Wakati dirisha la usajili barani ulaya, tumekuwa tukishuhudia ligi kuu ya England ikiendelea kufanya kufuru katika uhamisho wa wachezaji kutoka klabu moja hadi nyingine.
Recently tumeshuhudia Sunderland wakitumia Paundi million 8 kwa ajili ya mchezaji mwenye umri wa miaka 18, Cannor Wickham, huku Manchester United wakilipa mara mbili ya pesa hiyo kwa Phil Jones kutoka Blackburn.
Sasa tuangalie historia ya uhamisho ghali wa wachezaji makinda chini ya miaka 20 katika ligi kuu ya England.
10 - ROBBIE KEAN: WOLVES KWENDA COVENTRY (£6m)
Wolves wahitaji kunona kwa bank account yao ili kuweza kumwachia kijana wao wa ki-Irish na Coventry wakawajaza manoti.£6m ilikuwa ni rekodi ya usajili wa mchezaji kinda Robbie Kean mwaka 1999 akiwa na miaka 19 ambapo Coventry a.k.a Sky Blue walipomchukua kutoka Wolves.Hata hivyo ilikuja kuwa biashara nzuri kwa upande wa Coventry baada ya kocha wa Marcelo Lippi wa vigogo wa jiji la milan, Inter kulipa £13m kwa ajili Kean mwaka 2000.
9 - GLEN JOHNSON: WEST HAM KWENDA CHELSEA (£6m)
Akiwa na miaka 18, beki wa kulia alikuwa tayari ameshaichezea mechi 15 klabu yake ya West Ham kabla ya Chelsea kumchukua mwaka 2003 na kumfanya kuwa ndio mchezaji wa kwanza kusajiliwa chini ya utawala wa Roman Abramovich.Johnson ndiye mchezaji kinda ghali zaidi kuwahi kusajiliwa na Chelsea, lakini Jose Mourinho alipoingia Stamford Bridge alimuuza kwa Portsmouth.
8 - FABIAN DELPH: LEEDS KWENDA ASTON VILLA (£6m)
Ilikuwa ni kama nusu ya timu zote za EPL zilikuwa zinataka saini ya Delph katika kipindi kama hiki mwaka 2009.Kijana huyu aliyezaliwa Bradford alikuwa lulu katika kipindi cha usajili lakini hatimaye Aston Villa ilifanikiwa kupata saini ya kiungo huyu ambaye kipindi hicho alikuwa na umri wa miaka
7 . GARETH BALE: SOUTHMPTON KWENDA TOTTENHAM(£5m mpaka £10m)
Mwaka 2006, akiwa na miaka 17, Welsh-full back alikuwa katika kiwango kizuri ndani ya kikosi cha Southmpton, akiwa mtalaam wa mipira iliyokufa.
Man United walimtaka lakini Bale aliamua kwenda London na akasaini Tottenham kwa £5m katika hatua za mwanzo lakini baadae Spurs walilipa £10m kutokana na mafanikio atakayoyapata mchezaji husika.Usajili wa Bale kwa Spurs umekuwa na faida nyingi akiisaidia timu yake kucheza robo fainali ya klabu bingwa ya ulaya msimu uliopita, pia amekuwa mchezaji bora wa ligi kuu kwa chama ya wachezaji soka nchini England.
6- CONNOR WICKHAM: IPSWICH KWENDA SUNDERLAND(£8m mpaka £12M)
Japokuwa alikuwa akifuatilia na timu nyingi za ligi kuu tangu alipopata nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha Ipswich misimu miwili iliyopita.Wickham mwenye umri wa miaka 18, alikuwa moja ya washambuliaji waliounda safu ya mashambulizi ya kikosi cha England under 21 kilichoshiriki katika michuano ya EURO UNDER 21 iliyofanyika Denmark wiki kadhaa zilizopita.
5 - THEO WALCOTT: SOUTHMPTON KWENDA ARSENAL (£9m)
Alikuwa ni roomate na Gareth Bale wakiwa katika Academy ya Southmpton, lakini yeye aliamua kutofautiana na rafiki yake Bale baada ya kuamu a kwenda upande mwingine wa jiji la London.Walcott alijiunga na Arsenal mwaka 2006 kwa usajili uliowagharimu pesa nyingi Gunners, akiwa na miaka 16 alikuwa akizivutiaa na timu za Man United, Tottenham, Chelsea na Liverpool.Walcott alitawala katika vyombo vya habari pindi Sven Goran Eriksson alipomuita katika kikosi cha timu ya taifa ya wakubwa kilichoshiriki World Cup mwaka 2006-German ingawa hakucheza hata mechi moja.
4 - CRISTIANO RONALDO: SPORTING LISBON > MAN UNITED (£12M)
Liverpool na Arsenal zote zilikuwa zikimtaka lakini Manchester United hatimaye walimnyakua mwaka 2003 baada ya kucheza dhidi ya Red Devils katika mechi za pre season.Walikuwa ni wachezaji wa United waliomshawishi bosi wao amsajili Ronaldo, na hatimaye United walilipa paundi millioni 12 kumchukua Ronnie ambaye kipindi hicho alikuwa na umri wa miaka 18.United wamepata faida ya zaidi ya £68m baada ya Real Madrid kulipa £80m mwaka 2009 kupata saini ya mreno huyo.
3 - PHIL JONES: BLACKBURN > MAN UNITED (16.5M)
Mechi 35 alizocheza akiwa na kikosi cha Blackburn zilitosha kumshawishi kuvunja benki na kutoa £16.5m kupata saini ya beki wa kati mwenye umri wa miaka 19, Phil Jones.
Usajili wa Jones ambaye Liverpool na Arsenal walikuwa tayari kulipa pesa ili kupata saini muingereza huyu ulipata baraka kubwa kutoka kwa Wayne Rooney aliyesema "Jones ni moja ya mabeki wagumu kukabiliana nao".
2 - ANDERSON: PORTO > MANCHESTER UTD(£18M)
Inaweza kushangaza kujua kwamba alinunuliwa kwa gharama ya paundi million 18, £6m zaidi ya Cristiano Ronaldo, lakini ndio ukweli wenyewe.Kiungo huyu mbrazili kutoka Porto aligharimu zaidi United zaidi mchezaji bora wa dunia wa 2008, akiwa na miaka 19, Anderson alimvutia Sir Alex Ferguson na kumfanya mscotish kufungua pochi kwa ajili yake.Amekuwa sio mchezaji wa kikosi cha kwanza mara kwa mara, na mara kadhaa amehusishwa na kuondoka O.T lakini ni vigumu sana kuamini kama United watarudisha fedha waliyomnunulia ikiwa wataamua kumuuza.
1 - WAYNE ROONEY: EVERTON > MAN UNITED - £27M
Moja ya usajili mwingine ambao Sir Alex Ferguson hatokaa kamwe kujilaumu kuufanya ni usajili wa nguzo ya klabu ya United na timu ya taifa ya England, Wayne Mark Rooney.
Alisajiliwa na United katika siku ya mwisho wa usajili mwaka mwaka 2004 baada ya kuwa kiwango kizuri katika timu ya taifa ndani ya EURO 2004.Akiwa na miaka 18 alishacheza misimu miwili ya EPL katika klabu ya Everton.Ameisadia United kushinda makombe manne ya EPL PLUS UEFA Champions League.