Akizungumza jana mara baada ya kumaliza kwa kikao cha kamati tendaji cha ZFA Taifa, mjumbe wa kamati tendaji ambaye ni mwanasheria wa Zfa, Abdallah Juma, amesema kitendo cha TFF kuendelea kuwaruhusu wachezaji hao kufanya mazoezi na Timu ya Taifa ni dharau kwa ZFA ambao katika barua ya iliyoandikwa tarehe 11.12.2012 ikiwa na kumbukumbu namba Ref.ZFA/1/2012 kwenda kwa katibu mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF, ililitaka Shirikisho hilo kuwaondosha mara moja kwenye timu hiyo, mpaka pale Zfa watakapotoa taarifa nyengine.
Hata hivyo Akizungumza juzi, ofisa habari wa TFF Boniface Wambura, alisema kuwa barua hiyo haikuwataka kuwaondoa wachezaji hao kwa vile tu wamesimamishwa na sio kufungiwa.
Wachezaji ambao Zfa imetaka waondolewe katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars ni:
1. Mwadini Ali - Azam Sport Club
2. Agrey Moris - Azam Sport Club
3. Samir Haji Nuhu -Azam
Sport Club
4. Khamis Mcha - Azam
Sport Club
5. Nassor Masoud -
Simba Sport Club
6. Nadir Haruob - Young
Football Team
7. Twaha Mohamed-
Mtibwa Sport Club
8. Suleiman Kassim -
Coastal Union
9. Amir Hamad - JKT
Oljoro
10. Abdulghan Gulam -African
Lyon
Hata
hivyo kikao hicho kilichokaa jana mchana kimeshindwa kuangaza adhabu
watakazozitoa kwa wachezaji hao mpaka watakapopata baraka kutoka
Serikalini.
Wakati huo huo orodha ya wachezaji waliorejesha fedha imeongezeka na mpaka jana jumla ya wachezaji 12 wamerejesha fedha hizo.