Chairman wa Kamati ya Ligi, Wallace Karia amethibisha Azam, Mtibwa Sugar na Simba kwa pamoja zinalidai Shirikisho la Soka Tanzania zaidi ya shilingi 63 milioni kati ya sh 121 milioni inazodai TFF huku akisema klabu nyingine za Ligi Kuu zinadai pia.
Klabu ya Azam inaongoza kwa kudai sh 24,066, 619 huku Mtibwa Sugar ikishika nafasi ya pili kwa kudai sh 20,976,426 wakati Simba inakamata nafasi ya tatu kwa kudai sh 19, 731,887 na timu ya JKT Oljoro ikidai kidogo zaidi sh 465.
Tathmini iliyofanywa hivi karibuni na Kamati mpya ya kuendesha ligi hiyo iliyoteuliwa na rais wa TFF, Leodegar Tenga na Mwenyekiti wake Karia imebaini kuwa klabu zote 14 zinaidai TFF jumla ya shilingi 121,979,048.
Fedha zinazodaiwa na klabu hizo na klabu za Ligi Kuu ni zawadi na fedha za nauli za maandalizi zinazotolewa na wadhamini wa Ligi hiyo kampuni ya simu ya mkononi ya Vodacom.
Kwa upande wa Azam wanadai fedha za zawadi ya mshindi wa tatu wa Ligi msimu wa 2009/10, Sh10 mil ni fedha za udhamini wa Vodacom na sh 4, 789,166 za mgawo wa mwezi Novemba mwaka jana.
Simba inaidai TFF, sh 19,731,887mil na kati ya hizo Sh 8mil ni za zawadi ya ushindi wa pili Kombe la Kagame lililofanyika katikati ya mwaka jana, Sh 6mil ni baki la mshindi wa pili wa zawadi ya Ligi Kuu msimu wa 2009/10.
Pia, sh 4 mil ni ambazo zimetokana na tiketi walizochukua kwenye pambano la Simba na TP Mazembe mapema mwaka jana.
Mbali na timu hizo timu nyingine zinazoidai TFF na madeni yao kwenye mabano ni Ruvu Shooting (sh 15,137,507ml), Kagera Sugar (Sh 14,725,431ml), Yanga (Sh 9,323,322ml), Polisi Dodoma (Sh 8,359,621ml), Moro United (Sh 5,653,074ml), Toto Afrika (sh 3,255,650), Ruvu JKT (sh 3,255,650) Samai Magereza - Tanzania Prisons (Sh 3,228,512), AFC (sh 2,005,400), Maji Maji (Sh 2,462,334), Afrika Lyon (Sh 1,878,631ml), Villa Squad (Sh 1,907,738ml) na Coastal Union (Sh 532,535).
Search This Blog
Friday, January 27, 2012
AZAM NA SIMBA ZAONGOZA KUDAI MAMILIONI TFF
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment