Search This Blog

Saturday, March 3, 2012

MIDO AWATOA YANGA CHAMPIONS LEAGUE



Goli la Mshambuliaji aliyewahi kutamba na vilabu mbalimbali Ulaya na kurejea nyumbani kwao Misri, Mido lilitosha kuwaondoa Yanga katika mashindano ya klabu bingwa Afrika.

Yanga wakimaliza mchezo wakiwa pungufu kufuatia kadi nyekundu ya Athuman Iddi Chuji katika dakika ya 55, walionyesha kiwango kizuri katika kipindi cha pili, huku safu ya ushambuliaji ikiwaangusha yanga jijini Cairo.

Zamalek wakiwa katika jiji lao la Cairo katika uwanja wa jeshi na wakicheza bila mashabiki walijipatia goli pekee la ushindi katika dakika ya 31 kupitia kwa mshambuliaji wake Mido.

Katika kipindi cha pili nusura Zamalek wapate goli la pili kufuatia penati waliyoipata katika dakika ya 74 na kukosa penati hiyo. Huku yanga wakipoteza nafasi katika dakika ya 46.

Kwa matokeo hayo Yanga wametolewa katika michuano ya klabu bingwa Afrika, huku Zamalek wakisonga katika raundi ya pili.

Kikosi cha yanga kilichoanza leo: Shaban Kado, Shadrack Nsajigwa, Stephan Mwasika, Nadir Haroub, Athuman Iddi, Juma Seif, Omega Seme, Haruna Niyonzima, Jerry Tegete, Keneth Asamoah na Nurdin Bakari

RIO FERDINAND: NINGEKUWA BOSS WA FA NINGEMCHAGUA HARRY REDKNAPP KUIONGOZA ENGLAND.


Rio Ferdinand leo amefichua kwanini Harry Redknapp ni chaguo sahihi kuwa kocha wa England.
Ferdinand ambaye alitolewa kutoka timu za vijana na Redknapp wakiwa West Ham.
Aliliambia gazeti la The Sun: “Kama ningekuwa mtu ninayetoa maamuzi ningemteua Harry bila shaka.
“Unapomtumikia kama kocha wako, anakufanya ujionee kama mtu muhimu sana.”

Rio ambaye timu yake ya Manchester United inakutana kikosi cha Harry Redkanpp jumapili hii @White Hart Lane, anaamini kocha wake wa zamani na sifa na ubora wote wa kuwa kocha England.
FA inategemea kupata kocha mpya mwishoni wa premier league May 13 na wanasema kuna makocha zaidi ya mmoja wenye nafasi ya kumrithi Capello.

WENGER ASHANGAZWA NA KUTUNUKIWA TUZO YA KOCHA BORA EPL


Arsene Wenger anasema kuna makosa yalifanyika wakati wa kumteua kocha bora wa mwezi huu katika ligi kuu ya England.
Boss huyo wa Gunners anapitia katika kipindi kigumu zaidi katika uongozi wa benchi la Arsenal lakini ameiongoza timu hiyo kutofungwa katika premier league katika kipindi cha mwezi uliopita wote akishinda mechi 3 na katika nne.
Arsenal walitoka nyuma na kuwafunga Spurs kwa 5-2 at Emirates Stadium wikiendi iliyopita na kujiweka katika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi huku leo wakiwa na mechi ngumu dhidi ya Liverpool.
“Ilinishangaza sana. Sikuweza kuelewa kabisa. Kama ulikuwa unasoma magazeti wiki 2 zilizopita utagundua kulikuwa na makosa katika kunipa hii tuzo. Wakati wananiambia kuhusu kuchukua tuzo hii nilidhani wanaongea na mtu mwingine nyuma yangu. Kiukweli sikutegemea kabisa kushinda tuzo hii”

BALOTELLI AMKERA TENA MANCINI - APIGWA PICHA AKITOKA KLABU YA WACHEZA UCHI MASAA KADHAA KABLA YA MECHI.


Mario Balotelli anaweza kujikuta katika matatizo makubwa na kocha wake Roberto Mancini  baada ya kupigwa picha akitoka klabu ya wacheza uchi jana alfajiri.
Mancini alikuwa amepanga kumuanzisha muitaliano huyo katika mechi ya leo dhidi ya Bolton.
Na sasa kutokana na tukio la kuonekana alfajiri akitoka kufanya starehe muda mfupi kabla ya mechi ya leo anaweza kupigwa benchi .
Mancini ambaye juzi alimuonya Balotelli kuhusu tabia zake inasemekana amekarishwa na kitendo cha mchezaji huyo ambaye ndio alikuwa akimtegemea leo hii kutokana na Sergio Aguero na Edin Dzeko kuwa na uchovu baada ya kutumika katika mechi za kimataifa wiki hii.

UZINDUZI WA SIMBA TV WAFANA !


Mgeni rasmi,Naibu Waziri wa Nchi,Ofis ya Waziri Mkuu,tawala za Mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI),Kassim Majaliwa,akibofya kitupe kuzindua rasmi kipindi cha Simba TV kitakachokuwa kinarushwa na kituo cha cha runinga cha Clouds,hafla hiyo imefanyika kwenye jengo la Quality Center  kwenye ukumbi wa Cleopatra,jijini Dar,Kulia ni Mwenyekiti Msaidizi Simba,Geofrey Nyange 'Kaburu'Mh  Alhaj  Kapuya na shoto ni Mwenyekiti wa Simba Sc Alhaj Ismail Aden Rage,na Afisa habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga




Makofi tafadhali..!Mgeni rasmi,Naibu Waziri wa Nchi,Ofis ya Waziri Mkuu,tawala za Mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI),Kassim Majaliwa,akipiga makofi mara baada ya kuzindua kipindi cha Simba TV kitakachokuwa kinarushwa na kituo cha cha runinga cha Clouds,hafla hiyo imefanyika kwenye jengo la Quality Center kwenye ukumbi wa Cleopatra,jijini Dar,Kulia ni Mwenyekiti Msaidizi Simba,Geofrey Nyange 'Kaburu'Mh  Alhaj  Kapuya na shoto ni Mwenyekiti wa Simba Sc Alhaj Ismail Aden Rage,na Afisa habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga kwa pamoja urwakipiga makofi kufurahia uzinduzi huo uliofana kwa kiasi kikubwa.




Swed Nkwabi,Said Tully na Charles Amka wakifungua Champagne!


 Keki yenyewe ilivyokuwa imenoga.


kutoka kushoto ni Alex Luambano,Salum Mwalim,Ibrahim Masoud, Msafiri Mgoyi, Salum Abdallah na Mdau



Kocha wa Simba Sc, Milovan Cirkovic akicheers na meza kuu


Mgeni rasmi,Naibu Waziri wa Nchi,Ofis ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI),Kassim Majaliwa akikata keki huku sehemu ya meza kuu ikishuhudia tukio hilo adhimu na ka kihistoria









Mgeni rasmi Kassim Majaliwa akimlisha keki Mwenyekiti wa Simba Sc,Alhaji Aden Rage huku wageni waalikwa meza kuu wakishuhudia tukio hilo.



Mdau Nick Malayu a.ka. Nick Boy akifurahia kujinyakulia jezi ya mchezaji mahiri wa Simba SC.Haruna Moshi a.k.a Boban.






Baadhi ya Waandishi wa habari walioshuhudia uzinduzi huo uliofana kwa kiasi kikubwa.


Baadhi ya wageni waalikwa wakiwemo wachezaji wa Simba ndani ya hafla hiyo






Wadau wakifuatilia jambo ukumbini wakati hafla ikiendelea





Vijana kutoka THT,akiwemo Barnaba,Amin na wengineo walinosha  vilivyo uzinduzi huo.


Mzee wa Fullshangwe,ambaye pia ni mshabiki mkubwa wa Simba Sc.John Bukuku aliibuka na jezi yake kama uonavyo pichani.


Mshambuliaji Felix Sunzu akimkabidhi kwa heshima jezi yake mgeni rasmi,Mh Kassim Majaliwa


Mchezaji Nyota wa zamani wa Simba SC,Zamoyoni Mogella a.k.a Gholden Boy akizungumza machache kwenye hafla hiyo usiku wa kuamkia leo.

VILLAS-BOAS: LAMPARD SIO MKE WANGU SIHITAJI KUPATANISHWA NAE.


Bosi wa Chelsea Andre-Villas Boas amesisitiza hakuna haja kupatana na Frank Lampard huku akitania “Hatujaoana.”
Lampard wiki iliyopita alikiri kwa mara ya kwanza kwamba mahusiano yake na AVB sio mazuri, lakini AVB amesema haoni umuhimu wa yeye kukaa na chini na Lampard kumaliza tofauti zao, huku akisisitiza bado wanazungumza wanapokuwa mazoezini.
“Mwisho wa siku ni mahusiano kati ya kocha na mchezaji, maneno ya Frank ni ya kweli kutokana na mahusiano yetu yalivyo.
“Kwangu mimi nakubaliana na aliyoyasema, sina tatizo lolote.”
Lampard ameweka wazi kwamba hana furaha na idadi ndogo ya michezo aliyopewa msimu huu lakini AVB alisema: “Inanibidi kuchagua timu – kuchagua timu iliyo bora kwa kila mechi.
“Frank amekuwa hapati sana nafasi lakini haimanishi kwamba nina matatizo nae binafsi.”

Friday, March 2, 2012

CHANGAMOTO: JAPO KWA MARA MOJA - YANGA FUATENI MFANO WA SIMBA HII.


Hiki ndio kikosi cha timu ya simba kilichoitoa na kuivua ubingwa klabu ya zamalek mwaka 2003  kwenye michuano ya kombe la mabingwa wa afrika. ilikuwa ndio mara ya kwanza na mwisho kwa timu ya Tanzania kushinda katika ardhi ya Misri.

 Yanga kesho wanacheza na Zamalek inabidi na inapaswa wajitume na kuhakikisha wanaifikia rekodi ya watani wao wa jadi kwa kuwatoa Zamalek tena wakiwa nyumbani kwao Misri na kuweza kuiletea sifa nchi na maendelea ya mpira bongo kwa ujumla.

UNAPENDA KUSOMA HABARI ZA SIMBA S.C - HII HAPA TOVUTI YAO MPYA

UONGOZI wa klabu ya Simba leo unaingia mkataba wa miaka miwili na kampuni ya Etech kwa ajili ya kufungua tovuti (website) itakayokuwa ikitoa taarifa zote zinazoihusu klabu hiyo.

Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema jana kuwa wameamua kuingia mkataba ili wapenzi wa timu hiyo wapate habari kwa uharaka kupitia tovuti hiyo baada ya ile ya mwanzo kutofanya kazi katika kiwango kizuri na kuamua kuifunga.

Alisema kupitia tovuti hiyo uongozi wa Simba unaamini wapenzi wa klabu hiyo watapata habari zinazohusu timu hiyo kwa uharaka zaidi na kwa muda wowote sambamba na kutoa maoni yao juu ya maendeleo ya timu yao.

"Kuanzia Machi 1 Simba itaingia mkataba wa miaka miwili na kampuni ya Etech, ambapo itafungua tovuti kwa ajili ya kupata habari za klabu yetu kwa uharaka na kwa muda unaotakiwa, lengo hasa ni kurahisisha mawasiliano kati yetu na wadau wetu, ambapo tutakuwa tukienda kisasa zaidi,"alisema Kamwaga.

WAPINZANI WA SIMBA KUWASILI KESHO


Wapinzani wa vinara wa Ligi kuu ya Vodacom Simba SC katika michuano wa kombe la shirikisho CAF, Kiyovu SC wanataraji kuwasili kesho badala ya leo.

Kiyovu ilitarajiwa kuwasili leo jioni lakini kutokana na kukosa ndege watakuja nchini kesho kwa ajili ya mchezo wa marejeano, utakao chezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Katika mchezo wa awali uliochezwa katika jiji la Kigali ulimalizika kwa timu zote kutoka sare ya goli 1-1. Goli la Simba likifungwa na Mwinyi Kazimoto.

Katika hatua nyingine Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi anatarajiwa kuwasili nchini kesho na kujiunga na kambi ya Simba moja kwa moja. Okwi alikuwa na timu ya taifa ya Uganda iliyofungwa goli 3-1 na Congo.

Wakati huo huo Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga wamewasili salama jijini Cairo, kwa ajili ya mchezo wa marejeano dhidi ya Zamalek, mchezo utakao chezwa katika uwanja wa jeshi bila ya mashabiki.

Vilevile na Jamhuri ya Pemba nayo iliwasili salama nchini Zimbabwe, ambapo wanataraji kucheza na Hwange ya Zimbabwe, baada ya kuchapwa goli 3 katika mchezo wa awali wa kombe la shirikisho CAF uliochezwa katika uwanja wa Gombani.

Wawakilishi wengine wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mafunzo FC wao watasafiri machi 7 kwenda Msumbiji kwa ajili ya mchezo wa marejeano.


SAKATA LA MBWANA SAMATTA KUACHWA TIMU YA TAIFA LACHUKUA SURA MPYA,WADAU WAENDELEA KUTOA MAONI YAO!

mawazo/maoni yaliyotolewa na wadau hapo juu si mabaya sababu kila mtu anamtazamo wake kwenye kila jambo anapolitazama au kulifikiri. Ila mimi nataka kupingana na Bw. GEORGE [Mchangiaji wa kwanza kama ilivyoorodheshwa hapo juu] kwa hoja zifuatazo.

1. Timu yoyote ile ambayo ina uhai hapa duniani hata kama ikicheza team work 100 percent ni lazima pawepo na mtu angalau mmoja au wawili ambao watatumia uwezo binafsi na umakini wao kuleta ushindi kwenye timu, hilo huwezi kulipinga kutokana na mpira wa sasa ulivyo. Kwa mfano: Man United bila ROONEY utaona wanapata tabu sana kushinda, au ARSENAL ya leo bila ROBIN Van PERSIE pale mbele na pale kati akikosekana SONG BILLONG utata huonekana kwenye perfomance ya team. Hiyo ni mifano michache tu ingawa ipo mingi na yenye mantiki. Tazama mabingwa wapya wa Africa [ZAMBIA] pale kati walikuwepo watu wawili muhimu sana ISACK CHANSA na KALABA kukosekana kwa hawa watu zambia ingekuwa na wakati mgumu sana...pia pale mbele alikuwepo captain mwenye CHRISTOPHER KATONGO huyu mtu balaa bana we acha tu.

2. Napenda kukukumbusha tu kuwa NAPOLI ni timu moja nzuri yenye kucheza ki-team work huku ikiwa na wachezaji muhimu inaowategemea kufanya matokeo yawe mazuri kwao, utaizungumziaje NAPOLI bila EDINSON CAVANI na EZEQUIEL LAVEZZI pale mbele, au MAREK HAMSIK pale kati!!??? kama ni mpenzi wa mpira na unafuatilia serie A kwa karibu na si kusubiri uione NAPOLI kwenye UCL hapo utakuwa unakosea sana kaka

MWISHO, napenda kusema kuwa SAMATTA ni muhimu sana kwenye timu ya Taifa [TAIFA STARS] na kukosekana kwake ni tatizo kubwa sana, kuna kitu ambacho Kocha POULSEN anashindwa kufanya uamuzi wa maana, kuwa mfungaji bora wa league haimaanishi hata ukiperfom vibaya then watu wakae kimya eti kisa kwenye VPL unafunga magori. Huyu JOHN BOCCO hawezi kutufikisha kokote kule kwenye hii safari yetu, hebu jiulize kwanza tangu aanze kuvaa jezi ya timu ta taifa kafunga goli ngapi? then ukipata jibu ndo utajua kwanini wadau tunalia na uwepo wa SAMATTA pale mbele
NASHUKURU SANA KWA MJADALA HUU

Thursday, March 1, 2012

POGBA NA FRYERS WAPEWA MASAA 48 KUSAINI - LASIVYO WASAHU KUICHEZEA TENA UNITED


Wachezaji wawili wanaoweka ngumu kusaini mkataba mpya ndani ya klabu ya Manchester United Paul Pogba na Ezekiel Fryers wameambiwa wasaini mikataba mipya ndani ya masaa 48 au wasahau kuichezea tena Manchester United.
Teenagers hao wanaonekana kutaka kufuata mfano wa bad-boy Ravel Morrison nje ya Old Trafford  baada ya kukataa kuweka saini kwenye mikataba mipya kwa muda mrefu sasa.
Pogba 18, na Fryers 19, wanamaliza mikataba yao mwezi June mwaka huu na baada ya kubembelezwa sana sasa inaonekana mabosi wa United wamepoteza uvumilivu na kuawaambia ijumaa ndio mwisho na hatma yao wataichagua siku hiyo.

MAONI YA BAADHI YA WADAU JUU YA SOKA LA BONGO!

Mara tu baada ya mchezo baina ya TANZANIA na MSUMBIJI hapo jana kumalizika, niliandika article ya kuachwa kuitwa kikosini mshambuliaji Mbwana Samatta yenye kichwa cha habari,

Jan Poulsen hawezi kukwepa lawama za kutomuita Mbwana Samatta

kuachwa kwa Samatta kwenye kikosi cha Stars kwa mtazamo wangu ni kama vile kenya kuacha kumuita mshambuliaji Dennis Oliech ama Argentina kutangaza kikosi bila ya Messi au Ureno bila Ronaldo.
haya ni baadhi ya Maoni ya walioisoma hii article...

Kaka shafi napingana na wewe.

Kwa muda mrefu kumejengeka tabia ya waandishi ya habari za michezo kutoa uchambuzi wa michezo kwa kutegemea matokeo ya mechi husika.Mathalani ikitokea siku timu imeshinda, mchambuzi atatoa uchambuzi wenye kuonyesha ubora au uimara wa timu iliyoshinda huku mapungufu yakiwekwa kapuni (hata kama mapungufu yalikuwepo mengi tu). Wachezaji watapambwa na kusifiwa pasipo kifani utafikili walicheza mpira kama ule tunaoushuhudia ukichezwa na timu bora barani ulaya! Vilevile, wachambuzi hawa wamekuwa na mtazamo wa kuangalia performance ya mchezaji mmoja mmoja zaidi, wakati mpira wa kisasa unategemea zaidi timu kucheza pamoja yaani teamwork. Kuna timu zina wachezaji hawana majina makubwa lakini zinaogopwa kwa mchezo wao wa pamoja. Mfano mmoja ni Napoli ya italia! Kwa bongo si ajabu kusikia timu haikushinda kwa sababu mchezaji fulani alikosekana!

Lately kumekuwa na habari kwenye media eti national team jana haikushinda kwa sababu mbwana samatta hakuwepo. Napingana na hoja hii. Hiyo ni short sight, huyo ni mtu mmoja na sio kweli kama ana uwezo kama inavyoelezwa. Waandishi na wachambuzi hawa wanapaswa kuwa makini na wanayoyaongea. Wakati wa maximo wananchi wakisukumwa na waandishi/wachambuzi hawahawa walikuwa wakimshinikiza kocha kuchagua wachezaji fulanifulani. Leo hii watu haohao wanamponda mzungu pulsen wanasema afadhali ya maximo!. Jamani huyo mzungu habahatishi! hiyo ni taaluma yake kaisomea! Huyo ni mtaalam wa ngazi ya juu haitaji wiki nzima kumtazama mchezaji na kujua kama anamfaa au la!. Kwa mtazamo wangu, mwalimu alipata fursa ya kumwona samatta na naamini hata maamuzi ya kumwacha yalizingatia uchambuzi wake wa kitaalam kama mwalimu. Siamini kama angeweza kumwacha tu pasipo na sababu ya msingi, kwani timu ikishinda ni sifa kwake pia!.


Kwa upande mmoja tunatambua kuwa waandishi/wachambuzi wanapaswa kuandika au kusema! Kwao hii ni kazi! Na naamini wanalipwa kwa kazi hiyo! Hivyo ni lazima waseme au waandike! Lakini kwa upande wa pili naamini waandishi wana jukumu la kutoa taarifa sahihi pasipo kupotosha umma. Na ili waweze kutoa taarifa sahihi wanapashwa wajielimishe ili wajenge ‘competence’ kwenye eneo hili. Kwani si kila mtu anaweza kuandika habari za michezo, ni lazima awe amepata taaluma ya michezo! Jamani michezo ni taaluma inasomewa kama zilivyo taaluma zingine. Nimesema hivi kwa sababu ni rahisi kwa mwananchi wa kawaida kuamini kile anachokisoma au kukisikia kwenye media.

Mtazamo wangu kuhusu michezo hapa nchini ni kuwa tunahitaji kufanya uchambuzi mpana zaidi wa mfumo mzima wa mpira nchini na kuufanyia kazi. Mfano Je kuna Sera na Mkakati na Programu kuhusu michezo? Je kuna mfumo wa kitaasisi wa kutekeleza sera, mkakati na program? Je mfumo unakidhi au unahitaji maboresho? Je sera, mkakati na program vinatafsiriwa vipi kivitendo? Je mfumo unatoa fursa ya utambuzi, ukuzaji na uendelezaji wa vipaji? Muundo wa timu zetu ukoje? Je mfumo wa timu zetu unatoa fursa ya utambuzi, ukuzaji na uendelezaji wa vipaji?
Vinginevyo hizi hadithi za kulaumu makocha na wachezaji hazitaisha NG’O!

Mdau wa Michezo,
George

1.     Asalam alaykum wadau,
Nakushkuru sana kaka Shaffih kwa kutupatia maelezo/maoni/ushauri wa kina kuhusu soka la Tanzania. Hii ni faraja kwangu binafsi na baadhi yetu kwani tunapata sehemu ya kuanzia ama kuongezea pale ulipopaacha wewe.
Sikuweza kuiona mechi hii lakini kutoka na malezo yako nimepata picha fulani na mimi sasa naendeleza kidogo kama ifuatavyo:
Sijui pattern or system or formation waliyocheza lakini ki uhalisia kama walikuwa beki wa kati wanakwenda pembeni kuficha nafasi ya Mwasika nadhani huu ni utaratibu hasa pale timu inapomtumia beki kama winger ama kiungo, na hapo ilitakiwa viungo wa kati (Nditi/Kazimoto)na/au mawinger (Nizar/Barnabas) kuingia kati kuficha nafasi iliyoachwa na beki wa kati aliyekwenda kumfichia makosa beki wa pembeni huku Mwasika (beki wa pembeni) akirudi kwa style ya kuingia kati. System hii huchezwa zaidi timu inapocheza 4-4-2 au 4-4-1-1.

Kwa suala la timu kufanya vibaya naweza kusema inatokana na wachezaji kutokujiami, wachezaji wetu hawajiamini hata kidogo, wamezidiwa na papara kuanzia mabeki mpaka wafungaji isipokuwa kwa wachache sana ambao nathubutu kuwataja kuwa ni Shaaban Nditi, Mbwana Samatta na Shomari Kapombe. Wadau wanapiga kelele Samatta Samatta Samatta nawaunga mkono japo kuwa hawajui undani na ukweli wa Samatta. Uzuri wa Samatta ni utulivu anapokuwa na mpira ambao unamjengea kujiamini, kitu ambacho asilimia kubwa ya wachezaji wanakikosa. Chukulia mfano mechi ya nyumbani tulipocheza na Algeria, goli alilofunga Samatta ni kutokana na utulivu na kujiamini. Tunahitaji wachezaji wa namna hii na ndio maana wadau wanataja Samatta.
Wachezaji wenye utulivu na kujiamini wanaweza kupatika kuanzia soka la yosso (vijana wa umri mdogo), mchezaji anapoanza kucheza soka la ushindani akiwa mdogo anajijenga kujiamini, sio leo mtu ana miaka 27 (ya ukweli 35)ndio anaanza kucheza timu ya Taifa kwa mara ya kwanza, hivi unadhani kutakuwa na kujiamini hapo?
Wakati umefika kwa TFF (kamati ya ufundi/kocha) kuwaamini vijana, hii namaanisha kwa vile hivisasa wapo vijana wengi walioibuliwa kutoka michuano mbali mbali, kama vile Uhai Cup, Coca cola n.k inapotokea mashindano basi tusilenge kwamba lazima tuchukue kombe, badala yake watumiwe vijana ili kuwajengea kujiamini na utulivu, hii itasaidia kwa michuano ya baadae ambapo tutakuwa na timu nzuri na imara yenye kujiamini, wenzetu ndivyo wanavyofanya hivyo, wachezaji kama Henderson,Sturridge, Welbeck, Walcott na wengineo ndivyo wanavyokomazwa. Kama tunakumbuka mchezo wa kirafiki kati ya Stars na Zambia uliochezwa Morogoro na matokeo yalikuwa 1-1, Zambia walichezesha vijana wengi ambao kimsingi walikuwa wanawapa ukomavu, na ndio vijana wale leo walioiletea heshima nchi yao. Lakini kwetu ikitokea hata Stars inacheza mechi ya kirafiki hakuna sura mpya za vijana wanaokomazwa. Hapo ndio tunamkumbuka Marcio Maximo pamoja na lile la kuhamsisha wachezaji na wananchi kuipenda timu yao.

Maasalaam.

Bebeto.

1.     habari kaka shaffih mimi napenda sana soka, imi ni mdada napenda sana sana sana namizwa na viongozi, mackocha na wachezaji wenyewe, tufike mahali tuseme asante kwa maximo, japo halaiki ilimponda sana, nimekuwa nikikata tamaa hata kwenda kuangalia mechi za Taifa starz kwa sababu kubwa kuogopa kuumia kwa kufungwa, naona bora kesho yake niblog kwako nione, hii ni kwasabu hawana au hawatoi mvuto kwa mashabiki,na wapenzi wa soka. jamani vijana wadogo wanaochipukia wapo waitwe waunde timu ya taif nzuri na imara. tujifunze hata kwa hawa tuliocheza nao leo, wamepikwa tangu 2006 leo ije kuwa sisi tunakurupuka tu kutoka huko tutokako na kupasha siku 2 au 3 tu kisha tunawavaa jamii iliyoandaliwa vizuri, si vizuri jamani kocha pamoja na wadau wengine wakae waone huyu ibilisi anayetushikilia sisi kila mara anaitwa nani katokea wapi na wamkemee nasi siku moja tuone timu yetu kwenye nusu au robo fainali ya World cup jamani, kaka natamani sana kuongea mengi maana ninauchungu sana na timu yangu. kwa upande mwingine kama tumeshindwa kumkeamea huyu ibilisi kwa wakaka basi tumzibiti kwa wadada nao asiwaharibu pia, maana hao kidogo nyota inang'aa huenda tukaona neema kupitia wao, KAKA NAUMIZWA SANA NA MATOKEO MABOVU YA TIMU YETU HASA YA TAIFA STARS.

Ndimi mpenzi, mdau na shabiki wa timu zetu za TANZANIA, NAITWA LUCY IZENGO,

MUNGU IBARIKI TANZANIA,
MUNGU IBARIKI TAIFA STAZ NA TWIGA STAZ AMINA.

CHEMSHA BONGO: HUYU NI NANI?

NI MWANASOKA KIJANA ANACHEZA KATIKA TIMU YA LIGI KUU YA ENGLAND.

DAVID LUIZ AMBWATUKIA LAMPARD - AMWAMBIA HANA TOFAUTI NA YOYOTE NDANI YA CHELSEA NA AFUATE ANACHOAMBIWA NA KOCHA.


Luiz amejiingiza katika ugomvi na kipenzi cha Chelsea Lampard.


David Luiz ameingilia ugomvi kati ya Andre  Villas Boas na Frank Lampard baada ya kiungo huyo wa Uingereza inabidi afuate yote anayoambiwa na asifikiri yeye yupo tofauti na mchezaji yoyote ndani klabu hiyo.
Lampard amekuwa hana furaha na idadi ya mechi alizocheza msimu na wiki iliyopita alikiri kwamba hana mahusiano mazuri na AVB.
Mlinzi David Luiz amemtetea Villas-Boas  akisema, “Hakuna anayepaswa kuwa baba au mtoto wa Fulani katika timu ya soka. Hakuna kupendelewa. Lampard anabidi amsikilize kocha anapotokea amri na maelekezo na kufuata anachoambiwa au kuagizwa kufanya.
“Hamna mchezaji anayepaswa kujua kwamba yeye ni mwajiriwa tu klabu.”
Taarifa zimezidi kuzagaa kuhusu hatma ya AVB ambaye wiki kwa mara ya kwanza amekiri anaweza kufukuzwa kazi.
AVB amekalia kuti bovu @Stamford Bridge.



Lakini mbrazil Luiz anasema Mreno huyo amekuwa akionewa, pamoja na Chelsea kuwa nafasi ya tano katika ligi, na wakiwa katika hatari ya kutolewa katika champions league.
“Msimu uliopita, kulikuwa kuna timu ambazo zilikuwa nafasi mbaya katika msimamo lakini hakuna aliyezungumza hilo. Ni rahisi sana kuongea kuhusu AVB, kwa sababu Chelsea ni timu kubwa ambayo siku zote inatafuta nafasi ya kwanza na inapotokea ikiwa ya 3 au ya nne ni inakuwa rahisi kumpa lawama kocha. Lakini Andre ni mtu tofauti ana kila kitu kama kocha, ni mtu sahihi kabisa kwa Chelsea ana ataipa mafanikio makubwa klabu hii.”

MOURINHO ASEMA: "SIRUDI CHELSEA"


Mourinho akiwa na shabiki nje ya mgahawa uliopo jijini London.


Kocha wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho amesema hatorudi  Stamford Bridge msimu ujao.
Zilipotoka picha za mreno huyo akiwa anatafuta nyumba mjini London baadhi ya watu wakachukulia kwamba boss huyo wa Real Madrid alikuwa akitafuta nyumba kwa jili ya kuweza kurudi mjini humo kuchukua nafasi AVB.
Lakini, according to Daily Mirror, Mourinho amemwambia mmiliki wa mgahawa anaoupenda mjini London kwamba harudi Chelsea.
Marrietta Maccioni, motto wa kike wa Alvaro Maccioni, mmiliki wa mgahawa wa La Famiglia, alisema: “ Ilikuwa vizuri sana kumuona tena hapa baada ya muda mrefu sana.
“Alikuja na mkewe, shemeji yake pamoja na mume wa shemeji yake. Walikula chakula cha mchana na kufurahia sana.
“Jose alikuwa akiongea na baba yangu kwa muda mrefu akamwambia anatafuta nyumba katika eneo hilo kwa ajili ya familia yake.
Enzi hizo.



“Watu wengi wakiwemo wafanyakazi wa Chelsea walikuwa wanauliza kama amesema anarudi Stamford Bridge lakini kwa bahati mbaya Jose alisema harudi Chelsea. Tumesikitika sana kwa sababu Mourinho ni kocha mzuri. Hakutuambia kitu kingine chochote kuhusu mipango yake ya baadae.”

Wednesday, February 29, 2012

Tunahitaji kujitoa mhanga....

Kwanza nitumie nafasi hii kuipongeza Taifa Stars kwa kumaliza salama mchezo dhidi Msumbiji na kulazimisha sare ya bao 1:1, Tumepata sare matokeo ambayo hayakuwa ya kuridhisha sana,lakini niwapongeze kwa hilo.
Nilikua miongoni mwa watanzania tuliokuja Uwanja wa Taifa kuangalia mpambano huo lakini tukiwa na mahitaji tofauti. Mimi sikuja kuishangilia timu bali nilikuja kuwaangalia vijana wetu wanaochipukia kama vile Salum Abubakari ‘ Sureboy ’wanafanya nini. Kama nilivyowahi kusema huko nyuma ya kwamba timu yetu ya taifa ilivyo kufuzu kwa mashindano makubwa ni miujiza tu inayohitajika.
Mechi ya jana iliendelea kuchochea zaidi hoja yangu ya kuutumia mwanya huu ambao tunajua fika hatuna uwezo wa kwenda mbele kujenga timu mpya ya taifa.
Naombeni sana tufanye utafiti wa haraka haraka ni watanzania wangapi wenye matumaini ya timu yetu ya taifa kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwakani au Kombe la Dunia mwaka 2014 kule nchini Brazil,naamini huo utafiti utasaidia kuilinda hoja yangu ya kuachana na ndoto za alnacha za stars kufuzu mashindano makubwa pasipokuepo maandalizi ya dhati.
Tuwashukuru sana kina Nizar,Henry na Mrwanda pia tuwashukuru sana wachezaji wazoefu waliopo kwenye kikosi cha Stars cha sasa. 
Tuna takribani mechi 6 za kucheza kwa ajili ya  kufuzu kombe la dunia,miongoni mwa timu tutakazocheza nazo ni Ivory Coast na Morocco.
Atakachojifunza leo hii Nadir Haroub kumkaba Didier Drogba hakitatusaidia hata kidogo huko mbeleni kwasababu asilimia kubwa ya wachezaji wa kikosi cha sasa cha Stars viwango vyao vinaelekea ukingoni.
Lakini tukiwatumia makinda wenye umri chini ya  miaka 24 wakaburuzwa na kina Drogba litakua fundisho kwao hatimae litatusaidia kwa miaka mingine mingi tu ya mbeleni. Kwahiyo mimi nashauri tuwape nafasi vijana wetu wakapambane na kina Drogba na Chamakh ili wapate uzoefu ili waje kutusaidia mbeleni. Hapa matokeo siyo kipaumbele acha wafungwe ili wapate kitu kitakachokuja kuwasaidia huko mbeleni.
Sidhani kama huu ni muda wa  mjadala wa Timu ya taifa inatakiwa iundweje,nadhani huu ni mjadala wa namna gani mpira wa nchi yetu utapatiwa ufumbuzi kwa siku za usoni,kwa maana ya kutengeneza miundo mbinu pamoja na program endelevu za namna ya kuibua na kuviendeleza vipaji vipya maana kwasasa hakuna njia ya kujikomboa hapa tulipo.
Tunahitaji kujitoa mhanga na pa kuanzia ni kuivunjilia mbali hii timu iliyopo ya Taifa na hii itasaidia kutoa  changamoto kubwa kwa kizazi kijacho.
TFF msikubali kuyaburuza mashindano ya Copa CocaCola pasipokuwepo mikakati endelevu,yatumieni kama msingi wa kuibua na kupata vipaji vipya kila mwaka na  rasilimali za Airtel Rising Stars zitumike  ku-maintain vipaji vinavyotokana na Copa Cocacola,ni kweli tunahitaji wafadhili lakini lazima TFF tuwabane hao hao wafadhili waliopo ili program zetu za muda mrefu zilindwe. TFF, mlinufaika sana na vipaji vilivyotokana na mashindano ya UMISETA miaka ya nyuma na hapo hamkuwa na hela. Inakuwaje sasa hivi hampeleki pesa huko kwenye UMISETA wakati  wadhamini mnao? …itaendelea

YANGA WAENDA MISRI BILA BERKO, GUMBO

MSAFARA wa Yanga utaondoka kwenda Cairo Misri tayari kwa mechi yake ya marudiano ya ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Zamalek ya huko utakaopigwa Machi 4.
Hata hivyo katika msafara huo watakosekana nyota wake kadhaa wakiwemo kipa Mghana Yaw Berko na Rashid Gumbo.
Wachezaji watakaoondoka ni pamoja na Shaban Kado, Shadrack Nsajigwa, Athuman Iddy ‘Chuji’, Juma Seif, Nurdin Bakari, Chacha Marwa, Godfrey Taita, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Omega Seme, Davies Mwape, Pius Kisambale, Hamis Nombo, Oscar Joshua, Haruna Niyonzima, Jerry Tegete, Job Ibrahim, Stefano Mwasyika, Kenneth Assamoh na  Shamte Ally.

SIMBA TV KUZINDULIWA RASMI IJUMAA

KLABU ya soka ya Simba inatarajiwa kufanya hafla ya uzinduzi wa Simba Tv ambao unatarajiwa kufanyika Ijumaa katika hoteli ya JB Belmont iliyopo katika jengo la Benjamin Mkapa katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Ofisa habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga amesema kwamba Simba Tv itakuwa ikirushwa katika kituo cha Clouds Tv.
Alisema kupitia uzinduzi huo kutakuwa na burudani mbalimbali sambamba na kuonyeshwa kwa documentary maalum inayohusu klabu hiyo.
"Hafla hii itakuwa ni kwa waalikwa huku wengine watakaopenda kuhudhuria watapaswa kulipa shilingi 70,000.

Jan Poulsen hawezi kukwepa lawama za kutomuita Mbwana Samatta


 Timu ya taifa ya Tanzania kwa mara nyingine imeshindwa kuwapa raha mashabiki waliofurika uwanjani kuushuhudia mchezo baina yake na The Mambas ambao ni timu ya taifa ya Msumbiji.
Kwa mtu ambaye alikuwa anatazama mchezo huu kwa jicho la kawaida anaweza kusema kuwa ameshangazwa na matokeo yake lakini si kwa mtu aliyekaa na kutazama mazingira ya timu hii kuelekea kwenye mchezo huu. Ukirejea nyuma kwenye mchezo dhidi ya timu ya taifa ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo kwa uhalisi kabisa unaweza kupata taswira ya mchezo dhidi ya The Mambas.
 Hakuna asiyejua kuwa soka la Tanzania lina tatizo sugu la uhaba wa wafungaji na ndio maana wafungaji wakuu kwenye vilabu vikubwa vya hapa nchini wote wanatoka nje ya nchi.
Mchezo dhidi ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo ulionyesha uhaba wa wafungaji kama ambavyo imekuwa ikionekana kwa muda mrefu. Ukosefu wa mtu ambaye anabeba jukumu la ufungaji wa mabao muhimu umeendelea kuonekana hata kwenye mchezo wa Msumbiji ambapo nafasi chache zilizotengenezwa hazikuweza kutumiwa kwa ufasaha.


 Kocha Jan Poulsen alichagua kumpanga John Bocco kama mshambuliaji pekee huku akisaidiwa na Vincent Barnabas aliyekuwa akisaidia mashambulizi toka pembeni na Abdi Kassim ambaye alikuwa nyuma kama mshambuliaji wa pil yaani ‘second striker’.

John Bocco ni mchezaji mzuri kwa soka la hapa Tanzania na ndio maana anaongoza kwenye chati ya ufungaji kwa kiwango cha soka la Tanzania. Unapozungumzia ‘calibre’ ya mchezaji wa timu ya taifa John Bocco bado hajafikia kiwango cha kuwa mshambuliaji wa kuiongoza timu ya taifa.
 Rekodi yake katika michezo mbalimbali inamhukumu katika hili.Tanzania inaye mshambuliaji ambaye angeweza kuwa na msaada kwenye mchezo huu lakini hakuitwa kwenye timu.
 Upande wa pili Msumbiji walikuwa na mtu ambaye kwa timu yao ni kama Samatta, Elias Palembe ambaye anacheza Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini. Huyu ndiye aliyefunga bao la Msumbiji.Ukiachilia mbali Palembe timu hii ina wachezaji wengi wenye umri mdogo ambao kimsingi wengi wanaanza safari yao ya soka la kimataifa na aina ya mchezo waliouonyesha ilidhihirisha faida zilizopo kwenye kuwachezesha vijana.Ukiutazama mchezo kuanzia safu ya ulinzi, beki mkongwe Shadrack Nsajigwa alicheza katika kiwango cha kawaida. Mchezo wake uliingia dosari kutokana na balaa alilokumbana nalo toka kwa Elias Palembe aliyekuwa anacheza upande wake. Palembe alimlazimu Nsajigwa kucheza kwa asilimia kubwa sana upande wake wa uwanja na si kupandisha mashambulizi kama ilivyo kawaida yake.
Beki wa pembeni kwa upande wa kushoto alikuwa Stephano Mwasika . Masika alicheza vizuri kwa walau asilimia 45%. Alikuwa akisaidia vizuri sana kuipandisha timu mbele. Tatizo kubwa kwa upande wake lilikuwa jinsi ya kujipanga wakati timu ikiwa inashambuliwa . Mwasika alikuwa anajisahau sana wakati wapinzani walipokuwa na mpira mpaka kufikia hatua ya mabeki wa kati kutoka kwenye maeneo yao kwenda kuziba pengo linaloachwa wakati alipokuwa akipanda.
Wachezaji wa Msumbiji walimsoma vyema na walikuwa wakinasa mipira na kukimbilia upande wake kwa haraka kwani walikuwa wanajua kwa kufanya hivyo wanawavuta mabeki wa kati ambao walikuwa wanaacha maeneo yao wazi.Mabeki wa kati ambao walikuwa Juma Nyoso na Aggrey Morris walicheza vyema pia kwa kiasi chao japo ukosefu wa umakini na uwezo mdogo wa kuusoma mchezo na kufanya maamuzi kabla ya mshambuliaji wa timu pinzani yaani “danger anticipation” ilikuwa tatizo.

Juma Nyosso almanusra awape wapinzani bao wakati wa lala salama baada ya pasi yake fupi kunaswa na washambuliaji wa Msumbiji na kama isingekuwa umahiri wa Kaseja hali ingekuwa tofauti.Eneo la kiungo kuanzia kwa Shaban Nditi kwa kawaida huwa hakuna matatizo mengi kutokana na wachezaji walioko kwenye eneo husika kuwa wanatimiza majukumu yao vyema pengine kuliko maeneo mengine ya uwanja .
Shaban Nditi mara nyingi hujitolea kwa asilima zote akifanya kazi kubwa ya kuzima moto pale unapotaka kuwaka . Kitu kinachomtatiza ni kitu ambacho kinawatatiza wachezaji wote wanaocheza Tanzania nalo ni kudumazwa na mazingira ya soka la hapa nyumbani. Wanakosa ujanja wa ziada na pia hawana vitu vingi vya msingi ambavyo mchezaji anapaswa kuwa navyo .Kiungo mwingine aliyecheza katikati ya uwanja alikuwa Mwinyi Kazimoto. Alicheza kawaida lakini alama nyingi alizipata kutokana na juhudi zake binafsi na goli alilofunga . Ubora wa Kazimoto haukuonekana kwa sababu ya kukosekana kwa partnership kwenye timu hasa kwenye eneo la kiungo ambako kila mmoja anaonekana anacheza kivyake na hakuna rhythm yaani ule muunganiko wa kitimu ambao unapaswa kuwepo kwenye timu yoyote na ndio maana wachezaji wenye uwezo kama wa Mwinyi Kazimoto mara nyingi uwezo wao hauonekani. Viungo waliokuwa wanacheza kama ‘Maforward wa ziada toka pembeni walikuwa Vincent Barnabas alicheza upande wa kushoto na Nizar Khalfan aliyecheza upande wa kulia . Jinsi ambavyo Stars walikuwa na umiliki mdogo wa mpira uliwafanya viungo hawa washambuliaji toka pembeni waonekane kukosa umuhimu hali iliyomfanya kocha kumtoa Nizar na kumuingiza Mrisho Ngassa na baadaye alimtoa Vincent na kumuingiza Husein Javu , baadaye pia ilifanyika ‘sub’ ya Abdi Kassim ambaye nafasi yake ilichukuliwa na Salum Abubakar. Salum Abubakar na Ngasa walileta uhai kidogo lakini ukosefu wa umakini wa mshambuliaji John Bocco ulimfanya apoteze nafasi nyingi sana za wazi ambazo ingekuwa mtu mwingine angeweza kuleta uhai.Mwisho wa siku haikuwa ‘perfomance nzuri kutokana na matokeo ya mwisho ambayo yanaiweka Stars pabaya . Kocha Jan Poulsen hawezi kukwepa lawama za kutomuita Mbwana Samatta ambaye wengi wanajua uwezo wake na alistahili kuitwa kwa kuwa anafanya vizuri akiwa na timu yake Tp Mazembe.

Picha kwa hisani ya Fullshangwe.blogspot.com

STARS VS MSUMBIJI: TANZANIA KUANZA VIZURI SAFARI YA SOUTH AFRICA MWAKANI.

Timu ya soka ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ leo inaanza kampeni zake za kuwania kufuzu fainali za Afrika mwakani itakapocheza na Msumbiji ‘Mambas’ Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mechi hiyo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa ajili ya kufuzu fainali za Kombe la Shirikisho hilo kwa Mataifa ya Afrika (Afcon) ambazo zitafanyika mwakani nchini Afrika

Kusini.

Taifa Stars haijafuzu fainali hizo tangu ilipocheza kwa mara ya kwanza mwaka 1980, wakati fainali hizo zilipofanyika Lagos, Nigeria, wakati huo fainali hizo zikishirikisha timu nane tu

tofauti na 16 za sasa.

Mchezo wa leo Stars inakutana na Msumbiji ambayo katika mechi ya mwisho ya mashindano zilipocheza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwaka 2007 Stars ililala bao 1-0 lililofungwa na Tico Tico.


Lakini pia Msumbiji iliifunga Stars mabao 2-0 mwaka jana katika mechi ya kirafiki ya kimataifa ya kufungua Uwanja mpya wa Zimpeto.


Taifa Stars inaingia uwanjani ikiwa imepata mechi moja ya kujipima nguvu dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) iliyofanyika Alhamisi iliyopita na timu hizo kutofungana.


Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen alisema jana kuwa vijana wake wamejiandaa vizuri, hivyo kuwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuwaunga mkono.


“Naifahamu Msumbiji ni timu nzuri, tunajipanga iwezekanavyo kuhakikisha tunawapa raha Watanzania, nakumbuka mechi ya mwisho tulifungwa mabao 2-0, lakini tumejiandaa

kuwakabili.

“Naomba Watanzania tuuchukulie umuhimu mchezo huu, waje watushangilie,” alisema Poulsen.


Naye Kocha Mkuu wa Mambas, Gert Engels, alisema wanauchukulia uzito mkubwa mchezo huo na kwamba ushindi wa leo utakuwa wa umuhimu mkubwa kwao.


Taifa Stars leo itawategemea zaidi washambuliaji wake Abdi Kassim, John Bocco na Mrisho Ngasa, huku safu ya kiungo ikiwa na Nizar Khalfan na Shaaban Nditi, wakati kwenye

ulinzi ni Aggey Morris na Juma Nyosso ambao wanatakiwa kuhakikisha kipa Juma Kaseja hapati madhara.

Karibu wiki moja iliyopita kulifanyika mchezo wa fainali ya Afcon kati ya Zambia na Ivory Coast iliyofanyika nchini Gabon, ambapo nchi hiyo na Equatorial Guinea ziliandaa fainali za mwaka huu kwa ubia. Zambia iliibuka bingwa wa mashindano hayo.


Fainali hizo zinafuatana kutokana na uamuzi uliofanywa na Caf, ambapo lengo lake la kuandaa fainali nyingine za Afcon mwakani ni kutaka zipishane na zile za Kombe la Dunia inazoandaliwa

na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa), ambazo hufanyika kila baada ya miaka minne.

Baada ya Afcon ya mwakani itafanyika tena mwaka 2015.

MAZUNGUMZO YA MKATABA MPYA NA CHELSEA YAKWAMA - DROGBA ATAKA PAUNDI MILLIONI 6 KWA MWAKA - ANZHI WAPO TAYARI KULIPA HATA 8 KUMSAINI.

Chelsea striker Didier Drogba  maeanza mbio za kutaka kusaini mkataba mpya huku akivuta mshahara wa paundi million 6 kwa mwaka.
Mazungumzo juu ya deal mpya at Stamford Bridge yamesimama na Drogba sasa ameanza kuangalia sehemu nyingine.
Ivory coast captain amebakiza miezi mitano ya mkataba wake, hivyo anaweza kuanza kufanya mazungumzo na klabu kutoka nje ya England kwa ajili ya kuhamia mkataba wake utakapoishia.
Upatikanaji wa Drogba umezusha vita ya kumgombea kupata saini yake.
Huku washauri wake wa masuala ya kifedha wakimsisitiza kukubali kujiunga na timu ambayo itatoa ofa ya paundi million 6 kwa mwaka baada ya kodi.
Lakini pamoja na kwamba fedha hiyo ni kubwa lakini kumekuwa na timu nyingi zinazohitaji saini yake.
Drigba tayari amekataa ofay a paundi million 4 kutoka klabu ya Qatar Al Saad.
Drogba pia yupo katika listi ya Anzhi Makhachkala inayofundishwa na Guus Hiddink, na chanzo kutoka ndani ya klabu hiyo kinasema warusi hao wapo tayari kulipa kati ya paundi million 8 au 10ili kuweza kumsaini Didier.
Pia kuna ofa kutoka Marekani kwa Chicago Fire. Wakala wa Drogba Thierno Seydi alisema “Atajiunga na timu itakayompa fedha nyingi”