Taarifa zilizopatikana hivi punde zinasema FIFA imebaliki
taratibu za uhamisho wa mshambuliaji Emmanuel Okwi kutoka SC Villa kujiunga na
Yanga.
Taarifa kutoka ndani ya shirikisho la mpira wa miguu hapa
nchini TFF zinasema FIFA imemruhusu mchezaji huyo kuendelea kucheza, nakuhusu
suala la deni la Simba shirikisho hilo limesema bado linalifanyia kazi.
Haya Mdogowangu Shaffii AKA Muota Ndoto. Ile Kamati ilikuwa na wajumbe wengi wa Simba kwa hiyo walifanya kuikomoa Yanga. Sheria ziko wazi. Edgar Watson wa FUFA akiongea na wewe Shafii alisema OKWI ni Free Agent. So Mkataba wake na Etoile haupo, na Simba hayawahusu ila wao Wawatumie Majembe Auction - kuwadaia Etoile sio kuleta zengwe na kudaganya Uma. Ndoto zinategemea na Mawazo yako kabla ya kulala, kama ulikuwa unawaza Masomo utaota hayohayo, inaelekea Ulikuwa Unaota OKWI ni mali ya Simba.
ReplyDeleteBado Kapombe, Simba mikataba yao haina Umakini na wanawapa sifa za bure akina Seif na Binkleb. Au Mnyamwezi wa Kisomali anacheza Deal.
TFF Waifidie Yanga, Natamani Manji aombe FIDIA ya BILIONI MOJA.
Tehehe tehe tehe
Tatizo hapo sio kamat ina watu wengivwa simba tatizo hapo tff ilikuwa wanataka kujiridhisha kuwa wamefanya maamuzi sahihi na hii yote ni kwa manufaa ya yanga na ya tanzania kwa ujumla,cos angeruhusiwa kiholela alafu yanga angeonekana sio mchezaj wa yanga kihalal maana yake yanga angenyang'anywa point kama mech za lig na mashindano ya kimataifa wangemchezesha kama ilivyowatokea tp mazembe,so kama fifa wamemuidhinisha bas good kwa yanga na tanzania kwa ujumla but kama ingekuwa kinyume chake tungeanza laumiana na kunyoosheana vidole na kuambia fulan na fulan wazembe na wajiuzuru,hata huyo kapombe mchukueni tu ila hakikishen mnafuata sheria na hilo ndio la msingi na sio kwa lengo la kukomoana,ss mwisho wa cku tunataka yanga isonge mbele na tuwe na timu ya taifa bora hapo mbele
DeleteNi kweli akina Hanspope na wenzake ndani ya kamati walikuwa wakifanya haya wakiwa wanaujua ukweli ilikuwa ni kuikomoa Yanga kama Hanspope alivyoahidi tangu mwanzo lakini kwa hili watajua kwamba Yanga kuna watu makini sana akina sheikh Mansour(Binkleb) na Seif
DeleteTunajua TFF (ikiwa imesheheni manazi wa Yanga) wamekula njama na FIFA kumuidhinisha Okwi kuichezea Yanga. Lakini poa tu kwani hiyo ndiyo jeuri ya hela
DeleteNdi hao Kaburu,Kidau na Hanspope wameingia TFF kwenda kuendekeza ushabiki wa kijinga na kumpotosha Malinzi.Kwa kiwango alichoonyesha Okwi kwenye mechi za mazoezi,ni dhahiri mwaka huu kuna watu watanuna sana.Haki imecheleweshwa tu lakini ilikuwepo na ataanza na mechi dhidi ya Azam
ReplyDeleteKAMA NI KWELI OKWIII AMERUHUSIWA KUKIPIGA JANGWANI BASI NI FURSA NZURI KWA MSHAMBULIAJI HUYU KUONYESHA MAKALI YAKE HUSUSAN KATIKA MASHINDANO YA KLABU BINGWA AFRIKA NA VPL.
ReplyDeleteMALINZI KUWA MAKINI NA KAMATI ZAKO KUNA BAADHI YA WAJUMBE WAKE WANAENDEKEZA USHABIKI, FITNA BADALA YA KUKUSAIDIA KUKUZA KIWANGO CHA SOKA NCHINI. USIWAACHE WATAMBE FUATILIA KWA KARIBU UTENDAJI NA MAAMUZI YAO.
NINA IMANI NA WEWE JAMALI MALINZI, WANACHAMA WENZANGU, WAPENZI NA MASHABIKI YA DAR YOUNG AFRICANS "YANGA" DAIMA MBELE, NYUMA MWIKO.
OKWIII, LUHENDE, KIIZA, NIYONZIMA, DOMAYO NA BAHANUZI SAFARI HII LAZIMA TUWANG'OE AL-AHALY. WE MNYAMA SUBIRI MUZIKI WA "MWAGANE YEYA" HUKO MBEYA.
Muota ndoto mara nyingi huwa namuaminia sana katika maoni na mitazamo yake ya kina juu ya mambo ya soka na utawala wake kwa ujumla, lakini katika hili ulichemsha kama alivyosema mdau Mhungura aliposema kwamba ulilala ukiwa na mawazo ya Okwi ni mchezaji wa simba, yaani kwa kifupi katika hili mchambuzi wangu wa soka ninaye kuaminia ulichemsha kwani tokea mwanzo naweza kusema hukuwa nauelewa mzuri kuhusu hili suala japo toka mwanzo ulikuwa ukilifahamu na hata ukachukuwa hatua ya ziada kuongea na FUFA nao wakakuthibitishia kwamba kila kitu kiko sawa sasa shida yako Bwana Shaffih ilikuwa nini? Poa bado sijapoteza imani na wewe katika masuala ya uchambuzi lakini next time make sure unachimba kila kitu kwa undani.Kazi njema.Yasin
ReplyDelete1.Deo Munishi"Dida"
ReplyDelete2.Mbuyu Twite
3.Oscar Joshua
4.Nadir Haroub"Cannavaro"
5.Kevin Yondani"Vidic'
6.Frank Domayo
7.Mrisho Ngassa"Uncle"
8.Haruna Niyonzima"Fabregas"
9.Didier Kavumbagu
10.Emmanuel Okwi
11.Hamisi Kiiza"Diego"
Subs: Kaseja,Juma Abdul,Rajabu Zahir,Athumani Iddi"Chuji",Hassan Dilunga,Simon Msuva,David Luhende,,
Formation: 4-2-3-1
Tatizo la mashabiki hususan kama ninyi mamburura mnaoandika comments zenu za kishabiki tena msiojua mambo ya mpira na nadhani hamjacheza mpira hata wa sodo ndo mnapotosha watu. Shaffih hakuwahi kusema Okwi ni mchezaji wa Simba, yy alikuwa anasimamia kwenye kutoa tathimini na mtazamo wake kwa suala zima la Okwi. Na Yanga siku zote hawajui wachezaji wazuri lzima wafuatilie wanapopita Simba. Nusu ya team ni wachezaji wa zamani wa Simba. Bi kleb na Magari hawajui hata kupiga danadana ndo maana wanafuata wanapopita Simba. Chukueni Kapombe na mkimtaka na Singano pia tunawapa, pale ni chuo na watu wa mpira wapo Simba. Mamburura ninyi...
ReplyDeletewaswahili wanausemi wao kua MAFARI WAWILI HAWAKAI ZIZI MOJA,okwi kuruhusiwa yanga haisumbui kichwa simba ambayo daima inawaliza mashabiki wa simba B,maana si yanga tena mmekua simba B,au tuwaite maveterani wa simba
ReplyDeleteHaki imetendeka, tusubil moto wa Okwiiiiii
ReplyDeleteUMEPOTEZA HESHIMA YAKO SHAFII KWA KUENDEKEZA USHABIKI BADALA YA KUCHAMBUA SHERIA,,
ReplyDeletePOOR THINKER SHAFII
Acheni hasira jamani kueni wapenda mpira naco mashabiki..Mpira ni ajira hilo mlitambue,sasa yanga inalitambua hilo ndio maana mchezaji mzuri akionekana wao wanamchukua!! Kumbe mnapenda kua mwafurahia ushindi alafu maslahi kwa mchezaji hafifu..acheni wacheze kwny timu ambayo inaendana na kazi waifanyao! Mie sioni tatzo mchezaji akitoka simba ilimradi tu maisha yke yabadilike kwa mpira sasa ni ajira nasio ushabiki! Wachezaji mtambue hilo,usicheze yanga au simba kimapenzi km kuna timu itajali maslahi yako chomoka! Kapombe alikua anafny kazi nzuri lakin maslahi finyu,hata huyo singano km hamuoni thamani yke acheni wenye kujua thaman yke wamchukue! Kazi kusema chuo cha mpira wakati mnaona wachezaji hawana thaman mnamlipa laki 6! Mashabiki na wapenda mpira tubadilike,ofcoz utani uendelee tunapokutana lakin linapokuja suala la maslahi acheni siasa,waacheni waende kwenye maslahi na tufurahie km wanaondoka!! Km hampendi basi wapeni maslahi wanayostahili..
ReplyDeleteNi upuuzi na ushamba kusema Yanga inachukua wachezaji wa Simba kwani mchezaji lazima aangalie sehemu yenye maslahi kuliko ushabiki wa kijinga.Kama utakumbuka Yondani alitoka simba kwenda Yanga mara baada ya Simba kuifunga Yanga 5-0 huku Yanga ikiwa haishiriki mashindano ya kimataifa..Mchezaji anakuwa wa Simba pale anapochezea simba akishahama huyo ni wa tIMU ANAYOHAMIA.hAYO MABO YALISHAPITWA NA WAKATI NDIO MAANA LEO HII WACHEZAJI WALIOPITIA mTIBWA NA aZAM WAMEJAA KWENYE TIMU NYINGI ZA LIGI KUU.Okwi,Barthez,Ngasa w wamepitia timu nyingi kabla ya kwenda Yanga kama ilivyo kwa Ivo Mapunda,Kiemba,Berko,Kigi Makasi n.k ambao walitoka Yanga na kwenda simba
ReplyDeleteSasa Shabiki wa Simba mlibaki kushangilia OKWI kufungiwa badala kuuliza Pesa za Mauzo yake ziko wapi. Najua kesho pale Msimbazi Vikundi vikundi. Achaneni na Okwi nyie Muulizeni Huyo Mwanasiasa Hela ya Mauzo ya Okwi iko wapi Mpira ni Mchezo wa wazi SIO SIASA MCHEZO MCHAFU.
ReplyDeleteKwa kawaida duniani kote wachezaji huwa wanahama kutoka timu ndogo kwenda timu kubwa au kutoka timu yenye maslahi duni kwenda timu yenye maslahi ya juu BILA KUJALI MATOKEO YA TIMU UWANJANI,sasa kama wachezaji wengi wanatoka simba kwenda yanga ni kwa vile Yanga ni timu kubwa zaidi ya simba na kuna maslahi ya juu zaidi.Hivyo haya maneno ya kusema yanga inang'ang'ania kuchukua wachezaji wa simba ni maneno ya kujifariji tu kwa kuwa wachezaji wa kiwango cha Okwi,Yondani,Kaseja,Chuji na Ngassa ni wa kiwango cha juu na thamani ya juu mno kuliko uwezo wa simba
ReplyDelete