Rnk | Team | MP | W | D | L | GF | GA | +/- | Pts | |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
1 | Simba SC | 13 | 8 | 4 | 1 | 21 | 8 | 13 | 28 | |
2 | Young Africans | 13 | 8 | 3 | 2 | 20 | 9 | 11 | 27 | |
3 | Azam | 13 | 6 | 5 | 2 | 12 | 5 | 7 | 23 | |
4 | JKT Oljoro | 13 | 6 | 5 | 2 | 10 | 6 | 4 | 23 | |
5 | Mtibwa Sugar | 13 | 6 | 4 | 3 | 17 | 12 | 5 | 22 | |
6 | JKT Ruvu | 13 | 3 | 8 | 2 | 15 | 14 | 1 | 17 | |
7 | Kagera Sugar | 13 | 3 | 7 | 3 | 13 | 12 | 1 | 16 | |
8 | Moro United | 13 | 3 | 5 | 5 | 18 | 23 | -5 | 14 | |
9 | African Lyon | 13 | 3 | 5 | 5 | 11 | 16 | -5 | 14 | |
10 | Toto African | 13 | 2 | 7 | 4 | 14 | 16 | -2 | 13 | |
11 | Ruvu Shooting | 13 | 2 | 7 | 4 | 11 | 13 | -2 | 13 | |
12 | Coastal Union | 13 | 3 | 2 | 8 | 11 | 18 | -7 | 11 | |
13 | Polisi Dodoma | 13 | 1 | 6 | 6 | 10 | 15 | -5 | 9 | |
14 | Villa Squad | 13 | 1 | 4 | 8 | 10 | 26 | -16 | 7 |
Mzunguko wa kwanza Ligi Kuu Tanzania Bara ulioanza kitimua vumbi Agosti 20, mwaka huu ilifika tamati katikati ya wiki, huku mabao 185 yakifungwa katika michezo 91.
Simba na Yanga zikiendelea kuonyesha ukongwe kwa kushikilia nafasi ya kwanza na ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo.
Timu hizo zinalingana mechi za kushinda, ambapo kila mmoja amezoa pointi tatu mara nane.
Simba imepoteza mmoja dhidi ya mtani Yanga na kutoka sare mitatu dhidi ya Kagera (1-1), Toto African (3-3) na Moro United (3-3).
Watani Yanga wamepoteza miwili dhidi ya JKT Ruvu (1-0) na Azam FC (1-0) na kutoka sare mitatu dhidi ya Moro United (1-1), Mtibwa Sugar (0-0) na Ruvu Shooting (1-1).
Vibonde kwenye hatua hiyo, walikuwa timu za Villa Squad na Polisi Tanzania zimeshinda mechi moja tu. Polisi ilishinda Moro United mabao 5-2 na Villa ilionja ushindi pekee dhidi ya Polisi Tanzania kwa mabao 2-1.
Washambuliaji John Boko 'Adebayor' wa Azam FC na Mghana Kenneth Asamoah wanafukuzana kwa kupachika mabao ikiwa kila mmoja ameifungia timu yake mabao nane.
Mshambuliaji Juma Semsue wa Polisi Tanzania ndiye aliyeweza kufunga mabao matatu katika mechi moja dhidi ya Moro United katika ushindi wa mabao 5-2.
Katika hatua nyingine, kadi 21 nyekundu zimetolewa na waamuzi wa ligi hiyo. Villa Squad inaongoza kwa kuwa na wachezaji wanne.
Kiungo, Emmanuel Swita ameibuka kinara wa kulimwa kadi hizo katika mechi dhidi ya Mtibwa, Polisi na Kagera .
Timu za JKT Ruvu, Mtibwa Sugar, Coastal Union na Polisi Tanzania zimeonyesha nidhamu baada ya kumaliza mzunguko bila kuwa na kadi nyekundu.
Penalti 22 zimetolewa kwenye mzunguko wa kwanza, 15 zikifungwa na zingine kuota mbawa.
Hata hivyo, Mrisho Ngassa wa Azam FC ameweka rekodi kwenye ng'we hiyo kwa kufunga bao la mapema zaidi. Alifunga bao katika sekunde ya 36 ya mchezo dhidi ya JKT Ruvu. Azam ilishinda 2-0.
Naye Abdallah Juma wa Ruvu Shooting ndiye mchezaji aliyefunga bao la kwanza msimu huu dhidi ya Kagera katika dakika ya tatu ya mchezo.
Lakini Hussein Sued wa Kagera Sugar, alijibu mapigo kwa kufunga bao la kufunga pazia hilo dhidi ya Coastal iliyolala bao 1-0.
Uwanja wa Kaitaba, Kagera umeweka historia ya kuwa wa mwisho kuchezwa mechi ya mzunguko wa kwanza.