Search This Blog

Wednesday, December 12, 2012

MWINYI KAZIMOTO KUCHUKUA NAFASI YA MRISHO NGASSA EL MERREIKH

Baada ya mchezaji Mrisho Ngassa kuingia mitini huku taarifa za kuaminika kutoka kwa vyanzo vilivyo karibu na mchezaji husika na klabu ya Yanga vikisema - Mrisho amekubali kimsingi kujiunga na mabingwa wa Afrika mashariki na kati baada ya mkopo wake utakapoisha katika klabu ya Simba, hivyo dili lake la kujiunga na El Merreikh kuota mbawa - leo hii kuna taarifa kutoka klabu ya Simba kwamba El Merreikh wameonesha nia ya kumtaka nyota Mwinyi Kazimoto kama mbadala wa Haruna Niyonzima ambaye walikuwa wakimtaka lakini ameamua kubaki kwenye klabu yake.

Akizungumza na mtandao chanzo cha habari kutoka Simba kinasema kwamba, kumefanyika mazungumzo ya mwanzo tu na El Merreikh wameonekana kuvutiwa na Mwinyi kwa kuwa walikuwa wanatafuta kiungo baada ya Niyonzima kukubali kuendelea kuichezea Yanga.

"Simba tupo tayari kumuuza Mwinyi Kazimoto kwa sababu klabu yetu inaamini katika kutoa nafasi kwa wachezaji kujiendeleza zaidi. Mazungumzo yanaendelea na kama kila kitu kikiwa sawa basi hivi karibuni Mwinyi atakuwa mchezaji mpya wa El Merreikh."

23 comments:

  1. I wish Hilo deal lifanikiwe na hiyo nafasi aipate Kazimoto akawafanyie kazi Mereikh. Suala la ngasa limeonyesha jinsi wachezaji wetu wasivyojielewa. Ni mambo ya aibu katika soka letu mchezaji unazungumza na kukubaliana na timu baadae unaingia mitini. Pole sana Ngasa unahitaji maombezi

    ReplyDelete
  2. WAMCHUKUE HUYOHUYO KAZIMOTO LAKINI WAJUE UWEZO WA NGASA NA NAFASI SIO SAWA NA KAZIMOTO LABDA CMBA WANALAZIMISHIA BIASHARA ILI WASIKOSE UCHACHE COZ KWA SASA BAADA YA KUMSAINISHA OKWI KWA MIHELA LUKUKI NA KUVUNJA MIKATABA YA WACHEZAJI WA KIGENI OVYO ACC IMEBAKI NYEUPEE. WACHEZAJI WAPEWE HAKI NA KUSIKILIZWA NA WAHESHIMIWIE KWA MATAKWA YAO WAO NDIO WAVUJA JASHO

    ReplyDelete
  3. inshalla kapige soka kk mpira ajira yako

    ReplyDelete
  4. Dah!! wachezaji wetu bado sana upeo wao mdogo sana, namuonea huruma sana Ngasa.

    ReplyDelete
  5. Kiwango Cha Mwinyi Iniesta Kazimoto Kikubwa Sana Binafsi ntaumia sana...A nastahili Timu Kubwa Sana Kama ataondoka Simba.....Binafsi Nahisi Hata Moyo Na simba utaisha

    ReplyDelete
  6. msije mkawa ninyi ndio wenye matatizo, kama wakati viongozi wanazungumzia mkataba kwa nini mchezaji hahusishwi. cha kushauri wachezaji wawe na ajenti au mwanasheria ili kusaidia upande wao na kujua masilahi yao sio kuwaburuza buruza

    ReplyDelete
    Replies
    1. inaelekea mjomba hufuatilii vyombo vya habari, inelezwa ngasa mwenyewe ndo! kaanza kuongea na mereikh, simba na azam walikuwa hawajui, unasemaje ngasa ailkuwa hahui -POLE

      Delete
  7. Ni ulimbukeni wa maisha. Ngasa kaona kashamaliza maisha , amezoea akienda billicanas na Maisha club akipapatikiwa na kina Mwajuma msinune na kina Mage Mashuzi anajiona yeye kashakuwa Messi hajui kama maisha ya mpira ni mafupi sana hususani huko bongo. mwacheni acheze mpira wa kupigana misumari na kuendeana kwa babu kila kukicha , dogo akumbuke bahati haiji kila siku.
    mdau Ughaibuni.

    ReplyDelete
  8. mwinyi usituangushe katuwakilishe

    ReplyDelete
  9. kuna mijitu mingine inatetea ujinga huwezi kumtetea ngasa kwa upumbavu huu amuangalie mwenzie Bakari Malima anauza viaz baba,hiyo ilikuwa na kwa maisha yake mwenyewe na wala cyo kwa faida ya Simba.

    ReplyDelete
  10. wachezaji wetu sijui hawajaenda hata darasa la pili? sielewi.....

    ReplyDelete
  11. Kilichosibu Ngassa ni kukataa kupima afya, achezaji wetu hawaziamini afya zao ndo maana wanagoma kwenda kupima, ki kawaida pale licha ya kupimwa vyote hata Ngoma(HIV) nayo unapimwa, hali hii inamtokea hata Okwi, anaweza pita kwenye majarobio uwanjani siku akiambiwa akapime afya anaingia mitini.

    ReplyDelete
  12. mie nathani timu zitoe mafunzo ya kujitambua kwa wachezaji wetu...kitendo cha Ngasa ni cha kutojitambua na kinaonesha utoto mwingi..

    ReplyDelete
  13. kaka mi leo nazungumzia hili suala kwa ufupi tu kama ifuatavyo:
    1. ashukuriwe sana Mungu maana yeye ndie mpaji wa vipaji vyote kwa viumbe vyake vyote vya chini ya jua na vilivyoko huko juu ya mbingu. swala la Ngassa kujifanya kapotezea linaendana na mambo mengi sana hasa ikiwemo UTOTO, UJINGA, UVIVU WA KUFIKIRI, KUTOKUJITAMBUA NA KUOTA KIBURI. nitayanyamua mambo haya kama ifuatavyo kaka;-

    UTOTO: Nikisema utoto namaanisha huyu Ngasa bado ni kinda sana, kukua na kupata kibess basi anajiona amemaliza maisha, maisha bdo sasa ktk utoto wake watu wanaojua kuwazia wengine maovu ndo hao amewapa nafasi ili wampangie nini cha kufanya.

    UJINGA: Ninaposema ujinga namaanisha kuwa huyo Ngassa ameshindwa kabisa kutofautisha maji, mkojo, na juice. ninamaanisha kwamba Ngassa ameshuindwa kukubaliana na hali kuwa katika maisha ni lazima mtu aone vitu tofauti il aweze kujifunza, yeye ameng'ang'ania sana Tanzania tuuuuuuuu, kwani haoni wenzake wa akina ULIMWENGU NA SAMATTA walivyokubali nakwenda kujifunza vingine nje ya Nchi? hajui kwamba bahati yako inaweza isiwe mahala ulipozaliwa lakini ikwa sehemu nyingine? ameshindwa kabisa kuchangaya akili aangalie maisha yake ya baadae? pesa ipo ilikuwepo na itaendelea kuwepo na tutaiacha na wengine pua wataiacha vilevile maana ndio tabia ya pesa. wakati mwingine awe makini kwamba kipaji chako ndicho kinachokupatia pesa sasa yeye huyu mtotot yukoje jamani? amenihuzunisha sana na kunitia majonzi maana angekwenda angekuwa amefua milango kwa ajili ya wachezaji wengine ila yeye ameharibu hata sifa ya wachezaji wote wa Nchi hii. TABIA HII HAIFAI KUIGWA JAMANI NI KUUA SOKA LETU NA SI VINGINEVYO VILE.

    UVIVU WA KUFIKIRI: Nikisema uvivu w akufikiri namaanisha kuwa; Ngassa mekuwa akiwapa wenigne kazi ya kumfikiria yeye na wamuamulie yeye, inamaanisha kwamba hana muda wa kufikiri ila ana mda wa kuagizwa fanya hivi na wale anao waamin wanauwezo wa kutake chance ya kufikiria katika ubongo wake. Anasikitisha sana na anahitaji zaidi msaada wa counseling maana hajiwezi hata sielewi ni binadamu wa aina gani asiyejua kufikiri na kuajiri wenigne wafikiri badala yake. Kama anaweza kufikiri mbona aliweza kuongea na timu ya sudan kule Uganda/ ilikuwaje arudi ndipo ageuke sasa? ina maana mawazo yake hayakkuwa sahihi mpaka pale alipo mtu wa kufikiri afikiri badala yake na kisha ampe majibu ndo hayo ambayo leo tumeyasikia, mara kule mara hivi hata sielewi kwanini wachezaji wetu wanafanya hivyo, hawajali vipaji vyao ila wanaangalia maslahi bila kuonesha kipaji ili na milango mingine migum ifunguke kisha wapate maslahi zaidi.

    ReplyDelete
  14. KUTOKUJITAMBUA: Ninamaanisha kuwa Ngassa AMESHINDWA kabisa kujitambua kuwa yeye sasahivi ni Mchezaji wa kiwango gani? maana yake nini? ninamaanisha ameshindwa kutofautisha wachezaji wa mpira wa mchangi, mtaani na Professional, kila anachoambiwa kwake ni sawa hajui kujithamin hajaiona thamani yake katika mpira na mchango wake kwa Taifa letu, na hajui kama wenzake walioonyuma yake wanajifunza kutoka kwake yeye hajui hilo na alilonalo yeye ni PESA KWANZA CARRIER BAADAE, sasa anawaelekeza nini wanaochipukia sasa hivi? mimi binafsi sishangai maana kabla yake kunao wachezaji wengine ambao walikuwa huko nje na hatimae wako home na wanafanya nini kiwango chao kikoje kwa sasa, hakuna ubishi kila mmoja wao AMESHUKA KIWANGO, sasa basi nifanye nini ili nijikwamue niepukane na hali hiyo yeye mawazo hayo hana, jamani tufumbe macho au tufumbue hiki kipaji kitayeyuka kama barafu juani, thamani yake ndio maisha yake maskini ngasa unatia huruma sana. alie nyuma yako na mbele yako anaekuwazia na anaekushauri hayuko tayari kukupa mafanikio unayoyataka. Utaishia kuzeekea tu hapa nyumbani bila kutambulika thamani yako mdogo wangu. nasema haya kwa sababu haiwezekani kwamba samatta na ulimwengu watarudi tena nyumbani hapa, wakuwa wakirudi tu kuchezea timu ya Taifa na kuendelea na maisha yao huku waliko, na mi naamin kwa competition ambayo wanaipat huko nje ni lazima wajishughulishe sana ili waendelee kufanya vema katika timu zao waajiri. Ngass mdogo wangu umefanya mazoea na timu za kwenu hutaki kubadili mazingira oune wenzako wanafaya nini, hutaki kujifunza kutoka kwa wengine wewe unahatari sana na zaidi ya hatari.

    KUOTA KIBURI: Nikisema kuot akiburi maana yake ni kwamba timu ambazo zinaonesha nia ya kukuchukua wewe unaona kama wanajipendekeza kwako, unaona kama vile wanakufuatafuta wakati ww tayari umeshajishibia mda mrefuuu huna njaa, pesa unayo kipaji unacho sasa yanini kwenda kupoteza muda kwa wenye njaa. ACHANA NA MAWAZO HAYO NDO MAANA HATA WENYE FEDHA ZAO BADO HAWALALI WANAENDELEA KUTAFUTA FEDHA ZAIDI NA ZAIDI, Mtoto kiburi cha pesa kidogo hicho hakijengi bali kinakubomolea

    2. kaka mimi huu ulikuwa ni mtizamo wangu finyu tu na hata hivyo maisha ni popte lkn tuangaliea kwanza nini kinasababisha nini kwa wakati gani, tukubaliane au tusikubaliane KILA JAMBO NA WAKATI WAKE. KILA LA KHERI NGASSA KTK MAAMUZIO YAKO MAADAM HAYO NI KWAJJIRI YAKUJENGA NASI VINGINEVYO VILE.
    izengo baby, mdau na mpenzi wa soka

    ReplyDelete
    Replies
    1. Naomba mdau usome comment zangu hapa chini

      Delete
  15. Naomba watanzania tuwe na mtazamo chanya kwa wachezaji wetu na timu zetu. Tusipende kulaumu kwani hio El Merrekh iliundwa ndio maana leo hii manona kama timu kubwa na yenye maendeleo ya kuvutia. Tuipende soka yetu, tuwaache wachezaji wetu waweze kulikuza soka na virabu vyetu kwani wanapojaribu tu kuchipukia na kuchukuliwa kunaziacha timu zetu katika hali mbaya na kuzifanya zisiwe na ushindani kama hizo timu mnazoziona zinafaaa wachezaji nyota kucheza na sio Tanzania. Maendeleo ya soka hayajengwi kwa kubadishabadirisha wachezaji, kila mwaka na wachezaji wapya timu nzima, utakuja kushindana na hao El Merrekh, Al Ahly, TP Mazembe, n.k.
    Big Up Tanzanian Players for Valuing your hom team, Keep it up we shall reach where we need to go.

    ReplyDelete
  16. simba endeleeni kuuza wachezaji safii sana. wakati wenzenu ktk klabu bingwa kama Mereikh, TP mazembe na wengineo wanaimalisha vikosi tayari kwa kipute nyinyi mnauza uza uza

    ReplyDelete
    Replies
    1. MDAU NADHANI UPO KARNE NYINGI NYUMA, KWANINI UMBANIE MCHEZAJI KAMA AMEPATA GREEN PASTURE? HUO NI UJINGA, SIMBA HUWEZI KUILINGANISHA NA TP MAZEMBE, TP WANA UWEZO MKUBWA SANA NA WANALIPA VIZURI KULIKO HATA BAADHI YA KLABU ZA ULAYA. TEMBEA UONE, USILINGANISHE TUI NA MAZIWA.

      Delete
    2. Unafikiri huo uwezo unakujaje, Unajengwa. TP wameijena timu kwa mda mrefu, hawauzi wachezaji kama simba.Wataishia uuza wachezaji ikifika mashindano ya champion leage, chali

      Delete
    3. huyo jamaa apo juu akili zake ndogo, nenda Tp mazembe ukanunue mchezaj kama watakuuzia ovyo kama viongz wenu wa zembe wa simba na yanga. Mfano umeona kina samata kuja tu kuchezea nchi yako wamebaniwa je kuuzwa? acha ujinga ww

      Delete
  17. Kujitambua tu, hata kama angeenda huko lakini kama hajitambui ni bure tu hata kama angeenda huko. Wangapi wameenda na wamerudi hapa hapa na hakuna cha maana walichofanya. Acha samatta aitwe samatta na ngassa awe ngassa. Ni hayo tu..

    ReplyDelete
  18. Wapo wenye hela kuliko Ngasa na bado wanavaa bukta na kuingia uwanjani kama akina Beckam,Ronaldo,Messi,Etoo,Y.Toure
    Lakini Ngasa na mimi hata sijui wanosema anajua mpira.Hana sifa ya kucheza timu kubwa,hata huko Elmerek nina uhakika angechemsha tu. Hana umbo la kuwa mchezaji wa mpira. Kwa hiyo acheni ajiue mwenyewe.Bahati haiji mara2. Unaleta mchezo na Bongio! Utafulia mpaka utafute pa kuficha uso wako

    ReplyDelete