Search This Blog

Saturday, March 3, 2012

UZINDUZI WA SIMBA TV WAFANA !


Mgeni rasmi,Naibu Waziri wa Nchi,Ofis ya Waziri Mkuu,tawala za Mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI),Kassim Majaliwa,akibofya kitupe kuzindua rasmi kipindi cha Simba TV kitakachokuwa kinarushwa na kituo cha cha runinga cha Clouds,hafla hiyo imefanyika kwenye jengo la Quality Center  kwenye ukumbi wa Cleopatra,jijini Dar,Kulia ni Mwenyekiti Msaidizi Simba,Geofrey Nyange 'Kaburu'Mh  Alhaj  Kapuya na shoto ni Mwenyekiti wa Simba Sc Alhaj Ismail Aden Rage,na Afisa habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga




Makofi tafadhali..!Mgeni rasmi,Naibu Waziri wa Nchi,Ofis ya Waziri Mkuu,tawala za Mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI),Kassim Majaliwa,akipiga makofi mara baada ya kuzindua kipindi cha Simba TV kitakachokuwa kinarushwa na kituo cha cha runinga cha Clouds,hafla hiyo imefanyika kwenye jengo la Quality Center kwenye ukumbi wa Cleopatra,jijini Dar,Kulia ni Mwenyekiti Msaidizi Simba,Geofrey Nyange 'Kaburu'Mh  Alhaj  Kapuya na shoto ni Mwenyekiti wa Simba Sc Alhaj Ismail Aden Rage,na Afisa habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga kwa pamoja urwakipiga makofi kufurahia uzinduzi huo uliofana kwa kiasi kikubwa.




Swed Nkwabi,Said Tully na Charles Amka wakifungua Champagne!


 Keki yenyewe ilivyokuwa imenoga.


kutoka kushoto ni Alex Luambano,Salum Mwalim,Ibrahim Masoud, Msafiri Mgoyi, Salum Abdallah na Mdau



Kocha wa Simba Sc, Milovan Cirkovic akicheers na meza kuu


Mgeni rasmi,Naibu Waziri wa Nchi,Ofis ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI),Kassim Majaliwa akikata keki huku sehemu ya meza kuu ikishuhudia tukio hilo adhimu na ka kihistoria









Mgeni rasmi Kassim Majaliwa akimlisha keki Mwenyekiti wa Simba Sc,Alhaji Aden Rage huku wageni waalikwa meza kuu wakishuhudia tukio hilo.



Mdau Nick Malayu a.ka. Nick Boy akifurahia kujinyakulia jezi ya mchezaji mahiri wa Simba SC.Haruna Moshi a.k.a Boban.






Baadhi ya Waandishi wa habari walioshuhudia uzinduzi huo uliofana kwa kiasi kikubwa.


Baadhi ya wageni waalikwa wakiwemo wachezaji wa Simba ndani ya hafla hiyo






Wadau wakifuatilia jambo ukumbini wakati hafla ikiendelea





Vijana kutoka THT,akiwemo Barnaba,Amin na wengineo walinosha  vilivyo uzinduzi huo.


Mzee wa Fullshangwe,ambaye pia ni mshabiki mkubwa wa Simba Sc.John Bukuku aliibuka na jezi yake kama uonavyo pichani.


Mshambuliaji Felix Sunzu akimkabidhi kwa heshima jezi yake mgeni rasmi,Mh Kassim Majaliwa


Mchezaji Nyota wa zamani wa Simba SC,Zamoyoni Mogella a.k.a Gholden Boy akizungumza machache kwenye hafla hiyo usiku wa kuamkia leo.

1 comment:

  1. Hello Saffih.
    Shukrani kwa picha ilikuwa na shauku ya kuona kama watu wangejitokeza kwa wingi ila kwa picha zako kweli nimekubali ni mwanzo mzuri.
    Ila hapo ndipo utajiuliza kwanini hivi vilabu visitumia rasilimali hii kujenga viwanja vyao na vitega uchumi, hawa wadau ni rasilimali kubwa sana kwa klabu hizi za simba na yanga, simba ama yanga wanashindwa nini kuingia mikataba na mabenki, taasisi kama NSSF,PPF na nyingine nyingi kama mabenki wakajengewa viwanja then jamaa wakawa wanatumia viwanja hivyo kujitangaza kama sehemu ya malipo na nyingine wakawa wanapata kutokana na mapato ya vitega uchumi hivyo kurudisha fedha zao.
    Mimi bado sielewi huwa tatizo ni nini ama ni kwa kuwa niko nje ya system labda sielewi mambo yanavyokwenda, kwenye hivi vilabu kuna watu wa mpira sasa ila mbona sioni wakitatua matatizo haya, hakuna mtu kweli wa kujitoa muhanga kubadilisha hali katika klabu hizi ukiwa kiongozi wa simba ama yanga huitaji kutumia fedha zako kujenga uwanja hata siku moja wewe tangaza na weka mikakati uone wawekezaji wako tayari, mashabiki wenyewe wako tayari kuchanga.Mimi nakuambia shaffih Tanzania hii watu wanauzalendo na timu zao unakumbuka enzi za serengeti boys watu walileta mpaka maharage tena watu wa chini kabisa ni kwa kuwa wanatamani kuona timu inakwenda mbele.
    Mimi mpaka leo huwa sipati jibu ni kwanini Simba kwa mfano hawana udhamini wa Simba cement, na Twiga timu ya wanawake kwanini hawana udhamini wa Twiga Cement hiyo ni badhi tu mifano, hapa ujerumani shaffih mpaka supermarkt zinadhamini vilabu, yaani unakuta vilabu vina wadhamini chungu nzima.Fika uwanja wa Hamburg kwa mfano ingia katika duka lao unaweza ukalia machozi ni kwanini timu zetu hazifanyi mambo hayo, siku ambazo hakuna mechi watu wanalipa kwenda kuutembelea uwanja ni sehemu ya utalii tayari na klabu inaingiza mapato kwani vilabu vilabu vyetu havina Vision wala Mission, kwa kweli inasikitisha sana. Ni aibu kwa wachezaji wa timu kubwa kama simba na yanga kustaafu kisha wakaenda kuwa madereva daladala huko ni kuwadhalilisha si kwa sababu udereva daladala ni mbaya hapana ila ni kwa sababu mpira ungetosha kuwafanya wakawa na maisha bora sana mara baada ya kustaafu ila mchezaji anastaafu ukikutana nae unaweza kulia machozi. Angalia hali ya klabu ndogo kiumri kama ya Azam mbona wameweza leo hii wanapokea malipo ya uwanja wao kutumika na timu za simba na yanga na nyingine ambazo hazina viwanja vyao its disgusting hasa kwa simba na yanga ambazo zina miaka 70.
    Saffih wewe uko karibu na Maestro pamoja na Mayai hawa ni viongozi vijana katika hivi vilabu hivi wanaleta changamoto kweli za kimaendeleo katika hivyo vilabu ama nao wameingia wakamezwa na mawazo ya wazee ya kutaka kukumbatia klabu kama mali zao na kuziweka mifukoni, natamani kukutana na hawa mabwana niwasikilize nijue kama ni watu wa maendeleo ama nao wanatafuta kula tu.
    Mwisho kabisa Shaffih nifikishie salamu zangu kwa Alex Lwambano huwa namsikia tu akitangaza leo ndio nimepata fursa ya kuiona sura yake.

    Kila la kheri Yanga leo huko Misri pambaneni hakuna lisilowezekana mkicheza kwa kujituma na umakini hakuna atakaye chukua mpira na mkono na kwenda kuuweka golini na kusema ni goli mkiamua mnaweza, macho ya wadau wote yako Cairo leo na dhana ya kwamba mtaonewa uwanjani hiyo iondoeni chezeni mpira, naamini kama mmeiandaa timu vizuri basi matokeo ya uwanjani yatasema na sio maneno nje ya uwanja, nakumbuka simba wakati wanakwenda Cairo mwaka 2003 walipitia nchi moja hivi ya uarabuni kama sikosei walicheza mchezo mmoja wa kirafiki kisha wakaenda Cairo na wachezaji walikuwa wanaonekana kabisa jamaa hawa ni wapiganaji ile spirit ya timu hata wewe shabiki ulikuwa unai feel, kuna mdau pia kipindi kile nafikiri alitokea akawanunulia Simba viatu vya kucheza mpira kwenye utelezi kwani Cairo palinyesha siku hiyo kabla ya mechi hivyo kuna mdau akawatonya simba wakiwa huko uarabuni kwamba waandae viatu hivyo.
    Mike.
    Germany.

    ReplyDelete