Search This Blog

Saturday, September 15, 2012

KATIKA PICHA: Prisons 0 Yanga 0 .


 Hapa Nguvu zilikuwa sawasawa 


 Mashabiki kibao wanatazama mpira



 Mechi inaishia ishia hapa


 Na Mpira Umekwisha Shamla shamla kwa sana 
 Mashabiki kwa sana hapa wakiwa wanashangilia 
 Kocha wa Yanga haamini kama Mpira umekwisha 
 Polisi nao wapo wakihakikisha usalama 
Mwandishi wa habari akipansha tukio Live
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abas Kandoro akiongea na waandishi wa habari Mara baada ya mpira kwisha.

Tukio ndio limeishia hapa

PICHA ZOTE NA MBEYA YETU BLOG

LIVE SCORE: YANGA 0-0 TANZANIA PRISONS - SIMBA 3-0 AFRICAN LYON

Wakati refa alipopuliza kipenga cha kuashiria mwisho wa mchezo mashabiki wa Prisons waliingia uwanjani na kutaka kuleta fujo na polisi wakafanikiwa kuwatoa wachezaji wote nje ya uwanja salama.

 FULL TIME:  Prisons 0-0 Yanga
                          Simba 3-0 Africa Lyon
                          Kagera Sugar 0-1 Azam

Dakika ya 80, Tanzania Prisons 0 - 0 Young Africans
Wakati huo huo mjini Bukoba kwenye uwanja wa Kaitaba Azam wanaongoza kwa bao 1 kwa nunge mpira ni kipindi cha pili.

Dakika ya 60, Tanzania Prisons 0 - 0 Young Africans
Emmanuel Okwi anaifungia simba bao 3 kwa mkwaju wa penati. Simba 3-0 A.Lyon

Kavumbangu ametoka ameingia Hamis Kiiza 

Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza,Tanzania Prisons 0 - 0 Young Africans
Mpira ni mapumziko, Tanzania Prisons 0 - 0 Young Africans
DK 30: Yanga 0-0 Prisons

Uwanja wa taifa Dar - Emmanuel Okwi na Chollo wanaipa Simba uongozi wa 2-0 dhidi ya African Lyon -ambao wamekosa penati muda mfupi uliopita ikipigwa na Sammy Kessy.

DK 25: Mpira ume-balance na kila timu ikicheza kwa umakini kuzuia kufunga goli la mapema.

 DK: 10 - Prisons 0 - 0 Yanga

*******************************************************

1.Ally Mustafa 'Barthez' 1
2.Juma Abdul - 14
3.Oscar Joshua - 4
4.Nadir Haroub 'Cannavaro' (C) - 23
5.Kelvin Yondan - 5
6.Mbuyu Twite - 9
7.Nizar Khalfani - 7
8.Haruna Niyonzima - 8
9.Said Bahanunzi - 11

10.Didier Kavumbagu - 21
11.Stephano Mwasika - 3

Subs
1.Yaw Berko - 19
2.Shadrack Nsajigwa - 2
3.David Luhende - 29
4.Athuman Idd Chuji - 24
5.Shamte Ally - 15
6.Saimon Msuva - 27
7.Hamis Kiiza Diego - 20

Head Coach: Tom Saintfiet
Assistant Coach: Fred Felix Minziro
Goalkeeper Coach: Mfaume Athumani
Team Manager: Hafidh Saleh
Kit Manager: Mahmoud Omary 'Mpogolo'
Massagist: Jacob Onyango
Team Doctor: Dr Suphian Juma
TANZANIA PRISONS
1: Daudi Abdallah
2:  Henry Mwalungala
3: Laurian Mpalile
4: Lugano Mwangama
5: David Mwantika
6: Khalidi Fupi
7: Sino Agustino
8: Fred Chudu
9: Elias Magali
10: Peter Micheal
11: Ramadhan Katamba

MEREK HAMSIK NA WENZAKE KUTOLIPWA POSHO ZOTE ZA TIMU YA TAIFA KWA KOSA LA KWENDA DISKO WAKIWA KAMBINI

Marek Hamsik, Vladimir Weiss, Karim Guede na Miroslav Stoch hawatolipwa posho zao zamichezo yote ya kufuzu kombe la dunia watakayoichezea timu yao ya Taifa ya Slovakia kwa sababu wachezaji hao walienda disko baada ya mechi ya Ijumaa dhidi ya Lithuania. Ingawa usiku walioenda disko ulikuwa baada ya mechi, wachezaji hao bado walikuwa kwenye kambi ya timu ya taifa na ikizingatiwa Slovakia walikuwa na mchezo mwingine wa kufuzu dhidi ya Liechtenstein siku nne zilizofuatia (Slovakia walishinda 2-0)

Kutoka Football Italia:
Wachezaji wawili wa Seria A pamoja nana mchezaji wa Freiburg Karim Guede na wa Fenerbache Miroslav Stoch, waliripotiwa kwamba walitoka usiku mjini Vilnius baada ya mchezo wao wa sare ya 1-1 dhidi ya Lithuania wiki iliyopita.
Kwa mujibu wa La Republic, chama cha soka cha Slovakia waliamua kuwapa adhabu ya kutolipwa posho katika mechi zote zilizobaki za kufuzu wachezaji wote waliotoka na kwenda disko.
Kwa kawaida ya Slovakia kwa kosa kama walilofanya akina Merek - mchezaji au wachezaji huwa wanapewa adhabu ya kusimamishwa. Lakini kwanini haikuwa hivyo kwa wachezaji hao. Mmoja wa watu wa ndani wa shirikisho wanalsema - walitaka kuendelea kufanya vizuri na kupata matokeo - wachzaji watatu kati ya wanne waliopewa adhabu walianza dhidi ya Liechtenstein.

SERENGETI FIESTA YAUTIKISA MJI MKUU WA TANZANIA -DODOMA

Baadhi ya mashabiki wakishangweka vilivyo usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta usiku huu ndani ya uwanja wa Jamuhuri,Dodoma.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,mahiri katika miondoko ya miduara,IT akimrusha kimduara duara shabiki wake jukwaani usiku huu,huku shangwe za hapa na pale zikiwa zimetawala kutoka kwa watazamaji.
Wasanii mahiri wa filamu hapa nchini nao walikuwepo kuliunga mkono tamasha la Fiesta usiku huu ndani ya Dodoma,kutoka kulia ni Jacob Steven a.k.a JB,Wema Sepetu pamoja Aunt Ezekiel.
Ray Kigosi akilicheza sebene jukwaani.
Ray akimtambulisha Wema Sepetu kwa mashabiki.
Ray akiwaaga mashabiki wake mara baada ya kuwavunja mbavu mara baada ya kumaliza kulicheza sebene lake jukwaani.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mh.Dr Rehema Nchimbi akisoma jina la mshindi wa gari aina ya Vitz inayotolewa na kampuni ya Push Mobile,ikiwa ni sehemu ya mchakato wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012,pichani kati ni Meneja masoko wa kampuni ya Push Mobile,Rodney Lugambo,Muwakili shi wa michezo ya bahati nasibu ya Taifa,Bwa.Humudi pamoja na Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini,Mh Lephy Gembe. 
 Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini,Mh Lephy Gembe akiwasalimia wakazi wa Dodoma waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,kwenye uwanjawa jamuhuri.
 Pichani juu na chini Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Linah kutoka THT akitumbuiza jukwaani usiku huu wakati wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012 likiendelea usiku 
 Pichani juu na chini ni msanii anaetamba katika miondoko ya R&B hapa bongo,aitwaye Ben Paul akiwarusha wakazi wa mji wa Dodoma waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta linaleondelea usiku huu kwenye uwanja wa Jamuhuri.
 Msanii wa bongofleva aitwaye Shetta akiwaimbisha washabiki wake usiku huu.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Rich Mavoco akiwaimbisha washabiki wake kibao waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 linalofanyika usiku huu ndani ya uwanja wa Jamuhuri.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Dayna akijitokeza kwa mbwembwe jukwaani usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 linaloendelea hivi sasa kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma,ambapo wakazi wake wamejitokeza kwa wingi kuwashuhudia wasanii mbalimbali wanaotumbuiza kwenye jukwaa hilo.
 Wakazi wa mji wa Dodoma wakiwa wamejitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,ndani ya uwanja wa jamhuri mjini Dodoma.
 mmoja wa wasanii chipukizi katika anga ya muziki wa kizazi kipya,ambaye pia aliibuliwa na shindano la Serengeti Supa Nyota kutoka jijini Mwanza,aitwaye Young Killer akikamua jukwaani mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Dodoma usiku huu.
 Wasanii kutoka THT wakitumbuiza jukwaani usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
 Anaitwa Recho kwa jina la kisanii kutoka nyumba ya Vipati THT,akiimba jukwaani kwa madaha kabisa,huku umati wa watu (haupo pichani) ukishangilia kwa nguvu.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya akiwa amebebwa juu  mara baada ya kujitokeza jukwaani na wasanii waliopa  mtafu kutoka THT.
Kwa hakika wakazi wa mji wa Dodoma wamejitokeza kwa wingi usiku huu kwenye uwanja wa Jamuhuri,ambako ndiko tamasha la Serengeti Fiesta 2012 likiendelea hivi,shangwe tuu.

Friday, September 14, 2012

KUSHUKA NA KUPANDA KWA LEEDS UNITED

KUPOROMOKA KWA LEEDS

Leeds United waliwahi kuwa moja ya timu shindani kabisa katika ligi kuu ya England na UEFA Champions League (2001 -walicheza nusu fainali) japokuwa baada ya kushindwa kufuzu kucheza Champions league kwa msimu wa 2001/2002 kulimaanisha kwamba Peter Ridsdale ambaye alinunua wachezaji kama Seth Johnson na Robbie Fowler kwa ada kubwa ya uhamisho na kuwalipa mishahara mikubwa hakuweza kupata faida aliyokuwa akitegemea ili kuweza kulipa madeni. Leeds baadae wakaanza kuuza wachezaji wake tegemeo, Rio Ferdinand akaenda kwa mahasimu wao Man United kwa ada ya £30 million, uhamisho ambao ulipelekea kutimuliwa kwa kocha David O'learly na kuteuliwa kwa Terry Venables. Leeds wakaendelea tena na kuuza wachezaji wao wakiwemo Jonathan Woodgate, Lee Bowyer, Harry Kewell, Nigen Martyn, Robbie Keane & Robbie Fowler pia wakawaachia mastaa kama Oliver Dacourt & David Batty, na mwishowe Leeds United wakashuka daraja mwaka 2004 baada ya miaka 14 katika ligi kuu.
Mwaka 2005 Ken Bates aliinunua Leeds kwa £10 million na Kevin Blackwell akaiimarisha timu kwa kusajili wachezaji huru bure na kuwalipa mishahara midogo na Leeds United wakamaliza katikati mwa msimamo wa ligi daraja la kwanza, katika msimu wa 2005-2006 Leeds wakamaliza msimu wakicheza kwenye play-off na hatimaye wakafungwa katika mechi ya mwisho dhidi ya Watford. Msimu uliofuatia ukawa ndio msimu hovyo kuliko yote katika historia ya klabu hiyo ambao uliisha kwa timu hiyo kushuka tena daraja na kutokana makosa waliyokuwa wamefanya wakaanza kucheza lleague one wakiwa na pengo la pointi 15.


LIGI DARAJA LA 3 LA SOKA LA KIINGEREZA KWA LEEDS UNITED
July 3, 2007, CVA ilikuwa inaisha, jambo ambalo lingemaanisha Keb Bates angerudishiwa umiliki wote wa klabu, ingawa HM Revenue  & Custom wakapinga uamuzi huo na hili lingemaanisha kwamba Leeds ingefikia hatua ya kufilisiwa. Lakini kwa bahati nzuri HMRC wakaondoa pingamizi lao na Leeds ikaanza msimu chini ya Dennis Wise na msaidizi wake Guus Poyet - lakini muda mfupi baadae Dennis Wise akaenda Newcastle kuwa msaidizi wa Kevin Keegan January 28 na Guus Poyet kaenda kujiunga na Tottenham siku moja baadae, klabu ikamteua Gary Mcallister kuwa kocha, Mcallister akamsaini Dougie Freeman na ulikuwa usajili mzuri kwa Leeds, kwani aliwasaidia kumaliza katika nafasi za play off pamoja kuwa walikatwa pointi 15 kitu ambacho kiliwastua mashabiki, wachezaji na staff yote ya klabu hiyo! Jpokuwa klabu hiyo ilipoteza mechi yake ya mwisho dhidi ya Yorkshire Rivals -au Doncaster Rovers kwa 1-0 pamoja na kupewa nafasi kubwa ya kushinda. Mwezi wa Disemba 2007 kufuatiwa vipigo vitano mfululizo akatimuliwa na nafasi yake ikachukuliwa na Simon Grayson ambaye aliiongoza Leeds kumaliza katika nafasi ya nne.

KUPANDA TENA
Msimu wa 2009-2010 ulianza kwa Leeds kufungua msimu kwa ushindi mara 8 mfululizo chini ya Mr.Grayson baada ya kufanya usajili wa wachezaji kama Max Gradel, Patrick Kisnorbo na Richard Naylor.
Kuelekea nusu ya msimu mwezi Disemba Leeds walikuwa juu ya msimamo wakiw ana pointi 56 na kukawa na mchezo mzuri wa kuvutia na mkubwa kwa Leeds, January 3. Mashabiki 9,000 wa Leeds walisafiri  na timu mpaka Old Trafford ambapo Leeds walikuwa wakikutana na Manchester United katika raundi ya 3 ya kombe la FA. Leeds walikuwa wanaonekana hawana cha kuifanya United lakini mwisho wa mchezo matokeo yalisomeka Leeds 1-0 Man United shukrani kwa goli la kipindi cha kwanza la Jermain Beckford. Leeds then wakaenda kutoa sare na Spurs katika raundi 4 na wakasafiri mpaka White Hart Lane na kutoa sare nyingine ya 2-2, na mechi ikaenda kwenye penati na wakafungwa 3-1.

Baada ya FA Cup kiwango cha Leeds katika League one kikaporomoka na uongozi wao wa pointi ukapunguzwa japokuwa  mwishowe Leeds United waliweza kurudi katika Championship (ligi ya pili kwa ukubwa katika mfumo wa soka la kiingereza) katika siku ya mwisho baada ya kuwafunga Briston Rovers pamoja na kuwa na wachezaji 10 na goli moja nyuma kwa muda mrefu wa mchezo, mashabiki wa Leeds waliishangilia timu yao kwa moyo mpaka filimbi ya mwisho inalia matokeo yalikuwa 2-1 na Leeds wakiibuka na ushindi kwa magoli ya Jonny Howson na Beckford. Mashabikiwa Leeds waliingia uwanjani kushangilia ushindi huo  huku wakiimba Leeds inarudi.

NDANI YA CHAMPIONSHIP
Msimu wa kwanza ndani ya ligi ya championship kwa Leeds ulikuwa mzuri na baadhi ya mechi walicheza vizuri sana pale Elland Road. Mpaka kufika Christmas Leeds United walikuwa nafasi ya pili katika msimamo wa ligi na ndoto ya kurudi Premier league ikaanza kuonekana kuwa kweli. Mwezi January walisafiri mpaka uwanja wa Emirates na kuweza kupata matokeo japokuwa mechi ya pili Theo Walcott aliwaumiza na wakatoka kwenye kombe la FA.

Awamu ya pili ya msimu Leeds wakawa hawapo vizuri na hatimaye wakapoteza nafasi ya kurudi kwenye ligi kuu wakimaliza ligi katika nafasi ya 7. Msimu uliofuatia Leeds wakaanza kuuza tena wachezaji wao muhimu kama vile Bradley Johnson, Johnny Howson, Kasper Schmeichel na Max Gradel. Maandamano dhidi ya Ken Bates  baada ya mashabiki wa Leeds kuanza kuogopa kushuka kwa timu yao kama ilivyokuwa miaka kadhaa nyuma kutokana na uuzwaji wa wachezaji mastaa.

Mwezi wa pili tarehe 1, Simon Grayson akafukuzwa baada ya kufungwa 4-1 na Birmingham City na hatimaye Neil Warnock akateuliwa kuwa kocha, na akaiwezesha Leeds kumaliza katika nafasi za play-off.

NDOTO ZA KURUDI KWENYE PREMIER LEAGUE        
Simon Grayson alifanya kazi nzuri sana akiwa na Leeds na haijalishi kitu gani watu wanasema, kwani alifanikiwa kuiwezesha klabu kwenda mpaka kwenye championship na alishinda mechi kibao kubwa ikiwemo ya dhidi ya Manchester United. Japokuwa Grayson aliipeleka Leeds mpaka pale alipoweza, uteuzi wa  Neil Warnock ni mzuri sana na nafikiri Neil na Leeds waliumbwa kufanya kazi pamoja.

Neil Warnock amewasajili wachezaji kama Jason Pearce, uke Varney, Rudolph Austin, David Norris, Paul Green, Adam Drury, El-Hadji Diouf na Andy Gray. Naamini kwa usajili huu, Neil Warnock na mashabiki wenye mapenzi kaitika kila pande ya Yorkshire, Leeds United inaweza ikashindania ubingwa wa ligi hiyo cha championship au kucheza Play-offs kwa ajili kwenda Premier league mwaka huu. sababu pekee inayoweza kuwakwamisha ni ukosefu wa wachezaji wengi wenye ubora. Leeds mpaka sasa imeshapata majeruhi kibao na wanaokena kuwa wadhaifu kidogo, lakini chini ya Neil Warnock wengi ambao tulitokea kuipenda timu hii tutafurahi mwishoni mwa msimu huu, kwani Leeds United itakuwa inarudi ligi kuu ya England.

LIGI KUU TZ BARA: SIMBA VS A.LYON - YANGA KUWAKARIBISHA UPYA PRISONS LIGI KUU KESHO

Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara 2012/2013 inaanza kutimua vumbi kesho (Septemba 15 mwaka huu) ambapo timu zote 14 zitakuwa kwenye viwanja saba tofauti.
 
Mabingwa watetezi Simba wataikaribisha African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mjini Morogoro, Polisi Dodoma watakuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri wakati jijini Tanga, Mgambo JKT ambayo imepanda daraja msimu huu itaumana na Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani.
 
Tanzania Prisons ambayo nayo imerejea VPL msimu huu itaialika Yanga kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya. JKT Ruvu na Ruvu Shooting zitapambana kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam huku Azam ikiwatembelea Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Katiba.
 
Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Toto Africans dhidi ya Oljoro JKT. Mechi zote zitaanza saa 10.30 jioni.
 
Viingilio katika mechi ya Simba na African Lyon vitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani na bluu, sh. 8,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 viti vya VIP C na B wakati VIP A itakuwa sh. 20,000. Viingilio kwa mechi nyingine vitakuwa sh. 3,000 na sh. 10,000.

'MESSI NA HIGUAIN WANA TABIA ZA KIKE UWANJANI" - ZAMBRANO

Peru walilazimisha sare ya 1-1 na Argentina katika mechi yao ya kufuzu kombe la dunia usiku wa jumanne, lakini mfungaji wa goli la Peru, Carlos  Zambrano, hakuwa ameridhika na matokeo hayo. Pia alizungumzia juu ya tabia za mfungaji wa goli la Argentina. Gonzalo Higuain. Pia alitoa kijembe kwa Leo Messi kwa sababu Zambrano anadhani tabia alizonazo Messi ni za mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 23.

Beki huyo wa Eintracht Frankfurt aliuambia mtandao wa Depor.pe:

"Lionel Messi hakufanya chochote cha maana uwanjani, inawezekana alikuwa anaogopa. Tulikuwa na deni kwa mashabiki wetu na tulilipa deni hilo kwa mpira mzuri. Gonzalo Higuain na Messi  walikuwa wakilalamika kila muda na kila kitu kama wasichana  wadogo. Higuain alijaribu kunipandisha hasira kila muda lakini nilitulia na sikumpa alichotaka.

"Tulistahili kushinda, tulicheza mpira mzuri sana. Nina hasira kwa sababu tulipata pointi moja tu. Tulijua tungeweza kushinda lakini tumepoteza pointi mbili na hilo linatuuma. Waargentina walichanganyikiwa na na hawakujua namna ya kutuzuia. Hawakuweza kumiliki mpira kwa muda mrefu. Walijaribu kutukasirisha kwa kututukana. Walidhani hawawezi kuguswa, lakini hiyo sio sawa kwa sababu mpira ni kwa ajili ya wanaume"

HUU KWELI NI MKOPO AU ZUGA TU ?

KAZI NA DAWA! MUANGALIE MZEE WA VUVUZELA EVANS BUKUKU

CHEMSHA BONGO: WACHEZAJI HAWA NI AKINA NANI? WALIANZA KUCHEZA KWA PAMOJA MSIMU GANI NA KATIKA TIMU GANI?


KALI YA LEO: JAVI MARTINEZ NUSURA AITIWE 'MWIZI' BAADA YA KUTAKA KURUKA FENSI NA KUINGIA KWENYE UWANJA WA BILBAO

Imegundulika kwamba kulazimisha uhamisho kutoka Atheltic Bilbao kwenda Bayern Munich kumemtengenezea uadui mkubwa Javi Martinez na klabu yake ya zamani.

Kutokana na kufahamu kwamba tayari hana mahusiano mazuri na klabu yake ya zamani, akiwa hajawa na mawasiliano yoyote ya kibinadamu na mtu yoyote wa katika safu ya uongozi wa klabu hiyo aliyohama mwishoni mwa mwezi uliopita wakati Bayern walipofika bei ya €40 million - kwa bahati mbaya kutokana na kuondoka vibaya na kwa haraka akajikuta amesahau baadhi ya vitu vyake katika uwanja wa mazoezi wa Athletic - hivyo aliporudi Spain hivi karibuni akaamua kutumia njia yoyote ile aweze kupata mali zake.

Gazeti la Marca linaripoti: "Katika uwanja wa mazoezi wa Athletic Club de Bilbao, Ciudad Deportivo, mjini Lezama. Saa mbili asubuhi jumapili. siku ambayo mara nyingi kuna hakuna kinachoendelea uwanjani mpaka jumatatu. Mageti yamefungwa na hakuna mtu yoyote zaidi ya mlinzi ambaye muda mfupi baadae anashtuliwa na kuwasili kwa gari.

"Mlinzi yule anaiangalia gari ile akiwa kama mtu aliyeshangazwa baada ya kumuona aliyeshuka kwenye ile gari - na kwenda moja kwa moja kuruka fensi ili aweze kuingia kwenye mlango mkuu wa kuingilia ndani ya uwanja. Mlinzi yule anaenda kumzuia mtu yule akidhani ni mwizi, anamfikia na kugundua ni Javi Martinez, mchezaji wa zamani wa klabu hiyo - ambaye amehamia Bayern.

"Kiungo huyo wa kimataifa anamuomba mlinzi amfungulie mlango aende kwenye chumba cha kubadilishia nguo kwasababu anataka kuchukua vitu vyake (viatu vyake, nguo, na vitu vingine binafsi) ambavyo alishindwa kuvichukua wakati anaondoka na kukata mawasiliano na Athletic."

Javi Martinez hatimaye alifanikiwa kumbembeleza mlinzi na kuingia ndani, lakini alipofanikiwa kuingia ndani akakuta vitu vilivyokuwa kwenye droo aliyokuwa anaifadhia vitu vyake havipo! Kwa mujibu wa Marca alifanikiwa kupata baadhi tu ya viatu vyake na kuondoka huku akinung'uka.

Thursday, September 13, 2012

VAN PERSIE, HAZARD, CAZORLA, MODRIC NA WACHEZAJI WENGINE WALIOTIKISA VYOMBO VYA HABARI KATIKA DIRISHA LA USAJILI








Kipindi cha usajili ni kipindi ambacho mashabiki wa soka ulimwenguni kote huwa na presha kubwa ya kutaka makocha wa timu wanazoshabikia  zisajili wachezaji fulani au ziwaache wachezaji fulani, baada ya hapo dirisha la usajili linapofungwa mashabiki hukaa na kuanza kutafakari kilichofanywa na timu zao au kilichofanywa na timu nyingine kwenye usajil.

 Ifuatayo ni orodha ya wachezaji 10 waliosajliwa na kutengeneza vichwa vya habari kwa tetesi mbalimbali za usajili.

10. Oscar

Kabla hajasajiliwa na Chelsea kiungo huyu alihusishwa na usajili kwenye timu nyingi zikiwemo Tottenham, Ac Milan na PSG.

 Roman Abramovich aliamua kufanya biashara mapema akiwalipa Santos paundi milioni 25 kabla ya michuano ya olimpiki huku akiwaacha wachezaji wengine wakiwazingua waandishi kwa tetesi mbalimbali.

Uwezo wake ulishadhiirika kwenye michuano ya olimpiki akiichezea Brazil na anaingia kwenye kikosi cha Chelsea akiwa ana mzigo wa matarajio kwa mashabiki.

9. Shinji Kagawa 

Wakati Sir Alex Fergusson alipoonekana kwenye uwanja wa Olympic huko Ujerumani akifuatilia mchezo wa DFB Pokal kati ya Borrusia Dortmund na Bayern Munich wengi tayari walifahamu nini kinafuatia, siku tatu baada ya hapo Shinji alifichua kuwa yuko mbioni kukamilisha usajili kwenda Man United na baada ya hapo haikuwa siri tena.

Akiwa amecheza Dortmund misimu miwili huku aking'aa kwenye misimu yote Kagawa anaingia United akiwa na jukumu la kurithi nafasi inayotegemea kuachwa wazi na Paul Scholes, tofauti ya Bundesliga na EPL inaweza kuwa changamoto kubwa kwake lakini hakuna shaka juu ya ubora anayoongeza kwenye kikosi cha mashetani wekundu.

8.
Santi Cazorla
Tayari Arsenal ilishawasajili Lukas Podolski na Olivier Giroud wakiwa wanajiandaa kumkosa Robin Van Persie ambaye tangu mapema alishasema anataka kuondoka. 

Ghafla baada ya kuondoka kwa RVP, Alex Song naye akaondoka na hapo Wenger aliona haja ya kumsajili  Sani Cazorla, mchezaji ambaye matatizo ya kiuchumi ya Malaga yalifaya tetesi za usajili wake kuwa kweli .
7. Mousa Dembele.

Kila lilipotajwa jina la Luka Modric la Mousa Dembele halikuwa mbali, kama utakumbuka wakati usajili wa Modric kwenda Madrid unaonekana kuelekea kufeli Dembele alitajwa kutazamwa na Madrid kama mbadala na pale Modric alipoenda Madrid Dembele alikwenda Tottenham kuziba pengo lake akitokea Fulham masaa kadhaa kabla ya dirisha kufungwa.

6. Clinton Dempsey.

Moja ya sababu za Fulham kufanya vizuri kwenye misimu ya hivi karibuni ni jina la kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Marekani Clint Dempsey.
 Wakati kocha mpya wa Liverpool Brendan Rogers anaingia Anfield alimtaja Dempsey kama mmoja wa watu anaowahitaji, bahati mbaya paundi milioni moja iliwashinda Liverpool na ofa ya paundi milioni sita toka  kwa Tottenham ilitosha kusajili mchezaji mwingine toka Fulham baada ya Dembele.



4. Alex Song & Jordi Alba

Jordi Alba alijijengea jina kama beki wa kushoto wapili kwa ubora nyuma ya Ashley Cole na usajili wake uligubikwa na tetesi za kwenda Man United na kurudi kwenye klabu alikoanzia soka Barcelona. 

Tetesi zakwenda United zilififia haraka kama moto wa jiko la mkaa lililomaliza kupika baada ya beki huyo kusajiliwa na Barcelona akiwa mchezaji wa tatu wa Valencia kuitolea nje United ikiwa ipo tayari kutoa fedha zilizohitajika na Valencia, babu aliwahi kuchukua za uso toka kwa David Villa na David Silva pia.
Alex Song hakutengeneza vichwa vingi vya habari kwa kuwa taarifa yake kwenda Barca ilikuja ghafla na ilikuja baada ya Barca kushindwa kumsajili Javi Martinez ambaye Bilbao walikuwa wakitaka paundi milioni 40.


4
. LUKA MODRIC


Dirisha hili la majira ya joto halikuwa na vurugu za usajili zilizozoeleka nchini Hispania , unapotafakari kuwa Madrid na Barca wamesajili wachezaji watatu kati yao unaweza kushangazwa na pengine hii ni ishara kuwa vikosi vyao vimetimia na ndio maana hakuna usajili mkubwa uliofanyika.

 Moja ya tetesi ambazo karibu kila siku zilipamba vyombo vya habari ni ile ya Luka Modric, mwanzo aligoma kwenda pre-season, akagoma kufanya mazoezi lakini mwisho wake Spurs na Los Merengues Blancos walikaa kwenye meza moja na Modric akauzwa.


3. Lucas Moura.


Mwanzoni mwa dirisha la usajili magazeti ya Daily Mail, The Mirror, The Sun na mengineyo yaliripoti taarifa za United kutaka kumsajili winga kinda wa Sao Paolo Lucas Moura, baada ya hapo Clip za Youtube zinazomuonyesha dogo huyu akifanya vitu vyake ndani ya uzi wa Sao zilivunja rekodi ya kutazamwa.

Baada ya hapo mbio hizi zikawa ngumu baada ya timu nyingine kuingia, Inter Milan na Madrid walitajwa lakini tetesi zilizidi kuwapa nafasi kubwa United, baadaye mwishoni kabisa wakaingia PSG na mkwanja wa mafuta na hapo ikawa kilio kingine kwa United kwani Lucas alisajiliwa na wafaransa hao wanaofaidi fedha za kiarabu.

2. Robin Van Persie.


Babu Fergie akiwa amekula za uso kwa Jordi Alba, Lucas Moura na Eden Hazard hakuwa na jinsi zaidi ya kuhakikisha anampata RVP. 
Robin tayari alishasema kuwa anataka kuondoka kwenda mahali ambako atatwaa ubingwa. Kauli hii ilizua vita kati ya Man United na Man City huku Juventus nao wakifuatilia kwa karibu hali ilivyoendelea. Tatizo la City lilikuwa mkurugenzi Brian Marwood ambaye alikuwa akitekeleza maelekezo ya mabosi ya kutonunua hovyo na upande wa Juve kifungo cha kutokaa benchi alichokipata Antonio Conte kilimvunja moyo Van Persie na kumfanya awe na chaguo moja tu ambalo ni Man United, biashara iifanyika na RVP akavikwa jezi namba 20 yenye nembo ya Man United.

1. Eden Hazard.

Tetesi za Hazard zilianza katikati ya msimu uliopita. Mwanzoni aliwataja Tottenham kama klabu ambayo angependa kuvaa jezi zake, baada ya hapo alikaribishwa kwenye manchester derby na kisha akapewa tour ya uwanja wa Etihad, baadaye zilitoka taarifa kuwa anatafuta nyumba jijini Manchester na hapo vita ikawa ya United na City, kuelekea mwishoni mwa msimu Hazard alitoa taarifa kuwa angevaa jezi za mabingwa wa ulaya na hapa ndio Chelsea walipoingia huku United nao wakiwa mabingwa wa zamani wa ulaya wakihusishwa lakini kwa mbali.
 Mwishoni kabisa akasema atavaa jezi za blue na United wakaondoka , akaja Luis Saha kwenye twitter akitoa taarifa kuwa Hazard atasajiliwa na Chelsea, hakika tetesi za Hazard zilitawala vichwa vya habari kuliko usajili wowote ule.