Uongozi wa klabu ya Simba umemrudisha kundini beki wake Victor Costa kwa sharti la kumlipa nusu mshahara mwezi huu kama sehemu ya adhabu yake kwa kosa lake la kutoroka kambini.
Mbali na Costa naye Salum Machaku ameandikiwa barua ya onyo kwa kitendo chake cha utovu wa nidhamu alichokionyesha kwenye mazoezi ya timu hiyo ilipokuwa ikishiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi mwezi huu visiwani Zanzibar.
Akizungumza jana mmoja wa viongozi wa Simba alisema Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo ilikaa na kujadili suala la Costa na kuamua kumkata mshahara wake wa mwezi huo ikiwa ni onyo kwa wachezaji wengine na kuamua kumrudisha kambini ili aweze kuendelea na mazoezi na wenzake.
Alisema baada ya mchezaji huyo kuondoka kambini bila taarifa kwa viongozi wake iliamriwa apumzishwe kuendelea na kambi wakati wa michuano hiyo kabla ya kutoa hukumu ya mwisho ambayo ni kumkata mshahara wake.
"Mwezi huu tutamlipa nusu mshahara ikiwa sehemu ya adhabu yake na kutakiwa kuendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mechi za ligi, lakini kwa mwenzake Machaku ameandikiwa barua ya kutakiwa kujirekebisha," alisema kiongozi huyo.
Kuhusu suala la Emmanuel Okwi, chanzo hicho kilidai uongozi ulimsikiliza na uamuzi zaidi utachukuliwa hapo baadaye.
Search This Blog
Friday, January 27, 2012
COSTA ARUDISHWA KIKOSINI NA MASHARTI YA KUKATWA NUSU MSHAHARA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment