MAONI KUHUSU USAJILI WA OKWI: MMEIFIKIRIA RUHUSA YA ANGALIZO KUTOKA FIFA KUHUSU OKWI?
Na Baraka Mbolembole
Emmanuel Okwi, mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uganda, ameruhusiwa kuichezea klabu yake ya Yanga na Shirikisho la Soka Ulimwenguni, FIFA. Awali, Okwi alizuiwa kuiwakilisha Yanga na kamati ya sheri na hadhi ya wachezaji ilimsimamisha kwa muda mchezaji huyo kuitumikia, Yanga ili kuulizia, FIFA uhalali wa mchezaji huyo kuichezea Yanga. Majuzi, FIFA, wametoa taarifa kuwa Okwi anaweza kuichezea klabu yake mpya kwa sasa, ila wakisema kuwa sheria itachukua mkondo wake endapo mchezaji huyo ataonekana ni tatizo katika ' ukungu' uliotawala katika usajili wake.
JE, OKWI ANAPASWA KUICHEZEA YANGA MSIMU HUU?.
Ndiyo, kama walivyosema, FIFA, Okwi amepewa ruhusa ila kitendo cha Yanga kumtumia kinaweza kuwaletea matatizo katika siku za mbele, endapo itabainika Okwi alifanya udanganyifu katika klabu yake ya awali, Etoile du Salehe ya Tunisia, ambao bado wanasisitiza kuwa mchezo huyo ni mali yao na hawajui alipo tangu, mwezi Mei, 2013.
TFF KATIKA MTEGO?
Wao wenyewe tayari wamesema kuwa watakaa na kulipitia suala hilo katika mtazamo wa ndani ya nchi. Shirikisho hilo la soka Nchini, limesema kuwa ruhusa ambayo FIFA, wametoa katika matumizi ya Okwi kwa wakati huu , wameikubali. Umejaribu kujiuliza itakuwaje siku za mbele mchezaji huyo akionekana ni tatizo?
Itavuruga mpira wa Tanzania, hasa endapo Yanga watakuwa wamemtumia katika michezo ya ligi kuu.Labda kwa vile kuna kumbukumbu kubwa mbaya kuhusu uvunjifu wa kanani na sheria mbalimbali katika soka la Tanzania, Yanga wakamtumia kwa kigezo cha kutumia udhaifu huo hata kama itakuja kugundulika kuwa mchezaji huyo ni ' batili kwao'. Ila, sheria iliwafunga katika suala la kumcheza mchezaji hasiyetakiwa katika mchezo, wakati wa mchezo dhidi ya Coastal Union, misimu miwili iliyopita. Walipoteza ushindi katika mchezo mgumu, kisa ilikuwa kumchezesha Nadir Haroub aliyekuwa na adhabu. Ni tofauti na suala hili la Okwi, ila wakati mwingine ni lazima tahadhari ichukuliwe mapema.
TFF, kusema kuwa watalitazama vizuri suala hili kwa ndani ya nchi kutokana na matatizo ambayo yanaweza kuja kutokea katika soka la Tanzania, endapo Okwi atacheza michezo yote ya timu yake ya Yanga na kuisaidia kushinda. Na baadae ikagundulika kuwa mchezaji huyo alikiuka mambo mengi na kuingia mitini bila taarifa, Yanga itakuwa katika nafasi gani?. Je, sheria ikishikilia mkondo wake itamaanisha nini?. Je, itakuwaje kuhusu matokeo yake?. Kiushabiki, Okwi ataanza kuitumikia Yanga haraka sana, ila kwa manufaa ya soka la Tanzania, ni lazima jambo hili lichunguzwe kwa kina kabla mchezaji huyo hajaanza kuichezea Yanga katika ligi ya ndani.
Wammchezeshe tu, katika michuano ya kimataifa kama wanahitaji kufanya ujinga wa kufikiri kimantiki. Ni kweli, tupo tayari kuvuruga mpira wa Tanzania kwa makosa ya mchezaji wa ng'ambo?. Huwezi kuona athari zake kwa sasa, sababu wote tumekuwa tukisukumwa mtazamo wa ' tambo na majisifu', wale mashabiki wa Yanga wamekuwa wakiwapiga vijembe mashabiki wa Simba, baada ya kupewa ruhusa ya angalizo kumtumia Okwi. WAmejitahidi kuweka hisia zao zote kwa Mganda huyo huku nao wakiwasukuma viongozi wao, ' kuwa kama noma na iwe noma, Okwi aichezee timu yao'. Na, acheze sasa. Ila wasije kuwatumpia lawama viongozi wao siku wakiambiwa kuwa kutokana na matumizi ya mchezaji huyo katika michezo ya ligi kuu, nafasi ya Yanga ni hii…..
UNAYAKUMBUKA, YA JAMAL MALINZI NA VICTOR COSTA?
Yanga walimsaini, Victor Costa kutoka Simba bila ruhusa ya klabu yake. Baadaye Jamal Malinzi, rai wa sasa wa TFF, akiwa kiongozi wa juu wa klabu yake ya Yanga. Aliingia uwanjani na Victor Costa na mchezaji huyo alikuwa amevaa jezi namba tano, yenye jina la DEWJI. Nini kilikuja kutokea?. Costa aliishia kuoneshwa kwa mashabiki wa mashabiki wa timu hiyo waliokuwa katika michuano ya MAPINDUZI CUP, huko Zanzibar na aliporudi Dar es Salaam, akaonekana katika mazoezi ya Simba akiwa na jezi namba tano, yenye jina la MALINZI. Ilimaanisha nini?
Tambo za viongozi wa juu wa klabu za Simba na Yanga, Kassim Dewji kwa upande wa Simna, na Malinzi kwa upande wa Yanga. Ulikuwa ni wakati ambao hata viongozi wa juu wa mpira wa Tanzania walikuwa wakifanya kazi yao kwa mapenzi ya klabu zao. Je, tunapaswa kuishi katika dunia yenye fikra kama hizo hadi wakati huu?. Suala la Okwi, ni tofauti na lile la Costa, na lipo mbali na lile na Nadir. ILA, Malinzi anaweza kutumia historia ya adhabu aliyoipata katika utawala wake Yanga hasa baada ya kuwaadaa mashabiki wa timu yake kwa kuwadanganya kuhusu usajili wa Costa, pia anaweza kuchukulia adhabu ambayo TFF, waliisimamia wakati Yanga walipomtumia, Nadir walikatwa pointi na kumaliza katika nafasi ya tatu.
Msimamo wangu kuhusu suala hili upo palepale, kuwa bado hakuna uthibitisho wa moja kwa moja kuhusu suala la uhamisho wa Okwi. Hila muda bado umebaki kidogo tu ili jibu hili kufumbuliwa kwa uhakika. Wenzentu hawazungumzi, Etoile wapo kimya, Fifa wametoa ruhusa ya angalizo, caf wamemruhusu, TFF, wanatafakari. Duuh! Huyu, Okwi ni zaidi ya wachezaji wote Tanzania. ILA, asifikie hatua ya kuharibu soka la Tanzania katika siku za mbele. CAF, ni wajanja waliitega TP Mezembe na kuiondoa kimizengwe, miaka mitatu iliyopita wapotoa ruhusa kwa mchezaji hasiye halali. Wakairudisha mashindanoni, W. Casablanca, ambayo iliitoa Simba na kufika hadi fainali na kufungwa na Esperance.
Subiri baada ya gemu ya Yanga na wale Waarabu. Nguvu iendane na fikra pia, mapenzi kila mtu anayo. Kwa suala la Okwi, Simba ipo karibu pia. Hila kwa sasa haliwahusu. Naisubiri jezi namba 25 ya Yanga kwa hamu kubwa. Okwi, ni mtihani au mtego kwa utawala wa Malinzi?. Tusubiri tuone kwa kuwa uchunguzi wa kitaalamu unaendelea, hivi ile miezi sita ya fifa inamalizika lini?. Okwi, mwenyewe kafunga mdomo, je anatambua kosa lake?. Au, hapendi kuzungumzia mambo yaliyopita?. Unakumbuka ila makala, ' Yanga wamemnunua wapi Emmanuel Okwi?', sasa nauliza, MMEIFIKIRIA RUHUSA YA ANGALIZO KUTOKA FIFA KUHUSU OKWI? Ata, macho yanapenda kutazama vitu vizuri, ila vitu vibaya pia huonekana.
0714 08 43 08
Hapa umakini wahitajika. mimi binafsi sitopenda kuona soka la Tanzania likiharibiwa.
ReplyDeleteMaelezo yako yana hoja ndani yake kama ingekua ni kwenye mfumo wa usajili wa kawaida..sababu mchezaji hawez uzwa bila ridhaa ya timu yake..swali la kujiuliza..Okwi alikuja Yanga akitoka Etoile au Villa?..Kama ni Villa umeshawah jiuliza Villa walimpata wapi Okwi?..Kibali cha Okwi walikipata wapi?..Lakini Jiulize Pia..CAF..shirikisho la mpira Africa lilimpitisha Okwi kucheza timu ipi?..Lakini pia FIFA waliombwa na TFF kupitia utaratibu upi na wao wamejibu kitu gani?
ReplyDeleteEmmanuel Okwi aliruhusiwa na FIFA kucheza villa..mmeshawauliza FIFA mipaka ya ruhusa yao kwa VILLA ilikua wapi?..na Kama villa walimuuza kwa Yanga walimuuza kwa ruhusa ya aliye wapa au walimuuza tuu bila kumtaarifu aliyewapa..ambaye ni FIFA..?
Kaka angalizo lako ni zito sana sema tunatawaliwa na kukidhi kiu ya mashabiki badala ya kutathmini kwa kina.
ReplyDeleteMY TAKE ON OKWI's TRANSFER
ReplyDelete================================================
>>>FIFA issued provisional permit for Okwi to play for VILLA
>>>FIFA assured FUFA on transfer compliance of Okwi to YANGA from VILLA. Bearing in mind that FIFA were aware of Okwi’s saga with his former club Etoile du Sahel. If Okwi’s contract with Etoile Du Sahel is still in enforceable, what were the bases of FIFA issuing provisional permit for Etoile du Sahel player (OKWI) to serve for another club (VILLA)?
>>>Again FIFA’s Players’ Status panel has RECENTLY authorized TFF to register Okwi for Yanga. While taking this course, FIFA had since then been dealing with complaints from Simba on payment disputes on SIGNING FEES as payable or to be paid by Etoile Du Sahel and another complaints are; Etoile against Okwi for contractual non-performance and Okwi against Etoile Du Sahel for Club ‘s failure to meet its contractual liability to pay the salaries and other monies as per contract.
>>>With all these complaints still under FIFA proceedings for VERDICT, FIFA has upheld Okwi’s transfer to Yanga.
>>>@Shaffih_Dauda was supposed to ask himself these questions before alerting otherwise TFF on this saga; Is it conceivable that FIFA has been authorizing Okwi transfer from Tunisia to Villa and then to YANGA without justifiable reasons and with blind eyes on the lodged complaints at their office? Does Shaffih K Dauda want to assert that FIFA has decided this issue while knowing that Okwi has valid contract with Etoil du Sahel till 2016 but FIFA opted to ignore the contract? If this the case do they play their role as the world football governing body?“ have they considered IRREPERABLE LOSS as would result for its future verdict to re-transfer Okwi back to Etoile Du Sahel? Verily, for serious entity like FIFA they might have satisfied themselves on all these questions and that is why in different occasions and circumstances their answer for FUFA and TFF have remained UNCHANGED with regards to Okwi status quo on transfer saga...
leo ndo umeandka nac kama jana ipo haja ya kutafakari
ReplyDeletesubiri matusi kwa wapenzi wa yanga
ReplyDeleteilo angalizo liko wapi?tupe basi hiyo nakala tuione kwanini unaficha barua kama unataka kutuweka sawa.tuache porojo fifa sio wajinga kama hao tff na walopokaji kama nyie
ReplyDeleteMliingia kwenye web site ya Etoile du Saile ktk list ya wachezaji wake walioidhinishwa na FIFA umeliona jina la Emmanuel Okwi? Au mna interest zenu? Pigeni tena simu Etoile Du saile muongee nao vizuri maana mna mna Jua kazi kuliko FIFA, poleni mtakonda sana mwaka huu.
ReplyDeletewatanzania si wanajua na tunaye rais wa soka mwenye kupenda maendelo ya soka?
ReplyDeleteBaraka hivi unadhani watu wote wanayo mkononi hiyo barua kutoka FIFA iliyo mruhusu Okwi kucheza Yanga? sasa tutachangia vipi mawazo yako? kwanza chapisha hiyo barua halafu tuache tuisome halafu tutatoa maoni yetu- Vinginevyo siye tunakuona kama ni mpinzani wa uamuzi huo kutoka katika chombo cha juu kabisa cha kusimamia mpira wa Miguu!
ReplyDeleteProvision transfer waliyotoa fifa kwa Villa kwasabab dirisha la usajili lilikuwa limefungwa. Sasa iv Yanga wako halali kumtumia sema inamuwia vigumu shafii kula matapishi yake na ndoto yake feki eti atarudishwa simba.. Kumbukeni issue ya Yondani huyu jamaa alisema yanga wameingia mkenge wakafurahi sana kwenye kipindi chao sports xtra lkn what hapened.
ReplyDeleteShaffih na wengineo ambao bado wana hofu na ruksa ya Fifa kwa kutafsiri vinginevyo, walikwisha kuwa na msimamo huo hata kabla fifa hawajatoa ruksa, tuwaache kama walivyo. YANGA wana Baraka zote tena za maandishi toka FIFA, CAF na TFF kuhusu kumtumia Okwi. Wasiwasi wa watani ni namna yanga inavyoimarika na hivyo kutishia their club.
ReplyDeleteKWA AKILIN ZENU MLIOPST MAKALA HII MKO FEKI KIMAWAZO NA UCHAMBUZ WENU,MARA NYINGI SHAFII DAUDA UMEKUWA MJUAJI,HUKU UCHAMBUZI WENU HAUFANIKIWI,MNATAKIWA KUSOMEA SAIKOLOJIA YA MPIRA,NA SIO KUIBUKA FROM NOW WHERE,BARUA SI IPO,KUNA ANGALIZO GANI,YANGA IMEMSAJIRI OKWI TOKA VILLA NA HAIJUI KAMA OKWI ALICHEZA ETOLE DU SAHEL,UHAMISHO WA YANGA UKO SAHIHI,UMEWAULIZA FIFA ,KATIKA SAKATA LA OKWI HAPA NCHINI HAKUNA ALIYECHAMBUA UKWELI HADI LEO.HAPO NDIO MJUE NYIE MNAOJIDAI WACHAMBUZ WA MPIRA HAPA BONGO WOTE HAMJUI SOKA,VIONGOZI WA YANGA WALIVYOSEMA NDIO MATOKEO/MAAMUZI YA FIFA YALIVYOTOKA!UNATUPA MIFANO YA KITOTO HALAFU UNAJIKANUSHA WEWE MWENYEWE,UKIWA MWANASHERIA SI UTAFUNGISHA WATU!KAMA MAAMUZI HAYA YAKO KIMAANDISHI,YANGA WAMCHEZESHE OKWI,SUALA LA OKWI KUSAJIRIWA YANGA LIMEKWISHA,CAF,WANAMTAMBUA OKWI NI MALI YA YANGA,FIFA WANAMTABUA OKWI NI WA YANGA,WATZ WANAJUA HIVYO,ILA WEWE UNAMASHAKA.USIANDIKE USICHOKIFAHAMU.0783540994
ReplyDeleteUkiandika kwa kufuata unavyoona wewe ni sawa kwa sbb kila mtu anaruhusiwa kutoa maoni au mawazo yake akiwa huru kwa mujibu wa katba ya nchi hii..tatizo lipo kwenye namna ya kulifikisha wazo au hoja husika mahala sahihi na wakti muafaka..ukiandika kwa interest zako tu tena zikiwa hazina mashiko weledi tunalishangaa..waandishi wengi wa TZ wavivu kutafuta habari za uhakika zaidi ya kukopi na ku paste habari kutoka kwenye mitandao usiyo rasmi..suala la Okwi linataka ufafanuzi yakinifu na wenye nukushi kadhaa..sikuamini kabisa Baraka,Kuna makosa mengi sn kwenye nyingi ya habari au taarifa zako bro..
ReplyDeleteDhamana mliyobeba ni kubwa sana lakn angalizo langu kwenu, mkumbuke kukanusha huu upotoshaji wenu maana km huyo mdhamini wako Shaffih anakjikuta akiongea non sense kwa uelewa wake mdogo. Mclazimishe watu washeinde kupitia vi article vyenu vicvyo na maana huna hata uwezo wa kutafsiri kisheria page moja tu ya transfer laws iliyopo FIFA ama kwa vile Tanzania mna uhuru wa vyombo vya habari ndo kila mkihisicho mnaandika? Tuwaache TFF wafanye kazi yao km wanaridhia acgeze atacheza na kama hawataridhia hadi pale kesi itapoisha basi haina tatizo lakn c nyinyi kutoa prior decision kwa mabo yacyowahusu.
ReplyDeleteNOTE:Nyinyi ni waandishi wa habari za michezo c watafsiri wa sheria wala kanuni za FIFA kuna watu wapo wanalipwa kwa kazi hiyo, msifanye kazi kwa mazoea
Hiyo barua ya angalizo ya FIFA ndo naickia kwako!!
ReplyDeleteInaonekana Etoile Du saile kuna maonevu flani imemfanyia okwi, hasa katika makubaliano yao ya mkataba. FIFA ikaliona hilo, ndo maana imeendelea kutoa maamuzi yanayoashiria kama kumlinda okwi. Etoile Du saile nao roho zao kama vile zinawasuta hivi, kwa walicho mfanyia okwi ambacho wao wenyewe wanajua, ndo maana wapo kimya huku wakifanya harakati za kuwalipa simba fedha zao. Pia FIFA wameona kesi ya OKWI na Etoile, inaonekana waz okwi ndo mwenye haki. Na kwakuwa kutoa maamuz itachukua muda, ikaona imruhusu Okwi andelee kucheza mpira kwa kigezo cha kulinda kiwango chake.
ReplyDeleteTatizo wote hao hawajui sheria zinazoendana na usajili,wanajaribu kuandika kwa mtazamo wao wa kimbumbu ili waonekane wanajuwa kuchambua masuala ya soka. Okwi sio mpumbavu alipoamua kuachana na Etoel du Sahel, ninyi mnaojifanya kujuwa uchambuzi muulizeni lawyer wa Okwi au Okwi mwenyewe juu ya hili suala,halafu nendeni FUFA, FIFA, TFF, YANGA, ETOEL DU SAHEL pia na chama cha football Tunisia then leteni uchambuzi wenu, suala hili limekaa kisheria zaidi sio kama mnavyochambua ninyi mnatuchosha wachangiaji,mnaonekana hamuelewi mnachokifanya zaidi ya kulazimisha mawazo yenu yaonekane ya maana
ReplyDeleteNafkiri hujalielewa angalizo la fifa ni kwanza suala la simba halipo fifa suala lililopo fifa ni la okwi na etolle du salle ambalo halijatolewa maamuzi hivyo fifa imetoa angalizo kwa matokeo ya shauri hilo na kwa kuwa wameruhusu elewa kwamba ruhusa ya fifa ni kanuni tayari.chochote kitakacho tokea mbele basi matokeo ya Yanga hayata athiriwa. Soma vizuri ruhusa hiyo nafikiri utaelewa.
ReplyDeleteAfadhali muwaambie hao makanjanja. Wanasoma kwenye mitandao halafu wanajipanga eti wachambuzi, thubutuuuuuuu!!!! they are empty headed!!!! ushabiki wa kihuni tu studio sijui mwenye nayo naye ni kabila lake huyu jamaa!!
ReplyDeleteHivi huyu mtu angekuwa mwandishi wa habari halisi si angesubiri TFF itoe uamuzi kwanza?kwa nini aningilia suiala ambalo liko mikononi mwa TFF? Ana maslahi gani kwenye usajili wa Okwi yanga kiasi kwamba atenge nafasi kubwa ya blog yake kuzungumzia suala hili ambalo mwamuzi wa mwisho ni TFF?ANATAKA KUTUONYESHA KWAMBA IWAPO ANGEFANIKIWA KUSHINDA KATIKA UCHAGUZI WA TFF huu ndio utaratibu ambao angeutumia kulazimisha maamuzi yafanyike jinsi anavyotaka yeye.Au anafanya hivi kibiashara ili blog yake ionekane ina wasomaji wengi na kuvutia watu kutangaza biashara zao kwenye blog yake.Nwashauri wachangiaji sasa tusitishe kuchangia mada hii kwani tunageuzwa mtaji
ReplyDeleteKaka boss wenu RAGE kasema anakupongeza kwa juhudi zako ulizoonyesha za kusema kuwa eti FIFA inawatega TFF na YANGA. Anyway tunasubiri kuona utabiri wa nabii Shafih Dauda ukitimia.
ReplyDelete