Search This Blog

Friday, August 19, 2011

KWANINI UDHAMINI WA LIGI KUU VODACOM VILABU HAVIHUSISHWI ?

Timu za ligi kuu Tanzania Bara mwishoni mwa juma hili zilikabidhiwa vifaa vya michezo kwa ajili ya ushiriki wa ligi hiyo ambayo inataraji kuanza hapo kesho. Mimi ni mmoja wa wadau waliokuwepo katika ghafla hiyo ambayo ilihudhuriwa na wadau wote kutoka katika timu 14 zinazoshiriki ligi hiyo.
Mambo ambayo nimeyaona kama sikosei nilimsikia Ndugu George Rwehumbiza akizungumzia vifaa ambavyo vimetolewa kwa timu zote vilikua vina thamani ya shilingi milioni 352 kama sikosei lakini siku iliyofuata ndiyo lile zoezi zima la kukabidhi vifaa lilifanyika.

Nawapongeza sana Vodacom kwa nia yao nzuri ya kuendeleza michezo na katika kipindi chote wamekua mstari wa mbele kuhakikisha soka letu linachezwa with efficiency lakini napata tatizo moja Je? Vodacom wanaingia mkataba na nani? Vilabu au Tff na kama vilabu ni muhimu ,kwa nini viongozi wa vilabu hawapewi fursa japo ya kutoa maoni mbalimbali kuhusiana na mkataba ambao wao ndio stakeholders na ndio wanaitangaza Vodacom kwenye vifua vya jezi zao?

Moja kati ya maswali yanayonisumbua ni kutaka kufahamu vile vifaa vilivyotolewa ni msaada au ni sehemu ya mkataba.

Siku ya ugawaji wa vifaa nilimsikia kiongozi mmoja wa timu ya Moro United akiuliza kwa nini viatu walivyopata Yanga,Simba,Azam,na African Lyon havifanani na viatu walivyopewa timu zingine kama Polisi, Villa,Toto na zilizosalia.

Baada ya mabishano mmoja wa wagavi wa vifaa hivyo alisema kuwa Tff walishavikagua, yote hayo tisa jezi zenyewe ukizitazama zimefanana mno na huenda kuna Baadhi ya mechi timu zikashindwa kuwa na contrast ya rangi.

Ninapozungumzia Mkataba sibahatishi na nazungumzia Vilabu kushirikishwa ni muhimu ili ikikiuka matakwa ya mkataba iweze kushitakiwa.

Ligi ya 2008/2009 tulishuhudia kampuni ya kurusha matangazo ya television GTV ikisitisha mkataba huku timu zikiwa zimeahidiwa sh milioni ishirini na sita (26 Mil shs/=) kutokana na udhamini huo lakini kwa sababu vilabu havikushirikishwa hakuna aliyeweza kulitolea jambo hili ufafanuzi

Kuna vilabu vilishuka Daraja kutoakana na athari iliyojitokeza baada mkataba huo kuvunjika kutoka na bajeti kupelea, sasa nani anayesaini mikataba kwa niaba ya vilabu?

No comments:

Post a Comment