Mpaka kufikia sasa ligi kuu ya England imefikia katikati katika msimu huu wa 2011-2012, hivyo wacha leo tufanye review ya kuchagua mchezaji bora kutoka kwenye kila klabu katika premier league.
Tutawapanga wachezaji hawa kutokana na nafasi za timu zao katika msimamo wa ligi ulivyo.
20: WIGAN ATHLETIC: MOHAMED DIAME
Performance ya Mohamed Diame ndani ya kikosi cha Wigan inaonekana itamuongoza na kumletea mafanikio makubwa Msenegali huyu mzaliwa wa Ufaransa.
Sio tu anaongoza kwa kufanya tackles nyingi lakini pia ndio mchezaji wa pili wa timu hiyo ambaye anaongoza kwa kufanya dribbling nyuma ya Victor Moses.
19: WOLVES: WAYNE HENNESSEY
Ben Watson na Sebastian Larsson wanaweza kuwa mashahidi wazuri juu ya uwezo Wayne Hennessey katika kuokoa penati.
So far , mchezo bora kabisa wa Hennessey ulikuwa dhidi ya Arsenal.
Aliokoa magoli ya wazi zaidi ya 9 na kufanikiwa kuwa mchezaji bora wa mechi katika mechi ambayo Wolves walimaliza wakiwa 10 uwanjani ni kujipatia pointi moja kibindoni.
19: BLACKBURN: YAKUBU
What a comeback kutoka Yakubu.
Wengi tulifikiri his top flight career ilikuwa imeisha baada ya kufunga goli 11 katika misimu mitatu iliyopita akiwa Everton.
Msimu huu, Yakubu amefunga magoli 12 mpaka sasa akiwa na Blackburn, ambao wapo katika kupambana na vita ya kushuka daraja.
18: BOLTON WANDERERS: IVAN KLASNIC
Kwa asilimia 44 Ivan Klasnic ameisadia indirectly na directly upatikanaji wa magoli yote ya Bolton msimu huu katika premier league.
Huku Kevin Davies akipoteza nafasi yake kikosini na David Ngog akionekana kutojitosheleza kama mshambuliaji wa Premier league – Bolton wanamhitaji Klasnic katika kila mchezo.
17: QPR: ALEJANDRO FAURLIN
Kama Queens Park Rangers watakuja kushuka daraja, then kukosekana kwa Alejandro Faurlin kutokana na majeruhi inaweza ikawa sababu.
16: QPR wana tatizo la kutokufunga magoli, hivyo wanahitaji kuwa na uwezo wa kuzuia kiushindani.
Faurlin amefanikiwa kushinda kurudisha possession mara 146.
15: WEST BROM: CHRIS BRUNT
Magoli mengi yaliyofungwa na West Brom msimu huu yametokana usaidizi wa kutoa za mwisho za Chris Brunt, ambaye ametoa assists nyingi kuliko Graham Dorrans, Jerome Thomas, Peter Odemwingie, Shane Long, Somen Tchoyi na Zoltan Gera wakijumlishwa.
Ama kwa hakika West Brom watapata tabu sana kutokana na kukosekana kwa Brunt ambaye amepata matatizo ya enka.
14: EVERTON: LEIGHTON BAINES
Ni lazima iwe aidha Jose Enrique au Leighton Baines pale linapokuja suala la beki wa kushoto wa bora wa Premier kwa sasa.
Baines yupo balanced, anajua kusambaz mipira vizuri, kukaba, kupandisha timu na kuongoza mashambulizi yote ya Everton, pia ni hatari sana kwa set-piece.
Kama Fabio Capello anaagalia form katika kuchagua wachezaji wake then Leighton Baines anastahili kuanza mbele ya Ashley Cole in Three lions squad.
13: SWANSEA CITY: MICHEL VORM
Kama David De Gea angekuwa anacheza kama Michel Vorm, media zingekuwa zinamsifia sana ni ujio wa pili wa Lev Yashin katika premier league.
On form, Vorm kwa sasa ndio golikipa bora katika premier league.
12: FULHAM: CLINT DEMPSEY
Mousa Dembele yupo na kipaji kikubwa sana, ana ujuzi zaidi, pia ni hatari sana lakini kwa sababu zisizoelezeka amekuwa hatoi matunda ya mwisho ya kipaji chake.
Huku tofauti, Clint Dempsey, ambaye uwezo wa unazaa matunda makubwa nadani watoto wa Mohamed Al Fayed.
Minf you, ana wastani wa mashuti manne kila mechi, na goli 6 kati ya shots 79. Dempsey mpaka sasa ndio mfungaji bora wa Fulham akiwa magoli 9 in EPL.
Kama ulikuwa unajiuliza vipi kuhusu Andy Johnson na Bobby Zamora wote kwa pamoja wana wastani wa goli 7 katika shots 54.
11: ASTON VILLA: STILIAN PETROV
Nani anaongoza kwa kufanya interceptions katika premier league? Jibu ni Stilian Petrov.
Inaeleweka kama utakuwa una unafikiria kasi ya Gabriel Agbonlahor, lakini amekuwa akifanya nini msimu huu?
Amefunga magoli au kutoa asisists ngapi dhidi ya Arsenal, Chelsea, Manchester City, Manchester United na Tottenham Hotspur? Jibu ni zero.
Petrov hajasaidia katika midfield pia anatoa msaada wa nguvu katika kutoa pasi zinazoaa matunda, lakini pia kazi anayoifanya katika kukaba ni exceptional.
10: SUNDERLAND: STEPHEN SESSEGNON
Stephen Sessegnon ndiye best dribbler at Sunderland, na anamzidi Sebastian Larsson linapokuja suala la kupiga key passes.
Alikuwa yupo vizuri @Paris Saint Germain na hata sasa anaendeleza makali akiwa Sunderland.
Ingawa kwa mtu mwenye kipaji cha aina yake inilibidi awe na assists na magoli mengi pia.
9: NORWICH CITY: STEVE MORISON
Kijana huyu ndio nguzo kuu ya mashambulizi ya Norwich City, mipira yote ya Norwich inayoenda mbele inamlemnga yeye. NDio maana aliwapa tabu sana mabeki wa timu kubwa kama Manchester United, Chelsea, na hata Arsenal ambao aliwafunga.
Morison ndio top scorer wa Norwich City akiwa tayari ameshafunga magoli 7 katika premier league.
8: STOKE CITY
Stoke City wamefunga magoli ya penati kuliko ya kawaida.
Katika upatikanaji wa magoli hayo Jonathan Walters amekuwa na mchango mkubwa wa magoli na assists 10 katika mashindano yote.
7: NEWCASTLE UNITED: DEMBA BA
Rekodi zake Demba Ba zinaongea zenyewe hahitaji maelezo mengi.
6: LIVERPOOL: LUIS SUAREZ
Angalia hali mabayo amekutana nayo Suarez ndani ya Liverpool msimu.
Amecheza na mtu ambaye hayupo kabisa kwenye form, na asiye msaada wa maana Andy Carrol. Pia kuna huyu Stewart “Nothing” Downing ambaye ni winga ambaye hana goli wala assist mpaka sasa.
Lakini na hali hiyo Suarez ameibeba Liverpool katika mashabulizi na kufunga magoli 5 na kutoa assist 3 katika michezo 16 ya epl msimu huu. Na angekuwa na magoli mengi zaidi kama sio mashuti yake matano kugonga mwamba.
Suarez anaofa vision na pasi nzuri, huku uwezo wake wa kufanya dribbling ukiwa excellent.
5: ARSENAL: ROBIN VAN PERSIE
Kwa statistic, Robin Van Persie yupo katika mstari mmoja na Lionel Messi na Cristiano Ronaldo. Hii inaonyesha ni msimu mzuri kiasi gani alionao Van Persie.
Huyu ndio nguzo ya mashambulizi ya Arsenal. Akiwa ndio Top scorer wa ligi kuu ya England.
Kupata maumivu kwa Van Persie kunaweza kuharibu shughuli kabisa pale Emirates. Lakini sio mbaya Thierry Henry yupo pale.
Ukimuongelea Henry, ilimchukua dakika 10 tu kufunga bao, lakini ilimchukua Fernando Torres dakika 903 kufunga goli lake la kwanza la msimu.
4: CHELSEA: JUAN MATA
Nani aliyepiga key passes nyingi kuliko wote katika premier league? Juan Mata.
Huyu ndio mtu pekee anayeweza kumchezesha Fernando Torres, lakini bado Andre Villas Boas anakataa kumchezesha Mata nyuma ya Torres.
Kama sio Mata, Chelsea sasa hivi wangekuwa katikati mwa msimamo wa ligi na Villas-Boas angekuwa ameshafukuzwa.
Ndio mtu anayeipa uhai mkubwa safu ya ushambuliaji ya Chelsea.
3: TOTTENHAM HOTSPUR: LUKA MODRIC
Luka Modric kwa Tottenham ni kama Xavi kwa Barcelona.
Gareth Bale amesaidiwa sana na uwezo wa Modric kupiga accurate long balls kwa kwake.
Modric amepiga pasi zilizofanikiwa 1,074, na 140 kati ya hiyo ni mipira mirefu inayozaa matunda kwa timu. Form aliyonayo Modric ndio moja ya sababu kuu kwanini Spurs sasa nao wanagombea ubingwa na timu za jiji la Manchester.
2: MANCHESTER UNITED: WAYNE ROONEY
Katika mechi tano za mwanzo za Wayne Rooney msimu huu, alifunga mabao 8 na kutoa assist moja.
Rooney ameendela kuwa world class player ndani kikosi cha United. Sir Alex Ferguson alimuacha Rooney baada ya kutoka usiku na mkewe na adhabu hiyo ya Babu kwa Rooney iliishia kuwagharimu United dhidi ya Blackburn.
Hiyo pekee inaonyesha ni kiasi gani Rooney ana umuhimu ndani ya kikosi cha Mashetani Wekundu.
1: MANCHESTER CITY: DAVID SILVA
Ukiwa unapima kuhusu uzuri wa kiungo cha timu za premier league, hapo ndio utamkuta mtalaam David Silva.
Anfanya kila kitu ambacho Luka Modric anafanya, lakini pia kwa kuwa na consistency pia anafunga magoli na kutoa assists.
Huyu jamaa ni genius wa soka, ni anapaswa kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa ndani ya Manchester City.
Roberto Mancini kwa sasa, anaye golikipa bora wa kiingereza, pia ukuta bora wa katika ligi, safu bora kiungo katika premier league na pia the best forward line katika ligi.
Lakini kwa sababu zisizoelezeka Manchester City wapo nje ya Champions league, FA Cup, na Carling Cup.
Ningekuwa mimi ndio Shekhe Mansour ningeshamtimua Mancini, ana kila kitu ambacho Arsenal hawana lakini bado The Gunners wapo katika michuano mitatu msimu huu.