Hatimaye tambo zimefikia mwisho na dakika 90 zimeamua nani bora . Simba imeibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya mahasimu wao na kwa asilimia kadhaa walistahili kupata ushindi kwani kwa dakika zote 90 ni wao ndio waliotengeneza nafasi nyingi za wazi na walizitumia .
SAFU YA USHAMBULIAJI YA SIMBA.
Simba waliingia na mfumo wa 4-4-2 ambao ilikuwa unabadilika na kuwa 4-5-1 kuendana na movement ya mpira na wakati mwingine ilikuwa inabadilika na kuwa 4-3-3 .
Wakati ilipokuwa inabadilika na kuwa 4-3-3 Simba ilikuwa inawatumia Felix Sunzu , Emanuel Okwi na Haruna Moshi . Okwi alikuwa anashambulia kutokea kushoto Boban akishambulia kutokea kulia na Sunzu alikuwa katikati akicheza kama ‘target man’.
Safu hii ya ushambuliaji ilikuwa mwiba mchungu kwa Yanga kwani kufikia dakika 10 za mwanzo Simba walikuwa wameshabisha hodi langoni mwa Yanga mara mbili katika ‘move’ za hatari ambazo kama Salum Machaku na Amir Maftah katika nyakati tofauti wangekuwa makini basi Simba wangecheka mapema .
Washambuliaji hawa watatu walikuwa wana-link vizuri sana na viungo wao kina Jerry Santo,Patrick Mafisango na Salum Machaku huku waki-take ‘advantage’ kwa mawasiliano mabovu baina ya mabeki wa Yanga na haikushangaza kuwa kufikia dakika ya 17 Simba walikuwa wanaongoza kwa bao moja .
Kwa upande wa safu ya ulinzi ya Yanga kulikuwa na matatizo makubwa sana . Chacha Marwa na Nadir Haroub hawakuwa na mawasiliano kati yao . Mara nyingi walikuwa wanacheza pasipo kuwa na mpango wa jinsi ya kuwakabili wachezaji wa Simba .
Presha iliyokuwa inakuja upande wao ilizidi kuwachanganya na kuwalazimu kucheza rafu ambazo zilikuwa zina madhara kwao na mfano mzuri ni kwenye goli la pili ambapo Haruna Moshi alichezewa vibaya na Nadir Haroub na kusababisha penati iliyokwamishwa wavuni na Felix Sunzu .
Pembeni upande wa kulia alikokuwa Shadrack Nsajigwa kulikuwa na matatizo pia, Fusso hakuwa anapewa msaada wa kutosha na mwenzie aliyekuwa anacheza winga ya kulia Godfrey Taita hali iliyokuwa inasababisha mipira mingi ya hatari kupita upande wa kulia wa ‘defence’ ya Yanga hata goli la kwanza lilitokea huko baada Felix Sunzu kuambaa na mpira na kutoa krosi fupi iliyomalizwa na Haruna Moshi.
UKOSEFU WA HOLDING MIDFIELD KWA YANGA.
Moja ya mambo ambayo yalikuwa yanafanya ‘defense’ ya Yanga iwe ‘under pressure’ ni kukosekana kwa cover muhimu inayotoka kwa ‘Holding midfielder’ , labda ni kukosekana kwa Nurdin Bakari ambaye kwenye safu ya kiungo ya Yanga huwa anafanya kazi mbili kwa wakati mmoja wakati timu ikipanda juu huwa anakuwa kiungo mwendeshaji na timu inapokuwa ikishambuliwa anafanya kazi ya ‘holding midfielder’ na hivyo kuwahakikishia usalama mabeki wake .
Hilo halikuwepo leo na badala yake Yanga waliwapanga Juma Seif Kijiko na Haruna Niyonzima Fabregas .
Fabregas alipangwa kucheza kwenye dimba la chini jambo lililoigharimu sana Yanga kwa kuwa Niyonzima ni aina ya viungo ambao wana madhara wakiwa na mpira lakini timu inapokuwa kwenye presha anakuwa hana msaada.
Madhara yake yalionekana kwani Yanga walilikimbia dimba huku presha ikiwa kubwa mno kwenye safu yao ya Ulinzi na ndio maana Simba walimaliza mchezo kwenye kipindi cha kwanza .
Kulikuwa hakuna haja ya kuwapanga Juma Seif Kijiko na Niyonzima kwa pamoja kulikuwa na haja ya kumchezesha mtu kama Godfrey Bonny ambaye angeleta Balance kwenye midfield ya Yanga .
‘MAN OF THE MATCH PERFOMANCE’-HARUNA NIYONZIMA .
Si kitu cha kawaida kwa mchezaji bora wa mchezo kutoka kwenye timu iliyopoteza mchezo lakini mtu aliyestahili kuwa man of the match kiukweli alikuwa Haruna Niyonzima . Bahati mbaya ni kwamba alikuwa man of the match kwenye timu iliyofungwa .
Fabregas aliipa Yanga uhai kwa mpira wake alioucheza ambao ulikuwa wa kiwango cha juu kupita kiasi , huyu jamaa ana akili kupita maelezo . Alitengeneza movement nyingi ambazo kama isingekuwa mbinu ambazo si sahihi za Yanga pengine zingeleta faida kwa timu yake .
Mara nyingi alijaribu kupiga mashuti na alitawala mno eneo la kiungo kwa bahati mbaya hakuwa anapata msaada toka kwa wenzie .
UWEPO WA VICTOR COSTA KWENYE SAFU YA ULINZI YA SIMBA .
Kama ulipitia kwenye hii blog mapema kabla ya mchezo utakuwa umepitia ‘analysis’ ya vitu mbalimbali vya kutegemea toka kwa timu mbili za Simba na Yanga.
Kwa upande wa Simba moja ya matatizo makubwa ambayo yaliainishwa ni ukosefu wa umakini kwenye eneo la ‘defense’. Tatizo hili linasababishwa na kimo lakini sababu nyingine ya msingi ni mabeki wa kati wa Simba kuwa na aina moja ya uchezaji .
Juma Nyosso na Kevin Yondani wote ni watu wazuri sana wakicheza kwenye nafasi ya beki anayekaba , lakini kati ya watu hawa hakuna yoyote anayekuwa ‘ kamanda’ kwa wenzie .
Tatizo hilo limepatiwa ufumbuzi na ufumbuzi huo ni Victor Costa Nampoka aka Nyumba . Mashabiki wa Simba wanamkumbuka vizuri beki huyu na ndio maana taarifa za usajili wake zilipokelewa kwa shangwe na hilo lilidhihirika kwenye mchezo wa ngao ya hisani.
Mtu kama Nyosso ni beki mzuri sana lakini uzuri wake huwezi kuuona akicheza na Kevin Yondani au Meshack Abel , kwa sababu wote ni watu wa aina moja yaani ni kama vile jinsi ya mtindo huo huo lakini Victor Costa ameleta kitu tofauti ambacho Simba wamekikosa tangu alipoumia Joseph Owino .
Costa alikuwa anwaelekeza mabeki wenzie jinsi ya kukaba , jinsi ya kusimama , alikuwa anatuliza presha ya mchezo na uzoefu wake ulionekana .
KIPINDI CHA PILI.
Huu ulikuwa mchezo wa vipindi viwili ambapo Simba walicheza na kutawala kipindi cha kwanza lakini Yanga waliamka na kutawala kipindi cha pili japo hawakuweza kurudisha mabao waliyofungwa kipindi cha kwanza .
Sababu kuu ya Simba kushindwa kutawala kipindi cha pili ni kuumia kwa washambuliaji wawili wa Simba waliosumbua sana Yanga mwanzoni.
Haruna Moshi na Emanuel Okwi waliumia na kasi yao kwa kiasi Fulani ilipungua hali iliyosababisha kocha kuwatoa na kuwaingiza Shomari Kapombe na Gervais Kago.
Mabadiliko haya yalimaanisha kuwa Simba ilicheza kwa mfumo wa 4-4-2 flat ambapo ule ujanja wa kubadilisha na utumia 4-3-3 na 4-5-1 haukuwepo tena .
Pia Felix Sunzu na Gervais Kago hawakuweza kutengeneza ‘chemistry’ baina yao kwani wote wawili ni ‘terget men’ yaani watu wa kusimama jambo ambalo lilitengeneza shimo baina yao na viungo na japo kina Mafisango na Jerry Santo walikuwa wanafanya kazi kubwa sana , ‘momentum’ ya mchezo ilibadilishwa na mabadiliko haya .
KUINGIA KWA RASHID GUMBO NA HAMIS KIIZA .
Kutawala mchezo kwenye kipindi cha pili kwa Yanga kuliendana na matukio mengine ambayo ni mabadiliko ya Simba na wakati huo huo mabadiliko ya Yanga kwa kuwatoa Kiggi Makassi na Kenneth Asamoah na kuwaingiza Rashid Gumbo na Hamis Kiiza .
Walipoingia watu hawa Yanga ilikuwa inamiliki sana mpira na hivyo walionekana kuja na uhai hasa Hamis Kiiza ambaye alikuwa anamtoka sana Nassor ‘chollo’ beki wa kulia wa Simba ambaye mara nyingi sana alikuwa anamsahau mshambuliaji huyu toka Uganda.
Kwa bahati mbaya hakukuwa na matokeo yoyote ya utawala wa wachezaji hawa kwenye eneo la kiungo kwa Gumbo na Kiiza kwa upande wa ushambuliaji.
PATNERSHIP YA JERRY TEGETE NA KENETH ASAMOAH.
Safu ya ushambuliaji kwa Yanga ilikuwa chini ya Jerryson Tegete na Keneth Asamoh , huu ni muungano ambao haukufanya kazi kwa kuwa wachezaji hawa wana mitindo ya uchezaji inayofanana hivyo ili kucheza pamoja walilazimika kucheza tofauti na walivyozoea na hivyo hawakuwa ‘comfortable’.
Tegete ni mzuri akiachwa aongoze mstari mwenyewe kama ‘target man’ lakini uwepo wa Asamoah ulimlazimu Tegete kushuka chini ambako hana madhara yoyote .
Tegete ni mchezaji ambaye umahiri wake wote uko kwenye kufunga na maeneo yake uwanjani ni eneo la 6 au kama atatoka mbali basi asikae mbali sana na eneo la yadi 18 . Anapotoka kushuka hadi katikati ya uwanja hawezi kuwa na madhara yoyote .
Mwisho .
Simba walistahili kushinda mchezo huu kwani walitengeneza nafasi za wazi na kati ya hizo walitumia mbili kupata mabao ambayo watani wao hawakuweza kujibu .
Kipindi cha kwanza Simba waliingia na malengo ambayo yalitimia , kwa vyovyote kocha wao aliwaambia kuwa ‘biashara ni mapema’ na ndio kilichotokea kwani kipindi cha kwanza ndio kilichoipa Simba ushindi .
Kwa kawaida Yanga huwa wamezoea kuwa Simba huingia na lengo la kushambulia tangu mwanzo huku wao (yanga) wakiwasoma na kurudi mchezoni taratibu hadi wanafikia kuuteka moja kwa moja lakini hilo halikuonekana leo kwani Simba walitengeneza nafasi za wazi zilizowaacha Yanga wakiwa hawajui linalotokea na hawakurecorver kutoka kwenye huo mshangao .
Kocha wa Yanga hakutumia mbinu sahihi kwa timu yake kwani jinsi alivyoipanga safu yake ya viungo hakukuwa na ‘balance’ .
thats true broo sasa unawashauri nn YANGA wafanye nn game ijao ya ligi ili wakikutanatena na simba wasirudie makosa yaleyale.
ReplyDeletegood analysis kaka umesomeka! yaani imetulia wala haijaegamia upande wowote kiushabiki kama wachambuzi wengine hapa bongo. keep up good work! Nagabona.
ReplyDelete@jeinho, makosa hata mwalimu atakuwa kayaona. ila ukweli yanga kinatutesa sana kutokuwa na viungo wakabaji wa nguvu. na kwa aina yetu ya usajili wa kibongo bongo utakuta watu wanasajili tena aina ile ile ya wachezaji tuliokuwa nao. badala ya kuangalia ni nani tunamhitaji kuziba pengo na nani anafaa kusajiliwa kwa ajili hiyo. mara nyingi simba huwa wana combination nzuri ya viungo.
ReplyDeleteAnyway mpira huwa nao una siku zake, kleo hivi kesho vile.
cheers.