo dhidi ya Yanga, na matukio ambayo yalifanywa na Haruna Niyonzima, baada ya kiungo huyo wa Yanga kuwa na kadi ya njano, baadae alitakiwa kuondoshwa uwanjani kwa kadi ya pili ya njano ila haikuwa hivyo, mwamuzi akaamua kukataa bao lililokuwa halali la Hamis Kizza kama  njia ya kusahihisha makosa yake.

WANAPANGA MATOKEO?

Bado hakuna ushahidi wa moja kwa moja kuhusu hilo, ila  timu nyingi zimekuwa zikiandaa 'fungu' la marefa ili wapate upendelo. Katika mchezo wa Ntibwa Sugar na Simba, kocha wa Mtibwa, Mecky Mexime alionekana kuwa na jabza kuhusu uamuzi wa mwamuzi , Deonisia Kyura ambaye alimtoa nje kiungo na nahodha wa timu yake Shaaban Nditti. Awali Nditti alikuwa na kadi ya njano ila aliamua kumchapa kofi Amis Tambwe ambaye alimbana na miguu walipokuwa wameanguka wote chini.

Nditti, inadaiwa alitoa lugha chafu kwa mwamuzi huyo ndiyo maana akaadhibiwa, ila muda mwingi alionekana kushindwa kuendana na ukubwa wa mechi. Kwa nini alipangwa? Tafakari....
Bahati mbaya ni kuwa waamuzi hao wamekuwa wakilalamikiwa zaidi katika michezo dhidi ya timu kubwa tu, huku wanapokuwa wakichezesha michezo dhidi ya timu nyingine nje ya Yanga, Simba na Azam wamekuwa wakifanya vizuri.
WANACHEZESHA KWA KUFUATA MAELEKEZO...
Ndiyo ukweli ulivyo, ila ni vigumu mtu wa Yanga, Simba au Azam kusema kuwa wanakuwa wakipata ' mbereko' kutoka kwa waamuzi. Tatizo hili linajulikana na wahusika ni viongozi wa klabu, waamuzi na wasimamizi wao. Klabu ndiyo zimekuwa zikihusika moja kwa moja kwa nia ya kupata matokeo ya ushindi tu. Mambo haya yanakera. Waamuzi nao ni binadamu hivyo ni rahisi kuingia katika ushawishi wa kuchukua pesa zinazowekwa mezani na viongozi wa klabu.
Mambo haya naamini yanafahimika kwa wahusika hivyo wanatakiwa kuchukua hatua ya haraka ya kuachana na mambo hayo ili kufanya timu zetu zishinde kwa uwezo wao, na mwisho tupate mabingwa sahihi. Siku zaidi ya 100 za rais wa TFF, Jamal Malinzi, soka la Tanzania bado lipo majaribuni. Waamuzi ni changamoto nyingine kubwa kwake. Awakataze kuchezesha kwa maagizo kutoka nje ya uwanja.

9 KANEMBWA WATAKIWA KUWASILISHA UTETEZI

Wachezaji tisa wa Kanembwa JKT pamoja na timu yao wanaolalamikiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kumpiga mwamuzi Peter Mujaya wanatakiwa kujitetea mbele ya Kamati ya Nidhamu itakayokutana Jumapili (Februari 9 mwaka huu).

Utetezi huo unaweza kuwa wa mdomo kwa walalamikiwa kufika wenyewe mbele ya kamati itakayokutana saa 4 kamili asubuhi au kuuwasilisha kwa njia ya maandishi.

Kamati ilikutana jana Jumatano (Februari 5 mwaka huu) kusikiliza malalamiko dhidi ya wachezaji hao na timu yao kwa tukio hilo lililotokea Novemba 2 mwaka jana kwenye mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) dhidi ya Stand United FC iliyochezwa Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Wachezaji hao ni Abdallah Mgonja, Bariki Abdul, Philipo Ndonde, Mbeke Mbeke, Mkuba Clement, Mrisho Mussa, Nteze Raymond, Ntilakigwa Hussein na Uhuru Mwambungu. Mlalamikiwa mwingine ambaye naye anatakiwa kujitetea ni timu ya Kanembwa JKT.

Ikiwa chini ya Mwenyekiti wake Tarimba Abbas, Kamati hiyo baada ya kusikiliza malalamiko dhidi ya wahusika na kupokea ushahidi wa aina mbalimbali kutoka kwa mlalamikaji imesema ili iweze kutenda haki katika shauri hilo ni lazima walalamikiwa wapate fursa ya kusikilizwa.

Katika hatua nyingine, Kamati hiyo iliyokutana kwa mara ya kwanza tangu ilipoundwa imesema imesikitishwa na vitendo vya fujo ndani ya mpira wa miguu, na kuwataka watu wasijihusishe na aina yoyote ya fujo.

KUTOKA FB LEO,VIPI SUALA LA OKWI ?









NUSU FAINALI COPA DEL REY: REAL WAITANDIKA ATLETICO MADRID 3-0, MARUDIANO WIKI IJAYO


All Goals - Real Madrid 3-0 Atletico Madrid... by beingoal1

Wednesday, February 5, 2014

KOMBE LA DUNIA MWAKA 2014, CHANGAMOTO, FURSA KWA BIDHAA KWA AJILI YA KUTANUA MASOKO NCHINI BRAZIL.



Mwaka 2014 umetawaliwa na tukio kubwa zaidi la kimichezo nalo ni kombe la dunia. Ni wakati wa makampuni yenye misuli mikubwa na hata washirika na wadhamini kujipanga kwa ajili ya kwenda sawa na kipyenga kitakachopulizwa rasmi jijini Sao Paulo nchini Brazil.
Chapa kama Adidas, Coca-Cola, Visa, Continental na McDonald zimewekeza paundi bilioni 5.5, kwa ajili tu ya kushiriki kupata haki ya kufanya biashara kwenye michuano hiyo, inayoandaliwa kila baada ya miaka minne na shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA.  Ni wakati wa kujiuliza sasa ni zipi changamoto na fursa zitakazozikumba chapa hizi nchini Brazil?
Kombe la dunia ni nafasi kwa bidhaa mpya pia washirika wa kibiashara kupata nafasi ya kuwasiliana na asilimia 50 ya watu wote duniani, kwani mashabiki zaidi ya bilioni 4 watawasha televisheni zao kuangalia michuano hiyo, pia ulimwengu wa digitali pamoja na mitandao ya kijamii, hivyo ni nafasi kwa bidhaa kupata umaarufu ingawa kutakuwa na ushindani kwenye kupata nafasi.
Nani atawika? Hilo ni swali muhimu sana kwetu. Brazil ni nchi ambayo  itatawaliwa na rangi za kila aina kutoka kila kona ya dunia, pamoja na ushabiki uliotukuka wa mchezo wa soka nchini humo, na ni muda pia wa bidhaa kufikia malengo ya kibiashara kwa kuwa huo ni muda wa thamani.
Adidas kwenye ubora wametumia njia zote kukabiliana na wapinzani wao NIKE, ambayo ni bidhaa maarufu katika bara la Amerika kusini. Mnamo mwezi Disemba Adidas walizindua mpira maalum utakaotumika kwenye kombe la dunia uliopewa jina la BRAZUCA, ambapo kampuni hiyo kubwa kwa kuzalisha vifaa vya michezo yenye makazi yake nchini Ujerumani, ilifanya utafiti kwa kuwahoji wakazi zaidi ya milioni moja nchini Brazil, ili kufahamu namna walivyoupokea huo mpira, lakini pia kampuni hiyo ya Adidas iligawa mpira mmoja mmoja kwa kila mtoto aliyezaliwa ile siku ya uzinduzi. mmmhh mambo hayo!
Wanachi wa Brazil ni moja ya wateja lakini kwa upande mwingine watatumika kama njia ya kutangaza  bidhaa, na makampuni mengi yanategemea kufaidika na michuano hiyo kwa kuitumia  kama ngazi  kwa kuwa karibu na wananchi kupitia mitandao ya kijamii pia na biashara za kutembeza mitaani.
Mitandao ya kijamii ni njia nzuri na bora kwa mashabiki kufuatilia  michezo  kwa kubadilishana uzoefu kupitia Twitter, Facebook and YouTube.
Coca-Cola kama wadhamini wa michuano ya kombe la dunia, wameshaanza kutumia nafasi ya kufanyika kipindi cha kiangazi kwa kutumia ziara ya kombe la dunia wakijihusisha na mashabiki moja kwa moja kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram jambo ambalo linamvuto kwa mashabiki wa soka.
Pamoja na kufanya mitandao ya kijamii ni vyema  kwa mameneja bidhaa kutumia fursa  kama ilivyokuwa kwa (Super Bowl 2013 ) na Adidas (2012 kwenye michuano ya Olympic ) kufanikisha kuwatumia walaji kama mabalozi kupitia idadi zao kwenye mitandao ya kijamii..
Walaji watakuwa  na uwezo wa kuangalia video kwa mahitaji ya Brazil, na kutokana na mazingira kumetoa fursa kwa technolojia kuweza kumsaidia mlaji kupata fursa ya kushuhudia matukio .
Wadhamini wengine wa Kombe la dunia la FIFA 2014 ni kampuni ya VISA, wameikuza technolojia yao ya digitali kwa walaji  kupitia bidhaa yao ‘Go World’ inayofanana na ile ya  kampeni  ya michuano ya Olympic 2012.
VISA ni maarufu kwenye mtandao wa YouTube, kwa maudhui maalum ya video zinazoonyesha maisha halisi ya watu,  pia mashindano ya mbio  kuendana na matakwa ya walaji. Sasa katika hili itasaidia sana kujenga imani ya watu  juu ya VISA.
Moja ya changamoto kwa bidhaa ni wananchi kukosa imani na bidhaa husika kutokana na umaarufu wao, kwenye kujikita katika tasnia ya michezo.  Changamoto ya kombe la dunia la Fifa  2014 kwa washirika wa kibiashara,  ni kutafuta  nafasi ya  kujikita  kwenye nyoyo za watu ili kupata nafasi ya kuzungumza  kutakakopelekea kupata uhuru wa kujitawala kibiashara kwa muda mrefu, na bidhaa kupata fursa mpaka siku ya fainali  

TASWIRA YA MCHEZO KATI YA SIMBA NA MTIBWA SUGAR KATIKA UWANJA WA JAMUHURI MOROGORO,ZAFUNGANA 1-1.

Kikosi cha Timu ya Soka ya Simba Kilichoanza Dhidi ya Mtibwa leo
Nyuma Kuanzia Kushoto: Kocha Msaidizi Seleman Matola,Tambwe,Amri Kiemba,Joseph Owino,Jonas Mkude,Musoti.Mbele Kushoto:Singano,Awadhi,Haruna Chanongo,Ivo Mapunda,Rashid Baba Ubaya,Haruna Shamte.
 Kikosi cha Timu ya Soka ya Mtibwa Nyuma kuanzia Kushoto:JumaLuizio,Shaban Nditi, Hassan Ramadhan,Ally Shomary  Salim Mbonde.Mbele Kuanzia Kushoto : Jamal Mnyate,Said Mkopi,Shaban Kisiga, Husein Sharif,Salvatory Mtebe,Mussa Mgosi.
Waamuzi wa Mchezo wa Leo wakiwa na Manaodha wa Timu Zote Mbili.
 Wachezaji wa Timu ya Soka ya Mtibwa Sugar Wkishanilia Goli Lililofungwa na Musa Mgosi  Katika Dakika ya 18 ya Mchezo.
 Rashid Baba Ubaya Akitafuta Mbinu za Kumtoka Beki wa Mtibwa Sugar Said Mkopi.
 Kipa wa Mtibwa Hasani  Sharifu  
 Mashabiki waliojitokeza katika Mchezo huo wakishangilia muda wote wa Mchezo

 Golikipa wa Timu ya Mtibwa Sugar Hussein Sharif Akiwa Ameokoa Moja ya Purukushani katika Lango Lake.Akishihudiwa na Beki wake Salim Mbonde Pamoja na Mshambuliaji wa Simba Khamisi Tambwe.
 Simba wakishangilia Goli lao lilofungwa na Khamis Tambwe Bao lililofungwa dakika 50 ya mchezo.

Mpira Umemalizika Mtibwa 1 -1 Simba. Goli la Mtibwa Sugar Lilifungwa dakika ya 18 ya Mchezo bao Lililofungwa na Mussa Mgosi .Hadi Mapumziko Mtibwa walikuwa wanaongoza kwa Goli Hilo Moja.Kipindi cha Pili Mpira ulianza kwa kasi Simba walishambulia Lango la Mtibwa mara kwa mara Na kujipatia bao la Kusawazisha katika dakika ya 50 ya Mchezo.Katika Mchezo Mchezaji wa Mtibwa Shaban Nditi Alionyeshwa kadi Nyekundu Dakika ya 69 baada ya Kutoa maneno Machafu kwa Mwamuzi.Dakika ya 72 Said Ndemla anaingia Kuchukua nafasi ya  Haruna Shamte,Dakika ya 75, Juma Mpakala Aliingia Kuchukua nafasi ya  Jamal Mnyate. Dakika ya 87  wanafanya mabadiliko ya mwisho, aliingia Abdallah Salum Kuchukua nafasi  Mgosi..