Search This Blog
Saturday, December 31, 2011
Friday, December 30, 2011
KIPRE AIONGOZA AZAM KUIUA JKT RUVU CHAMAZI
Kiungo Michael Bolou Kipre wa Azam FC ameiongoza timu yake kupata ushindi wa 3-0 dhidi ya JKT Ruvu katika mchezo wa kirafiki uliochezwa leo jioni kwenye uwanja wa Azam Chamazi.
Azam FC imepata ushindi huo wa pili mfulilizo katika mechi zake za maandalizi ya ligi kuu na michuano ya Kombe la Mapinduzi, Azam waliifunga Yanga 2-0 kwenye mchezo wake wa kwanza wa kirafiki,
Kipre alikuwa wa kwanza kufungua kalamu hiyo ya magoli katika dakika ya 26 na dakika sita baadaye Khamis Mcha aliifungia klabu hiyo goli la pili na kupeleka timu mapumziko Azam wakiwa mbele kwa 2-0.
Katika mchezo huo uliozikutanishi timu zote zinazocheza ligi kuu ya Vodacom, JKT Ruvu walicheza katika kiwango kizuri na kufanya mchezo kuwa wa kiushindani japo walikuwa nyuma kwa idadi hiyo ya magoli.
Kiungo JKT ruvu kilikuwa chini ya mchezaji Mohamed Banka akishirikiana na wachezaji wengine wa timu hiyo huku Azam FC kulikuwa na Abdi Kassim, Mcha, Salum Aboubakar ‘Sure Boy’ na Kipre walioweza kuichezesha timu hiyo katika kipindi chote cha kwanza.
Kipindi cha pili timu zote ziliongeza kasi na kufanya mabadiliko Azam FC walitoka golikipa Mwadini Ally, Agrey Moris, Waziri Salum, Abdulhalim Humud, Abdi, Kipre na Gaudence Mwaikimba wakaingia golikipa chipukizi Aishi Mfula aliyechukua vyema nafasi hiyo katika dakika ya 72, Luckson Kakolaki, Samir Haji, Abdulghan Gulam, Himid Mao, Zahor Pazi na John Bocco.
Mabadiliko hayo yaliongeza nguvu kwa Azam na kupelekea dakika ya 78 Mcha kupachika goli la tatu baada ya kipa wa JKT Ruvu Amani Simba kupangua shuti la Bocco na mpira huo kumkuta mcha aliyeupeleka wavuni na kumaliza mchezo kwa Azam kupata ushindi huo wa 3-0.
Kocha msaidizi wa Azam, Kali Ongalah amesema ushindi wa mchezo huo ni maandalizi mazuri kwa ajili ya mechi zijazo.
“Tumeshinda huu mchezo wa pili, hatujaruhusu hata goli moja hivyo upande wa ulinzi inaonyesha tupo vizuri na tukiendelea hivi tutafikia malengo yetu” alisema Kali.
Azam FC itaondoka Dar es Salaam siku ya Jumapili kuelekea Zanzibar kwa ajili ya michuano ya Mapinduzi, watacheza mechi ya kwanza siku ya Jumatatu dhidi ya Kikwajuni FC mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa Amaan.
FERGUSON: NITAMPA MWAKA MMOJA ZAIDI BERBATOV
Finally, Manchester United manager Sir Alex Ferguson amesema klabu hiyo itamuongezea mkataba wa mwaka mmoja Dimitar Berbatov utakaomuweka Mbulgaria Old Trafford hadi mwaka 2003.
Ferguson amesema ofa ya mkataba mpya kwa Berba itatolewa mapema mwezi Machi, tarehe ya mapema zaidi that his contract cabn be renewed.
The 30-year old striker alijiunga na United kutoka Tottenham on 2008 kwa ada iliyovunja rekodi ya £30million na amefunga magoli 53 katika mechi 142 alizoitumikia United.
Barbatov amekuwa akikosa nafasi za mara kwa mara kupangwa katika kikosi cha kwanza cha United, lakini hivi karibuni alirudi na kufunga magoli manne katika mechi 2 including a hat trick @Old Trafford dhidi ya Wigan Jumatatu iiyopita.
GARY CAHIL NJIANI KUELEKEA DARAJANI KUUNDA UKUTA NA TERRY
Owen Coyle amethibitisha Bolton wamekubali kumuuza Gary Cahil kwenda Chelsea.
The England defender, ambaye anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu, anatarajiwa kujiunga na Chelsea kwa ada ya inayotajwa kufikia £7million.
Manager Andre Villas Boas amekuwa katika harakati kuimarisha safu yake ya ulinzi baada ya kumwambia Alec anaweza kutafuta klabu nyingine ya kuitumikia.
Akiongea juu ya mchezo unaofutia dhidi ya Wolves, Coyle alisema: “Hali ilivyo ndani ya klabu kwa sasa, Bolton Wanderers na Chelsea wameshakubaliana juu ya ada ya Gary Cahil.
“Sasa ni juu ya wawikilishi wa Gary kuongea na Chelsea. Nimeshaongea na Gary na kumwambia aendelee ku-focus kucheza soka akiwa bado mchezaji wa Bolton mambo yake ya usajili awaachie wawikilishi wake.
Cahil ambaye alijiunga na Bolton in 2008 kutoka Aston Villa, ikiwa atafanikiwa kujiunga na Chelsea atakwenda kuuunda ukuta imara kwa pamoja na mchezaji mwenzie wa timu ya taifa ya England John Terry, ambaye kwapamoja wameonekana kucheza vizuri kwa pamoja ndani ya kikosi cha Three Lions.
MABAO BORA 20 YA THIERRY HENRY.
19. Henry Touch and Volley vs. Chelsea
18. Showing Some Patience vs. Inter
17. Chipped Penalty vs. Newcastle
16. Thierry Henry vs. West Ham
15. Volley vs. Charlton
14. Free Kick vs. Middlesbrough
13. Header vs. Manchester United
12. Control and Volley vs. Manchester City
11. Venemous Strike vs. Manchester City
10. Free Kick vs. Manchester United
9. Back-Heel vs. Charlton
8. Long Range Strike vs. Manchester United
7. Free Kick vs. Charlton
6. Strong Run vs. Real Madrid
5. Outside the Foot vs. Sparta Prague
4. Record-Breaking Goal vs. Sparta Prague
3. Thierry Henry vs. Tottenham
2. Thierry Henry vs. Liverpool
1. Thierry Henry vs. Manchester United
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars) inaendelea na mazoezi jijini Dar es Salaam chini ya Kocha Mkuu Charles Boniface Mkwasa kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Namibia baadaye mwezi ujao. Mechi hiyo ya kwanza itachezwa ugenini Januari 14 mwakani jijini Windhoek. Timu hiyo ambayo sasa inafanya mazoezi kwa wachezaji kutokea majumbani (off camp) inatarajia kuingia kambini Januari Mosi mwakani. Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linahitaji zaidi ya sh. milioni 50 ikiwa ni gharama za safari, kambi na posho kwa wachezaji na benchi la ufundi kwa ajili ya mechi hiyo moja tu. Mechi ya marudiano itachezwa Januari 29 mwakani Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Tunatoa mwito kwa wadau mbalimbali zikiwemo taasisi, kampuni na watu binafsi kusaidia ushiriki wa Twiga Stars kwenye mechi hiyo na michuano hiyo kwa ujumla. Twiga Stars kama ilivyo kwa timu nyingine za Taifa ukiondoa Taifa Stars bado haina mdhamini.
WAAMUZI 14 WAPATA BEJI ZA FIFA
Waamuzi 14 wakiwemo wawili wapya wamefanikiwa kupata beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa mwaka 2012 baada ya kufaulu mtihani wa waamuzi uliofanyika mwaka huu na kusimamiwa na shirikisho hilo. Ferdinand Chacha na Ali Kinduli ambao ni waamuzi wasaidizi ndiyo wapya katika jopo hilo la waamuzi wa FIFA kwa Tanzania. Waamuzi wa kati waliopata tena beji hizo ni Ramadhan Ibada, Orden Mbaga, Israel Mujuni na Sheha Waziri. Mbali ya Chacha na Kinduli, waamuzi wengine wasaidizi kwa upande wa wanaume ni Josephat Bulali, Hamis Changwalu, Erasmo Clemence, Khamis Maswa na Samuel Mpenzu. Kwa upande wa wanawake, mwamuzi wa kati ni Judith Gamba wakati wasaidizi ni Mwanahija Makame na Saada Tibabimale. Mwamuzi pekee wa FIFA 2011 ambaye jina lake halikurudi ni John Kanyenye ambaye alikuwa mwamuzi msaidizi.
TAIFA STARS, DRC KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI
Timu ya Taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) imeomba kucheza mechi moja ya kirafiki na timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars). Mechi hiyo itafanyika Februari 23 mwakani kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. DRC inatarajia kuwasili nchini Februari 18 mwaka huu ambapo itaweka kambi yake ya mazoezi hadi Februari 25 mwaka huu kujiandaa kwa mechi yao ya mchujo ya Kombe la Afrika (CAN) dhidi ya Mauritius. Mechi ya DRC na Mauritius itachezwa Februari 29 mwakani nchini Mauritius. Stars yenyewe itacheza mechi ya kwanza ya mchujo kwa ajili ya fainali hizo za 2012 zitakazofanyika Afrika Kusini dhidi ya Msumbiji. Mechi hiyo itachezwa Februari 29 mwakani Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
13 WASHIRIKI KOZI YA UKAMISHNA
Kozi ya siku mbili ya ukamishna iliyomalizika Desemba 29 mwaka huu imeshirikisha washiriki 13 chini ya ukufunzi wa Stanley Lugenge, Leslie Liunda na Sunday Kayuni. Walioshiriki kozi hiyo ni Abdallah Zungo, Ally Mkomwa, Ally Mozi, Army Sentimea, Awadi Nchimbi, Beatus Manga, Christopher Mpangala, Hakim Byemba, Josephat Magazi, Juma Mgunda, Juma Mpuya, Mugisha Galibona, Ramadhan Mahano, Robert Kalyahe na Said Nassoro. Wakufunzi wanaendelea kusahihisha mitihani ya washiriki na baada ya kazi hiyo kwa ambao watakuwa wamefanya vizuri majina yao yataingizwa katika orodha ya makamishna kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano mengine yanayosimamiwa moja kwa moja na TFF.
RAMBIRAMBI MSIBA WA MCHUKA, NGAHYOMA
Thursday, December 29, 2011
KEBBY'S HOTEL YAIZINDUA SPORTS BAR!
MATUKIO MAZURI YA SOKA MWAKA 2011.
MWAKA 2011 ULIKUWA MWAKA AMBAO MAMBO MENGI YALITOKEA YA KUFURAHISHA KWENYE MCHEZO WA SOKA . KUNA TIMU YA TAIFA AMBAYO SIDHANI KAMA NI WATU WENGI WANAWEZA KUWA WANAIFAHAMU NAYO NI AMERICAN SAMOA.MWAKA 2001 TIMU HII ILIWEKA REKODI MBAYA YA KUFUNGWA MABAO 31-0 NA AUSTRALIA .MWAKA HUU AMERICAN SAMOA WALIWEZA KUPATA USHINDI WAO WA KWANZA KATIKA HISTORIA YAKE BAADA YA KUIFUNGA TIMU YA TAIFA YA VISIWA VYA TONGA . USHINDI HUU WA KIHISTORIA ULIIPA AMERICAN SAMOA BONUS YA KUPANDA NAFASI 18 JUU KWENYE VIWANGO VYA FIFA.
2. David Beckham ATWAA MLS Cup
LA GALAXY HAIKUMCHUKUA DAVID BECKHAM ILI ALETE MAFANIKIO KWENYE TIMU HII BALI SABABU ZA KBIASHARA LAKINI MOYONI KWA DAVID BECKHAM SIKU ZOTE MAFANIKIO NDIO YALIYOKO MBELE NA ILIMCHUKUA MIAKA MINNE KWA YEYE KUTWAA KOMBE LA MLS . BECKHAM ALICHEZA SEHEMU MUHIMU SANA KWENYE MAFANIKIO YA GALAXY KUTWAA KOMBE HILI NA KAMA KAWAIDA YAKE ALIONYESHA WELEDI WA HALI YA JUU PAMOJA NA JUHUDI AMBAZO SIKU ZOTE ZIMEKUWA SILAHA ZAKE AKIWA NA TIMU YOYOTE ALIYOCHEZA.
3. Sir Alex Ferguson A-Celebrates MIAKA25 AKIWA Manchester United
MWAKA HUU ULIMSHUHUDIA KOCHA AMBAYE KWA HAKIKA NI KOCHA ALIYEDUMU KWA MUDA MREFU MCHEZONI SIR ALEX FERGUSON AKITIMIZA MIAKA 25 AKIWA KWENYE KLABU YA MANCHESTER UNITED . HAKUNA ANAYEWEZA KUPIGA MAFANIKIO ALIYOYAPATA AKIWA KWENYE KLABU YA MANCHESTER UNITED .
SIR ALEX FERGUSSON ALITIMIZA MIAKA HIYO MWEZI NOVEMBA NA KUSHEREHEKEA MAFANIKIO HAYO MAN UNITED WALIMTUNUKU KOCHA WAO KWA KULIPA JINA LILILOKUWA JUKWAA LA KASKAZINI NA KUWA ‘THE SIR ALEX FERGUSSON STAND’.
4. Mexico YATWAA CONCACAF Gold Cup
MWAKA HUU ULIKUWA MWAKA WA HISIA MCHANGANYIKO KWA TIMU YA TAIFA YA MEXICO NA JUU YA HISIA ZOTE ILIKUWA MAFANIKIO YA KUTWAA KOMBE LA CONCACAF GOLD CUP AMBAKO WALIWAFUNGA MAHASIMU WAO WA MIAKA MINGI TIMU YA TAIFA YA MAREKANI KWA MABAO MANNE KWA MAWILI.WAMEXICO WENGI WATAKUMBUKA BAO LA NYOTA WAO GIOVANI DOS SANTOS ALIYEUNYANYUA MPIRA JUU YA KIPA TIM HOWARD NA KUMALIZA USIKU WA RAHA HUKU JAVIER HERNANDEZ CHICHARITO AKITUNUKIWA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MICHUANO SAMBAMBA NA UFUNGAJI BORA.
5. Republic of Ireland YAFUZU Euro 2012
SURA ZA MASHABIKI WA SOKA WA IRELAND ZILIREJEWA NA TABASAMU BAADA YA KUSONONEKA KWA MUDA MREFU . TIMU YA TAIFA YA IRELAND ILIFANIKIWA KUFUZU KUCHEZA KOMBE LA MATAIFA YA ULAYA KWA MWAKA 2012 BAADA YA KUWAFUNGA ESTONIA KWA JUMLA YA MABAO MATANO KWA MOJA KATIKA MICHEZO MIWILI.
MAFANIKIO HAYA YALIFUTA MACHUNGU YA MKONO WA THIERRY HENRY AMBAO ULIINYIMA IRELAND NAFASI YA KUFUZU KOMBE LA DUNIA MWAKA 2010.
6. Ronaldinho's Return
BAADA YA TAKRIBANI MWAKA MZIMA AKIWA HAELEWEKI ELEWEKI , NYOTA WA SOKA LA ULIMWENGU KAMA SIO LA HISPANIA MIAKA MICHACHE ILIYOPITA NA BRAZIL RONALDINHO GAUCHO ALIREJEA KWENYE TIMU YA TAIFA YA BRAZIL BAADA YA KUKOSEKANA MUDA MREFU .
GAUCHO ALIREJEA KWENYE MCHEZO DHIDI YA GHANA NA PIA ALICHEZA KWENYE MCHEZO ULIOFUATA , UREJEO WAKE ULIPAMBWA NA BAO ZURI LA FREE KICK YA HATARI ALILOFUNGA KWENYE MCHEZO DHIDI YA MEXICO , WABRAZIL NA MASHABIKI WA SOKA ULIMWENGUNI WANAOMBA UREJEO HUU UDUMU HADI MWAKA 2014 KWENYE KOMBE LA DUNIA .HUKU GAUCHO HUKU NEYMAR SIDHANI KAMA KUTAKUWA NA WA KUIZUIA BRAZIL.
7. MAREKANI YAIUA BRAZIL KWENYE KOMBE LA DUNIA LA WANAWAKE
KOMBE LA DUNIA KWA WANAWAKE MWAKA 2011 LILIKUWA LA AINA YAKE PENGINE KULIKO MIAKA YOTE AMBAYO MICHUANO HII IMEWAHI KUFANYIKA .MAMILIONI YA WATU WALIIFUATILIA MICHUANO HII NA HAKUNA WAKATI AMBAOP NYUSO ZA WATU ZILIJAWA NA FURAHA KAMA WAKATI AMBAPO TIMU YA TAIFA YA MAREKANI ILIPOIFUNGA TIMU YA TAIFA YA BRAZILKWENYE HATUA YA ROBO FAINALI.
WAMAREKANI WALIPATA BAO LA KUONGOZA MAPEMA LAKINI PENATI ILIYOPIGWA MARA MBILI NA MARTA ILISAWAZISHA BAO LA MAREKANI . MAPEMA KWENYE MUDA WA NYONGEZA NYOTA WA SOKA LA WANAWAKE KWA SASA MARTA ALIFUNGA KUIPA BRAZIL UONGOZI LAKINI ABBY WAMBACH ALIFUNGA NA KUSAWAZISHA . BAADA YA HAPO SHUJAA ALIKUWA MWANADADA AMBAYE PENGINE NDIYE MWANASOKA MREMBO KULIKO WOTE GOLIKIPA WA MAREKANI HOPE SOLO AMBAYE ALIOKOA PENATI ZA WABRAZIL NA KUIPELEKA MAREKANI KWENYE NUSU FAINALI.
8.UMARIDADI WA Barca
BARCELONA WALICHEZA NA MAN UNITED KWENYE FAINALI YA KLABU BINGWA BARANI ULAYA NA WALIREJEA KILE WALICHOKIFANYA KWENYE FAINALI YA MWAKA 2009 KATIKA HALI YA KUSTAAJABISHA .
KUFUATIA KIPIGO HICHO KOCHA WA MAN UNITED SIR ALEX FERGUSON HAKUSITA KUWAPA BARCA SIFA WANAYOSTAHILI KWA KUSEMA KUWA BARCELONA NDIO TIMU BORA KULIKO ZOTE ALIZOWAHI KUKUTANA NAZO KATIKA KIPINDI CHAKE KAMA KOCHA, KWA MANENO YAKE MWENYEWE BABU ALISEMA KUWA “ HAKUNA MTU ALIYEWAHI KUTUCHEZEA KAMA WALIVYOTUFANYA BARCELONA NA KIUKWELI WANASTAHILI’
9. FORLAN AIONGOZA URUGUAY KUTWAA COPA AMERICA
BAADA YA PERFOMANCE NZURI KWENYE KOMBE LA DUNIA AMBAPO ALIIONGOZA URUGUAY KUTWAA NAFASI YA TATU , DIEGO FORLAN ALING’AA TENA KWENYE SOKA LA KIMATAIFA AKIWA NA TIMU YAKE YA TAIFA KWENYE COPA AMERICA, FORLAN ALIKUWA KIMYA KWENYE MICHUANO HII LAKINI ALIKUJA KUIBUKA KWENYE FAINALI AMBAPO ALIFUNGA MABAO MAWILI HUKU MWENZIE LUIS SUAREZ AKIFUNGA BAO LINGINE . LUIS SUAREZ ALICHAGULIWA KUWA MCHEZAJI BORA WA MICHUANO HIYO LAKINI MCHANGO WA FORLAN HASA KWENYE FAINALI HAUPINGIKI .
10. UJIO WA NEYMAR
MCHEZO WA SOKA ULIPATA NYOTA MPYA KWA MWAKA HUU NA JINA LAKE NI NEYMAR DA SILVA JUNIOR .
KINDA HILI TOKA BRAZIL LILIWASHANGAZA WATU KWA VITU VYA HATARI ALIVYOONYESHA KWENYE MCHEZO WAKE DHIDI YA SCOTLAND AKIICHEZEA TIMU YAKE YA TAIFA YA BRAZIL NA MABAO YAKE MENGI AKIWA NA KLABU YAK YA SANTOS .
HATIMAYE ARSENAL WAMPA OFA YA KURUDI EMIRATES THIERRY HENRY
Klabu ya Arsenal hatimaye leo wamempa Thierry Henry ofa ya mkataba wa miezi miwili kurejea kuitumikia klabu hiyo.
Arsene Wenger amekuwa akifikiria kumchukua ama kumtomchukua mfungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo ili ku-boost nafasi ya timu yake kuweza kupata nafasi ya kugombea nafasi nne za juu.
Huku Gervinho na Marouane Chamakh wakielekea katika michuano ya African Cup of Nation mwezi ujao, Manager wa Arsenal ameamua kumpa usaidizi Robin Van Persie na kumpunguzia mzigo wa kuifungia timu hiyo.
Wenger ameamua kutoa ofa kwa Henry baada ya mchezaji huyo kurejea kutoka Mexico katika mapumziko. Henry ana mkataba wenye thamani ya $4.5million na New York Red Bulls lakini amekuwa akifanya mazoezi na Arsenal tangu msimu wa ligi ya MLS ulipoisha na ana muda kukaa Arsenal hadi machi mwakani.
Kama atakubali ofa hiyo anaweza kucheza katika mechi saba za Premier league, pia mechi za FA Cup, na mechi ya kwanza ya mtoano ya Champions league dhidi ya AC Milan. Lakini ni kwenye Premier league ambapo kikosi cha Wenger kinahitaji msaada zaidi, huku michezo muhimu dhidi ya Manchester United na Tottenham ikiwemo.
The former Arsenal captain aliweka ekodi ya kufunga magoli 226 na kushinda makombe mawili ya EPL katika klabu hiyo kutoka mwaka 1999 na 2007.
Kurudi kwake Emirates kutawafurahisha mashabiki hasa baada ya kuondokewa na vipenzi vyao Cesc Fabregas, Gael Clichy na Samir Nasri.
RAMBIRAMBI MSIBA WA RASHID MOYO
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa, Rashid Moyo kilichotokea usiku wa Desemba 25 mwaka huu kwao Msambweni, Tanga.
Moyo ambaye aliichezea timu ya Taifa kwenye miaka ya 70 alizikwa Desemba 26 mwaka huu kwenye makaburi ya Mabawa mkoani Tanga. Pia alikuwa mchezaji wa timu ya Coastal Union ya mkoa wa Tanga.
Msiba huo ni pigo kwa familia ya Moyo, TFF na familia ya mpira wa miguu kwa ujumla nchini kutokana na mchango alioutoa kwa Tanzania hasa wakati akiwa mchezaji. TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Moyo, Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Tanga (TRFA) na kuwataka kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki cha msiba huo mzito. Pia TFF itatoa ubani wa sh. 100,000 kwa familia ya marehemu kama rambirambi zake.
Mungu aiweke roho ya marehemu Rashid Moyo mahali pema peponi. Amina
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
KWANINI BERBATOV HAPASWI KUONDOKA UNITED JANUARY?
Performance ya Dimitar Berbatov dhidi ya Wigan na Fulham could be described as “come and get me” plea kwa timu yeyote inyomtaka, lakini Je Fergie atakuwa radhi kumuacha mbulgaria huyo aliyemnunua kwa fedha nyingi aondoke Old Trafford?
Tangu kipindi kilichopita cha usajili kilipofungwa, kumekuwepo na vilabu vingi vilivyohusishwa na kumsaini Berba, zikiwemo Paris Saint Germain, Valencia, Fulham, Galatasary, and Anzhi Makhachkala. Ingawa hivi taarifa zimetoka kwamba mchezaji huyo anatarajiwa kurejea katika klabu yake ya zamani, Bayern Leverkusen.
Mkataba wa Berbatov unamalizika mwishoni mwa msimu, hivyo United wanapaswa kufanya maamuzi juu ya kumuongezea mkataba mpya kabla ya January 2, vinginevyo Mbulgaria huyo anaweza kukubaliana na klabu yoyote kwa ajili ya kujiunga nayo atakapomaliza mkataba wake next summer.
Huku wengi wakisema Berba anataka timu ambayo atapata nafasi kikosi cha kwanza, manager Sir Alex Ferguson amewahi kukaririwa akisema Berbatov bado yupo katika mipango yake, “Unahitaji kuwa washambuliaji wengi wazuri ndani ya kikosi katika mpira wa siku hizi. Kama utaangalia nyuma in 1999, tulikuwa na washambuliaji wazuri wane. Wote waliplay part zao, na hilo ndilo litakalotokea sasa.” –Fergie
Wakati Rooney, Berbatov, Chicharito and Welbeck wakiwa hawana chemistry kama waliyokuwa nayo Cole, Yorke, Sheringham na Solskjaer unaweza kujua nini Ferguson anamaanisha nini.
Msimu uliopita Berbatov alishinda tuzo ya ufungaji bora ingawa hakuwahi kuwa chaguo la kwanza kabisa katika kikosi cha kwanza. Alifunga mabao 20 katika mechi 32, including hat-tricks dhidi ya Birmigham na mahasimu Liverpool, and ofcourse his magnificent 5 goals dhidi ya Blackburn katika ushindi wa 7-1 @Old Trafford.
Moja ya vitu vizuri kuhusu Berbatov as a person as well as a player ni tabia yake anayoionyesha kwa manager na klabu kwa ujumla. Pamoja na kutochezeshwa katika michezo mingi, Berba hajawahi kutoka nje na kuzungumza kwenye media kwa kutoheshimu maamuzi ya kocha wake. Halazimishi kwamba anataka kuanza katika kila mechi, tabia yake nzuri ndani na nje ya uwanja tofauti na wachezaji wengine wa EPL.
Kitu anachofanya ni ku-prove uwezo wake kiwanjani. Following his hat trick dhidi ya Wigan, hatolazimisha kuanza au ku-suggest kwamba yeye ni mzuri zaidi ya Rooney, Chicharito na Welbeck. Kitu atakachofanya ni kutulia na kusubiri muda na nafasi yake nyingine, and then atathibitisha ubora wake kwa vitendo.
Kila kocha anataka mchezaji wa namna hii, mchezaji/wachezaji ambao wataheshimu maamuzi yao na kutolalamika kuhusu maamuzi hayo ila pale wanapopata nafasi wanazipokea kwa mikono miwili. I have nothing but admiration kwa wachezaji wenye tabia kama ya Berbatov, ambao huweka maslahi ya timu mbele ya matamanio yao.
Je Berbatov ataendelea kuichezea United baada ya tarehe 31, January? Naamini ataendelea kuwepo THEATRE OF DREAMS.
HATIMAYE TP MAZEMBE YAUZINDUA UWANJA WAKE:
Wednesday, December 28, 2011
Tuzigeuze shule za msingi kuwa ‘soccer academies’
Fred Mwakalebela
PAMOJA na kuwapa pole Watanzania wenzetu waliokumbwa na mafuriko jijini Dar es Salaam na sehemu nyingine za nchi, ni vyema pia nikawapa heri ya Sikukuu ya Noeli wale wote waliopata bahati ya kuisherehekea siku hiyo.
Naam, ni bahati kwa kusema ukweli kwani kuna mashabiki wengi tu wa soka waliokuwa wakiishi maeneo ya mabondeni jijini hapa kwa sasa wamesahau hata neno ‘soka’ kutokana na maswahibu yaliyowakuta.
Lakini wiki moja kabla ya majanga haya, Shirikisho la Soka nchini (TFF) kwa kushirikiana na mabosi wao FIFA, waliandaa kitu kama tamasha lililojumuisha waalimu wa michezo kutoka shule mbalimbali za msingi jijini hapa.
Tamasha hilo lililopewa jina la ‘Grassroots Football’, ni jambo kubwa sana linalopaswa kupongezwa na kisha kuendelezwa ili ndoto za mashabiki wa soka za kuona soka la Tanzania linasonga mbele ziweze kutimia.
Sina uhakika sana kama walimu wa michezo nchini kwenye shule za msingi wana utaalamu kama waliokuwa nao walimu wetu enzi zile tukiwa shuleni.
Serikali ya Nyerere, ingawa wengi humchukulia mzee yule kama mmoja wa viongozi waliokuwa mbali na michezo, bado serikali yake ilitoa kipaumbele kwenye michezo.
Wakati ule walimu wa michezo walikuwa wakipata mafunzo ya kitaalamu kwenye Chuo cha Walimu Butimba, na hata wanapokuwa kazini, walikuwa wakipewa nafasi ya kwenda kujiendeleza kwenye Chuo cha Michezo cha Malya.
Kwa hiyo, mkusanyiko wa walimu wa michezo kutoka shule za msingi uliofanyika jijini wiki iliyopita, ulipaswa kuwa mkusanyiko wa wataalamu kabisa wa soka la vijana, na unapaswa kufanyika kila kona ya nchi, kila mwaka.
Je, hilo litafanyika? Na je, TFF na wadau wengine wa soka wamejiandaaje na changamoto ya uhaba wa viwanja? Wakati wenzetu wa Zanzibar wameendelea kuvitunza viwanja vyao vya Mnazi Mmoja na Maisela, sisi viwanja vya Jangwani vinauzwa! Tufanyeje?
Tumebaki tunategemea viwanja vya shule za msingi na sekondari zile za enzi za Mwalimu tu. Kwa sasa kila shule ya msingi ina pacha wake, lakini kiwanja kimabaki kimoja tu huku idadi ya wanafunzi ikiongezeka zaidi ya mara 10 ikifananishwa na idadi ya mwaka 1990.
Shule za kisasa, ambazo ni lazima zitanguliwe na jina la ‘Saint’ au ziwe na neno ‘Academy’, ziko kibiashara zaidi na suala la kiwanja wala haliwaingii akilini. Hapa ninadhani ni vyema Serikali ikaingilia kati na kuweka sheria kuwa shule isiyo na uwanja wa michezo haitasajiliwa.
Soka ni lazima lianzie kwa watoto au vijana. Kwa kuwa Tanzania tunaonekana kushindwa kuwa na academy za soka za ukweli, basi ni vyema ukasukwa mkakati endelevu chini ya TFF na Kamati ya Olimpiki ili vijana hawa walio shuleni leo wakapatiwa mafunzo huko huko, yaani tuzifanye shule ziwe academy za soka kwa kuwaendeleza watoto wenye vipaji.
Ukiwekwa mkakati wa ukweli, miaka kadhaa ijayo shule zetu zinaweza kuanza kupata matunda ya programu hiyo kwani iwapo itatoa mwanasoka atakayenunuliwa na timu kubwa, kwa mujibu wa sheria ya FIFA ya training compensation, zitakuwa zikipokea asilimia fulani ya malipo ya mchezaji huyo.
Mfano akienda Simba au Yanga na baadaye akachukuliwa na TP Mazembe kisha akaenda Chelsea, mlolongo wote huo utatakiwa kuwa ukitoa asilimia ya fedha kwenye academy iliyokuza au kufufua kipaji husika.
Ni hapo ndipo ninajiuliza kwanini TFF imeamua kuivunja Tanzania Soccer Academy (TSA) wakati fedha ya Vodacom ilikuwapo? Huu ni mfano mbaya sana kwa wengine waliokuwa na ndoto za kuanzisha academy kwani watajiuliza iwapo TFF yenyewe imeshindwa, sisi tutawezaje?
Nirejee kwenye tamasha la walimu. TFF na FIFA wanapaswa kulipeleka kwenye mikoa kama Tabora au Mwanza ambako walau viwanja vya soka bado vipo na watu wanapenda mchezo wenyewe.
Walimu wa mikoa hiyo wahamasishwe na ikiwezekana wapelekwa Malya kusomea soka la vijana! Tena nadhani walimu hawa ndio wangepaswa kupewa nafasi ya kushiriki ile kozi ya Nishani za Miaka 50 ya Uhuru.
Niwasilishe hoja kwa kumwomba bosi wa Kamati ya Olimpiki kuangalia uwezekano wa kuisaidia TFF kuzifanya shule za msingi kuwa academy za soka.
Si lazima ziwe shule zote, wanaweza kuteua shule moja katika kila wilaya au mkoa na kuisheheni walimu wataalamu wa soka la vijana, walimu hao wakawa wakiwakusanya vijana wenye vipaji na kuwaweka pamoja.
Niwatakie heri kwenye kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka.
COUNTDOWN : MATUKIO YA MICHEZO MWAKA 2011:
4. NAFASI YA NNE INAKWENDA KWA MWAMUZI ALIYETOA KALI YA KARNE KAMA SI YA MWAKA .SIKU ZOTE MCHEZO UNAPOKUWA MGUMU MASHABIKI NA WACHAMBUZI WA SOKA HUSEMA KUWA PAMBANO AU MECHI IMEMSHINDA MWAMUZI LAKINI SI MWAMUZI HUYU ALIYECHEZESHA MCHEZO WA LIGI DARAJA LA TANO NCHINI ARGENTINA.
DAMIEN RUBINO ALIONYESHA KUWA MECHI ZA KIHUNI SI LOLOTE WALA CHOCHOTE KWAKE KWANI ALITOA KADI NYEKUNDU 36 KWENYE MECHI KATI YA CLAYPOLE NA VICTORIANO ARENAS .
KWA MAHESABU SAHIHI MWAMUZI HUYU ALITOA KADI KWA WACHEZAJI KUMI NA MOJA WA TIMU ZOTE ZILIZOANZA YAANI KADI 22 NA KISHA AKAFUATIA KWA KUTOA KADI NYEKUNDU KWA WACHEZAJI 14 WA AKIBA TOKA TIMU ZOTE MBILI.
KWA KIFUPI REFA HUYU ALIMALIZA PAMBANO KWANI BAADA YA HAPA HALIKUWEZA KUENDELEA LAKINI ALITOA ADHABU HII KWA WACHEZAJI WOTE WAKOSE MECHI ZINAZOFUATA NA KUWALAZIMU KUSIMAMISHA MICHEZO YAO KWA KUKOSA WACHEZAJI WA KUCHEZA.
5. SIKU ZOTE SI MARA NYINGI UNAWEZA KUKUTA MWAMUZI WA MCHEZO AKIFANYA JAMBO LA KUKUMBUKWA NA MASHABIKI. LAKINI HII SI KWA MWAMUZI TOKA MEXICO MARCO RODRIGUEZ AMBAYE ANAONEKANA KULIELEWA SOMO LA FIZIKI KULIKO WAAMUZI WENGI WA MCHEZO WA SOKA.
KATIKA MCHEZO WA LIGI DARAJA LA PILI HUKO MEXICO , MWAMUZI HUYU ALIPATA MTIHANI WA UFITI WA MWILI WAKE KWA KUWA MCHEZO ULIKUWA WA KASI KUBWA .
KATIKA MCHEZO HUO , MWAMUZI HUYU ALILAZIMIKA KUTOA KADI TATU NYEKUNDU NA SABA ZA NJANO KUTOKANA NA MCHEZO MBAYA WALIOKUWA WANAONYESHA WACHEZAJI WA TIMU ZOTE.
REFA HUYU ALITOA KALI PALE ALIPOKUWA NA KADI MBILI MBILI YAANI NJANO MBILI NA NYEKUNDU MBILI , HIVYO ALIKUWA AKITOA KADI MBILI KWA WACHEZAJI WAWILI KWA MPIGO BADALA YA KUTOA KADI MOJA NA KUGEUKA KUTOA KWA MTU MWINGINE.
6. WAKATI TIMU YA RIVER PLATE ILIPOSHUKA DARAJA KWA MARA YA KWANZA NDANI YA HISTORIA YAKE YA ZAIDI YA MIAKA 100 MASHABIKI HAWAKUFURAHISHWA NA TUKIO HILI.MUDA MFUPI BAADA YA MCHEZO MASHABIKI WA RIVER WALIANZA MAANDAMANO JIJINI BUENOS AIRES HUKU WAKIFANYA VURUGU KUBWA , TUKIO HILI NI MOJA YA MATUKIO YA KUKUMBUKWA KWA MWAKA HUU.ENZI HIZO!!! WEWE ULIKUA WAPI?
COUNTDOWN: MATUKIO YA SOKA YA KUKUMBUKWA MWAKA 2011
2. WACHEZAJI WENGI WAMEJIJENGEA UMAARUFU KWA USTADI NA UFUNDI WA KUPIGA PENATI,KUNA KILA MTINDO WA KUPIGA PENATI AMBAO UMETUMIKA HADI KUFIKIA LEO LAKINI HAKUNA PENATI ITAKAYOFUNIKA ILE ILIYOPIGWA NA KIJANA AWANA THIAB WA UNITED ARAB EMIRATES.KIJANA HUYU ALIPIGA PENATI AMBAYO ILIMPA UMAARUFU ULIMWENGUNI KOTE AMBAKO PICHA ZAKE AKIPIGA PENATI ILE ZILIONEKANA . AWANA ALIPIGA PENATI KWA KUTUMIA KISIGINO HUKU AKIWA AMEMPA GOLIKIPA MGONGO. KWA BAHATI MBAYA REFARII HAKUONA KAMA AWANA AMEFANYA UUNGWANA , ALITAFSIRI KITENDO KILE KAMA UDHALILISHAJI WA MCHEZAJI NA MCHEZO WA SOKA KWA UJUMLA NA KWA HILO ALIMUONYESHA KADI NYEKUNDU .
KILICHOWASHANGAZA WENGI SIYO JINSI AWANA ALIVYOFUNGA BAO LILE BALI ILE HALI ALIYOKUWA NAYO BAADA YA KUFUNGA , HAKUONEKANA KUJAWA NA MSISIMKO KAMA INAVYOKUWA KWA WACHEZAJI WENGINE WANAPOFUNGA. KWA BAHATI MBAYA AWANA DIAB HAKUISHI MUDA MREFU KUSHUHUDIA JINSI UMAARUFU WAKE ULIVYOITEKA DUNIA KWANI ALIFARIKI DUNIA MIEZI MICHACHE BAADA YA TUKIO HILI KWA AJALI MBAYA YA GARI.
3. TUKIO LA TATU NI GOLI AMBALO JINSI LILIVYOFUNGWA HAKUNA ALIYESHUHUDIA AMBAYE ATAWEZA KUSAHAU KIRAHISI. BEKI WA TIMU YA FAGIANO OKAYAMA RYUJIRO UEDA ALIFUNGA BAO LA KICHWA KUTOKA NYUMA YA MSTARI WA KATIKATI YA UWANJA UMBALI WA KARIBU YADI 63 TOKA LILIPO GOLI . BAO HILI LILIINGIA KWENYE REKODI KAMA BAO LILILOFUNGWA TOKA MBALI ZAIDI KWA KUTUMIA KICHWA .
ENDELEA KUWA NASI MENGINE YATAFUATA MUDA SI MREFU!!!
Tuesday, December 27, 2011
Uteuzi huu ni kwa ajili ya Nishani za Uhuru?
TANZANIA Bara iliyokuwa ikifahamika kama Tanganyika kwa sasa ina umri wa miaka 50 na siku kama 10 hivi, umri ambao kwa hakika ni wa mtu mzima kabisa.
Jina la Tanganyika kwa mujibu wa historia lilianza kutumika kama miaka 100 tu iliyopita likiunganisha sehemu ya mwambao mwa Bahari ya Hindi na ukanda wa misitu (nyika) magharibi mwa pwani hiyo.
Wakati wa utawala wa kikoloni chini ya Mjerumani, eneo hili lilijulikana kama ‘German East Africa (Deutsch-Ostafrika)’ likijumuisha pia nchi za Burundi na Rwanda likiwa na ukubwa wa karibu mara tatu ya Ujerumani ya sasa.
Ni hapo ndipo wadau wa soka wanaposhangaa iweje mkoloni wetu wa zamani, Ujerumani, nchi yenye ukubwa wa kilomita za mraba 384,170 tu, leo hii ni miongoni mwa miamba wa soka duniani huku sisi tukiendelea kung’aa macho?
Jibu ni rahisi sana, hatuna vipaumbele. Na kama tunavyo, vina baki midomoni na kwenye makaratasi tu, havitekelezwi na wala wanaopaswa kuvitekeleza hawajali.
Wiki iliyopita anga la soka nchini lililokuwa likitarajiwa kugubikwa na mijadala kuhusu kiwango cha soka lilichoonyeshwa na timu zetu za taifa, Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes kwenye michuano ya CECAFA Challenge Cup, lilibadilika na kuanza kujadili uteuzi wa makocha watakaoshiriki mafunzo ya wiki moja ya CAF.
Kila mmoja, shabiki na hata kiongozi wa soka, anafahamu namna gani soka la vijana nchini limekuwa likipigiwa kelele na jinsi lilivyozibeba nchi kadhaa duniani zilizotilia maanani maendeleo ya vijana.
Ujerumani (wakoloni wetu hawa) ni moja kati ya mifano hai. Kwenye fainali za Kombe la Dunia mwaka jana, wachezaji wa Ujerumani wakifuatiwa na wa Ghana ndio waliokuwa na wastani mdogo zaidi wa umri, ikimaanisha kuwa nchi hizo zitaendelea kutesa katika soka la kimataifa kwa muda mrefu ujao.
Nilitumaini kabisa kuwa inapotokea nafasi ya mafunzo kama haya ya CAF, makocha vijana, au hata kama si vijana, wale wanao ‘practice’ kazi hii kila kukicha, ndio walipaswa kupewa nafasi ya kushiriki ili kuwabeba wachezaji wadogo (watoto) na vijana kwa manufaa ya baadaye ya nchi yetu.
Lakini cha ajabu mengi miongoni mwa majina ya washiriki hao ni wale wanaokaa maofisini wakiwa na shughuli nyingine kabisa mbali na soka, au hata kama wanajishughulisha na soka, si lile soka hasa la kwenye ‘field’.
Mifano ni wazi, Leodegar Tenga kwa sasa ni Rais wa TFF na Mwenyekiti wa CECAFA na huenda hajafanya kazi za ukocha tangu alipofanya hivyo miaka ya mwanzoni ya 1980 akiifundisha Pan African.
Mwingine ni Kassim Majaliwa. Yeye ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI. Sina uhakika kwa majukumu aliyonayo kwenye wizara nyeti kama TAMISEMI atakuwa na nafasi ya kufanya kazi ya ukocha kwa kipindi hiki hadi 2015.
Joel Bendera, mmoja wa makocha wenye heshima kubwa nchini naye atakuwamo kwenye kozi hiyo, lakini kwa majukumu aliyonayo sasa ya ukuu wa mkoa wa Morogoro, mkoa unaokumbwa na mapigano ya mara kwa mara kati ya wakulima na wafugaji; ajali za barabarani; ujambazi na nyakati nyingine mafuriko, atapata nafasi ya kuendeleza soka la vijana uwanjani?
Sidhani, labda majukwaani na huko hakuna haja ya kupewa mafunzo ya wiki nzima na CAF. Hata akina Salum Madadi na Mshangama kwa sasa wamekuwa ni viongozi wa kisera zaidi, hivyo walipaswa kuwapa nafasi makocha waliopo kwenye ‘field’.
Eugene Mwasamaki, bosi wa chama cha makocha naye amejiweka kwenye orodha ya watakaopata mafunzo hayo bila kuwaeleza Watanzania ni vigezo vipi walitumia kuteua washiriki, naye ananishangaza kwa kiasi kikubwa.
Jamani, tunalipeleka wapi soka la Tanzania? Timu ya vijana majuzi imerejea kutoka Gaborone, Botswana ilikokuwa imealikwa kushiriki mashindani ya vijana ya COSAFA Castle Cup na kuonyesha kiwango bora, kweli miongoni mwa waheshimiwa hawa kuna atakayerejea kuifundisha tena timu hiyo? Labda… lakini sina uhakika hata kwa hili.
Kwa muda sasa, NMB imekuwa ikisaidia mafunzo kwa makocha wa soka na tayari zaidi ya makocha 2,000 wamehitimu mafunzo hayo na wapo tayari kuendeleza soka la vijana. Ni nani kati ya watakaoshiriki kozi ya CAF imetokana na mafunzo hayo ya NMB?
Kweli tunawaacha akina Kenny Mwaisabula (TEFA Technical Director), Joseph Kanakamfumu (kocha kijana mwenye shahada) na Salum Mayanga wa Kagera Sugar kwenye kozi hii, kama si kujitakia lawama ni nini?
Wasiwasi wangu ni kwa waheshimiwa hawa walio na majukumu mengi ya kitaifa kama kweli watapata nafasi ya hata kushiriki kozi yenyewe kwani sina uhakika kuwa ‘sitting allawance’ (kama ipo) italingana na ile waliyoizoea.
Na ndio maana mimi niliposikia majina haya redioni na kwenye runinga sikuamini. Kwanini? Kwa kuwa nilidhani na kuamini kabisa kuwa huenda majina haya yalikuwa ni kwa ajili ya kutunukiwa Nishani za Miaka 50 ya Uhuru.
Nilipoamka kesho yake na kuyakuta gazetini na kuhabarishwa kuwa ni kwa ajili ya kozi ya ukocha, nilichoka kabisa. Nikajiuliza, hivi waheshimiwa hawa, kabla ya kutangazwa, walikuwa wamewasiliana na waliowateua na kukubaliana? Wanadhani kushiriki kwao kutakuwa na tija kwenye soka letu, hasa la vijana?
Hakika hawa walipaswa tu kuwamo miongoni mwa watunukiwa wa Nishani za Uhuru zilizotolewa na Rais Jakaya Kikwete Desemba 9 mwaka huu. Bado tuko pamoja… ila tutekeleze kwa vitendo vipaumbele tulivyo navyo.