Fainali ya mashindano ya Uhai Cup imemalizika dakika chache zilizopita na Simba sports club under 20 imefanikiwa kuchukua kombe hilo baada ya kuwafunga Azam FC kwa penati.
Search This Blog
Saturday, November 26, 2011
BREAKING NEWS: SIMBA BINGWA UHAI CUP, YAITANDIKA AZAM.
KALI YA LEO: BORUSSIA YAONGOZA LIGI YA BUNDERSILIGA BAADA YA MIAK 26
Timu ya Borussia Moenchenglabach imeamaliza ukame wa maiak 26 baada ya ushindi wa jana kwenye ligi kuu ya Ujerumani dhidi ya FC Colegne wa mabao 3-0, ushindi ambao umeawafanya waongeze ligi .
Klabu hiyo haijawahi kuongoza ligi hiyo tokea miaka 26 iliyopita.
EXCLUSIVE: KOCHA MPYA WA SIMBA KUWASILI LEO BONGO
Baada ya aliyekuwa kocha wa timu ya Simba Moses Basena kutemeshwa kibarua chake kwa kukosa kibali cha kufanya kazi nchini, klabu hiyo inatarajiwa kupata kocha leo. Boss mpya wa benchi la ufundi la Simba, Mserbia Milovan Cirkovic, anatarajiwa kuwasili nchini leo, kabla ya kesho kusaini mkataba wa kuinoa timu hiyo kwenye Ligi Kuu na michuano ya kimataifa.
Hii ni mara ya pili kwa Milovan kuja kuinoa timu hiyo ambapo awali aliifundisha mwaka juzi kabla ya kuiacha na nafasi yake kushikwa na Mzambia, Patrick Phiri.
Makamu Mwenyekiti wa Simba, Goefrey Nyange ‘Kaburu’, alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa, Milovan ambaye anambadili Mganda Moses Basena, anawasili leo usiku na pindi atakaposaini mkataba huo, atabaki kuendelea na shughuli nyingine.
Alisema walishafanya mazungumzo na kocha huyo na hivyo ujio wake unatokana na makubaliano waliyoafikiana baina yao.
MIZENGO PINDA KUTINGA TAIFA LEO KUWAPA SAPOTI KILI STARS.
Kiranja Mkuu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda, leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa michuano ya CECAFA Chalenji 2011 ambapo wenyeji Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ wataumana na Rwanda ‘Amavubi’ kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema, Pinda angezindua michuano hiyo iliyoanza jana kwenye uwanja huo.
Kilimanjaro Stars inayonolewa na Charles Boniface Mkwasa na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, ambao ndio mabingwa watetezi, itashuka katika dimba hilo kukuvaana na Rwanda majira ya saa 10:00 jioni.
Michuano hiyo ilianza jana ambapo Burundi iliitandika Somalia mabao 4-1, katika mchezo wa kwanza, huku Uganda ikifunga Zanzibar mabao 2-1 katika mchezo wa pili.
Katika hatua nyingine, TFF imetangaza viingilio katika hatua ya makundi ya michuano hiyo ambapo kwa mashabiki watakaokaa viti vya rangi ya bluu na kijani ambavyo ni zaidi ya 30,000 kiingilio kitakuwa sh 1,000, wakati viti vya rangi ya chungwa zaidi ya 10,000 kiingilio kitakuwa sh 3,000.
Wambura alisema kwa watakaokaa VIP C na B ambayo jumla ya viti vyake ni 8,000 kiingilio kitakuwa sh 5,000 wakati VIP A yenye viti 700 kiingilio ni sh 10,000.
CECAFA TUSKER CHALLENGE CUP: ZANZIBAR YAANZA KWA KIPIGO
Mchezaji wa Zanzibar Heroers Ali Badru akichuana na mchezaji wa Uganda Cranes Andrew Mwesigwa wakati timu hizo zikichuana katika mchezo wa kombe la TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP
Waziri Mkuu wa Kenya Bw. Raila Odinga katikati akifurahia jambo kwa pamoja na Rais wa Shirikisho la vyama vya Michezo Afrika Mashariki Leodger Tenga kushoto pamoja na Balozi wa Kenya nchini Tanzania Mutinda Mutiso wakati walipkuwa wakishuhudia pambano la pili katika mashindano ya kombe la TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP 2011 linalofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Tayari mpira umekwisha ambapo Uganda Cranes imeifunga Zanzibar Heroers magoli 2-1 goli la kwanza la Uganda Cranes limefungwa na Mchezaji Danny Wagaruka katika kipindi cha kwanza, huku Mike Serumaga akifunga goli la pili katika kipindi cha pili, goli la kufutia machozi kwa upande wa Zanzibar Heroers limefungwa na mchezaji Ali Badru katika kipindi cha pili.
Wadau kutoka Serengeti Breweries nao walikuwepo kwani wao ndiyo wawezeshaji au wadhamini wa mashindano haya mtari wa juu kutoka kulia ni Moses Keba, Mr. Ssebo, mstari wa chini kutoka kulia ni Ritah Mchaki na Maurice Njowoka
Kocha Micho ambaye amewahi kuifundisha Yanga sasa ni kocha mkuu wa kikosi cha timu ya taifa ya Rwanda- nae alikuwepo uwanjani kuangalia mchezo
Friday, November 25, 2011
BECKHAM MBIONI KUJIUNGA NA PSG KWA £12M
David Beckham yupo katika mazungumzo ya mwisho ya kusaini mkataba wa kujiunga na Paris Saint-Germain baada ya kupewa ofa ya mkataba wa miezi 18 wenye thamani ya £12m.
Beckham amekuwa kipenzi cha raisi wa PSG Nasser al-Khelaifi anayemuona Becks kama mtu sahihi wa kuipa mageuzi klabu hiyo kuwa moja ya timu kubwa barani ulaya.
Jana Al-Khelaifi alikiri kwamba uamuzi wa timu gani ya kujiunga nayo ulikuwa kati ya Tottenham na PSG, lakini inaeleweka kuwa muingereza huyo anapendelea zaidi kujiunga na wafaransa hao.
Fedha sio tatizo kwa PSG na wana imani kubwa watafanikiwa kumshawishi Beckham kusaini mkataba wa kuitumikia klabu yao in January. Spurs hawawezi kupambana na matajiri wa kiarabu wanaoimiliki klabu hiyo, ukiachana na mshahara pia hana uhakika kama atapata nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha Harry Redknapp.
PSG wametoa ofa hiyo nzuri katika mazungumzo yao yanayoendela kati yao na wawikilishi wa Becks na wanaamini watashinda mbio za kumsajili kiungo huyo.
RIHANNA ALIPOKUTANA USO KWA USO NA JERMAIN DEFOE
UNAJUA KILICHOTOKEA ?
KABLA YA TAMASHA KUANZA RIHANNA ALIAMBIWA MIONGONI MWA WATU MAARUFU WATAKAOHUDHURIA ONYESHO LAKE NI WACHEZAJI WA ARSENAL,
BAADA YA TAMASHA ALIENDA KWENYE ENEO LA WATU MAARUFU NDI O AKAMUONA DEFOE AKAMFUATA AKAMWAMBIA NAKUJUA WEWE SI JERMAIN DEFOE UNACHEZEA ARSENAL... DEFOE AKAMWAMBIA HAPANA MI NACHEZEA TOTENHAM WALA SI ARSENAL,BAADA YA HAPO RIHANNA AKAZUGA ETI NAJUA UNACHEZEA TOTENHAM LAKINI UNAONEKANA UTAPENDEZA ZAIDI UKIVAA JEZI NYEKUNDU YA ARSENAL...
HIVI NDO VIGEZO VINAVYOTUMIKA KAMA TIMU ZINALINGANA POINTS KWENYE UEFA CHAMPIONS LEAGUE
1) The results of games between the teams in the tie (if tied, by goal difference and then by away goals counting double).
2) Goal difference in all group games.
3) Highest number of goals scored in all games.
4) Highest Uefa ranking over the previous five seasons.
Watanzania wawili kucheza ligi daraja la pili Sweden
Watanzania wawili kucheza ligi daraja la pili Sweden Wachezaji wawili wa kitanzania, Joseph Kaniki (Golota) na William John wamefanikiwa kujiunga na timu ya ligi daraja la pili KonyaSpor (KIF) nchini Sweden, baada ya kufanikiwa kupita katika majaribio( Trials). Majaribio hayo yalijumuisha wachezaji zaidi ya thelathini ambapo wachezaji watano walichaguliwa kujiunga na klabu hiyo ya ligi daraja la pili KonyaSpor (KIF)
EXCLUSIVE: DANNY MRWANDA AULA VIETNAM- AONGEZEWA MKATABA MWINGINE/
Mrwanda ambaye msimu uliopita alikuwa anaichezea klabu ya Dong Tam Long An iliyoshiriki ligi kuu ya Vetnam msimu uliopita amesaini mkataba wa mwaka mmoja lengo likiwa ni kuhakikisha timu hiyo inarudi tena ligi kuu msimu ujao.
baada ya kuonyesha kiwango kizuri mchezaji huyo wa zamani wa Simba ya Tanzania amefanikiwa kuongezewa mkataba mwingine wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo.
FAINALI YA UHAI CUP KATI YA SIMBA NA AZAM SASA KUCHEZWA JUMAMOSI ASUBUHI
Taarifa zilizotufikia hivi zinasema kuwa, baada ya wadau kupiga kelele juu ya umuhimu wa mchezo wa fainali michuano Uhai Cup kati ya Simba na Azam kuchezwa siku jumamosi na sio kesho jioni kama ilivyopangwa awali ili kuwapa nafasi mashabiki kwenda kuhudhuria mchezo wa timu ya Zanzibar dhidi ya Uganda, shirikisho la soka nchini TFF limeamua kwa uamuzi mmoja kuwa mchezo huo sasa utachezwa siku ya jumamosi asubuhi katika uwanja wa Karume-DSM.
Hongereni TFF kwa hili.
EXCLUSIVE: BASENA KUTOENDELEA KUIFUNDISHA SIMBA MSIMU HUU
Taarifa za kuaminika 100% ambazo blog hii imezipata ni kwamba kocha Moses Basena hatoendelea kuifundisha klabu ya Simba katika duru la pili la mzunguko wa ligi kuu ya Tanzania bara.
Chanzo cha Basena kushindwa kuendelea na kazi katika klabu ya Simba ni kutokana na kukosa kibali cha kuendela kufanya kazi permanently nchini hali iliyopeleka klabu hiyo kushindwa kuendelea nae kama kocha mkuu wa ndani ya timu hiyo.
Simba kwa sasa wapo katika mchakato wa kutafuta kocha atakayeziba pengo la Basena na kuiwezesha klabu hiyo kufanya vizuri katika mzunguko wa pili wa ligi kuu na hatimaye kutwaa uchampion wa Tanzania bara.
Thursday, November 24, 2011
NIZAR KHALFAN AJIUNGA NA PHILADELPHIA UNION.
Nizar Khalfan ambaye ni mzaliwa wa mkoa wa Mtwara, ameichezea Whitecaps katika michezo 22 ya ligi ya MLS kwa mwaka 2011 ambapo alianza michezo 9. Katika dakika 1,066, kiungo huyu mwenye umri wa miaka 23 alifunga bao moja huku akitoa pasi 4 za mabao kwa wenzake .
Nizar alijiunga na Whitecaps katikati ya msimu wa mwaka 2009 wakati klabi hiyo bado ikiwa kwenye ligi daraja la kwanza na kwa jumla amecheza michezo 58 ambayo ni sawa na dakika 3,029 .
Khalfan alianza soka lake nchini Tanzania akiwa na klabu ya Mtibwa Sugar kwenye msimu wa mwaka 2005/06 na katika msimu wa mwaka 2006-7 aliichezea Moro United.
Katika misimu hiyo miwili Nizar alicheza michezo 57 akifunga mabao 16 akiwa na Mtibwa na mabao matano katika katika michezo 16 akiwa na Moro United. Katikati ya misimu hiyo miwili Nizar alicheza soka la kulipwa nchini Kuwait
Khalfan ameichezea timu ya taifa ya tanzania Taifa Stars katika michezo 25 ya kimataifa na amefunga mabao matano,
Khalfan alifunga bao la ushindi katika mchezo wa kihistoria dhidi ya Burkina Faso kwenye uwanja wa taifa wa Dar es salaam tarehe 2 septemba 2006 kwenye uwanja wa taifa Dar es salam, na pia alifunga bao la nne kwenye ushindi wa 4-1 dhidi ya Mauritius septemba 6 mwaka 2008.
Hivi karibuni Khalfan aliichezea timu yake ya taifa katika mchezo wa kufuzu kwa mataifa ya afrika ambapo alitoa pasi ya bao lililofungwa na Mbwana Samatta kwenye mchezo dhidi ya Algeria ulioisha kwa sare ya 1-1, na pia alianza kwenye michezo yote miwili ya awali ya kufuzu kwa kombe la dunia 2014 ambako timu yake ilifuzu kuingia kwenye kundi lenye timu za Ivory Coast, Morocco na Gambia.
ASANTE KUWASILI NCHINI SIKU YA UHURU - KUCHEZA NA KOMBAINI YA SIMBA NA YANGA DES.11
MKWASA NA JULIO WATANGAZA WACHEZAJI 20 WALIOPITA KATIKA CHUJIO LA KILI STARS
BREAKING NEWS: TENGA ACHAGULIWA TENA KUWA RAISI WA CECAFA
VALENCIA YAIPIGA GENK 7-0 NA KUWEKA REKODI ULAYA
BIGGEST CL WINS | THE TOP 10 |
Wednesday, November 23, 2011
ETI JAMANI HII KWELI NI OFFSIDE?
KWENYE MCHEZO WA MWISHONI MWA JUMA KATI YA AS ROMA NA LECCE MWAMUZI WA PEMBENI ALILIKATAA BAO HULI ETI MFUNGAJI ALIKUA AMEOTEA....
HIVI KAMA WEWE NDO MWAMUZI AFU LINAFUNGWA BAO ZURI KAMA LILE HATA USIPONYOOSHA KIBENDERA UTALAUMIWA KWELI?
COUNTDOWN TO CECAFA CHALLENGE CUP: TIMU ZAANZA KUWASILI-FAHAMU WATAKAPOFIKIA NA WATAKAPOFANYA MAZOEZI
HATMA YA TENGA CECAFA KUJULIKANA KESHO
BOBAN NA MKWASA WAKAMILISHA KAMBI YA KILI STARS
Kambi ya timu ya soka ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’, imekamilika baada ya
mchezaji Haruna Moshi ‘Boban’ na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Charles Boniface Mkwasa nao kuripoti kambini.
Boban alishindwa kuripoti kambini mapema kutokana na matatizo ya kifamilia, lakini juzi Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ alitishia kumtema kama asingejiunga
hadi kufikia jioni juzi, wakati Mkwasa alikuwa Afrika Kusini kuendesha mafunzo ya ukocha.
Akizungumza kwenye mazoezi ya timu hiyo jana, Julio alisema Boban aliripoti kambini juzi jioni. “Wakati nazungumza na waandishi mapema juzi alikuwa hajaripoti, lakini jioni tulipomaliza mazoezi tuliporudi hotelini tukamkuta tayari amefika,” alisema Kihwelo.
Kihwelo alisema ana furaha sasa idadi ya wachezaji 28 aliyowateua kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Chalenji, sasa imekamilika na kikosi chake kiko kamili kwa ajili ya mashindano hayo.
Kihwelo alisema ataandaa ripoti ya timu hiyo na kumpa Mkwasa ambaye alirejea juzi kutoka nchini Afrika Kusini alipokwenda kama mkufunzi wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ili
kuijadili na kupata majina ya wachezaji 22 wanaotakiwa kwa michuano ya Chalenji ambao atawatangaza leo.
Alisema nidhamu, kujituma mazoezini na uwezo binafsi ndio vitu vya msingi atakavyoangalia kabla hawajateua majina hayo ya mwisho kwa ajili ya mashindano hayo.
Katika mashindano ya mwaka huu, Kilimanjaro Stars ambayo iko Kundi A na nchi za Nambia, Djibout na Rwanda, itaanza kampeni za kutetea kombe lake kwa kupambana na Rwanda ‘Amavubi’ Jumamosi hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Tuesday, November 22, 2011
PHIL JONES AANZA MATANUZI, ANUNUA GARI LA MIL.377
Beki wa Manchester United na England Phil Jones amesherekea mwanzo wake mzuri wa msimu kwa kuamua kutumia zaidi ya £130,000 ambayo ni sawa Mil.377 za kibongo kununua gari aina ya Aston Martin.
Mchezaji huyo wa zamani wa Blackburn, 19. Amejihakikishia namba katika kikosi cha kwanza cha United baada ya uhamisho wake wa £16.5million in the summer.
Na sasa ni wazi Jones ameanza kuzoea maisha ya hali juu, baada ya kuvuta mkoko wa bei mbaya.