Search This Blog

Friday, September 14, 2012

KUSHUKA NA KUPANDA KWA LEEDS UNITED

KUPOROMOKA KWA LEEDS

Leeds United waliwahi kuwa moja ya timu shindani kabisa katika ligi kuu ya England na UEFA Champions League (2001 -walicheza nusu fainali) japokuwa baada ya kushindwa kufuzu kucheza Champions league kwa msimu wa 2001/2002 kulimaanisha kwamba Peter Ridsdale ambaye alinunua wachezaji kama Seth Johnson na Robbie Fowler kwa ada kubwa ya uhamisho na kuwalipa mishahara mikubwa hakuweza kupata faida aliyokuwa akitegemea ili kuweza kulipa madeni. Leeds baadae wakaanza kuuza wachezaji wake tegemeo, Rio Ferdinand akaenda kwa mahasimu wao Man United kwa ada ya £30 million, uhamisho ambao ulipelekea kutimuliwa kwa kocha David O'learly na kuteuliwa kwa Terry Venables. Leeds wakaendelea tena na kuuza wachezaji wao wakiwemo Jonathan Woodgate, Lee Bowyer, Harry Kewell, Nigen Martyn, Robbie Keane & Robbie Fowler pia wakawaachia mastaa kama Oliver Dacourt & David Batty, na mwishowe Leeds United wakashuka daraja mwaka 2004 baada ya miaka 14 katika ligi kuu.
Mwaka 2005 Ken Bates aliinunua Leeds kwa £10 million na Kevin Blackwell akaiimarisha timu kwa kusajili wachezaji huru bure na kuwalipa mishahara midogo na Leeds United wakamaliza katikati mwa msimamo wa ligi daraja la kwanza, katika msimu wa 2005-2006 Leeds wakamaliza msimu wakicheza kwenye play-off na hatimaye wakafungwa katika mechi ya mwisho dhidi ya Watford. Msimu uliofuatia ukawa ndio msimu hovyo kuliko yote katika historia ya klabu hiyo ambao uliisha kwa timu hiyo kushuka tena daraja na kutokana makosa waliyokuwa wamefanya wakaanza kucheza lleague one wakiwa na pengo la pointi 15.


LIGI DARAJA LA 3 LA SOKA LA KIINGEREZA KWA LEEDS UNITED
July 3, 2007, CVA ilikuwa inaisha, jambo ambalo lingemaanisha Keb Bates angerudishiwa umiliki wote wa klabu, ingawa HM Revenue  & Custom wakapinga uamuzi huo na hili lingemaanisha kwamba Leeds ingefikia hatua ya kufilisiwa. Lakini kwa bahati nzuri HMRC wakaondoa pingamizi lao na Leeds ikaanza msimu chini ya Dennis Wise na msaidizi wake Guus Poyet - lakini muda mfupi baadae Dennis Wise akaenda Newcastle kuwa msaidizi wa Kevin Keegan January 28 na Guus Poyet kaenda kujiunga na Tottenham siku moja baadae, klabu ikamteua Gary Mcallister kuwa kocha, Mcallister akamsaini Dougie Freeman na ulikuwa usajili mzuri kwa Leeds, kwani aliwasaidia kumaliza katika nafasi za play off pamoja kuwa walikatwa pointi 15 kitu ambacho kiliwastua mashabiki, wachezaji na staff yote ya klabu hiyo! Jpokuwa klabu hiyo ilipoteza mechi yake ya mwisho dhidi ya Yorkshire Rivals -au Doncaster Rovers kwa 1-0 pamoja na kupewa nafasi kubwa ya kushinda. Mwezi wa Disemba 2007 kufuatiwa vipigo vitano mfululizo akatimuliwa na nafasi yake ikachukuliwa na Simon Grayson ambaye aliiongoza Leeds kumaliza katika nafasi ya nne.

KUPANDA TENA
Msimu wa 2009-2010 ulianza kwa Leeds kufungua msimu kwa ushindi mara 8 mfululizo chini ya Mr.Grayson baada ya kufanya usajili wa wachezaji kama Max Gradel, Patrick Kisnorbo na Richard Naylor.
Kuelekea nusu ya msimu mwezi Disemba Leeds walikuwa juu ya msimamo wakiw ana pointi 56 na kukawa na mchezo mzuri wa kuvutia na mkubwa kwa Leeds, January 3. Mashabiki 9,000 wa Leeds walisafiri  na timu mpaka Old Trafford ambapo Leeds walikuwa wakikutana na Manchester United katika raundi ya 3 ya kombe la FA. Leeds walikuwa wanaonekana hawana cha kuifanya United lakini mwisho wa mchezo matokeo yalisomeka Leeds 1-0 Man United shukrani kwa goli la kipindi cha kwanza la Jermain Beckford. Leeds then wakaenda kutoa sare na Spurs katika raundi 4 na wakasafiri mpaka White Hart Lane na kutoa sare nyingine ya 2-2, na mechi ikaenda kwenye penati na wakafungwa 3-1.

Baada ya FA Cup kiwango cha Leeds katika League one kikaporomoka na uongozi wao wa pointi ukapunguzwa japokuwa  mwishowe Leeds United waliweza kurudi katika Championship (ligi ya pili kwa ukubwa katika mfumo wa soka la kiingereza) katika siku ya mwisho baada ya kuwafunga Briston Rovers pamoja na kuwa na wachezaji 10 na goli moja nyuma kwa muda mrefu wa mchezo, mashabiki wa Leeds waliishangilia timu yao kwa moyo mpaka filimbi ya mwisho inalia matokeo yalikuwa 2-1 na Leeds wakiibuka na ushindi kwa magoli ya Jonny Howson na Beckford. Mashabikiwa Leeds waliingia uwanjani kushangilia ushindi huo  huku wakiimba Leeds inarudi.

NDANI YA CHAMPIONSHIP
Msimu wa kwanza ndani ya ligi ya championship kwa Leeds ulikuwa mzuri na baadhi ya mechi walicheza vizuri sana pale Elland Road. Mpaka kufika Christmas Leeds United walikuwa nafasi ya pili katika msimamo wa ligi na ndoto ya kurudi Premier league ikaanza kuonekana kuwa kweli. Mwezi January walisafiri mpaka uwanja wa Emirates na kuweza kupata matokeo japokuwa mechi ya pili Theo Walcott aliwaumiza na wakatoka kwenye kombe la FA.

Awamu ya pili ya msimu Leeds wakawa hawapo vizuri na hatimaye wakapoteza nafasi ya kurudi kwenye ligi kuu wakimaliza ligi katika nafasi ya 7. Msimu uliofuatia Leeds wakaanza kuuza tena wachezaji wao muhimu kama vile Bradley Johnson, Johnny Howson, Kasper Schmeichel na Max Gradel. Maandamano dhidi ya Ken Bates  baada ya mashabiki wa Leeds kuanza kuogopa kushuka kwa timu yao kama ilivyokuwa miaka kadhaa nyuma kutokana na uuzwaji wa wachezaji mastaa.

Mwezi wa pili tarehe 1, Simon Grayson akafukuzwa baada ya kufungwa 4-1 na Birmingham City na hatimaye Neil Warnock akateuliwa kuwa kocha, na akaiwezesha Leeds kumaliza katika nafasi za play-off.

NDOTO ZA KURUDI KWENYE PREMIER LEAGUE        
Simon Grayson alifanya kazi nzuri sana akiwa na Leeds na haijalishi kitu gani watu wanasema, kwani alifanikiwa kuiwezesha klabu kwenda mpaka kwenye championship na alishinda mechi kibao kubwa ikiwemo ya dhidi ya Manchester United. Japokuwa Grayson aliipeleka Leeds mpaka pale alipoweza, uteuzi wa  Neil Warnock ni mzuri sana na nafikiri Neil na Leeds waliumbwa kufanya kazi pamoja.

Neil Warnock amewasajili wachezaji kama Jason Pearce, uke Varney, Rudolph Austin, David Norris, Paul Green, Adam Drury, El-Hadji Diouf na Andy Gray. Naamini kwa usajili huu, Neil Warnock na mashabiki wenye mapenzi kaitika kila pande ya Yorkshire, Leeds United inaweza ikashindania ubingwa wa ligi hiyo cha championship au kucheza Play-offs kwa ajili kwenda Premier league mwaka huu. sababu pekee inayoweza kuwakwamisha ni ukosefu wa wachezaji wengi wenye ubora. Leeds mpaka sasa imeshapata majeruhi kibao na wanaokena kuwa wadhaifu kidogo, lakini chini ya Neil Warnock wengi ambao tulitokea kuipenda timu hii tutafurahi mwishoni mwa msimu huu, kwani Leeds United itakuwa inarudi ligi kuu ya England.

No comments:

Post a Comment