Sakata la mshambuliaji Emmanuel Okwi limeshika hatamu tena baada ya FIFA kutoa ruhusa kwa mchezaji huyo kuichezea klabu ya Yanga.
Taarifa hii imepokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki wa soka hapa nchini, kuna walioipokea kwa vifijo na nderemo na kuna wengine taarifa hii ilikuwa ni kama vile ya msiba.
Pasipo kutawaliwa na hisia za upenzi miongoni mwetu sakata hili si jepesi kama tunavyolifikiria,
Raisi wa Etoile Du Sahel, Ridha Charfeddine amefanya mahojiano maalum na mtandao huu na kuuambia kwamba wao bado wanamtambua Okwi kama mchezaji wao, Okwi alipoondoka kujiunga na timu yake ya Taifa ya Uganda mnamo mwezi mei mwaka 2013 hakurejea tena klabuni.
‘‘Mnamo May 19 mwaka 2013 shirikisho la soka nchini Uganda kupitia mtendaji wao mkuu ndugu Edgar Watson lilituma barua kwa shirikisho la soka nchini Tunisia likimuombea ruhusa Okwi ya kujiunga na kambi ya timu ya Taifa iliyokuwa inajiandaa na michezo miwili dhidi ya (Angola na Liberia) ya kufuzu kombe la dunia la mwaka 2014 nchini Brazil, michezo hiyo ilikuwa ichezwe mnamo June 8 na 15 jijini Kampala kwenye uwanja wa Mandela, baada ya michezo hiyo Okwi hakurejea tena klabuni kwetu’’.
Mr Charfeddine aliendelea kusema ya kwamba baada ya kumsubiria Okwi kwa karibia wiki nzima bila kutokea huku akipigiwa simu na meneja wa timu bila mafanikio ilibidi wamuandikie barua ya kumueleza namna utovu wake wa nidhamu utakavyomgharimu.
‘’Ilibidi tumuandikie notisi ya kumfahamisha ya kwamba akiwa kama mchezaji wa kulipwa kutokana na kutofika klabuni tangu mnamo tarehe 23/6/2013 alikuwa anavunja vipengele vya mkataba baina yake na klabu, mkataba wa Okwi na Etoile du Sahel unamalizika mnamo june 30 mwaka 2016 kwahiyo kwa kitendo chake cha kutorejea klabuni ndani muda muafaka alikuwa anavunja vipengele vya 2,8 na 16 vilivyomo kwenye mkataba baina yake na klabu.
"Baada ya hapo tulimpa muda hadi July 10 mwaka 2013 awe amerejea klabuni la sivyo tulikuwa tunalipeleka shauri lake kwenye vyombo husika vya kisheria’’.
Wao kama Etoile wana mpango gani na Okwi?
Emmanuel Okwi bado ni mchezaji wetu kwasababu tuna mkataba nae mpaka tarehe 30/06/2016 na kwasasa tumepeleka kesi yake FIFA kwa kitendo chake cha kutorejea klabuni, tunaamini FIFA watalifanyia uchunguzi suala hili na haki itapatikana.
Baada ya kufanya hayo mahojiano na Raisi wa Etoile du Sahel tumepata mawazo yafuatayo ya kuwashauri TFF na YANGA kwa ajili ya manufaa ya mchezo wa soka hasa YANGA na mchezaji husika.
1.
TFF WASIWE NA HARAKA KUTOA MAAMUZI YA KUMRUHUSU OKWI KUICHEZEA YANGA.
Naamini maamuzi ya barua ya FIFA ni kitanzi kwa TFF na YANGA, kwahiyo wanahitaji kuwa makini sana kuisoma na kuielewa kwa kina kabla ya kutoa maamuzi.
Naamini FIFA hawana tatizo na Okwi kuicheza YANGA kama atakuwa hana matatizo na klabu yake ya Etoile du Sahel.
Mapungufu makubwa ya utawala uliopita wa TFF yalikuwa ni kufanya maamuzi ya msingi kishabiki pasipo kuwapa nafasi wataalamu wenye uweledi wa jambo husika kulifanyia kazi, sasa katika hili la Okwi itakuwa jambo la busara kama wataalamu wa mambo ya kisheria watapewa nafasi ya kulifanyia kazi kwa kina ikiwa ni pamoja na kuwapatia hiyo nakala ya barua ya FIFA kuisoma neno kwa neno ili kujihakikishia kwa kilichomo kwenye barua hiyo, kwasababu kwenye FIFA Regulations on status and transfer of players .
ARTICLE 5 kwenye kipengele kidogo cha pili kinazungumzia mchezaji lazima asajiliwa na klabu moja tu (A player may only be registered with one club at a time.)
Sasa hapa imekaaje kama Etoile wanadai wana mkataba na Okwi na wakati huo huo Yanga nao wameshamsajili mchezaji huyo huyo?
Article 18 IV. MAINTENANCE OF CONTRACTUAL STABILITY BETWEEN PROFESSIONALS AND CLUBS
3. A club intending to conclude a contract with a professional must inform the
Player’s current club in writing before entering into negotiations with him. A
Professional shall only be free to conclude a contract with another club if his
Contract with his present club has expired or is due to expire within six months.
Any breach of this provision shall be subject to appropriate sanctions.
Kutokana na hicho kipengele hapo juu, najiuliza baada ya Etoile du Sahel kudai wana mkataba na Okwi, SC Villa walimuuzaje kwa mkataba wa miaka miwili Yanga? Ni klabu ipi kati ya VILLA na SAHEL iliyokuwa na haki ya kuwasiliana na YANGA kabla ya usajili wa Okwi?
Naamini kuna vipengele vingine vingi tu ambavyo vinahitaji kuangaliwa kwa jicho la kisheria na kujihakikishia kwanza, iwapo maamuzi ya kesi zilizopo FIFA yatakapotolewa basi yasije yakaiathiri YANGA na Mchezaji husika wakati tayari atakuwa ameruhusiwa kucheza.
Nawasilisha