Search This Blog

Friday, September 14, 2012

KALI YA LEO: JAVI MARTINEZ NUSURA AITIWE 'MWIZI' BAADA YA KUTAKA KURUKA FENSI NA KUINGIA KWENYE UWANJA WA BILBAO

Imegundulika kwamba kulazimisha uhamisho kutoka Atheltic Bilbao kwenda Bayern Munich kumemtengenezea uadui mkubwa Javi Martinez na klabu yake ya zamani.

Kutokana na kufahamu kwamba tayari hana mahusiano mazuri na klabu yake ya zamani, akiwa hajawa na mawasiliano yoyote ya kibinadamu na mtu yoyote wa katika safu ya uongozi wa klabu hiyo aliyohama mwishoni mwa mwezi uliopita wakati Bayern walipofika bei ya €40 million - kwa bahati mbaya kutokana na kuondoka vibaya na kwa haraka akajikuta amesahau baadhi ya vitu vyake katika uwanja wa mazoezi wa Athletic - hivyo aliporudi Spain hivi karibuni akaamua kutumia njia yoyote ile aweze kupata mali zake.

Gazeti la Marca linaripoti: "Katika uwanja wa mazoezi wa Athletic Club de Bilbao, Ciudad Deportivo, mjini Lezama. Saa mbili asubuhi jumapili. siku ambayo mara nyingi kuna hakuna kinachoendelea uwanjani mpaka jumatatu. Mageti yamefungwa na hakuna mtu yoyote zaidi ya mlinzi ambaye muda mfupi baadae anashtuliwa na kuwasili kwa gari.

"Mlinzi yule anaiangalia gari ile akiwa kama mtu aliyeshangazwa baada ya kumuona aliyeshuka kwenye ile gari - na kwenda moja kwa moja kuruka fensi ili aweze kuingia kwenye mlango mkuu wa kuingilia ndani ya uwanja. Mlinzi yule anaenda kumzuia mtu yule akidhani ni mwizi, anamfikia na kugundua ni Javi Martinez, mchezaji wa zamani wa klabu hiyo - ambaye amehamia Bayern.

"Kiungo huyo wa kimataifa anamuomba mlinzi amfungulie mlango aende kwenye chumba cha kubadilishia nguo kwasababu anataka kuchukua vitu vyake (viatu vyake, nguo, na vitu vingine binafsi) ambavyo alishindwa kuvichukua wakati anaondoka na kukata mawasiliano na Athletic."

Javi Martinez hatimaye alifanikiwa kumbembeleza mlinzi na kuingia ndani, lakini alipofanikiwa kuingia ndani akakuta vitu vilivyokuwa kwenye droo aliyokuwa anaifadhia vitu vyake havipo! Kwa mujibu wa Marca alifanikiwa kupata baadhi tu ya viatu vyake na kuondoka huku akinung'uka.

1 comment:

  1. Asking questions are in fact fastidious thing if you are not understanding something completely, but this paragraph presents pleasant understanding
    even.|

    Also visit my web blog: program do rozliczania pit 2013

    ReplyDelete