Watanzania wawili kucheza ligi daraja la pili Sweden
Watanzania wawili kucheza ligi daraja la pili Sweden Wachezaji wawili wa kitanzania, Joseph Kaniki (Golota) na William John wamefanikiwa kujiunga na timu ya ligi daraja la pili KonyaSpor (KIF) nchini Sweden, baada ya kufanikiwa kupita katika majaribio( Trials). Majaribio hayo yalijumuisha wachezaji zaidi ya thelathini ambapo wachezaji watano walichaguliwa kujiunga na klabu hiyo ya ligi daraja la pili KonyaSpor (KIF)
Habari hii imeletwa kwenu na:http://www.africa4life.com/
Duh hivi kumbe Kaniki bado anasukuma kabumbu mimi nilifikiri alikwishatundika daluga, wadau naomba msaada hivi huyu jamaa ana miaka mingapi sasa,Namkumbuka sana kwenye mechi kati ya Simba na Ismailia uwanja wa shamba la bibi jamaa alipiga mpira wa hali ya juu vibaya sana ni moja wachezaji wenye uwezo wa kupiga mawe ya hatari sana, Kwenye mechi na Ismailia ambayo baadae refa aliisimamisha kutokana na mvua jamaa alipiga penati kwenye dimbwi la maji waarabu wakakaa chini wakasema hatuchezi,sitaisahau hiyo mechi kwani mpaka mechi inavunjwa simba walikuwa mbele kwa bao 2 kipindi cha kwanza na walikuwa wanateleza vibaya ila bahati haikuwa yao mechi ikasimamishwa na waliporudiana simba wakashinda 1-0 na wakatolewa.
ReplyDeleteKumbukumbu nyingine ya kaniki ambayo siwezi kuisahau ni mechi kati ya simba na mtibwa akiwabado anachezea Simba alifunga goli moja la tiktaka mpaka benchi la ufundi lamtibwa walisimama kushangilia wakati walikuwa wamefungwa wao lilikuwa bonge la tiktaka, huyo jamaa alikuwa hatari.Alikuwa na mgu wa kushoto wenye nguvu ajabu na kimbia yake ndani ya uwanja ya kibabe ilikuwa ni burudani sana.
Kila la kheri Golota (mzee wa mawe).
Shukrani Shaffih kwa kupost current news za Golota umenikumbusha mbali sana.
Mike - Germany.