Dunia nzima inazizima kwa msisimko ikingojea kwa hamu pambano la masumbwi la uzito wa juu baina ya Wladmir Klitschko toka Ukraine na David Haye toka England.Ni vigumu sana kutabiri mshindi wa pambano hili kwa sababu kila mmoja anafaida ambazo zinaweza kumsaida kupata ushindi na kila mmoja ana mapungufu ambayo yanaweza kumpa mpinzani wake faida hivyo mpaka sasa kila mtu ana ‘chance’ ya kushinda 50-50.
Ila katika hali halisi ya mtazamo wa rekodi za mabondi hawa wawili ni dhahiri kuwa Wladmir Klitschko ana angalau faida ya silimia chache dhidi ya Haye , faida hiyo ni rekodi bora ya kushinda mapambano 55 na kupoteza mapambano matatu na ukweli kuwa yeye ndiye bondia wa uzito wa juu aliyeshikilia mkanda kwa muda mrefu kuliko wote kwenye historia ya mchezo . Faida hizi zinamaanisha kuwa Wladmir Klitschko ana uzoefu mkubwa sana katika ngazi hii kuliko Haye . Turudi nyuma kidogo , kwenye rekodi hiyo hiyo utona kuwa Wladmir amepoteza mapambano matatu na mara ya mwisho kupoteza pambano ilikuwa miaka 7 iliyopita .Wladmir ni bondia wa aina yake na ndio maana kwa muda mrefu amekuwa hana mpinzani , na katika mapambano haya matatu aliyopoteza aliyapoteza haswa kwani kwa umahiri alio nao Wladmir basi hao jamaa waliompiga kweli jasho liliwatoka .

Ross Puritty, raundi ya 11, 5 Desemba 1998, Kiev
Vladimir Klitschko alikutana na dhahama la kipigo kwamara ya kwanza toka kwa Ross Purity, Katika pambano lililopigwa tarehe 5 desemba mwaka 1998 huko Kiev Ukraine nyumbani kwao kina Klitschko Ross Purity alimsimamisha Wladmir kwenye raundi ya 11. Kwa maneno yake mwenyewe Ross anasema kuwa hakujiandaa kwa pambano hili kwani halikuwa kwenye ratiba na lilitokea tu kwa sababu bondia aliyekuwa apigane na Wladmir alimumia na kujitoa kwenye pambano hivyo kuokoa mamilioni ya fedha za udhamini Ross Purity aliletwa kujaza nafasi . Mazingira ya hali ya hewa ya baridi yalimpa tabu sana Ross kwa kuwa hajazoea mazingira hayo na ukizingatia ukweli kuwa hakupata hata wiki mbili za kujiandaa aliambiwa tu kuwa wiki ijayo utaenda kiev kupigana na wala hakupata hata muda wa kutazama mikanda ya mapambano ya nyuma ya Wladmir na wala hakujua anaenda kukutana na bondia wa aiana gani ili aandae mbinu za kumkabili . Katika mazingira kama haya ‘game plan’ ya Ross Purity ilikuwa si kujaribu kutafuta ushindi kwa kutupa makonde mfululizo bali kumzuia Wladmir asimwangushe kwa makonde yake . Alichofanbya Ross ni kuweka guard muda wote , kuzuia ngumi za Wladmir zisimdhuru , hi iliimaanisha kuwa Wladmir alikuwa anshinda kwenye kila raundi kwa kuwa Ross alikuwa hatupi makonde ambayo yangempa pointi , ila hayo yalienda hadi raundi ya 11 ambapo Wladmir alikuwa amechoka na kona yake ikaomba pambano lisimamishwe na Ross Purity akapewa ushindi wa TKO yaani technical knock-out . Kimsingi kilichompa ushindi Ross ni ukweli kwamba Wladmir alitupa makonde mpaka kufikia hatua ambapo hakuweza tena kutupa konde kwa sababu alikuwa amechoka vibaya na akashindwa kuendelea . Uzoefu wa Ross Purity kumsoma Wladmir na kujua kuwa anachotakiwa kufanya ni kumchosha ndio ilikuwa siri ya ushindi wake.
Corrie Sanders, raundi TKO, 8 Machi 2003, Hanover
Mara nyingine ambayo Wladmir alikutana na kipondo ilikuwa tarehe 8 machi mwaka 2003 ambapo aligongwa na Corrie Sanders kwenye raundi ya pili ya pambano lililofanyika huko Hannover Ujerumani . Corrie Sanders alikuwa hajapata fight yoyote kwa muda wa takribani miaka miwili na hivyo katika hali ya kawaida hakuwa kwenye condition ya kimchezo . Ila kwenye mazoezi yake , Corrie alipigana na mabondia wenye maumbo makubwa na hilo lilimsaidia sana kwa sababu alipata mbinu za ziada za kumkabili mpinzani wake(Wladmir) ambaye naye ana umbo kubwa .Alichoona Corrie na kukitumia na footwork na movement mbovu za Wladmir ambazo ni kwa sababu ya umbo lake kubwa na pia wakati ambapo pambano linakuwa gumu kwake Wladmir hupandwa na hasira na anashindwa kufocus kwenye pambano jambalo ambalo linampunguza makali kwa kiwango kikubwa sana na kwa hilo Corrie aliongeza presha na kasi ambayo ilimshinda kabisa Wladmir na kumfanya apoteza pambano katika staili mbaya kuliko mapambano yote aliyopoteza . Corrie anasema kuwa “unapopigana na Wladmir unapaswa kutumia akili nyingi sana, ongeza presha kwa kutupa makonde , kwepa sana kwa kutumia movement ya miguu ambayo yeye mwenyewe hana na wakati mwignine unapaswa kumngoja aje kwa sababu pambano linapokuwa gumu anakuwa anapoteza focus na anakuja kwa hasira jambo ambalo linamfanya asiweke guard na hapo ndio unapopaswa kuchukua ushindi wako ”Anachosema Corrie Sanders ndio kitu alichokifanya kwenye pambano lao na hakika yote hayo yalitokea kwani Wladmir alipigwa ndani ya Raundi tatu. Aliangushwa mara ya kwanza na akasimama kwa hasira na pambano lilipoendelea akaja kwa nguvu zote akijaribu kudhihirisha kuwa Corrie hakumuumiza alipomuangusha na hilo lilimgharimu mno kwani kama hakuumizwa mara ya kwanza basi hakika aliumizwa mara ya pili na mwamuzi akasimamisha pambano .
Lamon Brewster, raundi TKO, 10 April 2004, Las Vegas
Mara ya mwisho Wladmir kushindwa mchezo ilikuwa mwezi aprili tarehe 10 mwaka 2004 huko Las Vegas dhidi ya Lamon Brewster . Lamon aliingia kwenye pambano hili dhidi ya Wladmir akiwa na mpango madhubuti na akiwa amejiandaa vya kutosha. Brewster alijua wazi kuwa hawezi kushinda kutupa makonde na Wladmir kwa sababu Wladmir ana akili na nguvu nyingi na anavitumia vitu hivyo kwa utaalamu mkubwa . Lamon alitazama mapambano karibu yote ya nyuma ya Wladmir na kujaribu kucheza na mapungufu yake . Nilitazama pambano lake dhidi ya Ray Mercer lililochezwa juni 2002 ambapo Wladmir alishinda kwenye raundi ya sita . Katika pambano hili Ray Mercer alikuwa anamshambulia sana Wladmir na japo alishinda lakini alishinda huku akiwa amechoka sana , hivyo alichofanya Lamon ni kufanya kama Ray kwa kuwa yeye ni mdogo kuliko Ray Mercer kwa tofauti ya miaka 12 na alikuwa na mbinu bora zaidi ya Ray na uwezo wa kuzitumia mbinu hiozo kwa sababu ya umri na u-fit wa mwili hivyo aliamini kuwa kama Ray Mercer alimchosha kiasi kile basi Lamon angekuwa na nafasi zaidi ya kumpiga Wladmir . Kama ilivyokuwa kwenye pambano la kwanza alilopoteza Wladmir alipigwa na Lamon kwa kuwa alilazimika kutupa makonde mengi ambayo yalimchosha sana kwa sababu Lamon alikuwa akimfuata sana karibu kila raundi na kumfanya aamini kuwa angeweza kumshinda na hivyo ili kumshinda Lamon Wladmir alitupa makonde mengi sana hali ambayo ilimchosha vibaya . Baada ya pambano hilo timu ya Klitschko ilitoa kisingizio kuwa alipewa sumu kwenye chakula (food poisoning) lakini ukweli ni kuwa Wladmir alijichosha mwenyewe kwenye raundi nne ambazo alitupa makonde mengi kupita uwezo wake mwenyewe na kwenye raundi ya tano Lamon alimmaliza .
Ni dhahiri kwamba Wladmir Klitschko ni mtihani mgumu kuliko yote aliyowahi kukutana nayo na atakayowahi kukutana nayo kijana wa Kiingereza David Haye . Wengi wanaamini kuwa bondia mrefu kuliko wote Nikolay Valuev alikuwa mtihani mgumu kwa haye lakini si hivyo kwa sababu Valuev ni mvivu sana , hana movement nzuri, yuko slow tofauti na Haye ambaye ni kinyume cha hapo kwani yeye ni mwepesi zaidi na ana kasi ya ajabu hivyo alimmudu vyema Valuev . Wladmir Klitschko ni mtu mwenye uzoefu mkubwa sana , na amejifunza kutokana na mapambano ambayo amepoteza na ndio maana kwa miaka saba sasa hajapoteza mchezo wowote , amejijenga na kuyadhibiti mapungufu yake ambayo yalimfanya apoteze michezo hiyo mitatu pekee aliyopoteza hadi leo hii na ndio maana ili kushinda David ana kazi kubwa ya kufanya .
Upande wa pili kambi ya Klitschko imekiri kuwa kijana wao hajawahi kukutana na mtu ambaye anajiamini kama Haye , hii inamaanisha kuwa maneno ambayo Haye amekuwa akiyatoa kumkejeli Wladmir yamemuingia kichwani na yanamsumbua jambo ambalo huenda likampa Haye faida kisaikolojia kwani anampotezea Wladmir focus ya mchezo . Gwiji wa ngumi wa England Lenox Lewis amesema kuwa kama Haye anataka kushinda basi lazima ahakikishe anamchapa Wladmir kwa knock out kwa sababu ni njia hiyo pekee ambayo itampa ushindi kwa sababu akisema awategemee majaji na mwamuzi hali itakuwa ngumu kwake kwani anaenda Ujerumani kama mgeni na Wladmir yuko nyumbani hivyo kuna uwezekano mkubwa kuwa maamuzi makubwa yatakuwa ya faida kwa bondia wa nyumbani . Gwiji mwingine Mike Tyson yeye amesema kuwa haoni ni jinsi gani Haye anaweza kumshinda Bondia kwenye mchanganyiko wa nguvu na akili kaka Wladmir Klitschko . Sababu yake kuu ni uzoefu alio nao kijana toka Ukraine .
Ukweli kuwa hatutashuhudia pambano jingine kama hili kwa muda mrefu sana kama ambavyo imetuchukua miaka trakribani 10 kupata pambano hili ni kitu kitakacholifanya liwe la kipekee , na kwenye boxing tuna msemo mmoja unaosema kuwa “the punches will be the only talk when tha rounds begin” yaani makonde ndio pekee yatakayotoa sauti wakati raundi zikianza na hapo ndio maneno na tambo zote zitakapofikia ukomo .

No comments:
Post a Comment