Sakata la mshambuliaji Emmanuel Okwi limeshika hatamu tena baada ya FIFA kutoa ruhusa kwa mchezaji huyo kuichezea klabu ya Yanga.
Taarifa hii imepokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki wa soka hapa nchini, kuna walioipokea kwa vifijo na nderemo na kuna wengine taarifa hii ilikuwa ni kama vile ya msiba.
Pasipo kutawaliwa na hisia za upenzi miongoni mwetu sakata hili si jepesi kama tunavyolifikiria,
Raisi wa Etoile Du Sahel, Ridha Charfeddine amefanya mahojiano maalum na mtandao huu na kuuambia kwamba wao bado wanamtambua Okwi kama mchezaji wao, Okwi alipoondoka kujiunga na timu yake ya Taifa ya Uganda mnamo mwezi mei mwaka 2013 hakurejea tena klabuni.
‘‘Mnamo May 19 mwaka 2013 shirikisho la soka nchini Uganda kupitia mtendaji wao mkuu ndugu Edgar Watson lilituma barua kwa shirikisho la soka nchini Tunisia likimuombea ruhusa Okwi ya kujiunga na kambi ya timu ya Taifa iliyokuwa inajiandaa na michezo miwili dhidi ya (Angola na Liberia) ya kufuzu kombe la dunia la mwaka 2014 nchini Brazil, michezo hiyo ilikuwa ichezwe mnamo June 8 na 15 jijini Kampala kwenye uwanja wa Mandela, baada ya michezo hiyo Okwi hakurejea tena klabuni kwetu’’.
Mr Charfeddine aliendelea kusema ya kwamba baada ya kumsubiria Okwi kwa karibia wiki nzima bila kutokea huku akipigiwa simu na meneja wa timu bila mafanikio ilibidi wamuandikie barua ya kumueleza namna utovu wake wa nidhamu utakavyomgharimu.
‘’Ilibidi tumuandikie notisi ya kumfahamisha ya kwamba akiwa kama mchezaji wa kulipwa kutokana na kutofika klabuni tangu mnamo tarehe 23/6/2013 alikuwa anavunja vipengele vya mkataba baina yake na klabu, mkataba wa Okwi na Etoile du Sahel unamalizika mnamo june 30 mwaka 2016 kwahiyo kwa kitendo chake cha kutorejea klabuni ndani muda muafaka alikuwa anavunja vipengele vya 2,8 na 16 vilivyomo kwenye mkataba baina yake na klabu.
"Baada ya hapo tulimpa muda hadi July 10 mwaka 2013 awe amerejea klabuni la sivyo tulikuwa tunalipeleka shauri lake kwenye vyombo husika vya kisheria’’.
Wao kama Etoile wana mpango gani na Okwi?
Emmanuel Okwi bado ni mchezaji wetu kwasababu tuna mkataba nae mpaka tarehe 30/06/2016 na kwasasa tumepeleka kesi yake FIFA kwa kitendo chake cha kutorejea klabuni, tunaamini FIFA watalifanyia uchunguzi suala hili na haki itapatikana.
Baada ya kufanya hayo mahojiano na Raisi wa Etoile du Sahel tumepata mawazo yafuatayo ya kuwashauri TFF na YANGA kwa ajili ya manufaa ya mchezo wa soka hasa YANGA na mchezaji husika.
1.
TFF WASIWE NA HARAKA KUTOA MAAMUZI YA KUMRUHUSU OKWI KUICHEZEA YANGA.
Naamini maamuzi ya barua ya FIFA ni kitanzi kwa TFF na YANGA, kwahiyo wanahitaji kuwa makini sana kuisoma na kuielewa kwa kina kabla ya kutoa maamuzi.
Naamini FIFA hawana tatizo na Okwi kuicheza YANGA kama atakuwa hana matatizo na klabu yake ya Etoile du Sahel.
Mapungufu makubwa ya utawala uliopita wa TFF yalikuwa ni kufanya maamuzi ya msingi kishabiki pasipo kuwapa nafasi wataalamu wenye uweledi wa jambo husika kulifanyia kazi, sasa katika hili la Okwi itakuwa jambo la busara kama wataalamu wa mambo ya kisheria watapewa nafasi ya kulifanyia kazi kwa kina ikiwa ni pamoja na kuwapatia hiyo nakala ya barua ya FIFA kuisoma neno kwa neno ili kujihakikishia kwa kilichomo kwenye barua hiyo, kwasababu kwenye FIFA Regulations on status and transfer of players .
ARTICLE 5 kwenye kipengele kidogo cha pili kinazungumzia mchezaji lazima asajiliwa na klabu moja tu (A player may only be registered with one club at a time.)
Sasa hapa imekaaje kama Etoile wanadai wana mkataba na Okwi na wakati huo huo Yanga nao wameshamsajili mchezaji huyo huyo?
Article 18 IV. MAINTENANCE OF CONTRACTUAL STABILITY BETWEEN PROFESSIONALS AND CLUBS
3. A club intending to conclude a contract with a professional must inform the
Player’s current club in writing before entering into negotiations with him. A
Professional shall only be free to conclude a contract with another club if his
Contract with his present club has expired or is due to expire within six months.
Any breach of this provision shall be subject to appropriate sanctions.
Kutokana na hicho kipengele hapo juu, najiuliza baada ya Etoile du Sahel kudai wana mkataba na Okwi, SC Villa walimuuzaje kwa mkataba wa miaka miwili Yanga? Ni klabu ipi kati ya VILLA na SAHEL iliyokuwa na haki ya kuwasiliana na YANGA kabla ya usajili wa Okwi?
Naamini kuna vipengele vingine vingi tu ambavyo vinahitaji kuangaliwa kwa jicho la kisheria na kujihakikishia kwanza, iwapo maamuzi ya kesi zilizopo FIFA yatakapotolewa basi yasije yakaiathiri YANGA na Mchezaji husika wakati tayari atakuwa ameruhusiwa kucheza.
Nawasilisha
acha unazi na usimba ww,okwi lazma akipige yanga
ReplyDeleteIngawa hoja yako imekuea na mifano kuntu pamoja na hoja jadidi bado binfsa naona kama umejikita zaidi kutoa opinion badala ya fact! Mfano hujaeleza kwa nini FIFA wamemruhusu acheze? Kwani naamini wao ndio waamuzi wa mwisho kwa uhalai wa mchezaji.
ReplyDeletePili umeegemea sana upande wa ESS club, hadi umefikia hatua ya kufanya mohojiano na rais wa club,lakini mbona hujafanya mahojiano na Okwi ili ubalance story?
Sawa lakini tumekuelewa
Hajui hata kubalance story, anataka kuibua meeengi yasiyo na msingi. pili yeye ameengemea huko Tunisia, hawa ndio wanaotaka OKWI afie benchi
DeleteLakin kabla ya hili la jana la kuruhusiwa okwi kukipiga jangwani siku 1 nyuma c walitoa nakala tatu za barua kuhusiana na Okwi na taifa lake,sc villa na etoule du,simba na etoule pia walipomruhusu xaxa wao FIFA hawajakiona kipengele hicho cha 1 cloub
ReplyDeleteNa hizo nakala Rage amesema anazo, mbona hajazioma huyo shafii,?
DeleteNi wazo zuri mkuu na labda umeliangalia upande wa etoile peke yake..kwani mkataba unasemaje etoile ikivunja mkataba?
ReplyDeleteOkwi anasema hakulipwa pesa zake..si ni kinyume na mkataba?..au malipo sio sehemu ya mkataba wao?
As you have said..tatizo bado ni kubwa...waulize tena etoile hawakumlipa Okwi for how long and what did they expect?
Duh we jamaa ndio nimekuelewa vizuri sana kuliko wote.
Deleteyaani haulizi maswali ya msingi,,,, hata hamuonei huruma mchezaji
DeleteAwali ya yote Shafii ungejiuliza maswali madogo tu kabla ya kutumia nguvu nyingi katika mambo ambayo huna weledi nayo, tafsiri za kisheria haziji kwa mapenzi wala kwa kwa kuangalia article moja tu. Ungeweza kujiuliza tu kama ARTICLE 5 kwenye kipengele kidogo cha pili inavyosema, kuna uwezekano wa FIFA kutoa leseni 2 kwa mchezaji mmoja? Kama FIFA wameridhishwa Okwi kuchezya Yanga hii inamaana gani kwa hao jamaa zako waarabu? Au wao Au wewe Shafii unatoa leseni siku hizi? Etoile du Sahel wanawezaje kuwa na leseni nyingine ya Okwi na kudai ni mchezaji wao?
ReplyDeleteNnachokiona mm, Shafii anajisikia guilty kwa ndoto na kuongea mambo asiyo na weledi nayo, endelea kukusanya habari uchambuzi sio kazi yako maana upeo wako ni mdogo sana!
Okwi kafanye kazi bwana mdogo, haya maneno ya Shafii ni kama ya kanga za wazaramo tu!
Duh yaani umeongea point tupu, naona amepata donge nono kutoka Tunisia
DeleteNdugu yangu Shaffih usiingie kwenye huu mtego wa Mhesh. Aden Rage, kama ambavyo siku za nyuma ulikuwa humwamini. Katika barua ya FIFA kwa TFF hakuna sehemu ambayo pametajwa kuwa kuna malalamiko ya Club ya Etoile du Sahel yaliyowasilishwa FIFA, isipokuwa kilichotajwa ni madai ya Simba kwa Sahel. Hivyo nakusihi usikisemee kitu ambacho huna uhakika nacho na kujikuta umeingia kwenye mtego wa Mhesh ambaye kwa maneno hajambo. Nikinachonishangaza zaidi sasa umeanza kula matapishi yako, kama unakumbuka vizuri ulishawahi kutuwaambia kwamba umefanya mahojiano na kiongozi mmoja wa FUFA na ukatuahakikishia kwamba Okwi kimkataba na Free Agent, ikimaanisha anaweza kuingia mkataba mwingine na Club yoyote. Shaffih unachokifanya kumsaidia Mhesh kuwatia hofu TFF ata baada ya kibali cha FIFA kutoka. Hivi unataka sasa TFF wakaombe wapi ufafanuzi wa kikanuni ambao wameshaufanya kwa chombo cha mwisho FIFA. Hivi unadhani FIFA hawaruhusiwi kufafanua kanuni kwa kuwa eti zipo kwenye maandishi kila mtu anapaswa kuzielewa. siwezi kukulaumu kwani sidhani kama una taaluma ya sheria na kama unayo basi umeshindwa kuitendea haki. Shaffih, kama ni suala la kuendeleza mjadala ili kuipa umaarufu Sports Extra na Shaffih Dauda Blogspot, basi tuendelee ingawa tutakuwa hatumtendei haki Okwi kwa kumfanya ashindwe kucheza mpira! MR GEORGE
ReplyDeleteKwa kweli umenifumbua macho, unajua jana wakati katibu mkuu wa TFF anelezea barua alitaja mambo mawili ya msingi yaliyomo kwenye barua. La kwanza, nijuu ya kuruhusiwa kwa Okwi kuchezea Yanga na la pili ni ya suala la malipo ya Simba kwa SAHEL basi. Masuala ya malalamiko ya SAHEL juu ya mkataba wake na Okwi FIFA hawakuyazungumkia kabisa wakiwa na maana hawawezi kuzungumzia kitu ambacho hakipo. Hayo ya mkataba ni ya M/kiti wa Mnyama. Kungekuwa na suala la mkataba FIFA wasingesita kusema Okwi asiruhusiwe kucheza pending utatuzi wa mgogolo wa mkataba wake.
DeleteNaona hii issue ya Okwi imekuchanganya kweli, unasite vipengele ambavyo hata havibebi issue yenyewe. nakuheshimu saba shaffii ila umezidi kuwa mnazi kwenye baadhi ya issues. na kwa vile mna mic basi mnaongea hovyo hovyo na kudanganya watu. tunisia walimtoa kwa mkopo? na kibali cha muda kimeanza lini. watu na akili zao wamefanya research, wameona haina shida. Jana nimewasikia sports extra mkiwahoji rage na mwesige, sijui hao ndo wana interest na issue ya okwi kuliko yanga yenyewe. mkajificha na maestro kwenye mic mkiendesha ushabiki wenu. Mwesige anawazingua wakati wamewapelekea yanga barua ya kuanza kumtumia. mlishindwaje kuwahoji yanga. jamii inawasikiliza sana msitumie mwanya huo kuwapotosha ni dhambi sana
ReplyDeleteshafii hivi vitu vipo kisheria zaidi sasa unapopiga kelele unaonekana mtu wa ajabu fifa wanaelewa kama aliweza kucheza villa kwanini asicheze yanga acheni ushabiki na kuongea sana watu wanajua kufuatilia kila kona tulia bro
ReplyDeleteAcheni roho mbaya zenu nyie, okwi ni halali hucheza yanga as fifa wanazo kesi zote. Zingatia kwamba okwi alidai kutokulipwa mshahara wake kwa miezi mitatu na kwamujibu wa sheria za fifa kuzingatia haki na hadhi za wachezaji, mkataba baina ya timu na mchezaji utavunjiak endapo mchezaji hatalipwa mshahara kwa miezi mitatu mfululizo kama ilivyo kwa okwi a Etoe. Kilichotokea ni fifa kutoa kibali maalum cha miezi 6 ili okwi asajiliwe villa alikoomba, kibali kile ni kutokana na unwell kwamba dirisha la usajili kwenye ligi mbalimbali lilifungwa so asingeweza kusajiliwa popote ndo maana fifa walitoa kibali kile ili aweze kusajiliwa alinde kiwango chake. Ikumbukwe pia kwamba fifa hawawezi kumchagulia mchezaji timu ya kucheza so kibali cha miezi sita kililenga ukweli kwamba dirisha la usajili sehemu mbalimbali litakuwa wazi hivyo okwi kuwa huru kuchagua nchi na klabu atakayoridhika mwenyewe. Naomba kutoa hoja
ReplyDeleteThat's point nimeipenda
DeleteHayo maswali yako ulitakiwa uwaulize FIFA na siyo Yanga au TFF. KWANI HIVI SASA UHAMISHO UNAFANYIKA KIDIGITALI KUPITIA tms NA taarifa zote ziko mtandaoni hivyo aliyetoa ITC ndiye mwenye mkataba halali na mchezaji.Ilikuwaje ITC itoke FUFA wakati mchezaji ni wa Etoile du Sahel?Nafkiri huhitaji kuwa profesa kujibu swali hili na kufahamu mkataba wa Okwi na Etoile haupo na ndio maana taratibu za uhamisho zimewezekana.I wapo FIFA itabaini mkataba wa Okwi na Etoile bado uko hai baso taratibu zinazofuata zitaanzia hapo kwenda mbele na sio kurudi nyuma na litakuwa na suala la Okwi na Etoile na sio Yanga
ReplyDeleteHivi sheria inasemaje kama klabu imeshindwa kumlipa mchezaji mshahara wake???
ReplyDeleteNaona umezungumzia upande wa klabu tu na haki zake mbona hujazungumzia upande wa mchezaji na haki zake???
Nakuomba jaribu kubalance unavyozungumzia masuala kama haya kuliko kuzungumzia kuishabiki zaidi.
wewe unaandika makala yako kishabiki,FIFA ndio final decision maker sasa unaishauri TFF isifanye maamuzi wakati iliomba maelekezo FIFA,NIMEKUDHARAU
ReplyDeleteDuh, haya. Ukiangalia Mlolongo wa Kesi za Okwi kuna kitu kipo hapo, Okwi aliishtaki Etoile kwamba Hawajamlipa Mshahara kwa kipindi zaidi ya Miezi mitatu, Etoile nao wakamshitaki kama vile kujibu mapigo kuwa huyu bwana ni Mtolo.
ReplyDeleteEtoile ina mkataba wa OKWI na pia ilifanya sales agreement na Simba.
(1) Mkataba wa Simba na Etoile ulifanyika na ukawa na consideration zake ambazo Etoile imeshindwa kutimiza, so simba wanadai.
(2) Mkataba wa Okwi na Etoile nao vile vile Etoile imekiuka vipengele vya mkataba na pia umekiuka haki za binadamu kwa kutompatia mshahara kwa miezi isiyopungua mitatu. ukiangalia hapa ni hivi kuna hoja za kubishania kati ya OKwi na Etoile na hawa watu hawawezi kufanyakazi pamoja. kwa hiyo basi kiharaka tu kama Etoile hawana sababu za msingi za kumyima mshahara basi Mkataba unakufa na Okwi ni Free Agent labda kama Etoile wamlipe huo mshahara na malimbikizo yake lakini na yeye akubali kurudi kufanya kazi na Etoile basi mkataba utaendelea kuwepo. Simba ni third party haihusiki na OKWI, na kisheria Third party cannot sue the contract. Kwa hiyo Uliota Ndoto kuwa FIFA ilimuhizinisha OKWI kuchezea Simba kama sikosei. Ndio hapo ninasema fikra zako umeegemeza upande mwingine.
(3) Yanga na Villa wamekiuka taratibu za usajili au wamefanya njama toka mwanzo kumshawishio Okwi atoroke Etoile na kufanya Ujanja ujanja mpaka akatua Yanga. Hii hoja inabidi ichunguzwe kama yanga walikuwa wanamkono wao kwa Okwi kumisbehave. Lakini ukiangalia taratibu za usajili kati ya yanga na vila zilifuatwa na FIFA wameulizwa marambili na wamejibu kuwa Kesi zote ni za madai ambazo haziingiliani na taratibu za usajili.
HII HOJA NDIO NIMEKUSIKIA MUOTA NDOTO JANA KWENYE KIPINDI CHETU UKIIONGELEA NA UKIWA NA CONCLUSIVE REACTION.
MIMI NAONA TUSIENDE MBALI MPAKA TUKAJIFANYA SIE MAHAKIMU AU MAJAJI WAKATI UELEDI WA SHERIA HATUNAO. MAAMUZI YAMETOKA BASI TUSUBIRI KAMA YATATOKA MENGINE TUYAPOKEE, KAMA YANGA WATAAZIBIWA BASI HASARA KWAO NA FUNDISHO NA KAMA ETOILE NAO WATAAZIBIWA BASI NI KWAO.
TUKISISITIZA KUMKATAZA OKWI ASICHEZE TUTAKUWA HATUMTENDEI HAKI YEYE NA TUNAPINGINA NA AGIZO LILILOPO MEZANI KUWA OKWI RUKSA NA SIMBA WANADAI ETOILE. KWANI KIPENGELE NAMBA 3 KINA ASSUME KUNAMKATABA KATI YA OKWI NA ETOILE, LAKINI VILE VILE INAWEZEKANA MKATABA UMEKUFA KWA PANDE MOJA KATIKA MKATABA KUTOTIMIZA MASHARTI YA MKATABA.
NAWASILISHA KUTOKA BOKO BEACH VETERAN - UWANJA MZURI WENYE NYASI, SHAFI KARIBU NIKUTIE NJAAA KAMA KAWAIDA YANGU.
Hiki ni kizungumkuti, yaani watu wapo kwa ajili ya kujitafutia umaarufu tu, ishu imewekwa clear kuwa uhamisho hauna tatizo na madai ya vilabu hayamhusu mchezaji.
ReplyDeleteHaya mengne ni porojo tu
Hongera kwa tahadhali yako Shaffih, upo makini mdogowangu.
ReplyDeleteMtakoma mwaka huu, mwisho wa siku jamaa atacheza Yanga na nyie na vi article vyenu mtabaki na aibu tu
ReplyDeleteLakini waliomruhusu kuchezea Yanga ndio hao hao waliotunga hizo sheria na kuzitafsiri.. Ebu tusomee sheria inayoeleza kuwa endapo Club itashindwa kutekeleza makubaliano yaliyopo kwenye mkataba ni nini kinatakiwa kifanyike? Au mchezaji anatakiwa kuchukua hatua gani bwana Shaffih.?? Usiangalie upande mmoja washilingi bali unatakiwa kuangalia pande zote..!! Okwi angeishije Tunisia pasipokuwa na mshahara na stahili zake nyingine zilizomo kwenye mkataba wake na klabu..?? Angewezaje kuyaendesha maisha yake na familia yake kwa hali ya kutumika pasipo kupewa chochote.. Kumbuka pia kuwa uke ni mkataba na kuna vipengele vya kuvunja mkataba pia, na upande wowote unaohusika kwenye mkataba unaweza kuvunja mkataba kama mambo hayaendi sawa sawa...
ReplyDeleteStori imejaa jazba na mikwala kibao. Mbona hukumuuliza 'ngawira' ya Simba mbona hawajatoa?
ReplyDeleteACHENI UNAZI.
ReplyDeleteArticle 5: A player may only be registered with one club at a time - Shaffih kwani Mkataba na Usajili ni kitu kimoja.? Kanuni inasema Mchezaji anaweza kusajiliwa na timu moja tu kwa wakati. Sasa Okwi inawezekana alikuwa na mkataba na Etoile Du Sahel lakini Usajili wake Unaotambulika kwa sasa TFF, CAF na FIFA ni mchezaji wa Yanga..
ReplyDeleteArticle 18.3: Yanga pia ilifanya mawasiliano na klabu yake ya SC Villa na sio Simba, Etoile Du Sahel wala Shaffih SC.. Yanga hawajakiuka vifungu vyote ulivyovitaja.. Pole kwa uandishi wake ulioegemea upande mmoja.
Shafffi unawazo la msingi sana kuhusu swala hili la Okwi ila ngoja tuchangiye mawazokidogo, hivi nakumbuka Et'oo walishawai kumshitaki okwi fifa kwamaelezo hayo uliyopewa na huyo jamaa wa Et'oo, pili Fifa hao hao ndiyo walitoa kibali cha Okwi kucheza uganda, tatu inamaana wao Fifa hawajui kuwa Okwi alikuwaanatakiwa kucheza uganda tu au alistahili kuama? Nne, iweje leo wanajua hatakiwi kutoka uganda alaffu wanasema ni mchezaji sahihi kwa yanga? napenda kukuchauli kaka yangu mtafute Okwi muulize akuonyeshe barua yake ya breach of contract yake na Et'oo mbona Ally Salehe anazo vitu vyote hivyo, Embu jiulizeni wakati TP Mazembe walipo katiwa rufahaa na Simba kuhusu mchezaji wao je kesi yao walishinda kwanini walikuwa na vielelezo vyote, nadhani fifa wanawatu makini sana nawanajua swala la Okwi sababu lipomezani kwao sitalajii kama angekuwa astahilikucheza yanga wangemruhusu wakati wanajua anamatatizo.
ReplyDeleteTizama tu barua ya TFF waliyoandikia FiFa kuhusu kujua swala hili ilikuwa wazi kabisa yaani kama Fifa wangejuakuwa mchezaji mwenyewe anamatatizo naamini wangetoa majibu tofauti kabisa na sasa ila haya ni maoni yangu tu kaka pamoja na fikra zangu navyoona katika swala hili vitu vimeshaisha tusiendeleze tuache kuchokonea chokonoa mambo
shafih kwenye sharia kuna kitu kinaitwa "double standard" kwamba mahakama haiwezi kuwa na maamuzi mawili kwenye suala moja yaan leo inaamua hivi nakesho inaamua vingine, vivyo hivo na FIFA kama chombo cha juu cha maamuzi kuhusiana na mambo yote ya mpira dunian haiwezi kuwa na "double standards" kwenye maamuzi yake kama yenyewe ndo imeamua hivo kwa kuangalia vielelezo vyote do not expect tomorrow FIFA will come up with different decision. the issue of OKWI has finally come to an end
ReplyDeletewewe ni msemaji wa simba au muandishi wa makala za michezo? kwa uwezo duni wa kufiri kwa waandishi wengi wa habari wa TANZANIA kama wewe hususani wa siasa na michezo mnajua kuwa mnavyo fikiri ninyi ndiyo final,mnamatatizo gani lakini? hamuamini kwamba nje ya tasnia ya habari kuna watu postive zaidi ya vichwa vyenu ndo maana wengi mmekua wapiga ramli wa mechi badala ya kuwa wachambuzi.nilikua nakurespect sana bro nilichokigundua dunia inakusumbua.hebu acheni okwi afanye kazi yake ungekua msuva ningesema labda wahofia kupoteza namba lakini muhuni flan tu
ReplyDeleteShafii kaka yangu nakuheshimu sana katika kazi yako ila unataka kutuambia kuwa TFF ni chombo chenye maamuzi ya juu kuhusu FIFA? na kama hao waarabu wanahaki na Okwi si watapeleka utetezi wao baadae? Kwa sasa ameruhusiwa muache acheze Yanga kwanza,
ReplyDeleteShaffih acha kupotosha uma kwani ww na fifa nanianajua sheria za soka, elewa ww ni mwandishi watu wengi wanategemea kupata taarifa toka kwako ,usimba na uyanga utaaribu blog yako .
ReplyDeleteSababu zilizotumiwa kuchaza Villa ya Uganda ndizo hizo hizo zimetumika Yanga Kaka mgogolo upo hakuna Hatia mpaka sasa na FIFA hawawezi kumzuia wakati Okwi alishitaki hapewi mshahara Automatic Etoile du Sahel walivunja mkataba ingawa Etoile hawajakanusha hili na hawajasema kwanini walishindwa kumlipa mshahara,FIFA imeona upo ugumu hadi wapate ushahidi na maelezo ya kina kwa hiyo hawawezi kumzuia Okwi wakati hadi sasa hajawa na hatia na hata kama Okwi atashindwa kesi Haitadhuru club wa TFF kwa maana ya kuadhibiwa ila Yanga wataathirika kama atafungiwa watakuwa wamekosa huduma yake na peasa za usajili walizompa na kama Leseni kutoka CAF ipo hakuna shaka kabisa atacheza tu bila matatizo.
ReplyDeleteMwisho mashabiki na wapenzi baadhi tujaribu kuheshimu mawazo ya wengine si vema kutoa Lugha kali kwa wenzenu ninaamini Shaffih hana nia mbaya na niaamini ni mzalendo wa dhati hayo mawazo ndivyo aonavyo yeye hakuna sababu ya kumshambulia toeni hoja kama baadhi yetu pia wamefanya.
Chibura, tatizo la Shaffih ni kwamba anawafanya watanzania mburura wakati yeye ndo mburura. Hivi inakuingia akilini kama kweli huyu ni mzalendo anaanza kuingiza gossips kwa watu kwa kutumia ndoto... eti ameota? halafu watanzania tuishi na kujadili ndoto zake hizo siyo dharau kwetu? leo anasema inabidi tff na Yanga wasimtumie Okwi... eti wachunguze kwanza. Hivi watachunguza kwa nani wakati FIFA wenyewe ndo wamesema? Simba waliandika barua fifa na wakaeleza kwa nini hawataki acheze yanga, kwa maelezo ya tff ni kwamba iliandikwa kwa kiswahili na ikarudishwa ili itafsiriwe hilo limefanyika mwisho wa siku uamuzi umekuja, nini tena? Haya mawazo yake potofu si mazuri lazima yakemewe. tumeyaheshimu ndo maana tunapoteza muda kumjibu. Halafu usimtetee as if ni mzalendo la! hana uzalendo zaidi ya kutumikia watu fulani na kuleta unazi wa kipuuzi katika maisha ya watu. Huyo mchezaji hamtaki acheze? halafu mbona hasemi juu ya sheria ya fifa ya kuvunja mkataba iwapo mchezaji hajalipwa mshahara? Hata siye tunasoma mitandao ambayo yy anadanganyia watu kwamba anajua kuchambua soccer pale clouds, we all know wapi anachukua hizo info. so he is empty!!!!!!!!!!!!!
DeleteKAKA WEWE KWANZA BADO KIJANA NASHANGAA UNAFANYA KAZI YA UANDISHI,UTANGAZAJI KTK MEDIA BILA KUFUATA MIIKO YA UANDISHI ALWAYS UKO UPANDE MMOJA [ MNYAMA] KUMBUKUMBU ZANGU HATA ISSUE YA YONDANI ULIKUWA UPANDE MMOJA NA KUTAMKA KUWA LABDA MKATABA NA SIMBA ALIINGIA YONDANI MTOTO HATIMAYE AKACHEZA YANGA MPAKA LEO.KM KWELI UNAMPENDA MNYAMA KWA NINI HUKUULIZA PESA ZENU MTALIPWA LINI AU HUYO RAIS WAO NAWE KAKUMEGEA KAMISHENI? NA HILO JAMBO LA MSINGI KWA WANASIMBA WOTE.UKIENDELEA HIVYO UTAZIDI KUPOTEZA MVUTO NA TAALUMA KWAKO NA REDIO YENU ALAFU SASA UMEMUINGIZA MKUMBO HATA MBWIGA.
ReplyDeleteSHAFFII UNGEKUWA NA AKILI YA KAZI YK UNGEANZA KUULIZIA PESA ZA SIMBA THEN NDIO UULIZIE UHALALI WA OKWI KUCHEZA YANGA AU UMEKATAZWA KUULIZIA PESA YENU SIMBA?
ReplyDeleteShafii acha unazi
ReplyDeleteKatika vipindi vya michezo vy redio vinavyoboa na vimejaa unazi ni sport extra, watangazaji wake wote ni wanazi wa timu fulani ambapo na we Shaffih umo so sitegemei kama unaweza ukata na positive mind kwenye swala la OKWI, ulishakuja na doto yako feki na bla bla nyingiii sasa umeona hukufanikiwa unaanza kupiga mayowe mweh
ReplyDeletewewe shaffih kwani unataka mtaalamu gani asome neno kwa neno? naomba uache ushabiki wa kwenda hadi kufanya mahijiano na hao watunisia. Unataka kutuambia hao viongozi wako wa TFF hawana akiri au unataka ndoto yako uilazimishe iwe kweli?
ReplyDeletewewe mbona huongelei yeye kutokulipwa mshahara wake na watunisia mbona huongelei?
ReplyDeleteShaffih nilikusikia jana ulivyolishupalia swala la okwi..as if huyo mchezaji ndio kashika magoli..ya yanga... hapa norway..nilitega clouds (aka radio ya unafki)..unaongea kiunazi sio ki professional. . Mi nilifikiri utaliongelea swala kwa njia tatu..we umeliongelea kwa upande mmoja ...yaani mnatakiwa mpate dalasa mtafuteni mkufunzi wa media awaeleze jinsi ya kufanya watu waelewe topic na topic iwe ballance ili kupata uwiano sawa.....mwambie kusaga awapeleke mkapigwe msasa kidogo.......
ReplyDeleteMdau denmark
Kaka heshimu miiko ya kazi yako na heshima yako.Achana na unazi.Ushauri:Kabla hujapost habar mtandaoni jaribu kuwashirikisha wadau wenzio wa michezo ili wakushauri kwanza.Hii ishu ya leo haijabalansi ime base upande mmoja,ili habar ikamilike hoji pande zote.
ReplyDeleteshaffiii nimekudharau mbayaaaaaaa, huna lolote hata mtoto mdogo akisoma huu upuuzi ulioandika anajua umeegemea upande gani badilika kaka.....unaboa sana
ReplyDeleteNaomba Mtaalam wa sheria za usajili aingie ktk mjadala huu tujue mbivu na mbichi.
ReplyDeleteNa nyinyi Simba sc hebu sasa amkeni mwambieni Rage awatajie kiasi cha fedha alizopewa na Esperance mwaka 2011 ili akate rufaa CAF kupinga ushindi wa TP Mazembe kwa kumchezesha mchezaji asiyestahili.Vinginevyo huyu jamaa ataendelea kuwafanyeni wajinga kila siku kama hivi alivyowaingizeni mjini kwenye mauzo ya Okwi na Kapombe.Inakuwaje mtu mmoja tu anawazidini akili maelfu ya watu na elimu zenu tena wengine wabunge,mawaziri , maspika wastaafu na maprofesa?
ReplyDeleteHuyu jamaa hajielewi kabisa.FIFA siyo wajinga kiasi hicho kama wao walijua ili suala bado ni gumu wasingeweza kutoa maamuzi mapema after all inaonekana umeumizwa sana na uamuzi wa FIFA unless wewe kama mwandishi ilibidi uwaulize hao Etoile du sahel mapema sana hata kabla ya uamuzi wa fifa kama hutpendi Okwi hacheze yanga mtafutie wakala basi ampeleke nje.
ReplyDeleteKIMSINGI.....MKATABA KATI YA OKWI NA WATUNISIA ULISHAVUNJIKA PALE WALIPOSHINDWA KUMLIPA MAFAO YA MCHEZAJI...
ReplyDeleteNi ajabu kwa mtu mwelewa wa soka kama wewe (Shafii) kutoa mawazo ya kinazi kama haya,(kana) kwamba wewe una akiri na busara kuzidi watumishi wa FIFA waliopewa mamlaka ya kutoa maamuzi kama haya. Kwakuwa wewe ni mwanahabari chunguza vyema kesi mbalimbali zinazopelekwa kwenye shirikisho hilo la Dunia, isije kuwa labda FIFA wanauzoefu wa kesi kama hii alafu we ukaonekana Tutusa! Rweye.
ReplyDeletemimi nasema huyu jamaa kavurugwa kabisaa kwanza anawashauri TFF wamemuomba ushauri? kwa nni umekimbilia kupiga sm Tunisia baada ya FIFA? kwani nani karuhusu okwi kucheza yanga? FIFA au au marafiki zako unaowapigia debe? kweli kutoka moyoni mwangu nimekushusha thamani sna sna tena ufaiiiiiiiiiii
ReplyDeleteBinafsi naona mnamshambulia Shaffih bure tu,nionavyo mimi Shaffih hana kosa lolote yeye kwa mtazamo wake na uzoefu wake katika mambo ya soka ameona hivyo,sasa sisi tunaomkosoa nadhani ingebidi tumuelimishe tunavyoona sisi kwa mtazamo wetu na uzoefu wetu ili na yeye apate kuelewa pengine alioversight baadhi ya vifungu na kuelewa vinginevyo,tunapomshambulia bila ya kuwa na ushahidi kisa suala analolizungumzia tunaona kama linatuumiza na timu yetu tutakuwa tunafanya makosa, hebu tuliangalie hili suala kama anavyoliangalia yeye halafu tuone tutatoka na jibu lipi,na pia ndio tutapata mjadala bora kuliko kumshambulia mleta hoja bila ushahidi wa kutosha juu ya unazi wake,na pia Shaffih sio mnazi kwani mara nyingi nimemsikia akiwaponda Simba kwa maamuzi yao ya kinazi na kuacha kufanya mambo kwa weledi kama wanavyosema wao wenyewe na wenzake kwamba wao katika simba na yanga wao wapo kati hawataki kuegemea upande wowote huwa wanajiita tetracycline dawa ile yenye rangi mbili njano na nyekundu.
ReplyDeleteYASIN.
Kaka,,uwez kula matapishi yako,,Fifa imetoa mwongozo juu ya Okwi, Fifa ndo kila kitu,,iwez Leo wageuke maelekez yao,,Sheria haiko hvyo, alafu katika hoja yako jaribu Ku balance,, baada ya kueleza ya Tunisia, nilitegemea unipeleke Yanga or Villa ukamaliza name Mhusika Okwi,, Huu ushabiki tuweke pembeni, ujamtendea okwi hata kidogo. Una uka kiwango. 40/100%
ReplyDeletejamani mbona mnapata shida. Hamjsoma introduction yake, yeye ni miongoni mwa walio kwenye msiba. Muoneeni huruma kachanganyikiwa na msiba
ReplyDeleteLafiki zangu ambao nilisoma nao na ni Wanasheria Nguli (Hata huyu Ndumbaro - Golikipa wetu wa UD enzi hizo) walisema KAMWE USITHUBUTU KUTAFASIRI SHERIA WAKATI WEWE SI MWANASHERIA.
ReplyDeleteNARUDIA TENA SHERIA NI PANA SASA KAMA UNAWASIWASI USITOA CONCLUSIVE COMMENTS KAMA HIZO, WEKA KATIKATI KILA UPANDE THEN WAACHE WAHUSIKA WAITAFAKARI.
SEHEMU NYINGI ULIENDA CHAKA, niliwahi kusema wakati simba wanamsainisha ngasa kuwa Hakuna duniani mkataba juu ya mkataba labda iwe addendum na hii haitolewi na third party. Ukaja na hoja nyepesi mwisho chali, leo tena unang'ng'ana na existence ya contract kati ya Okwi na Etoile ambayo kimsingi Haipo kwani kuna breach of contractual terms na hivyo Okwi ni Free agent.
Nimesoma kwa bin Zuber kuwa Kapombe nae ameshtaki FC Canes, naona huyu naye itakuja kuwa kama ya Okwi, Rage anasema kapombe mali yao huku Wakala na FC canes wanasema kama simba inamtaka basi ilipe kiasi fulani cha pesa, sasa simba akitokea mjanja mjanja akawalipa hao FC canes watakata rufaa pia? hebu wadau Tujadili na hili?
inamaana unaifundisha FIFA kaz au,,,ushatuona sie wote hatuna uwezo wa kufikiria,,,FIFA sio kama uongoz wa Simba wenye record ya kukurupuka katika kufanya maamuz, kama FIFA imeruhusu Okwi achezee yanga we unazan mwenye kutafuta kasoro hiyo casy yake itasikilizwa wap si ni FIFA na hao hao ndio wametoa kibali Okwi achee Yanga...umepata jibu gan apo,,,tuliza akili au bado unaendelea kuota!
ReplyDeleteshafii bora ukalime huna ujualo zaidi ya kupotosha watu. unaharibu professional yako ya uandishi sababu ya unazi wako kwa simba. huwezi kufika mbali wewe umeniboa sana. mbona habari zipo nyingi .... unaweza kuongelea hata simba wanavyoenda kubemendwa kesho na mbeya city.
ReplyDeleteShaffi sikia Kama Okwi hana haki kucheza Yanga nakushauri fuatilia sheria za FIFA Zinasemaje iwapo timu itashindwa ama kugoma kumlipa mchezaji mshahara wa miezi 3 mfululizo hatua gani itachukuliwa kwi club husika na haki za mchezaji zitakuwaje at the same time mchezaji akiondoka kwenye club husika na akatoa taarifa yenye malalamiko ya kutolipwa mishahara yake ya miezi 3 FIFA. Nikushauri tu kwa hatua hii nani mkosaji? Hivi wewe ni mfanyakazi wa Clouds Leo hii Kusaga asikulipe mshahara wa miezi 3 mfululizo ninavyokufahamu wewe utaandika makala itafika hadi UMOJA WA MATAIFA sasa Okwi hana kisemeo kama ulivyo wewe tulitegemea ninyi waandishi ndo muwe msaada wa kupigania haki za mchezaji lakini wewe unapigania Okwi afe na njaa ili wewe na Unazi wako wa Usimba na Uyanga mkanywe bia na kufurahia mwenzenu akifa njaa ninyi mkikuna vitambi vyenu kufurahia Okwi aendelee kufa na njaa. Acha hizo Shaffi.
ReplyDeleteShaffih usiwe biased zungumzia na swala la etoile kutomlipa okwi nini adhabu kwa Club,pia tambua maisha ya Okwi yanategemea mpira unataka asicheze Yanga ili nn
ReplyDeletejana nimewasikiliza kwenye sports extra wewe shafii na maestro mnaongea vitu kishabiki wakati nyinyi ni kioo cha jamii last time mlisema yanga wameliwa mkaapia na mungu leo mmeumbuka mnaanza majungu yasiyo na msingi wowote kipindi chenu kinapoteza ladha kwa ushabiki hasa shafii na maestro ni fifi ndio waamuzi wa mwisho sasa mnasema tff wasikurupuke kumpa kibali okwi basi hao ess watakata lufaa kwaenye chombo gani kikubwa zaidi ya fifa? muheshimiwa rage ni mtu wa maneno asiwaingize kwenye kuchukiwa na watu fanyeni kazi yenu ya utangazaji sio ushabiki tutakuwa hatusikilizi kipindi chenu maan hamna habari ningine zaidi ya okwi ni ufupi wa mawazo mikoani kuna habari kibao za michezo
ReplyDelete.....Lakini labda turud kwenye sheria mkuu..
ReplyDeleteKwani sheria gani imetumika kumruhusu Okwi kucheza Villa?..na ilikuaje CAF wampitishe Okwi Yanga?..kwani status ya okwi CAF inasema yeye ni mchezaji wa wapi?..
Kama ulivyosema kua TFF iliyopita ilifanya maamuzi kishabiki(sina uhakika wewe unafahamu zaidi)..na CAF walimpitisha kwa ushabiki pia?..CAF wao ni timu gani?...
mm ni mshabiki wa Simba nimefurahshwa sana kuskia blog hii iliweza kuwacliana na moja ya viongoz wa ess sasa nachoomba chooonde chonde muwaulize pesa za usajili wa ukwi wanampango gani??hilo suala la yeye kucheza Yanga halituhusu wanasimba ila wat we need z our money
ReplyDeleteleo ndio nimegindua uwezo wako wa kufikiria ni mdogo....vitu vingine ahavihitaji hata kuwa na degree hili kujua ukweli wa mambo....FIFA ndio yenye uamuzi wa mwisho...purplex
ReplyDeleteHili ndio tatizo kubwa la waandishi wetu wa habari hapa Bongo.....Kujua kwingi, Mbwembwe kibao, Uwelewa mdogo.....Namuuliza Mkubwa Shafii...Hao FIFA waliojibu barua ya TFF kuhusu utata wa Okwi, Wana bifu gani na YANGA kiasi mpaka wajibu barua ya mtego? na lengo la FIFA kwnye jibu lao TFF ni nini? Kuiumiza YANGA siku za usoni, ili iweje? Unataka kunambia ya kwamba TFF,FUFA, CAF, FIFA...hawa wote hawazijui sheria zao zinavyosema katika masuala kama haya yanapotokea?....Ushauri wangu kwako Mr. Shafii Dauda wa Sports Extra Clouds FM....ni huu, Umeshafanya mahojiano na Raisi wa ESS, Katibu wa FUFA Edgar Watson, sasa hebu mtafute OKWI na kiongozi wa FIFA, tuwasikie nao wanasemaje juu ya hili sakata la OKWI......Kila la kheri Brother
ReplyDeleteJamani huu usimba na uyanga unaleta ugumu kwa baadhi ya watu kufanya maamuzi!mimi kinachonishangaza huyu shafi anajifanya kama hajui suala la okwi lilianzaje mpaka ikafikia hatua ya kuruhusiwa kucheza villa na sasa yanga!hao ssc alipowahoji kwanini okwi alikuwa anacheza villa wakati ni mchezaji wao walimjibu nini?pia huyo shaffih anaijua miezi gani ambayo okwi anadai hakulipwa?anajua okwi aliishitaki fifa lini kuhusu kutolipwa?anajua ess walishitaki lini fifa kuhusu utolo wa okwi?anajua fifa ilimruhusu lini okwi kucheza villa na iliangalia sababu na sheria gani?anajua kwamba katika hatua zote alizopita okwi fifa ilishirikishwa?kuanzia simba kwenda ess, ess kwenda villa na villa kwenda yanga.je kwa swali alilowauliza ess alitarajia wampe jibu gani?Sasa kama atapata majibu ya maswali hayo sidhani kama atapatwa na shida tena kwenye suala la okwi.afuate mtililiko wa matukio mkataba ni vile unavyotambulika kisheria sio tu mtu fulani akisema kuna mataba basi unakuwepo,mkataba ni wa pande zote sio wa ess peke yao,kwanini anaamini ess wakisema tuna mkataba na okwi na anashindwa kuamini okwiakisema ameuvunja?
ReplyDelete