Iliwahi kutabiriwa miezi kadhaa iliyopita kwamba mshambuliaji wa Barcelona na Argentina Lionel Messi angeifikia rekodi ya mjerumani Gerd Muller aliyoiweka mwaka 1972 kwa kufunga mabao 85 katika mwaka mmoja.
Wakati kijana huyo mfupi alipofanikiwa kuifikia na kuivunja rekodi, kwa kufunga mabao 86 tarehe 9 Disemba mwaka huu, jamii ya soka iliachwa mdomo wazi kwa rekodi hii.
Sasa kwa takribani siku nne zilizopita kumekuwepo na maswali kadhaa yanayoizunguka rekodi hii ya ufungaji wa mabao mengi ndani ya mwaka mmoja.
Kwanza walikuwa chama cha soka cha Zambia ambacho kilisema kwamba gwiji wa soka wa nchi hiyo Godfrey Chitalu alifunga mabao 107 ndani ya kipindi cha mwaka 1972, rekodi ambayo imeifunika ile ya Messi.
Then, wakafuatia klabu ya Flamengo ya Brazil ambao walikuja wakasema kwamba mshambuliaji Zico alifunga mabao 89 katika kipindi chote cha mwaka 1979, namba ambayo ni zaidi ya rekodi ya Messi 9ingawa Messi anaweza kupita rekodi hiyo)
Hatimaye, wa mwisho ni hii rekodi mpya anayotajwa kuwa Pele alifunga mabao 127 mwaka 1959, rekodi ambayo inasapotiwa na FIFA katika wasifu kumhusu gwiji huyo wa soka wa Brazil.
Lakini pamoja na takwimu zote hizo, FIFA ambayo ndio taasisi kuu inayosimamia soka, imezungumzia suala hilo siku ya ijumaa: kwa kifupi hawazitambui rekodi za ufungaji za wakali hao.
Katika mahojiano na BBC Sport, msemaji wa FIFA Alex Stone alisema:
Kiujumla, rekodi ambayo Messi aliivunja haikuwa rasmi kwa maana ya kutotambuliwa na FIFA. Hivyo sio Messi wala Chitalu, wala Zico wala Pele atakuwa akitambuliwa kama mtu anayeshikilia rekodi hiyo ya ufungaji wa magoli mengi katika mwaka mmoja.
JE WADAU MNA MAONI GANI KUHUSU SUALA HILI.
Wakati kijana huyo mfupi alipofanikiwa kuifikia na kuivunja rekodi, kwa kufunga mabao 86 tarehe 9 Disemba mwaka huu, jamii ya soka iliachwa mdomo wazi kwa rekodi hii.
Sasa kwa takribani siku nne zilizopita kumekuwepo na maswali kadhaa yanayoizunguka rekodi hii ya ufungaji wa mabao mengi ndani ya mwaka mmoja.
Kwanza walikuwa chama cha soka cha Zambia ambacho kilisema kwamba gwiji wa soka wa nchi hiyo Godfrey Chitalu alifunga mabao 107 ndani ya kipindi cha mwaka 1972, rekodi ambayo imeifunika ile ya Messi.
Then, wakafuatia klabu ya Flamengo ya Brazil ambao walikuja wakasema kwamba mshambuliaji Zico alifunga mabao 89 katika kipindi chote cha mwaka 1979, namba ambayo ni zaidi ya rekodi ya Messi 9ingawa Messi anaweza kupita rekodi hiyo)
Hatimaye, wa mwisho ni hii rekodi mpya anayotajwa kuwa Pele alifunga mabao 127 mwaka 1959, rekodi ambayo inasapotiwa na FIFA katika wasifu kumhusu gwiji huyo wa soka wa Brazil.
Lakini pamoja na takwimu zote hizo, FIFA ambayo ndio taasisi kuu inayosimamia soka, imezungumzia suala hilo siku ya ijumaa: kwa kifupi hawazitambui rekodi za ufungaji za wakali hao.
Katika mahojiano na BBC Sport, msemaji wa FIFA Alex Stone alisema:
Hizi sio rekodi rasmi za FIFA.
Hatuna database ambayo inaweka rekodi zote za mchezo wa soka unaochezwa katika kila nchi dunaini kote kwa siku zote.
Hii haihusiani kabisa na kupendelea mtu - ikiwa tutaweza kuthibitisha kutoka kwenye michuano yetu tungependa kufanya hivyo.
Hizi ni data ambazo mashabiki na media wanapenda kuziona.
Ni rekodi ambayo mtu fulani kwenye vyombo vya habari alikusanya takwimu kutoka mahala fulani na kusema kwamba Messi amekaribia kuivunja rekodi hiyo.
JE WADAU MNA MAONI GANI KUHUSU SUALA HILI.
wana wivu na record za messi,cku zote hizi wakati vyombo vya habari zinasema messi anakaribia kuvunja record ya muller hao zfa na brazil na zico wao pmj na pele walikuwa wapi?wamesubir jamaa kavunja ndio wanaanza kujitokeza,cku zote dunia ilikuwa inatambua record sahihi ya magol ni ya muller,hivyo vyombo vingine vya soka kwann havijajitokeza na kusema no jamani kuna record hizi wamekaa kimya mpaka mtu anaifikia hiyo record ndio wanajitokeza,messi anastahili na sisi jamii ya soka tunatambua hilo kuwa messi ndio aliyevunja hizo record cha kujiuliza walitakiwa wasimpinge messi wangempinga muller so wamebugi,tangu 1972 wakati muller anatangazwa kuweka hiyo record zfa na zico na pele hawajaipinga wanawezaje kuipinga hii ya messi baada ya miaka 42?wivu wa kike jibu rahic
ReplyDeleteyote kwa yote Messi ni MKALI jamani! apewe haki yake maana alichokifanya si cha kawaida.
ReplyDeletebravo Messi!!
Hao ndo Fifa chama chenye maskani yake ulaya. MULLER mgerumani ndo maana haya yote yanatokea.
ReplyDeletePele,Messi na Zicco wote Amerika kusini pamoja na Ucar mtu mweusi tena mwaafrika je watatambulika vip mbele ya mzungu
Messi yupo juu na atazidi kuongeza rekodi zake duniani,rekodi y muller inajulikana mda mrefu hao zambia walikua wapi kwanza wangepinga rekodi ya muller wameona dogo anaweka cfa wanataka kumuharibia, CHITALU ATAKUA KAFUNGA MAGOLI MENGNE KWNY MAKOMBE Y MCHANGANI WAMEJUMUISHA
ReplyDelete"Like father like son!" FIFA na TFF wote yaleyale! sishangai kwa lolote linalotokea kwa Messi! Wote ni GENGE LA WAHUNI!
ReplyDeleteMapps.
yana hapo angekuwa mzungu mwenzao ingekuwa poa kwa kuwa wote ni black ndio kipingamizi
ReplyDeleteFifa acheni wivu kama mlitambua record ya MULLER iweje ya messi mshindwe kutambua? Kwa kuwa hata enzi za MULLER database haikutumika, mpeni haki yake messi dunia. hata msipompatia hatabaki kuwa bora duniani. messiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!
ReplyDeleteWazungu wamefaulu kwa ubaguzi,iweje Fifa watambue ligi aliyocheza Muller lkn mwaka 1972 wasitambue ligi anayocheza Messi 2012?
ReplyDeleteMimi nakubaliana na FIFA kabisa, inaudhi sana ukifuatilia jinsi tuzo na rekodi za soka zinavyokwenda. Kwanza huwezi kuwa mchezaji bora wa dunia kama huchezi club za Ulaya, hivyo mtu kama Ronaldo de Lima, Ronaldinho, Messi mwenyewe asingeweza kuwa mchezaji bora wa dunia kama wasingecheza Ulaya. Kuna wachezaji kibao wenye uwezo ila kwakuwa hawapo Spain, England, Italy nk kamwe hawawezi kuwa wachezaji bora. Pili, Mimi binafsi Messi namuona ni mshambuliaji wa kawaida tu ila anafunga mabao mengi kutokana na mfumo wa barca, ndio maana Argentina hana msaada sana. Ningependa kuona siku Messi akicheza kwenye club nyingine yenye viungo tofauti ndio nitajua uwezo wake. Hebu tumuangalie C.Ronaldo kwanza yeye sio mshambuliaji wa kati kama Messi pia alishaonyesha uwezo wake kwenye timu mbili tofauti zenye mifumo tofauti kabisa, hapo ndio utajua tofauti na ubora wa mchezaji. Najua mwisho wa mismu watu wataibuka na kusema Tito Valanova ni Kocha bora duniani! Je utakubaliana nao? Hivyo mimmi naona sawa tu tuachana na hizo rekodi
ReplyDeleteAise ndugu yangu, ushabiki wa messi na c. ronaldo ni kama imani we baki na unacho amini. Pili namna c.r anavyocheza hakuna cha tofauti style yake tumeshaiona kwa wengi like ,Ronadinho, De lima, na wengine wengi ingawa hawafikii hata chembe. Messi ni tofauti sana, style ya messi hutokea mara 1 baada ya miaka kama 65 hivi, niambie kwa sasahivi au hivi karibuni ni nani anacheza au alikuwa anacheza kama messi, control ya mpira, namna anavyo dribble, concentration yake akiwa na mpira, stamina haanguki hovyo kama c.r, akianguka ni foul kweli, namna anavyoscore magoli N.K Jamani mwacheni messi aitwe messi ni mtu wa tofauti kabisa hat C.R analitambua hilo sema ni ubishi tu hata kwao wanajua kuwa ni mbishi
Deletekelele hizi zilianza mapema sana za messi kukaribia hii record...kwanini walikaa kimya siku zote wasiseme kuwa hakuna record anayoikaribia???????..why now?
ReplyDeleteclassic
swali lingine...muller alifunga magoli 85 mwaka 1972....messi hadi leo kafunga zaidi ya magoli 85 kafunga 88..je hajavunja record ya muller?...ok fine may be warekebishe statement kuwa messi hajavunja record ya dunia cuz hawana database ila kavunja record ya muller which is clearly true!!
ReplyDeletewaache wivu...walijua hatoweza!!
classic
Ni kweli Andunje amevunja record ya Muller na inawezekana kabisa pele,zico au mwana SADC mwenzetu Chitalu wamefunga zaidi ila hawa wametoka ktk nchi ambazo hawatumii sana media kujitangaza,kilichomsaidia mr Andunje ni yupo ulaya media zinammulika kila siku ndo mana dunia yote inafaham alichokifanya,na tushukuru tu si muingereza maana angetokea uk tusingehema hiyo misifa hata kwenye utabiri wa hali ya hewa ingekuwa stori ya yeye tu,sasa huyo chitalu inawezekana kabisa wakat anafunga hapo zambia hata station ya tv ilikuwa hakuna.na Tff nao wanajiandaa kupeleka data zao fifa kuwa mnamo mwaka 1980 PETER TINO alifunga magoli 93 kwa hiyo andunje ni cha mtoto tu
ReplyDeleteYesse we nawe unaongelea ushabiki huongelei mpira, mbona Messi kwenye timu yake ya Taifa anatupia kama kawaida?kwani ipi ligi bora kati ya ile ya England na ya Spain hadi unasema mpaka acheze timu nyingne ndo ujue kama yeye ni bora?mbona Ronaldo wanacheza ligi moja kashindwa kumfikia?kwanza kumlinganisha Ronaldo na Messi ni kukosa kuona uhalisia wa mpira, umewah kumuona Messi akiwa na hasira uwanjani au akicheza rafu za kijinga kama anazocheza Ronaldo? Messi ni Messi tu kama mnamchukia mtaumia sana mwaka huu, ila ukweli utabaki palepale, kacheza club bora duniani bado mnaona gele, manataka acheze Wigan ndo mmmkubali?watu wengne mnachekesha kweli.
ReplyDeleteAnyway!Tatizo litabaki palepale kwa sisi wabongo, tunaongea sana kuliko vitendo. Kwanza sijui ubora wa ligi wewe unaangalia nini? Hilo ndio tatizo lakusoma magazeti ya Global Publisher, Juzi Chelsea imechapwa na Wakorinto toka Brazil ila kwa mawazo yako utasema Ligi ya England ni kubwa kuliko ya Brazil sababu ni kuwa unaangalia ligi ya England kuliko Brazil. Lingine nyie nyie ndio mnampenda Messi mpaka mnasema ni mwenzetu yaan ni kama Mwafrika mwenzetu, Mnasahau kuwa pia hao watu ni wabaguzi wa rangi vile vile, na mifano unayo! Au sio?
Deletewana wwivu tu hao wote. si ronaldo wala nani. Hizo takwimu wangezileta b4 hajafikisha hata magoli 80. sio eti kuvunja tunazozijua ndo watuletee mengine. wapuuzi na hawana lolote. Dogo mkali tena mbaaaaaaaaaaya messi mbaaaaaaaaaaaaya. hawaoni tu katika timu yake yeye pekee magoli alofunga jumla ni sawa na magoli ya wachezaji wa madrid 4 na ronaldo wao akiwemo. em mcheki dogo alivyomkali na bado eti hawamkubali!! hawanalolote hao
ReplyDeleteFIFA wako sahihi kabisa, kwani hawajasema kuwa messi hakuvunja rekodi ya muller ila wamesema hawazitambui rekodi za namna hiyo kwani hawana database ya nchi zote duniani kwa ajili ya kurekodi takwimu mbalimbali na kuzichanganua kwa pamoja, takwimu au rekodi kama ya messi haiwezi kuwekwa kwa kuangalia ligi zinazoonekana zinaushindani au ligi bora kama wengi wanavyofikiri ila rekodi hutambuliwa pasipo kuangalia ubora wa ligi, watu wanachanganya kwa kuwa messi amevunja rekodi ya muller ya mwaka 1972 na sio kwamba messi amefunga magoli mengi kuliko mchezaji mwingine yeyote yule duniani katika kalenda ya mwaka mmoja, kwa hiyo kina chitalu,pele,zico hawana cha kupinga kwani rekodi zao hazikufananishwa wala haziendani na rekodi ya muller ya barani ulaya, wangepinga endapo messi angetangazwa kuwa mchezaji aliyefunga magoli mengi kuliko mchezaji mwingine yeyote duniani kwa kuwa hakuna rekodi ya namna hiyo katika database ya FIFA. NA PIA NI MUHIMU KUZINGATIA CHANZO KILICHOTUNZA KUMBUKUMBU HIZO, JE NI CHA KUAMINIKA NA CHENYE MAMLAKA YA KUTUNZA REKODI HUSIKA? SI KILA MTU AJE NA TAKWIMU ZAKE AMBAZO HAZIJAHAKIKIWA NA MAMLAKA ZINAZOTAMBULIKA NA KUAMINIKA, TATIZO LA VIUMBE HAI WENGI HAWAJUI UMUHIMU NA MATUMIZI SAHIHI YA TAKWIMU SAHIHI.
ReplyDeleteMessi yuko hapo alipofikia, tujaribu kumkubali kwa hili alilonalo, kwa ufupi Messi kavunja record ya Muller na hili ndo muhimu, kuhusu takwimu za dunia nzima nazo tusubiri wakati wake.
ReplyDelete