Search This Blog

Saturday, September 29, 2012

LIVE MATCH CENTRE: SIMBA 2 - 1 TANZANIA PRISONS - FULL TIME

Amir Mafta anakula kadi nyekundu hapa kwa maana hiyo ataukosa mchezo dhidi ya Yanga.

DK 75: Simba bado wanaongoza katika kipindi hiki cha pili.

DK 68: Simba 2 - 1 Tanzania Prisons

DK 55: Mrisho anaingia kwenye box na kupiga shuti kali linalompita kipa wa Prisons na kutinga nyavuni na kuandikia Simba bao la pili.

Kipindi cha pili kimeanza kwa kasi sana, Mrisho Ngassa anaingia vizuri kwenye winga ya kulia, anapiga krosi safi na Sunzu anakosa bao la wazi.

Mpira ni mapumziko - Simba 1 - 1 Prisons 

DK 45+1: Mrisho Ngassa anawapiga vyenga mabeki wa Prisons na kuachia shuti kali linalotoka nje kwa sentimita chache.

DK 45: Felix Sunzu anaipatia Simba bao la kusawazisha.

DK 35: Edward Christopher anaingia vizuri kwenye lango la Prisons, lakini anaingiliana na Sunzu na mabeki wa Prisons wanaokoa mpira langoni mwao.

DK 30: Simba wanalishambulia sana lango la Prisons wakitafuta bao la kusawazisha.

DK 20: Simba 0 - 1 Tanzania Prisons
SIMBA vs TANZANIA PRISONS LINE UPS
Timu za Simba na Tanzania Prisons zinapambana jioni hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11 kamili jioni. Tayari makocha wa timu zote mbili Jumanne Charles (Tanzania Prisons) na Circo Milovan (Simba) wameshataja vikosi vyao.
Simba:                                                  Tanzania Prisons:
01.Juma Kaseja (c)                            18.David Abdallah
02.Nassoro Masoud                             03.Aziz Sibo
17.Amir Maftah                                  05.Laurian Mpalile
15.Shomari Kapombe                          16.Lugano Mwangama (c)
24.Juma Nyoso                                   15.David Mwantika
14.Mwinyi Kazimoto                            13.Khalid Fupi
28.Amri Kiemba                                  07.Misango Magai
08.Ramadhan Chombo                         12.Fred Chudu
19.Edward Christopher                        14.Elias Maguri
10.Felix Sunzu                                     17.Peter Michael
16.Mrisho Ngasa                                   19.John Matei
Wachezaji wa akiba;
22.Wilbert Mweta                                 01.Daudi Mwasongwe
23.Paul Ngalema                                   04.Jumanne Elfadhili
20.Jonas Mkude                                     09.Sino Augustino
12.Salim Kinje                                       22.Julius Kwaga
04.Komanbil Keita                                 08.Henry Mwalugala
13.Daniel Akuffor                                   11.Hamisi Ally
05.Pascal Ochieng                                  23.Jeremiah Juma
Refa: Paul Soleji (Mwanza)
Mwamuzi Msaidizi 1: Jesse Erasmo (Morogoro)
Mwamuzi Msaidizi 2: Mwarabu Mumba (Morogoro)
Mwamuzi wa Akiba: Israel Nkongo (Dar es Salaam  
 

HIVI NDIO VIINGILIO VYA MECHI YA SIMBA NA YANGA

KIINGILIO MECHI YA YANGA, SIMBA SH. 5,000
Kiingilio cha chini kwenye mechi ya Yanga na Simba itakayochezwa Jumatatu (Oktoba 3 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo ni 19,648 kwenye uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000.
 
Mechi hiyo namba 80 ya Ligi Kuu ya Vodacom itachezwa kwenye uwanja huo kuanzia saa 11 kamili jioni. Watazamaji watakaotaka kuona mechi hiyo wakiwa wameketi kwenye viti vya rangi ya bluu ambavyo ni 17,045 watalipa sh. 7,000 kwa tiketi moja.
 
Viingilio vingine kwenye mechi hiyo ni sh. 10,000 kwa viti vya rangi ya chungwa ambavyo viko 11,897 wakati VIP C inayochukua watazamaji 4,060 itakuwa sh. 15,000. Kwa upande wa VIP B tiketi ni sh. 20,000 na VIP A yenye watazamaji 748 tu kiingilio kitakuwa sh. 30,000.

HUYU NDIO KOCHA MPYA WA YANGA - ERNIE BRANDTS

 
Hatimaye leo hii klabu bingwa ya Afrika mashariki na kati Dar Young Africans imemtambulisha rasmi kocha wake mpya Mholanzi Ernie Brandts.

Kocha huyu ambaye miezi michache iliyopita alikuwa mwalimu wa klabu bingwa ya Rwanda, APR aliwasili jijini Dar es Salaam jana usiku na leo asubuhi ametambulishwa rasmi kwa waandishi wa habari na kusaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuifundisha klabu hiyo ya Jangwani.

Brandts ambaye amewahi kuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Uholanzi na klabu kubwa ya nchi hiyo PSV Eindhoven akicheza kwenye nafasi ya ulinzi, amekuja Yanga kuchukua nafasi ya mbelgiji Tom Saintfiest aliyetimuliwa wiki iliyopita baada ya kukaa kwenye klabu hiyo kwa siku 81.


HII NDIO PROFILE YA KOCHA MPYA WA YANGA ERNIE BRANDT.


Ernie Brandts
Ernie Brandts 1978.jpg
Personal information
Full name Ernstus Wilhelmus Johannes Brandts
Date of birth 3 February 1956 (age 56)
Place of birth Nieuw-Dijk, Gelderland
Height 1.81 m (5 ft 11 12 in)
Playing position Defender (retired)
Club information
Current club APR FC
Youth career

De Sprinkhanen (Nieuw-Dijk)
Senior career*
Years Team Apps (Gls)
1974–1977 De Graafschap 38 (2)
1977–1986 PSV Eindhoven 251 (23)
1986–1989 Roda JC 68 (4)
1988–1989 MVV Maastricht 16 (0)
1989–1991 K.F.C. Germinal Beerschot 59 (5)
1991–1992 De Graafschap 20 (0)
National team
1977–1985 Netherlands 28 (5)
Teams managed
1993–2002 PSV Eindhoven (youth and assistant)
2002–2004 RKSV Nuenen
2005–2006 FC Volendam
2006–2008 NAC Breda
2009 Rah Ahan
2010– APR FC

KWANINI CRISTIANO RONALDO NI TIGER WOODS WA SOKA

Cristiano Ronaldo ni mmoja ya wachezaji bora kabisa wa juu katika kizazi hiki. Jinsi alivyoitawala La Liga katika misimu miwili inatukumbusha mmoja wa wanamichezo bora kabisa katika karne hiii: Tiger Woods.

Pamoja na kwamba wanacheza kwenye michezo miwili tofauti, wawili hawa wana vitu vingi wanavyofanana. Wote wawili ni wachezaji muhimu sana katika michezo yao na wamaekuwa ni wenye mafanikio. Wameweza kupata madili mengi ya udhamini na huku wakicheza kwenye kiwango cha kuvunja rekodi.


Tiger na CR7 wamejituma sana mpaka kufikia malengo yao: wakicheza kwa kiwango cha juu ili kuwa wachezaji bora kabisa kwenye michezo yao husika.

Wawili hawa wanafanana katika vitu na hivi vifuatavyo ni baadhi.

MAPATO

Kwa mujibu wa Forbes, Tiger Woods ni mwanamichezo wa tatu anayelipwa vizuri zaidi duniani. Mshahara pekee unafikia kiasi cha $4.4 million kwa mwaka.

Cristiano Ronaldo pia yupo katika listi hiyo, akishika nafasi ya 9. Ingawa David Beckham anaongoza kwa mapato ya jumla, lakini mshahara wa Cristiano Ronaldo kwa mwaka upo karibia na $20.5 million, jambo ambalo linamaanisha anamzidi $11.5 million Beckham.

Hii inawafanya kuwa wanamichezo wenye kulipwa vizuri zaidi kwenye michezo yao - bila kuingiza mapato ya udhamini.

KUPENDWA NA KUCHUKIWA
Wanamichezo hawa wawili wana fan base kubwa sana na pia wanachukia sana. Kwa Tiger mambo yote yalianza ilipotoka skendo yake ya kumsaliti mkewe mwaka 2009. Taswira yake ya kuwa mume bora ikafutika na kuchukiwa na watu wengi.

Cristiano yeye na mwenzake Lionel Messi wamewagawa wapenzi wa mpira wa miguu duniani. Pia tabia zake za nje ya uwanja zimezidi kumuongezea maadui, muda mwingine tambo zake tu zimekuwa zikimfanya watu wamchukie.

Kwa wale wanaowapenda hakuna kitu kingine wanachojali zaidi ya ushujaa wao.

KIWANGO
Tiger ni mmoja kati ya wacheza gofu bora kabisa kuwahi kutokea duniani. Wengi wanamuona kama ni bora zaidi ya Jack Nickalus, wengine wanaamini kwamba hatoweza kumshinda Jack mpaka pale atakaposhinda makombe makubwa zaidi ya 18.

Cristiano amekuwa nae akihusishwa na mjadala kama huo, lakini kwa mara nyingi zaidi amekuwa akifananishwa na Lionel Messi. Mwaka 2008 alishinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia na amekuwa akiendelea kutisha tangu wakati huo.

Wote wamekuwa kwenye viwango vya juu kwa miaka mingi, kwa Woods kipindi chake kizuri kabisa kilikuwa mwaka 2000.

Alishinda makombe sita mfululizo, kitu ambacho hakuna yoyote aliyeweza tangu mwaka 1948, alishinda katika michuano ya US Open,, kitu ambacho Sports Illustrated walisema kiwango cha Woods kwenye michuano hiyo kilikuwa bora kuliko vyote katika historia ya gofu.

Katika misimu 16 kama mcheza gofu, Tiger ameshinda katika michuano 102, 74 kati ya hiyo ameshinda katika PGA Tour.

Ronaldo amekuwa akicheza soka la ushindani wa juu kwa miaka 10 sasa ambayo amefanikiwa kufunga mabao 275 na Sporting Lisbon, Manchester United na Real Madrid, na mabao mengine 37 katika timu ya taifa ya Ureno, jumla ya mabao yote ni 312.

CR7 aliwakusanya mashabiki 85,000 katika utambulishwaji wake pale Bernabeu, akivunja rekodi ya Maradona ya kutambulishwa mbele ya mashabiki 75,000 alipoiunga na Napoli.

Alihitaji mechi nne kuweka historia na Los Blancos, alifunga katika kila mechi zake nne za mwanzo, akiwa ndio mchezaji wa kwanza kufanya hivyo.

Moja ya mafanikio yake makubwa hivi karibuni aliweza kumaliza msimu wa La liga akiwa amefunga mabao 40, kitu ambacho hakuna aliyewahi kufanya hivyo; Hugo Sanchez na Telmo Zarra walikuwa wamefunga mabao 38 kila mmoja huko nyuma.

MITANDAO YA KIJAMII
Tiger Woods ndi mcheza gofu mwenye mashabiki wengi kwenye mtandao wa Twitter.

Alipofungua akaunti yake akuwa akitweet sana, lakini baada ya skendo ya kuisaliti ndoa yake, akaanza kuitumia akaunti yake.

Cristiano Ronaldo nae ana sifa hiyo hiyo ya Woods, lakini pia ameweza kuwa mwanamichezo mwenye mashabiki wengi zaidi kwenye mtandao huo akiwa na followers zaidi ya millioni 13.

MIKATABA YA UDHAMINI
Nike, NetJets, EA Sports, Konami, Rolex, na wengine kibao. Wote wanawadhamini hawa vijana. Wachezaji hawa wawili hawa wana wadhamini bora kabisa kwenye michezo.

Woods anatengezea kiasi cha $55 million kwa mwaka kutokana na mapato ya mikataba ya matangazo. Mchezaji huyo bora namba 1 wa zamani aliwapoteza wadhamini kama Gatorade, AT&T, Buick na Tag Heur katika miaka kadhaa iliyopita, lakini ndio mwanamichezo anayeokea fedha nyingi kutoka mikataba ya matangazo.

Katika upande wa Ronaldo anashika nafasi ya 10 na wa pili nyuma ya David Beckham kama mwanasoka mwenye mapato makubwa kutokana na mikataba ya matangazo ya biashara.

Friday, September 28, 2012

DJ JD IS BACK IN THE THE BUSINESS!

OFFICIAL: MWANGALIE RICK ROSS AKIZUNGUMZIA UJIO WAKE KWENYE FIESTA 2012 TAREHE 6 OCTOBER

SIMBA MPENI NAFASI HUYU KINDA: ANAWEZA KUZIBA PENGO LA OKWI DHIDI YA YANGA


Wakati joto la pambano la kwanza la ligi la watani wa jadi Simba na Yanga likizidi kupamba moto, huku Simba wakiwa na pengo kubwa la kumkosa mshambuliaji wao tegemeo Emmanuel Okwi ambaye ana adhabu ya kufungiwa mechi tatu - mashabiki na wanachama wa klabu hiyo pamoja na benchi la ufundi la Simba hawapaswi kuwa fikra kubwa kuhusu pengo la Okwi.

Bahati nzuri ni kwamba Simba walijitahidi kufanya usajili mzuri kwenye safu ya ushambuliaji msimu huu hivyo wapo baadhi ya wachezaji ambao wanaweza kucheza vizuri na kuziba pengo la Okwi. Mmoja ya wachezaji hao ni kinda huyu aliyepandishwa kutoka Simba B iliyochukua ubingwa wa BancABC Super8 anayeitwa Haruni Athumani Chanongo.

Kijana huyu mwenye miaka 20, alikuwa ni mmoja ya wachezaji waliong'ara vilivyo katika michuano hiyo ya Super8, akizisumbua vilivyo ngome za vilabu vya ligi kuu vya Azam na Mtibwa katika mechi za nusu fainali na fainali huku akiwa mmoja ya wafungaji wazuri.

Staili ya uchezaji ya kinda huyu haitofautiani sana na ya Okwi, ana kasi na ujuzi wa kupiga vyenga. Anajiamini na ana uwezo wa kupambana katika kuisadia Simba kipindi hiki ikiwa na pengo la mshambuliaji tegemeo Okwi.


Haruni ambaye mwanzoni alishawahi kuichezea Polisi Dodoma katika ligi kuu chini kocha Sekilojo Chambua, tayari ana uzoefu wa kucheza mechi kubwa na kupafomu vizuri. Hapa anaelezea:
 "Nilipokuwa na umri wa miaka 18 nikiwa na timu ya Polisi Dodoma,kocha Sekilojo Chambua alinipa nafasi ya kucheza mchezo wangu wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom. Nafasi hii ilitokea baada ya baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza kuondoka kutokana na timu kuwa na matokeo mabaya,mchezo wangu wa kwanza ulikua dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Jamhuri uliomalizika kwa sare ya bao 1:1.
Nikiwa na Polisi pia nilifanikiwa kucheza michezo dhidi ya Simba na Yanga iliyomalizika kwa timu yetu kufungwa mechi zote mbili mabao 2:0."

Kwa mujibu wa makocha ambao tayari wameshamfundisha kinda huyu wanasema Haruni ana uwezo mkubwa na anaweza kucheza vizuri kwenye yoyote kwa sababu ana uwezo na anajiamini.

DERRICK WALULYA, TONY NDOLO, NA ERNEST BOAKYE WAOMBEWA UHAMISHO WA KIMATAIFA

TFF YATOA ITC KWA WACHEZAJI WANNE
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa wachezaji wanne waliokuwa wakichezea timu mbalimbali nchini.
 
Wachezaji hao ni Tony Ndolo aliyejiunga na KCC ya Uganda kutoka Toto Africans, Felix Amech Stanley aliyekwenda Bahla ya Oman kutoka Coastal Union, Ernest Boakye kutoka Yanga aliyejiunga na Tripoli Athletics Club ya Lebanon na Derrick Walulya aliyerejea URA ya Uganda kutoka Simba.
 
15 WACHUKUA FOMU UCHAGUZI TWFA
Wanamichezo 15 wamechukua fomu kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao.
 
Waliochukua fomu za kuwania uenyekiti ni Lina Kessy, Isabellah Kapera na Joan Minja. Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imeombwa na Roseleen Kisiwa pekee wakati Katibu Mkuu ni Amina Karuma na Cecilia Makafu. Macky Mhango pia ni mwombaji pekee aliyeomba nafasi ya Katibu Msaidizi.
 
Waombaji watatu wa nafasi ya mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ni Furaha Francis, Juliet Mndeme na Zena Chande. Nafasi ya Mhazini nayo ina mwombaji mmoja tu ambaye ni Rose Msamila.
 
Sophia Charles, Rahim Maguza, Telephonia Temba na Jasmin Badar Soud wao wanaomba nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya chama hicho kwenye uchaguzi huo ambao utaendeshwa na Kamati ya Uchaguzi ya TWFA chini ya Ombeni Zavalla.
 
MKUTANO VODACOM, KLABU ZA LIGI KUU
Klabu za Ligi Kuu na mdhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom zimekutana jana (Septemba 27 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo yalilenga kipengele ya upekee (exclusivity) kilichopo kwenye mkataba wa udhamini ambacho kitaendelea kuwepo. Klabu zilikuwa zimeomba kwa mdhamini kuangalia uwezekano wa kukiondoa.
 
Pande hizo zimekubaliana kuunda kamati ya pamoja kwa ajili ya kuitafutia kila klabu mdhamini binafsi kwa lengo la kuhakikisha zinashiriki kikamilifu katika ligi hiyo.
 
Klabu zote zimeshapata vifaa kutoka kwa Vodacom ukiondoa African Lyon ambayo ilitarajia kuchukua vifaa hivyo leo kutoka kwa mdhamini wa ligi hiyo.
 
MCHAKATO WA UCHAGUZI WA VIONGOZI TAFCA
Mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) unaanza rasmi Septemba 30 mwaka huu kwa uchukuaji fomu kwa wagombea.
 
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA, Ramadhan Mambosasa, fomu kwa waombaji uongozi zitaanza kutolewa Septemba 30 mwaka huu, na mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu hizo ni Oktoba 4 mwaka huu.
 
Fomu hizo zinapatikana ofisi za TAFCA zilizopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 10 alasiri. Ada ya fomu kwa waombaji wa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu na Katibu Msaidizi ni sh. 200,000.
 
Nafasi zilizobaki za Mhazini, mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na wajumbe wa Kamati ya Utendaji, ada ya fomu ni sh. 100,000. Uchaguzi wa TAFCA umepangwa kufanyika Novemba 10 mwaka huu.

CHEMSHA BONGO! IANDIKIE CAPTION PICHA HII!

MCHEZO WA MASUMBWI, TAA INAYOZIZIM​A – SEHEMU YA PILI

UNAPENDWA NA KUOGOPWA NA WATU WENGI DUNIANI
UKO HATARINI KUPOTEZA ASILI YAKE KABISA

Na Onesmo Ngowi
 Masumbiwi au kwa majina mwengine ndondi au ngumi na kwa majina ya mitaani ndogwa, mawe n.k. ni mchezo unapoendwa sana na watu wengi. Aidha mchezo huu ni kati ya michezo inayoogopwa sana duniani. Mchezo wa ngumi uko hatarini kupoteza maana yake ya asili yaani kucheza kama burudani, kuwakilisha nchi na kujenga ushupavu wa mchezaji. Mamilioni ya watu wanaojazana kuutazama wasingependa kabisa kujiingiza kuucheza mchezo wa ngumi. Sasa endelea………………………………….!              Kuanzia karne ya 16 matukio mbalimbali yaliyotokea katika bara la Ulaya na Mashariki ya mbali yalichochea ustaarabu uliopelekea mambo mengi kubadilika. Mabadiliko haya ni pamoja na watu walivyokuwa wanachukuliwa na kuthaminiwa.
 Dola mbalimbali kubwa kama Mongolia, Manchuria, Ujapan, Urumi, Uyunani, Ottoman n.k zilikuwa kama zimekufa au kupungua nguvu kiasi cha kuruhusu mabadiliko hayo. Ustaarabu huu ulishinikizwa haswa na mabadiliko ambayo dunia ilikuwa inapitia. Wanadamu walianza kuwa na mwelekeo tofauti kabisa katika kuyajali maisha yao.                 Pengine ni katika Mitholojia ya Kigiriki (Greek Mythology) ambapo ushujaa ulipoelezwa kwa ufafanuzi zaidi. Kwenye Mitholojia ya Kigiriki neno Shujaa au Bingwa (Hero) limeelezwa kama “Mwanamke au mwanamme wa ushupavu na nguvu kubwa anayeheshimika kwa mafanikio yake”
 Mitholojia ya Kigiriki inatuelezea mashujaa wa aina mbalimbali kama vile Hercules, Perseus, Theseus, Odysseus, Bellerophon na Atlas. Wengi wa mashujaa hawa kwenye Mitholojia ya Kigiriki walijijengea sifa kubwa sana kwenye jamii na wengine walifananishwa na baadhi ya miungu yao.
 Ugiriki pia ilitoa mashujaa wengine mbalimbali kama vile Alexander the Greatj ambaye alikuwa ni Jemadari na shujaa wa vita aliewahi kuwa Jemadari mdogo kuliko wote duniani na kuweza kueneza dola ya Kiyunani toka ukanda wa bahari ya Mediterania hadi Afrika ya Kaskazini.
 Aidha ni huko huko Uyunani ambako mashujaa wakubwa wanafalsafa kama kina Soctates, Plato na Aristotle walisheheni hekima na upeo wa kuyachambua masuala makubwa katika jamii. Falsafa mbalimbali zilichangia kwa kiasi kikubwa kuweko na mabadiliko katika maisha ya wanadamu.                  Maisha na hata kifo cha mwanafalsafa Socrates yalikuwa ni ya ajabu. Aliishi kama mwanafalsafa akiwa kama dira ya jamii na alitakiwa apembenue kila jambo alilonena na mwishoni alitakiwa kunjwa sumu ili ahakikishe kuwa haitamuua na akafa!
 Afrika haikuwa nyuma katika matukio ya kishujaa. Katika ukanda wa kusini mwa jangwa la Sahara ambako dola ya Kizulu nchini Afrika ya Kusini ilikuwa na michezo yao iliyoonyesha ujasiri mkubwa wa mashujaa wa kivita. Chini ya utawala wa mfalme Chaka vijana wengi wa jika la kupigana vita walitakiwa kuonyesha ujasiri wao katika mikusanyiko mikubwa ikiwa ni pamoja na michezo iliyowaandaa kuingia vitani.
 Ujio wa wazungu katika ukanda huu haukuwa wa kirahisi kabisa kwani walipambana na wenyeji ambao ni Wazulu walishirikiana na makabila mengine shujaa kwelikweli. Hapa Tanzania nako makakabila kama Wahehe, Wangoni, Wasambaa, Wachagga nayo yalikuwa na ujasiri wa kipekee katika kujilinda na maadui zao ikiwa ni pamoja na uvamizi wa wakoloni wa kizungu. 
 Pengine kwa namna moja matukio yote haya na mengine mengi yana mchango mkubwa sana katika mchezo wa ngumi. Japokuwa mabadiliko ya mchezo huu yametokea sehemu mbalimbali duniani kwa njia moja au nyingine yamekuwa na lengo moja tu nalo ni kujenga ujasiri wa wanadamu.
 Mtu anapopigana ngumi na kushinda anapendwa na kila mtu. Ni shujaa wa kila mtu. Ni mfano wa kuigwa kwa wale wanaopenda mashujaa. Wanadamu wana asili ya kupenda mashujaa. Hata kama mashujaa hao wana kasoro fulani za kimaumbile lakini wanatukuzwa na kuheshimika kwa ushujaa wao.
 Mashujaa daima ni watu ambao jamii inawaona kama kioo chake na mfano wake wa kuigwa. Ili mtu au bondia awe shujaa kwelikweli hana budi kufuata yafuatayo: 1) Awe ni mtu anayefanya vizuri kuliko wote
2) Awe ni mtu anayeishi maisha yasiyo na kasheshe
3) Awe ni mtu aliyefikia kiwango cha juu katika fani yake na kuitetea bila ya matatizo.
4)Na zaidi ya yote awe mtu anayependa nchi yake na kuitetea katika fani yake bila kujali faida anayoweza kuipata.
 Mara nyingi katika fani ya ngumi kumetokea mashujaa wengi waliodumu kwa muda mfupi na hivyo jamii kuwasahau kabisa. Katika nchi za wenzetu kuna utaratibu wa kuhifadhi kumbukumbu za kazi / michango inayotolewa na kila mtu katika fani mbalimbali. Zipo website (tovuti) mbalimbali ambazo ukimtafuta mtu katika fani hizi utapata mara moja. Iaendelea………………………….!
 Mwandishi wa makala haya ni; Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Shirkisho la Ngumi za Kulipwa Afrika Mashariki na Kati (ECAPBF), Shirikisho la Ngumi la Kimataifa bara la Afrika, Masharilki ya Kati, Ghuba ya Uarabu na Uajemi (IBF/AFRICA) na Mkurugenzi wa Baraza la Ngumi la Jumuiya ya Madola (CBC) E-mail:ibfafrica@yahoo.com                                                         

TFF,FA MIKOA NA NMB MNATUPELEKA WAPI ?

Habari zenu ndugu wasomaji. Leo nina maswali machache na hoja kadhaa ambazo nahitaji majibu toka kwa TFF, FA MIKOA na Benki ya NMB kama wadau wakubwa wa Soka hapa nchini.

Naamini kila mtu anakumbuka kozi za Walimu wa Soka zilizokuwa zinafanyika hapa nchini takiribani mikoa yote ya Tanzania na baadhi ya mikoa ilijirudia mara kadhaa, Na nyingi ziliendeshwa kwa Walimu wa Sekondari na Shule za msingi ili kuinua vipaji toka mashuleni, hii inatokana na TFF kuangahika kwa muda mrefu kutafuta Wadhamini na hatimaye Benki ya NMB kujitokeza na kudhamini kozi hizi kitu ambacho ni kizuri kinachohitajika katika kukuza Soka letu Tanzania.

Kilichonishtua ni mwaka 2009/2010 ilitakiwa kuendeshwa kozi hiyo kwa mikoa 26 ya Tanzania Bara na Benki ya NMB ilitoa fedha za kuendesha kozi hiyo pamoja na mipira 30 kila mkoa,koni 18 kila mkoa, jezi jozi moja kwa ajili ya mkufunzi na fedha walipewa TFF ili watume kwa kila FA mkoa kwa mikoa yote 26.

Lakini cha kushangaza hawa TFF walituma pesa hizi na vifaa hivyo kwa mikoa kama kumi tu ikiwamo Shinyanga, Mwanza, Singida, mikoa ya Kisoka Ilala,Temeke na Kinondoni na pia fedha Tshs 710,000 kwa ajili ya posho ya mkufunzi, chakula, malazi na mawasiliano sasa swali je fedha nyingine za mikoa 16 zimekwenda wapi mimi na wewe msomaji wangu hatujui.

FA za mikoa teule ambayo ilipewa fedha hizo pia nao walichakachua kwa mtindo wao na kutoa fedha hizo kwa ufinyo Mfano ni Mkoa wa Shinyanga ambao kozi iliendeshwa januari 26, 2010-Februari 7,210 na mkufunzi alikuwa Marehemu Suleiman Gwaje ambaye pia alilalamikia hili, pia ulitokea ugomvi na kurushiana maneno kati ya viongozi wa FA mkoa na Wajumbe Watendaji kutokana na fedha hizo mpaka baadhi ya wajumbe kutaka kupindua uongozi huliopo madarakani.

Utaratibu ulitakiwa kuwa hivi mkufunzi akabidhiwe fedha zake katika mchanganuo ufuatao: - Posho ya siku 16 @ Tshs30, 000 jumla 480, 000, Nauli Tshs 230,000 yaani kwenda na kurudi pamoja na mawasiliano akiwa katika kituo chake cha kazi. Matokeo yake haya hayakufanyika na mkufunzi alipelekwa katika migahawa ya ajabu yenye bei nafuu na huduma hisiolidhisha ili kupiga panga fedha hizo.

Wanafunzi waliotakiwa kushiliki kozi hizi walikuwa ni Walimu na idadi ni 45 kwa kila mkoa yaani katika ile mikoa 10 teule ya TFF. Kwa mjibu wa TFF wenyewe walisema gharama ya Cheti kimoja ni Tshs 10,000 na fedha hizi ulipwa na NMB na tayari zilishakabidhiwa kwa TFF lakini cha kushangaza hakuna hata mkoa moja kati ya mikoa hii 10 walioendesha kozi hii mwaka 2009/2010 wamepata Vyeti hivyo. Sasa piga hesebu mikoa 26, kila mkoa Walimu 45 na kila mmoja gharama ya cheti ndio hiyo je ni Shilingi ngapi zimechakachuliwa na hawa jamaa?

Kinachoendelea sasa kuna kampeni ya TFF ya chini kwa chini kuhamasisha makatibu wa TAFCA wa ile mikoa ambayo ilibahatika kufanya kozi hii kuwaomba Walimu walioshiriki kozi hii wachange elfu kumi (Tshs 10,000) ili watengenezewe Vyeti hivyo kwa kupitia kwa Katibu wa TAFCA Taifa ili kuficha hili lilofanyika ambalo pia limekwama kutokana na kutokuwa na imani tena na TFF, sasa mimi najiuliza Soka letu litakua kwa mtindo huu? TFF, FA MIKOA na Benki ya NMB wanatupeleka wapi?

Pia baadhi ya mikoa kozi hii ilifanyika mwezi Oktoba 2009 kama Singida, Mwanza na mingineyo lakini Shinyanga ilifanyika tarehe 26 Januari, 2010 pia badala ya kuwa na Walimu 45 wa sekondari na shule za msingi waliotakiwa kushiriki walishiriki 26 tu tena katika mazingira magumu kwani hapakuwa na hata maji ya kunywa na washiriki walio wengi walifanya kuwakamata tu barabarani na kuwataka washiriki kozi hii na hili lilifanywa makusudi kwani fedha ya kuendesha kozi hii kwa mkoa huu ilikuwa ishaliwa na viongozi wa FA mkoa.

Na maelezo kutoka TFF, washiriki walitakiwa kujigharamia chakula na malazi kitu ambacho walikifanya Walimu hawa tena bila kinyongo. Je ni kweli ndio mkataba unavyosema maana mkataba huu ni siri kati ya TFF na Benki ya NMB hakuna mdau wala TAFCA anayeufahamu mkataba huo sasa tujiulize watu wakikataa kujitokeza kushiriki kozi hizi tutamlaumu nani kwa ubabahishaji huu?
Na kwa nini fedha hizi zisikabidhiwe kwa chama cha makocha Taifa na kuwambia waendeshe kozi hizi badala ya FA za kila mkoa kwani wao ndo wanajua watu gani ambao wanapenda na wanataka kuwa walimu wa soka.

Mimi kama mimi siamini kama Benki ya NMB hailifahamu hili kwani kama hawafahamu inaamana hawafanyi ukaguzi wa fedha zao wanazotoa kwa TFF? Na kama wanafahamu wamechukua hatua gani? Na kama wamechukua mbona taarifa hatujaiona wala kuisikia? Kama hawajachukua hatua inamaana na wao pia wanahusika katika hili?

Mimi kama mdau wa Soka hili la Bongo inaniuma sana na kubakia na maswali TFF, FA MIKOA na Benki ya NMB wanatupeleka wapi? Na wapo kwa ajili ya kuendeleza Soka au maslahi yao binafsi? TFF Na Benki ya NMB naomba mchunguze au mtoe maelezo kuhusu hili maana linatia kinyaa na aibu katika Soka letu na kama hamna taarifa basi Habari ndiyo hiyo.


Na Magesa Japhari
E – Mail: japharimagesa@yahoo.com
Mobile phone: +255 784 269 812 or +255 764 318 844, +255 714 368 843.

NB:
Kwa haraka haraka tu, Fedha inayosadikika kutafunwa na TFF na FA MIKOA
Watu 45 @ mkoa × 10,000 gharama ya cheti × 26 mikoa iliyotakiwa kushiriki jumla 11,700,000.
FEDHA ya Wakufunzi mikoa 26,ilitolewa kwa mikoa 10, je mikoa 16@Tshs 710,000 × 16 mikoa ambayo haikutumiwa jumla 11,360,000
GRAND TOTAL Tshs 23,060,000
Hizi ndizo tulizojua kwa mjibu wa hesebu iliyopo je tusizozifahamu ni ngapi? AKILI KUMKICHWA!

Thursday, September 27, 2012

UAMUZI WA NEYMAR KWENDA ULAYA - MKUBWA ZAIDI TANGU MESSI ALIPOSAINI BARCELONA KWA KUTUMIA LESO


Lionel Messi alikuwa na miaka 13 tu alipojiunga na Barcelona. Hakukuwa na vita yoyote ya kugombea saini yake, na mkataba wake ulisainiwa kwenye leso haukuwa na shamra shamra nyingi wala kuwasili kwake Nou Camp. 


Messi hakuchagua sehemu bora kwake; alikuw na chaguo moja na ndilo alilochagua. Barcelona ndio ilikuwa klabu pekee iliyokuwa tayari kulipa fedha za kumtibu ugonjwa wake wa upungufu wa homoni, na kutokana na imani yao kwa kijana huyu wa Kiargentina leo hii dunia inashuhudia ladha ya soka na klabu inanufaika.

 "Nilihitaji fedha kwa ajili ya dawa zangu kunisaidia niweze kukua na Barcelona ilikuwa ndio klabu pekee iliyotoa ofa. Hivyo mara tu walipokubali kunitibia nikajua nitakiwa kuondoka nyumbani na kwenda Catalan," Messi aliliambia jarida la Match of the day. Hiyo ilikuwa mwaka 2000. 

Miaka 12 tangu wakati huo kutoka sasa, Messi ameibuka kuwa mchezaji bora kabisa katika kizazi hiki - akiiongoza Barcelona kupata mafanikio makubwa kuliko katika historia ya klabu hiyo, kuanzia nyumbani mpaka ulaya, huku akitajwa mara 3 kuwa mchezaji bora wa dunia (2009,2010, 2011).

Barcelona ingekuwaje bila kuwepo kwa Messi? Unapoangalia takwimu zake za mabao, na mchango wake wote kwa ujumla na namba ya mechi alizocheza kwa kiwango kikubwa na kuipa ushindi Barca, kuna hitimisho moja tu: Wasingekuwa na mafanikio haya au wangekuwa duni kama ilivyokuwa miaka ya 90.

Je wangekuwa wameshinda makombe matano ya La Liga, mawili ya Spanish Super Cup na matatu ya ulaya ambao wameshinda wakati wa uwepo wa Messi?

Ofcourse wasingeweza. Hivyo sio kusema timu za Frank Rijkaard na Pep Guardiola zingetoka mikono mitupu, kwa sababu bila Messi pia walikuwa na timu nzuri kulinganisha na vikosi vya timu nyinginezo barani ulaya. Lakini ni mara ngapi   tumeishuhudia Barca ikicheza vizuri bila uwepo wa Messi au akiwa yupo chini ya kiwango?

Ukiangalia nyuma, unaweza kusema uamuzi wa Messi kuondoka nyumbani kwao Argentina na kujiunga Barcelona ndio ulikuwa uamuzi uliobadilisha hatma ya soka la ulaya ndani ya miaka 10 iliyopita.

Ni wazo ambalo linatuleta kwa Neymar - mtu ambaye wengi wanamtaja kuwa Messi mpya ambaye ana machaguo mengi katika timu kubwa za ulaya tofauti na ilivyokuwa kwa Lionel.

Hali ya Neymar ni tofauti sana na ilivyokuwa kwa Messi mwaka 2000. Kijana huyu wa Kibrazil tayari ni jina kubwa sana kwenye soka na tayari ameshaanza kuitawala soka ya dunia.

Ni shujaa wa kuteuliwa pale Santos - akifuata nyayo za Pele - huku akitajwa kuwa ndio mchezaji anayetazamwa kuwa bora zaidi katika miaka 10 ijayo katika ulimwengu wa soka.

Uhamisho kwenda Ulaya ni jambo ambalo linangoja muda tu, kitu ambacho kinaeleza kwanini Neymar amekuwa ndio mchezaji anayeandikwa sana kwenye tetesi za vyombo vya habari katika kipindi cha miaka 3. Kila mtu anajua anaondoka Brazil, lakini ni wachache sana au kuna hakuna anayejua kwa hakika ni lini, ni wapi na jezi ya timu gani atakuwa akivaa huko Ulaya.

Mbrazili mwenzie Dani Alves ni mmoja ya wengi wenye matumaini ataungana na Messi pale Barcelona - dili ambalo mwandishi wa ESPNsoccernet, anaamini limeshafanyika.

Ni kitu cha kusisimua sana kumuona Neymar akiungana Messi, lakini pia kama ilivyo kumuona akiungana na Cristiano Ronaldo pale Real Madrid, Eden Hazard pale darajani Chelsea, Wayne Rooney na Robin van Persie pale Old Trafford au kuungana na David Silva na Sergio Aguero pale Etihad Stadium na Man City.

Timu zote kubwa barani ulaya kwa sasa zimetajwa kuwa zinaweza kumchukua mchezaji huyo, huku gazeti la Metro likiripoti kwamba klabu ya PSG ipo tayari kulipa £85 million mwezi January kumsaini kinda huyo.

Pia kumekuwepo na mawazo kwamba Santos hawatomuuza mchezaji huyo mpaka litakapofanyika kombe la dunia 2014,  lakini bei ya Neymar sokoni inapanda, ni vigumu kuamini kwamba wataweza kuimiri na kukataa fedha nyingi katika kipindi cha madirisha matatu makubwa ya usajili yajayo.

Uamuzi wa Neymar kuondoka Brazil - utamaanisha kumpa nafasi kubwa ya mchezaji bora wa kizazi chake kwenye soka. kwa kipaji alichonacho, ana kila kitu cha kumfanya aweze kuitawala soka ya ulaya na kuipeleka timu atakayoichagua katika levo nyingine ya mafanikio - sio tu uwanjani bali pia katika biashara na kuifanya kuwa kubwa zaidi ya ilivyo sasa.

MJADALA: SUAREZ ALIFUNGIWA MECHI 8 KWA UBAGUZI - BARTON MECHI 12 KWA RAFU: JOHN TERRY MECHI 4 KWA UBAGUZI. JE HII NI SAWA???




HAYA NI MAONI YA MCHEZAJI WA JOEY BARTON
"Mechi nne tu? Mwaka mzima wa uchunguzi, siku nne za usikilizwaji wa kesi na adhabu ya kufungiwa mechi 4 tu? Suarez alifungiwa 8.

"Mimi nilifungiwa mechi 12!!! Kwa uamuzi huu wa FA, ina maana ningepata adhabu ndogo kwa kuwatukana kibaguzi wachezaji wa Man City kuliko ambavyo nimeadhibiwa kwa kuwachezea faulo. Kwa namna hiyo inaweza ikawa sawa???

WAZIRI MKUU WA CAMEROON AINGILIA KATI ISHU YA ETO'O KWENYE TIMU YA TAIFA - AMSHAWISHI ARUDI KIKOSINI


Takribani mwezi mmoja baada ya kuandika barua ya kugoma kuichezea timu ya taifa ya Cameroon, mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi duniani kwa upande wa soka, Samuel Eto'o sasa anaonekana yupo tayari kwenda kinyume na msimamo wake wa mwanzo na kurudi kuitumikia timu ya taifa lake baada ya kuwa na mazungumzo na waziri mkuu wa nchi hiyo.

Mshambuliaji huyo wa klabu ya Anzhi Makhachkala alifungiwa kwa miezi nane baada ya kuongoza mgomo wa wachezaji dhidi ya Chama cha Soka cha Cameroon kuhusiana na posho zao.

Hata alipomaliza kutumikia adhabu hiyo na kuitwa kikosini, Eto'o alikataa na kusema kwamba hataichezea tena timu ya taifa hadi hapo viongozi wa chama cha soka nchini mwake watakapobadilika na kufanya kazi kwa weledi mkubwa na unaostahili.

Jambo hilo sasa linaelekea kupata ufumbuzi baada ya Waziri Mkuu Philemon Yang kuzungumza yeye mwenyewe na mtupia mabao huyo wa zamani wa Barcelona na kumuomba arudi kikosini ili aisaidie nchi yake inayohaha kupata nafasi ya kufuzu kwa fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2013).

“Mkuu wa Nchi ameamua kulishughuilikia suala hilo yeye mwenyewe na ametupa maelekezo,” amesema kocha wa Cameroon, Jean-Paul Akono.

“Baadaye tulikutana kuweka mambo sawa na sasa kila kitu kiko vizuri. Hivi sasa yuko tayari, lakini anaweza kukosekana kwa sababu ya majeraha. Tutaendelea kuomba na kusubiri siku za mwisho kabla ya mechi."

Cameroon walichapwa 2-0 katika mechi yao ya ugenini dhidi ya Cape Verde, ambayo ni ya kwanza katika raundi ya mwisho ya kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON 2013, na kurejea kwa Eto’o kunatarajiwa kuwaongezea nguvu katika mechi yao ya marudiano mjini Yaounde Oktoba 13.

OFFICIAL: JOHN TERRY AADHIBIWA MECHI NA FAINI YA £220,000 - KUZIKOSA MAN UNITED NA ARSENAL

John Terry ameadhibiwa na chama cha kandanda cha England, FA, asicheze mechi nne, na vile vile alipe faini ya pauni 220,000, kutokana na matamshi ya ubaguzi wa rangi dhidi ya mchezaji wa QPR, Anton Ferdinand.

Chama cha FA kilithibitisha Terry alifanya makosa hayo, baada ya kusikiliza kesi dhidi yake kwa kipindi cha siku nne.

Msemaji wa John Terry alisema mchezaji huyo "alisikitishwa" na hatua ya FA, kwa kuamua tofauti, kinyume na mahakama, ambayo awali ilisema hana makosa.

Mwezi Julai, mahakama ya Westminster mjini London ilipitisha uamuzi kwamba mchezaji huyo, mwenye umri wa miaka 31, hakufanya kosa hilo, la kutumia matamshi ya ubaguzi wa rangi dhidi ya Ferdinand.

Hata hivyo wengi watajiuliza kwa nini adhabu dhidi ya Terry ni nyepesi mno, ikilinganishwa na ile iliyopitishwa dhdi ya mchezaji wa Liverpool, Luis Suarez mwaka jana.

Terry ana muda wa siku 14 kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo, mara tu atakapopokea maelezo ya adhabu hiyo kupitia maandishi.

Adhabu hiyo haitatekelezwa hadi Terry atakapopata nafasi ya kuamua atafanya nini.

Taarifa kutoka klabu yake ya Chelsea iliongezea: "Klabu ya Chelsea inafahamu vyema uamuzi uliopitishwa, na inaheshimu uamuzi huo uliotolewa leo na chama cha FA kumhusu John Terry." 


Kutokana na adhabu hiyo John Terry atazikosa mechi nne zilizo chini ya FA, ikiwemo mechi dhidi ya mahasimu wao wa jiji la London Arsenal na Spurs pamoja na Norwich na Manchester United.

LIGI KUU SUPER WEEKEND KUANZA KESHO

Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom inaingia raundi ya nne kesho (Septemba 28 mwaka huu) kwa mechi za Super Weekend ambazo zitaoneshwa moja kwa moja (live) na kituo cha televisheni cha SuperSport cha Afrika Kusini.
 
Mechi ya kwanza ambayo itachezwa kesho itakuwa kati ya Azam na JKT Ruvu Stars. Mechi hiyo itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam itaanza saa 1 kamili usiku kwa viingilio vya sh. 3,000 mzunguko, sh. 5,000 kwa VIP C na VIP B wakati VIP A kiingilio kitakuwa sh. 10,000.
 
Jumamosi (Septemba 29 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Simba na Tanzania Prisons itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11 kamili jioni. Yanga na African Lyon zitapambana Jumapili (Septemba 30 mwaka huu kwenye uwanja huo huo kuanzia saa 11 kamili jioni.
 
Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam wenyewe utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar itakayochezwa Oktoba 1 mwaka huu kuanza saa 10.30 jioni. Mechi ya mwisho ya Super Weekend itachezwa Oktoba 3 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ikizikutanisha Yanga na Simba kuanzia saa 1 kamili usiku.

PICHA YA SIKU!

Photo: Coastal Union 2012 Tunatisha......Ndio Inavyosomeka.Mmoja wa Shabiki wa Coastal Union Akitoa ujumbe wake Kwa njia ya Bango.
Mechi 4 points 8=Nafasi ya 2
Ni Balaaaaaaaaaaaaaa(LIKE)

BREAKING: HUYU NDIO MSANII WA KIMATAIFA KUTOKA MAREKANI ATAKAE KUJA KUPERFORM FIESTA 2012!! BHAAAAAAAAS!!!

1
RICK ROSS.
Imfahamika rasmi kwamba msanii atakaekamilisha shangwe za SERENGETI FIESTA 2012 ni RICK ROSS TUFLON DON october 6 2012 Dar es salaam,

MAN UNITED YAIKANDAMIZA NEWCASTLE - SASA KUKUTANA NA CHELSEA MWEZI UJAO KWENYE CAPITAL ONE


М-Н footyroom.com by footyroom

NURI SAHIN AIPELEKA LIVERPOOL RAUNDI YA NNE KOMBE LA CAPITAL ONE


w 1-2 l by Futbol2101

HATIMAYE GIROUD AFUNGA BAO, ARSENAL IKIIUA COVENTRY 6-1


Arsenal vs Coventry City by Arsenal2011Season

RADAMEL FALCAO AZIDI KUTISHA - APIGA BAO 2 ATLETICO IKIITUNGUA BETIS


ريال بيتيس 2 - 4 أتلتيكو مدريد by nike7sport

REAL MADRID WAFANYA MAUAJI - WAMPA MTU 8-0

COASTAL WASHIKA NAFASI YA PILI LIGI KUU BAADA YA KUIFUNGA KAGERA SUGAR

Siku moja baada ya aliyekuwa kocha wao mkuu Juma Mgunda kujiuzulu, klabu ya Coastal Union ya Tanga leo imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Kagera Sugar katika mechi yao ya Ligi Kuu ya Bara iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Magoli ya Coastal katika mechi hiyo yalifungwa na Daniel Hanga na Nsa Job akaongeza mengine mawili. Mpaka refa anapuliza kipenga dakika ya 90 Wagosi walikuwa wameshinda 3-2, hivyo kupanda mpaka nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu wakiwa na pointi 8, nyuma ya Simba wenye tisa baada ya kucheza mechi tatu.

Matokeo ya mechi nyingine ya Ligi Kuu ya Bara leo, Polisi Moro ilishikiliwa kwa sare ya 0-0 na Toto African ya Mwanza.

USAJILI WA MAMILIONI WA HULK NA WITSEL WACHAFUA HALI YA HEWA URUSI - RAISI PUTIN AINGILIA KATI

Raisi wa Russia Vladimir Putin ameingilia kati mjadala wa matumizi ya fedha katika soka la nyumbani la nchi hiyo, hasa kuihusu klabu tajiri ya nchi hiyo Zenit St Petersburg.

Mabingwa wa Russia Zenit wamekuwa kwenye mgogoro mkubwa wa ndani ya klabu katika siku za hivi karibuni, wachezaji wengi wakubwa wa timu hiyo hawana furaha baada ya klabu kutumia zaidi ya £100million katika usajili wa mshambuliaji wa kibrazil na Mbelgiji kiungo Alex Witsel muda mchache kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Zenit walimshusha nahodha Igor Denisov mpaka kwenye timu ya reserve jumapili  baada ya kukataa kucheza, akitoa masharti ya kufanyika kwa mazungumzo mapya juu ya mkataba wake. Mshambuliaji Alexander Kerzhakov pia nae alishushwa kwenye reserve timu kwa kukosa la ukosefu wa nidhamu.

Putin, ambaye ni mzaliwa wa St Petersburg alisema, Zenit wana msaada mkubwa kutoka kwa kampuni ya nishati ya Gazprom, ilikuwa inatumia fedha za kampuni kuliko za nchi.

"Mimi pia ninalalamika muda mwingine. Lakini ningependa kutoa ufafanuzi kwamba ni makampuni yanayonunua wachezaji na sio serikali," aliwaambia maofisa wa eneo hilo Jumanne iliyoipta.

""Lakini mashabiki wanataka kuwaona mastaa wa dunia, sio wale ambao ndio vyao vinaishia bali wale ambao sasa ndio muda wao."

Jumatano wiki hii, mkomunisti wa St Petersburg aliingilia kati suala hilo, akimwambia Putin kuiokoa klabu yaona kumbadili kocha wa sasa wa kiitaliano Luciano Spalleti kwa pamoja na msaidizi wake mmmojawpo kwenye benchi la ufundi anayetokea Korea.

"Tuna hali mbaya sana katika mji wa Zenit, na dhahiri timu ipo nje ya control, kumekuwepo na maugomvi  ndani ya klabu kati ya wachezaji juu ya nani anayelipwa fedha nyingi," Aliandika mkomunisti huyo kwenye barua ya wazi kwenda Putin.

Ni ngumu kutofautisha yupi sahihi au hayupo sahihi katika mtafuruku huu - wate wanakosa ubora wa adabu.

Mkomunisti huyo pia alidokezea pia kumsemea mbovu Kocha Luciano Spalletti ambaye ameizewesha klabu ya Zenit kumtwaa ubingwa wa Russia mara mbili mfululizo tangu awasili St Peterburg mwezi Disemba  2009, akimsema kuwa amezoea maisha ya kifahari sana..

"Zenit inahitaji mwalimu imara kutoka DPRK mahala ambapo michezo ni sehemu ya utafutaji wa maisha kila siku.

MASHABIKI NA WANACHAMA KUAMUA HATMA YA MENEJA MKUU WA SEATTLE SOUNDERS

Mashabiki wa klabu ya ligi kuu ya Marekani Seattle Sounders watapiga kura za kuamua kurefusha au kutorefusha mkataba wa meneja mkuu wa klabu yao, kitu ambacho klabu hiyo inasema itakuwa ni kura ya kwanza ya aina ya katika historia ya michezo ya Marekani.

Wanunuzi wa tiketi za msimu na wanachama wa kulipiwa, kundi la watu linalofikia watu 42,000, watakuwa na uwezo wa kupiga kura kwenye mtandao za kuamua kuendelea kumpa ajira au kumchinjia baharini  Adrian Hanauer

Hanauer alikuwa sehemu ya kundi la umiliki liloileta Sounders katika MLS mwaka 2009 huku wakitoa ahadi ya kura ya demokrasia katika kumchagua meneja mkuu.

Hii sio mara ya kwanza kwa Sounders kuwaambia mashabiki wao kupiga kura kwenye issue muhimu.

Wednesday, September 26, 2012

ALEX SONG: USAJILI MWINGINE MBOVU KWA BARCELONA - MVIVU, MZITO NA ANAYEPEWA SIFA ASIZOSTAHILI


Ukiwa ni mwanachama wa klabu ya Alex Song, inabidi uachane na mpango wa kuendelea kuisoma makala hii kwa sababu takribani maneno 700 yanayofuatia hayatokufurahisha. Ikiwa wewe ni shabiki wa Arsenal, tafadhali endelea kusoma.

Kipande cha kwanza hapo juu kinaweza kikaleta kutokueleweka kwa sababu miaka kadhaa iliyopita, Song amekuja kuwa mmoja ya wachezaji waliopendwa na mashabiki pale Emirates. Alipendwa zaidi kiasi kwamba msimu wa 2011-2012 alipigiwa kura nyingi nyuma ya Robin van Persie katika tuzo ya mchezaji bora wa msimu wa Arsenal - kura zinazopigwa na mashabiki wa klabu hiyo.

Mtandao wa Arsenal.com ulitoa hongera kwa Song: "Kwa miaka sasa, Alex amekuwa ndio msingi wa safu ya kiungo ya Arsenal, akitoa msaada mkubwa katika kuilinda safu ya ulinzi kutoka kwenye mashambulizi ya timu pinzani."
Wakati ikieleweka kwamba tovuti za vilabu mara nyingi zinakuwa zenye kutoa taarifa nzuri za wachezaji wao, lakini hili ni tofauti kwa upande mwingine. Ukweli ni kwamba Alex Song hana sifa anazopewa hasa katika kuilinda safu ya ulinzi. Katika misimu minne iliyopita, Arsenal wameruhusu mabao 170 ya kwenye ligi kuu tu. Katika kila msimu kati ya hiyo minne (kasoro 2009-10 wakati Spurs nao waliporuhusu kiasi sawa cha mabao), Arsenal wameruhusu mabao mengi kuliko timu yoyote katika Top 4 ya Premier League.

Sababu kuu juu ya suala hili sio udhaifu wa ukuta watu watano nyuma au mbinu mbovu za Wenger - au hata kama hizo nazo ni sababu lakini kubwa zaidi ni kwamba Song alishindwa kuilinda safu ya ulinzi.

Katika soka la kisasa ambapo unaweza ukawa na utegemezi kwa mabeki wa kiwango cha dunia, kui-control na kuiwezesha safu ya kiungo ndio mfumo mzuri wa ulinzi. Hii ndio maana timu zenye safu ya ulinzi ya kawaida zimeendelea kufanikiwa. Mfano mzuri ni safari ya Uholanzi mpaka kufika fainali ya World Cup 2010, ambapo Mark van Bommel na Nigel de Jong waliunda safu nzuri ya kiungo cha ulinzi kuwalinda akina Van der Wiel, Heitinga, Mathijsen na Van Bronckhorst. Song hawezi kuulinda ukuta wake kama ambavyo Van Bommel alivyokuwa akifanya. 

Song hana nidhamu ya kimchezo kiasi kuweza kupewa jukumu la mlinzi wa ngome ya timu. Wakati wachezaji wenzie wanapokuwa na kwenye kumiliki mpira, anashindwa kujizuia kujiunga na safu ya mashambulizi - hivyo mwishowe anaiacha nafasi yake na kuacha uwazi kwa wapinzani kuanzisha mashambulizi ya kushtukiza. Wakati wapinzani wanapokuwa na mpira, uwezo wake kujitambua katika kujipanga na kuusoma mchezo ni dhaifu sana. Hizi mbinu ambazo huwezi kufundishwa, aidha uwe nazo au hauna. Spidi ndogo ya Song inamzuia kutoka kwenye kurudi kutoa ulinzi kwenye safu ya ulinzi mara anapoenda kushambulia. 

Kuna michezo mingi ya kuangalia jinsi Arsenal walivyodhuriwa kutokana na kuachwa kwa mashimo mengi kwenye mipaka ya ulinzi wa Song. Mchezo ambao ulionyesha vizuri udhaifu wa Song hivi karibuni kabla hajaondoka ulikuwa kwenye ligi ya mabingwa ulaya walipofungwa 4-0 na AC Milan.

Mashabiki wa Arsenal wanaimba nyimbo za kusifia assists 14 za msimu uliopita zilizotolewa na Song kama kigezo cha ubora wake, lakini kazi kuu ya kiungo huyo pale Arsenal ilikuwa ni kulinda magoli yasiingie kwenye lango lao na sio kuyatengeneza magoli. Rogerio Ceni amefunga mabao zaidi ya 100 pale Sao Paulo, lakini hilo halimfanyi kuwa golikipa bora.

Usajili wa Song kwenda Barcelona ni wa kushangaza. Ni usajili ambao sio makini kwa staili na filosofia ya uchezaji wa Blaugrana. Sio tu kwamba Song sio mwepesi tu pia ni mzito katika kukaba wapinzani, mara nyingi amekuwa akituhumiwa kuwa mvivu pia. Hii haitavumiliwa pale Catalunya ikiwa anataka kufanikiwa.

Kijana huyo mwenye miaka 24 hafanyi movements za haraka akiwa na mpira na hivyo yupo kinyume na staili ya Barca kumiliki mpira na kupiga pasi za haraka haraka na kuupeleka mchezo kwenye goli la wapinzani. Wakati Song ni mzuri ana katika kupiga pasi kuliko Mascherano, kuna wasiwasi kwamba kama ilivyotokea kwa Muargentina, Song nae atapata wakati mgumu kuweza kuendana na pasi za haraka, fupi na za pembe tatu na wenzie akina Xavi, Iniesta, Busquets, Messi na wengine.

Mascherano alihamishwa kwenda safu ya ulinzi katika jaribio la kuwa mbadala wa wa nahodha wao anayeandamwa na majeruhi Carles Puyol - na tangu wakati huo hajaangalia nyuma. Kuna uwezekano mkubwa Song nae anaweza akawa anatumika kwenye safu ya ulinzi, lakini hili litakuwa sio jambo zuri hasa kwenye mechi kubwa kama dhidi ya Madrid, Bayern au Man City. Katika mechi zake ambazo aliwahi kucheza nyuma Song alicheza hovyo, akionekana kukosa kujiamini.

Song ameanza career yake Barcelona akitumia muda mwingi kwenye benchi na hili linaonekana litaendelea, lakini €19 millioni ni fedha nyingi kutumiwa kwa mtu ambaye humtumii ipasavyo, na Tito Vilanova - ambaye mwenyewe aliomba Song asajiliwe anajiweka katika nafasi ya kuanza kulaumiwa.

Wakati aliyemtangulia Vilanova, Pep Guardiola alifanya usajili  mbovu wa wachezaji kadhaa - Dmytro Chygynskiy kwa ada ya €25m ndio uliotia fora - ni vigumu kuamini Guardiola angeweza kufanya usajili usio na tija kama huu wa Song - mchezaji anayepewa sifa asizostahili. Sio kwa mara ya kwanza katika masuala ya uhamisho kati ya Barcelona na Arsenal, lakini kwa mara ya kwanza ni upande wa Waingereza wamepata faida kubwa safari hii.

HATIMAYE VODACOM YAZUNGUMZIA JUU YA KIPENGELE CHA 'UPEKEE' KWENYE UDHAMINI WA LIGI KUU



Vodacom yazungumzia kipengele cha Upekee (Exclusivity) katika mkataba wa
udhamini wa Ligi Kuu.

Dar es salaam 25th September 25, 2012, Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania imesema
suala la kuwepo kwa kipengele cha Upekee “EXCLUSIVITY” katika mkataba wa udhamini wa ligi kuu soka Tanzania bara kati ya kampuni hiyo na shirikisho la soka nchini - TFF ni la muhimu katika kuepuka migongano ya kimasilahi ya kibiashara miongoni mwa wadhamini.

Mkuu wa Udhamini na Mawasiliano wa kampuni ya Vodacom Tanzania Bw Kelvin Twissa amesema
kampuni ya Vodacom inajali na kuthamini maendeleo ya vilabu nchini na kwamba itaendelea kufanya hivyo kwa kutoa fursa zaidi zinazolenga kukuza kiwango cha uwekezaji katika soka kwa masilahi ya vilabu na taifa kwa ujumla.

Twissa amesema katika kutambua umuhimu wa kupanua wigo wa uwekezazi katika ligi kuu ya Vodacom na maendeleo ya vilabu kwa ujumla, kampuni ya Vodacom Tanzania ilikubali kwa moyo mkunjufu kuruhusu vilabu kutafuta wadhamini wengine ambao siyo makampuni yanayofanya baishara sawa na Vodacom.

Twissa alikuwa akizungumza katika kikao cha pamoja kilichowakutanisha Shirikisho la Soka Tanzania – TFF, Kamati ya Ligi Kuu na Mdhamini Mkuu kampuni ya Vodacom Tanzania kilichoketi jana jijini Dar es salaam.

“Tunatambua na kuheshimu utayari wa makampuni mengine ambayo yapo tayari kushirikiana na sisi katika kudhamini Ligi kuu ya Vodacom nasi tupo tayari kushirikiana nao na hivyo kuleta maendeleo ya mpira wa miguu nchini”Alisema Twissa

“Vodacom Tanzania inajivunia kuwa wadhamini wakuu wa ligi hii,tumeamua kuboresha udhamini wetu kwa sababu tunatambua umuhimu wa michezo kwa Taifa letu, sasa michezo si kwa ajili ya burudani tu bali imekuwa chanzo cha ajira na kuboresha maisha ya wanaojihusisha nayo,” Aliongeza Twissa.

“Tunaviomba vilabu vinavyoshiriki ligi kuu, vyombo vya habari na umma kwa ujumla kutambua kuwa azma ya Vodacom ni kuona mpira wa miguu unasonga mbele zaidi na ndio maana tumekuwa katika udhamni huu kwa zaidi ya miaka saba tukipitia vipindi tofauti lakini hatukuwahi kukata tamaa. Hivyo si vyema wakati huu soka yetu inapokua tukaruhusu hali inayoweza kusababisha changamoto katika uwekezaji wa soka.” Aliongeza Twisa

Twissa amesema kampuni ya Vodacom itaendelea kushirikiana na TFF, Kamati ya Ligi na wadau
wengine wote wa mpira wa miguu nchini katika kukuza uwekezaji kwa kusaidia vilabu kupata wadhamini watakaosaidia maendeleo ya vilabu hivyo.

Mwisho