Yakiwa yamesalia masaa machache kabla ya mpambano kati ya David Haye na Vladmir Klitschko kila mtu amejaribu kutoa utabiri wake kuhusu nani atafanya nini kwenye pambano hilo lakini mabondia mbalimbali kwa upande wao wanasemaje ?
MIKE TYSON
BINGWA WA ZAMANI WA UZITO WA JUU.(Klitschko atashinda)
“Haye hataweza kudumu zaidi raundi mbili . Napenda jinsi Haye anavyopambana lakini nadhani Klityschko atakuwa amemzidi sana na hilo litaonekana , sidhani kama Haye atakuwa na mbinu za kutosha kumzuia Klitschko, ni wazi kuwa Klitschko atamchapa kisawasawa.
Bingwa wa WBA light-welterweight, Amir Khan: DAVID HAYE
“David Haye ni bondia mwenye staili ya kusisimua sana ya kupigana kwa sasa tangu enzi za Lenox Lewis . Najua kuwa Klitschko ana nguvu sana kumshinda Haye ila David ana ‘movement’ nzuri sana na kasi yake pia inaweza kumdhuru Klitschko , nadhani David atashinda kwenye raundi za mwisho.
Bingwa wa WBC super-middleweight Carl Froch: DAVID HAYE
"Nampa nafasi kubwa David Haye . Vladmir ni mrefu , ana nguvu na staili ya kupambana ya ajabu kidogo na kiukweli ni hatari kwa David . Ila jinsi anavyopigana David ndio sababu inayonifanya nimpe nafasi , nadhani anajiamini sana na atampa tabu Vladmir kwa sababu Haye si mtu wa kurudi nyuma , akija anakuja kweli na haangalii nyuma , nadhani ni kitu ambacho Vladmir hatarajii ila kinaweza tokea na ikiwa hivyo Vladmir atapata tabu sana"
Bingwa wa zamani wa uzito wa juu duniani . Lennox Lewis: DAVID HAYE
“On paper , Klitschko ni mtu ambaye wengi watampa nafasi kubwa kwa sababu anamzidi Haye kwa karibu kila kitu na ni bondia halisi wa uzito wa juu tofauti na Haye .Lakini kama Haye akiingia na mpango thabiti wa kumkabili Vladmir kama ambavyo amekuwa akifanya kwenye mapambano ya nyuma ana nafasi ya kufanya vizuri.
Bingwa wa zamani wa super-middleweight king na Ring magazine light-heavyweight
Joe Calzaghe: DAVID HAYE
“Vladmir ni mkubwa na ana mkono unaofika mbali na ana kila kitu ambacho Haye hana .David Haye ana kasi ya ajabu , na ana uwezo wa kuskuma makonde kwa Klitschko , na pia Klitschko si bonida sugu kwa sababu anadondoka kirahisi hata ukitazama kwenye mapambano ya nyuma amewahi kudondoshwa mara zisizopungua kumi . Kama akimuotea vizuri , David ana nafasi kubwa ya kushinda .
Promota wa ngumi za kulipwa Frank Warren: WLADIMIR KLITSCHKO
“Kwangu Klitschko ana nafasi kubwa ya kushinda. Kwanza ana umbo kubwa ambalo ni faida , najua wengi watasema kuwa hata Nikolay Valuev alikuwa mkubwa kwa Haye na akashinda lakini Vladmir ana uwezo halisi wa kupigana kuliko Nikolay , ngumi zake ni kali mno , sioni Haye akimzuia .
Mshindi wa medali ya dhahabu kwenye Olimpiki . James De Gale: WLADIMIR KLITSCHKO
“Unapopambana na yoyote kati ya wanandugu wa wawili wa Klitschko mjini Hamburg ujue huna nafasi ya kushinda hata kidogo , itakuwa ngumu sana kwa Haye kushinda , Naona kabisa jinsi Vladmir atakavyomuangusha Haye kwenye raundi za mwisho . Amemzidi kila kitu kuanzia umbo , uwezo na akili ya mchezo wa ndondi na kiukweli ni ngumu sana kwake kushindwa kumchapa Haye hapa. Ila huwezi jua kinachohitajika kushinda pambano la ngumi kama hili ni ngumi moja tu kali kama ilivyokuwa kwenye pambano la kwanza la Lewis na Rahman na Haye anao uwezo wa kufanya hivyo , ila sidhani kama tutaona maajabu hayo , namuona Klitschko akimuangusha Haye mara kama nne hivi kabla refa hajasimamisha pambano . Haye ana kasi ila ni bondia wa uzito wa juu mdogo na tunajua yanayowakuta mabondia kama hao .
Hayo ndio maneno ya mabondia mbalimbali juu ya pambano la leo , muda unazidi kwenda , tumgoje kuona kama itakuwa Haye au Vladmir .
No comments:
Post a Comment