Mwaka 2014 umetawaliwa na
tukio kubwa zaidi la kimichezo nalo ni kombe la dunia. Ni wakati wa makampuni
yenye misuli mikubwa na hata washirika na wadhamini kujipanga kwa ajili ya
kwenda sawa na kipyenga
kitakachopulizwa rasmi jijini Sao Paulo nchini Brazil.
Chapa kama Adidas, Coca-Cola, Visa, Continental na McDonald zimewekeza
paundi bilioni 5.5, kwa ajili tu ya kushiriki kupata haki ya kufanya biashara
kwenye michuano hiyo, inayoandaliwa kila baada ya miaka minne na shirikisho la
mpira wa miguu duniani FIFA. Ni wakati
wa kujiuliza sasa ni zipi changamoto na fursa zitakazozikumba chapa hizi nchini
Brazil?
Kombe
la dunia ni nafasi kwa bidhaa mpya pia washirika wa kibiashara kupata nafasi ya
kuwasiliana na asilimia 50 ya watu wote duniani, kwani mashabiki zaidi ya
bilioni 4 watawasha televisheni zao kuangalia michuano hiyo, pia ulimwengu wa
digitali pamoja na mitandao ya kijamii, hivyo ni nafasi kwa bidhaa kupata umaarufu
ingawa kutakuwa na ushindani kwenye kupata nafasi.
Nani atawika? Hilo ni swali muhimu
sana kwetu. Brazil ni nchi ambayo
itatawaliwa na rangi za kila aina kutoka kila kona ya dunia, pamoja na ushabiki
uliotukuka wa mchezo wa soka nchini humo, na ni muda pia wa bidhaa kufikia
malengo ya kibiashara kwa kuwa huo ni muda wa thamani.
Adidas kwenye ubora wametumia njia zote kukabiliana
na wapinzani wao NIKE, ambayo ni bidhaa maarufu katika bara la Amerika kusini.
Mnamo mwezi Disemba Adidas walizindua mpira maalum utakaotumika kwenye kombe la
dunia uliopewa jina la BRAZUCA, ambapo kampuni hiyo kubwa kwa kuzalisha vifaa vya
michezo yenye makazi yake nchini Ujerumani, ilifanya utafiti kwa kuwahoji
wakazi zaidi ya milioni moja nchini Brazil, ili kufahamu namna walivyoupokea
huo mpira, lakini pia kampuni hiyo ya Adidas iligawa mpira mmoja mmoja kwa kila
mtoto aliyezaliwa ile siku ya uzinduzi. mmmhh
mambo hayo!Wanachi wa Brazil ni moja ya wateja lakini kwa upande mwingine watatumika kama njia ya kutangaza bidhaa, na makampuni mengi yanategemea kufaidika na michuano hiyo kwa kuitumia kama ngazi kwa kuwa karibu na wananchi kupitia mitandao ya kijamii pia na biashara za kutembeza mitaani.
Mitandao ya kijamii ni njia nzuri na bora kwa mashabiki kufuatilia michezo kwa kubadilishana uzoefu kupitia Twitter, Facebook and YouTube.
Coca-Cola kama wadhamini wa michuano ya kombe la dunia, wameshaanza kutumia nafasi ya kufanyika kipindi cha kiangazi kwa kutumia ziara ya kombe la dunia wakijihusisha na mashabiki moja kwa moja kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram jambo ambalo linamvuto kwa mashabiki wa soka.
Pamoja na kufanya mitandao ya
kijamii ni vyema kwa mameneja bidhaa
kutumia fursa kama ilivyokuwa kwa
(Super Bowl 2013 ) na Adidas (2012 kwenye
michuano ya Olympic ) kufanikisha kuwatumia walaji kama mabalozi kupitia idadi
zao kwenye mitandao ya kijamii..
Walaji watakuwa na uwezo wa kuangalia video kwa mahitaji ya
Brazil, na kutokana na mazingira kumetoa fursa kwa technolojia kuweza
kumsaidia mlaji kupata fursa ya kushuhudia matukio .
Wadhamini wengine wa Kombe la dunia
la FIFA 2014 ni kampuni ya VISA, wameikuza technolojia yao ya digitali kwa
walaji kupitia bidhaa yao ‘Go World’ inayofanana
na ile ya kampeni ya michuano ya Olympic 2012.
VISA ni maarufu kwenye mtandao wa YouTube,
kwa maudhui maalum ya video zinazoonyesha maisha halisi ya watu, pia mashindano ya mbio kuendana na matakwa ya walaji. Sasa katika
hili itasaidia sana kujenga imani ya watu
juu ya VISA.
Moja ya changamoto kwa bidhaa ni
wananchi kukosa imani na bidhaa husika kutokana na umaarufu wao, kwenye
kujikita katika tasnia ya michezo. Changamoto ya kombe la dunia la Fifa 2014 kwa washirika wa kibiashara, ni kutafuta
nafasi ya kujikita kwenye nyoyo za watu ili kupata nafasi ya
kuzungumza kutakakopelekea kupata uhuru
wa kujitawala kibiashara kwa muda mrefu, na bidhaa kupata fursa mpaka siku ya
fainali
No comments:
Post a Comment