Search This Blog

Thursday, June 30, 2011

Thomas Ulimwengu: Nampenda sana ALICIA KEYS.

Number 10: Umezaliwa mwaka gani na wapi?
Ulimwengu: Nimezaliwa tarehe 14/6/1993, Dodoma .

Number 10: Ulianza kucheza timu gani kabla ya kujiunga na Moro United?
Ulimwengu: Nilitokea katika michuano ya Copa Coca Cola 2008, nikitokea Dodoma baada ya michuano nikaitwa Tanzania Soccer Academy ndipo nilipoenda Moro United.

Number 10: Wakati unakua ni timu gani ulikuwa ukiipenda sana hadi sasa?
Ulimwengu: Manchester United ya England .

Number 10: Unapokuwa uwanjani kitu gani hutumia kama silaha kwako?
Ulimwengu: Kasi (speed) na kupia mashuti makali niwapo uwanjani

Number 10: Mapungufu gani umeyagundua pindi uwapo uwanjani?
Ulimwengu: Nasumbuliwa sana na mabeki wa timu pinzani japokuwa sipendi hali hiyo.

Number 10: Mchezaji gani unamchukulia kama shujaa kwako?
Ulimwengu: Didier Drogba wa Chelsea na Mussa Hassan Mgosi wa Simba.

Number 10: Nini matarajio yako katika mpira wa miguu?
Ulimwengu: Kuwa mchezaji wa kulipwa nje ya nchi.





Number 10: Katika kucheza mpira ni siku gani ulihuzunika sana ?
Ulimwengu: Siku nilipoumia nyonga, nilipata maumivu makali sana sitakuja kusahau.

Number 10: Kitu gani kilikushawishi hadi ukaamua kuwa mchezaji?
Ulimwengu: Mpira ulikuwa ni ndoto yangu hivyo nilitaka siku moja kuitimiza.

Number 10: Nani alikushawishi uendelee kucheza mpira?
Ulimwengu: Marafiki zangu mbalimbali walinishauri, nikaamua kuendelea.

Number 10: Ulijisikiaje ulipoanza mazoezi na Tanzania Soccer Academy ?
Ulimwengu: Nilijisikia furaha na kuamini kuwa ndoto zangu za kuwa mchezaji zinaanza kutimia.

Number 10: Kwanini uliamua kuvaa jezi namba 11?
Ulimwengu: Kutokana na washambuliaji wengi kuvaa namba 11 nami nikiwa mshambuliaji nikaona nastahili kuvaa namba hiyo.
Number 10: Mchezaji gani unamuona bora kwa sasa?
Ulimwengu: Didier Drogba wa Chelsea

Number 10: Mchezaji yupi unamuona mtukutu lakini anafurahisha na kuwa kiburudisho katika timu?
Ulimwengu: Ni Keiko Master, tupo naye TSA huyu ni mtundu kupita kiasi ila ni muhimu sana katika kikosi chetu.

Number 10: Unapenda aina gani ya muziki pindi unapokuwa umepumzika?



Brad Pitt


Ulimwengu: Muziki wa taratibu ‘blues’, napenda pia nyimbo za mwanamuziki Timberland wa Marekani.

Number 10? Ukifanikiwa kupata fedha ungependa kununua gari aina gani?
Ulimwengu: Napenda sana Range , ni gari zuri sana hasa kwa barabara zetu hapa Tanzania .

Number 10: Mwanadada gani unamhusudu sana ?
Ulimwengu: Nampenda sana mwanamuziki anayeitwa Alicia Keys, anaimba vizuri sana .

Number 10: Ni filamu ipi unaipenda na kwa nini?
Ulimwengu: Napenda filamu ya Mr and Mrs Smith ya Angelina Jolie na Brad Pitt inafundisha na kuburudisha hasa kwa vijana.

Number 10: Unaweza kutueleza jambo lolote tusilolifahamu kuhusu wewe:
Ulimwengu: Sipendi kuongea ongea kila mara, mimi ni mkimya sana ila marafiki zangu hawalijui hilo .

Number 10: Unaonekana bado kijana mdogo, unasoma?
Ulimwengu: Nimemaliza kidato cha nne mwaka jana 2009.
Number 10: Kama usingekuwa mwanamichezo ungependa ufanye kazi gani?
Ulimwengu: Nilipenda kuwa mchezaji hivyo sikupanga kufanya kazi nyingine

Number 10: Ukipata nafasi ya kuchagua mchezaji wa kucheza nae, ungependa ucheze na nani?
Ulimwengu: Ningependa kucheza na mchezaji Steven Gerrard kwa kuwa ana uwezo wa kutoa pasi vizuri.



Alicia Keys


Number 10: Kipindi gani cha runinga cha vijana unachokipenda?
Ulimwengu: Vipindi vyote vya michezo, pia taarifa za habari za michezo.

Number 10: Kipindi gani cha michezo cha redio unachopenda kukisikiliza?
Ulimwengu: Sports Extra cha Clouds FM watangazaji wanajua kuchambua michezo kwa ufasaha.



SOURCE: NUMBER10 FOOTBALL MAGAZINE.


1 comment:

  1. Safi sana Thomas....kaza buti,mazoezi ndo silaha yako,usibweteke....all in all make ur dream 2 become true

    ReplyDelete