COASTAL UNION 1:1 MTIBWA SUGAR
TOTO AFRICANS 3: 0 VILLA SQUARD
POLISI 0: 0 AFRICAN LYON
AZAM FC 1: 0 MORO UTD
Siku ya Jumatano tarehe 17, August, ilikuwa ni siku nzuri sana kwa mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania Joseph Haule a.k.a Professor Jay, baada ya timu yake ya soka anayoishabikia kuifunga timu pinzani.
Professor Jay ambaye ni mnazi na shabiki mkubwa wa Simba Sports Club, watoto wa Msimbazi, anasema alianza kuipenda Simba tangu alipopata ufahamu wa soka mpaka sasa amekuwa mpenzi mkubwa klabu hiyo ndio maana siku ya Jumatano iliyopita ilikuwa siku ya furaha baada ya Mnyama kumuumiza Yanga 2-0 katika mchezo wa Ngao ya Hisani.
“Mimi shabiki wa kutupwa wa Mnyama kiasi kwamba tukifungwa nakosa sana amani na furaha kwa siku nzima, na kama ilivyo kawaida timu ambayo sina kabisa mapenzi nayo hapa Bongo ni mtani wetu wa Jadi Yeboyebo “Dar Young African”.
“Kwa upande wa nje ya Bongo, kwanza siipendi kabisa Manchester United kwa kuwa mimi ni Liverpool damu, yaani huniambii kitu kuhusu The Reds.Huu ndio muda wetu wa kurudisha heshima yetu iliyopotea kwa kipindi kirefu, kwa sababu timu chini ya King Kenny Daglish imefanya usajili mzuri sana.Watu kama Luis Suarez, Stewart Downing, Charlie Adam na wengineo watatusaidia sana.Man U na timu nyingine wajitaarishe kwa vipigo tu msimu huu na kazi inaanzia kwa Arsenal kesho, na wengine waelekee Qibra mapema tukija tunachinja tu.
Liverpool “we will never walk alone”. – Prof.Jay
Arsene Wenger anaweza kuacha kazi ya ukocha Arsenal ikiwa mashabiki wataendelea kuwakosea adabu yeye na kikosi chake, makamu mwenyekiti wa zamani wa Gunners David Dein amesema.
Akiongea na shirika la habari la Uingereza, alionya kuwa kocha huyo mfaransa yupo njia njiapanda, huku mashabiki wakiendelea kuonyesha hasira zao juu ya Arsenal kukosa ubingwa kwa miaka 6 mfufulizo.
Dein alisema kuondoka Emirates inaweza ikawa chaguo kwa Wenger kwa sababu itafikia kipindi atasema “Imetosha”.
“Hivyo mimi ndivyo ninavyoona na ni vizuri na mashabiki wakawa na mtazamo huo, wanatakiwa atleast kumpa heshima anayostahili kwa mambo mazuri na makubwa aliyoifanyia klabu hii,
“Watu wanazungumza kuisha kwa muda wake kuwepo klabu kuisha?
“Hilo ni jambo la hatari kuzungumza kwa sababu ni rahisi kuwatimua watu kazi halafu nini kinafuata?Watu wanaongea kuhusu kununua wachezaji wapya.Sawa lakini hilo linaweza lisiwe suluhisho,
“Naelewa wasiwasi wa mashabiki , lakini Arsene Wenger amekuwa nasi kwa zaidi ya miaka 15 na kila msimu tumekuwa tukifaulu kucheza ligi ya mabingwa, ingawa mashabiki bado wana hamu ya kushinda kombe.
“Chini ya uongozi wa Arsene Wenger tumekuwa na vipindi vingi vya furaha na naamini hakuna sababu itakayotufanya tusiwe tena na furaha tuliyowahi kuwa nayo.”
Mchezaji wa kimataifa wa Kenya na klabu ya Inter Milan McDonald Mariga amewasili nchini Hispania kwa ajili ya kufanyiwa vipimo na kujiunga Real Sociedad, na anategemewa kutambulishwa leo Ijumaa baada na atapewa jezi namba 18.
Mchezaji huyo wa zamani wa Parma ameuzwa kwa mkopo na Inter lakini anaweza akasajiliwa moja kwa moja baada ya kuisha kwa muda wa mkopo mnamo June 30 mwakani.
Mariga ambaye atavaa jezi namba 18, atatambulishwa leo Ijumaa mbele ya mashabiki wa wapenzi wa klabu hiyo ya Spain.
Siku inayofuata Mariga atakuwa jijini Nairobi kujiunga na timu ya taifa ambayo itawakaribisha Guinea Bissau katika yenye ulazima wa kushinda ya michuano ya kugombea nafasi ya kushiriki African Cup of Nations
Beki wa kimataifa wa Uganda Cranes Joseph Owino amejiunga rasmi na Azam Fc kwa ada ya uhamisho wa dola za kimarekani 30,000.
Owino ambaye msimu uliopita alikuwa akiitumikia Simba Sports Club kabla ya kupata majeraha ya goti yaliyomweka nje ya uwanja kwa msimu wote uliopita na mwishowe aliachwa na Simba katika usajili wa msimu huu.
Beki huyo ambaye kwa sasa anaendelea vizuri na majeraha yake ya goti baada ya kuachwa na Simba, matajiri wa Vodacom Premier League Azam FC waliamua kumchukua na kumpeleka nchini India kwa ajili ya matibabu yaliyogharimu kiasi cha pesa kinachofikia dola 15,000 na baadae wakamsainisha mkataba wa miaka 3 wenye thamani ya $30,000.
Owino anatarajiwa kujiunga rasmi na Azam na kuanza kuitumikia klabu hiyo mwezi January mwakani wakati wa dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa.
Atletico Madrid wamefanikiwa kuwasajili wachezaji wawili kutoka Porto Rademel Falcao & Ruben Micael kwa ada ya uhamisho ya Euro million 45.
Porto wametangaza katika soko la hisa la Ureno kwamba wamekubali kumuuza mshambuliaji Rademel Falcao na kiungo Ruben Micael kwenda Atletico Madrid kwa ada ya jumla ya uhamisho ya Euro million 45.
Mabingwa wa Ureno hao waliongeza kuwa usajili wa wachezaji hao umebakiza uchukuaji wa vipimo na na wachezaji kukubaliana mahitaji binafsi na Atletico.
Ruben Micael amenunuliwa kwa 5, na Falcao amejiunga na Atletico kwa dili lenye thamani ya, lakini fedha ya usajili ya Falcao inaweza kuongezeka mpaka kufikia euro million 47 ikiwa mchezaji atafanya vizuri akiwa na timu hiyo kutoka Vicente Calderon.
Simba waliingia na mfumo wa 4-4-2 ambao ilikuwa unabadilika na kuwa 4-5-1 kuendana na movement ya mpira na wakati mwingine ilikuwa inabadilika na kuwa 4-3-3 .
Wakati ilipokuwa inabadilika na kuwa 4-3-3 Simba ilikuwa inawatumia Felix Sunzu , Emanuel Okwi na Haruna Moshi . Okwi alikuwa anashambulia kutokea kushoto Boban akishambulia kutokea kulia na Sunzu alikuwa katikati akicheza kama ‘target man’.
Safu hii ya ushambuliaji ilikuwa mwiba mchungu kwa Yanga kwani kufikia dakika 10 za mwanzo Simba walikuwa wameshabisha hodi langoni mwa Yanga mara mbili katika ‘move’ za hatari ambazo kama Salum Machaku na Amir Maftah katika nyakati tofauti wangekuwa makini basi Simba wangecheka mapema .
Washambuliaji hawa watatu walikuwa wana-link vizuri sana na viungo wao kina Jerry Santo,Patrick Mafisango na Salum Machaku huku waki-take ‘advantage’ kwa mawasiliano mabovu baina ya mabeki wa Yanga na haikushangaza kuwa kufikia dakika ya 17 Simba walikuwa wanaongoza kwa bao moja .
Kwa upande wa safu ya ulinzi ya Yanga kulikuwa na matatizo makubwa sana . Chacha Marwa na Nadir Haroub hawakuwa na mawasiliano kati yao . Mara nyingi walikuwa wanacheza pasipo kuwa na mpango wa jinsi ya kuwakabili wachezaji wa Simba .
Presha iliyokuwa inakuja upande wao ilizidi kuwachanganya na kuwalazimu kucheza rafu ambazo zilikuwa zina madhara kwao na mfano mzuri ni kwenye goli la pili ambapo Haruna Moshi alichezewa vibaya na Nadir Haroub na kusababisha penati iliyokwamishwa wavuni na Felix Sunzu .
Pembeni upande wa kulia alikokuwa Shadrack Nsajigwa kulikuwa na matatizo pia, Fusso hakuwa anapewa msaada wa kutosha na mwenzie aliyekuwa anacheza winga ya kulia Godfrey Taita hali iliyokuwa inasababisha mipira mingi ya hatari kupita upande wa kulia wa ‘defence’ ya Yanga hata goli la kwanza lilitokea huko baada Felix Sunzu kuambaa na mpira na kutoa krosi fupi iliyomalizwa na Haruna Moshi.