Klabu ya Arsenal hatimaye leo wamempa Thierry Henry ofa ya mkataba wa miezi miwili kurejea kuitumikia klabu hiyo.
Arsene Wenger amekuwa akifikiria kumchukua ama kumtomchukua mfungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo ili ku-boost nafasi ya timu yake kuweza kupata nafasi ya kugombea nafasi nne za juu.
Huku Gervinho na Marouane Chamakh wakielekea katika michuano ya African Cup of Nation mwezi ujao, Manager wa Arsenal ameamua kumpa usaidizi Robin Van Persie na kumpunguzia mzigo wa kuifungia timu hiyo.
Wenger ameamua kutoa ofa kwa Henry baada ya mchezaji huyo kurejea kutoka Mexico katika mapumziko. Henry ana mkataba wenye thamani ya $4.5million na New York Red Bulls lakini amekuwa akifanya mazoezi na Arsenal tangu msimu wa ligi ya MLS ulipoisha na ana muda kukaa Arsenal hadi machi mwakani.
Kama atakubali ofa hiyo anaweza kucheza katika mechi saba za Premier league, pia mechi za FA Cup, na mechi ya kwanza ya mtoano ya Champions league dhidi ya AC Milan. Lakini ni kwenye Premier league ambapo kikosi cha Wenger kinahitaji msaada zaidi, huku michezo muhimu dhidi ya Manchester United na Tottenham ikiwemo.
The former Arsenal captain aliweka ekodi ya kufunga magoli 226 na kushinda makombe mawili ya EPL katika klabu hiyo kutoka mwaka 1999 na 2007.
Kurudi kwake Emirates kutawafurahisha mashabiki hasa baada ya kuondokewa na vipenzi vyao Cesc Fabregas, Gael Clichy na Samir Nasri.
Welcome hom Thiery!!ze Gunners 4rever
ReplyDelete