Hiki ndio kikosi cha timu ya simba kilichoitoa na kuivua ubingwa klabu ya zamalek mwaka 2003 kwenye michuano ya kombe la mabingwa wa afrika. ilikuwa ndio mara ya kwanza na mwisho kwa timu ya Tanzania kushinda katika ardhi ya Misri.
Yanga kesho wanacheza na Zamalek inabidi na inapaswa wajitume na kuhakikisha wanaifikia rekodi ya watani wao wa jadi kwa kuwatoa Zamalek tena wakiwa nyumbani kwao Misri na kuweza kuiletea sifa nchi na maendelea ya mpira bongo kwa ujumla.
eti hapo unaambiwa juma kaseja na athumani machupa eti wana miaka 27 na 28 respectively hainiingii akilini kabisa hawa jamaa nimeenza kuwasikia toka niko primary na saiz nafanya masters eti watu bado wana miaka hiyo hiyo,ndio maana hatuendelei kwaajili ya kuchakachua umri.pambaf
ReplyDeleteKweli kabisa nadhani Yanga wakiwa na ari ya kutaka kukifanya kile ambacho Simba walikifanya tunaamini ushindi unaweza kupatikana hasa tukiamini kuwa na wao Zamalek watakosa sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wao, na hivyo Yanga kuwatoa Watanzania kimasomaso.
ReplyDeleteHata hivyo, kikosi hiki cha Simba kilisaidiwa na jambo la ziada badala lile la ari. Umri wa wachezaji hawa wa Simba kipindi kile nadhani ulikuwa ni wastan wa miaka 23. Nasema wastan huo kwasababu vijana walikuwa wengi na wazoefu wachache akina Madaraka seleman, Seleman matola na Willium Fanbula kama sikosei.
Kila la Kheri Yanga.
Mungu Ibariki Yanga, Mungu Ibariki Simba, Mungu ibariki Tanzania.
Bebeto.
Hello Shaffih.
ReplyDeleteDah, ebwana umenikumbusha mbali sana,sitakuja kuisahau mechi hiyo marudiano kati ya Simba na Zamalek, kwa bahati mbaya sikufanikiwa kuona mechi ya marudiano live ila nakumbuka tulisubiri matokeo kupitia ITV walikuwa wanatoa update, kuna mtangazaji mmoja wa ITV jina nimemsahau ila alikuwa mwanamke ambaye alikuwa anatangaza taarifa ya saa 4 kwa lugha ya kiingereza, kwa kuwa tulikuwa na tension mara tukamuona ameapia kwenye TV akiwa na koti jekundu kiroho kikaanza kutupasuka alitoa tabasamu la nguvu kisha kusema Mnyama ameunguruma Cairo, it was so emotional tulishangilia sana huwezi amini usiku huo tulikwenda klabuni pale.
Mapokezi yao dar yatabaki kuwa historia pamoja na kwamba kuna washabiki walifariki kutokana na wingi wa watu, kama nitakuwa nimekosea wadau mtanisahihisha ila mapokezi yaliongozwa na Mh Yusuf Makamba, ila pale uwanjani siku hiyo muda mchache kabla simba hawajatua alishuka Rais Mkapa alikuwa anatokea kwenye ziara zake za kikayi nje ya nchi alipigwa na butwaa kuona ule umati ulivyokuwa mkubwa alihamaki sana akauliya hawa watu wamekuja kunipokea akaambiwa Mzee wewe nenda tunawasubiri vijana wanatoka Cairo ilikuwa shangwe kubwa sana najua wengi mnakubuka kwani mwaka 2003 si mbali.
Natamani Yanga wafanye jambo la kishujaa namna hiyo tena kwani uwezo wanao kama watajituma na kuondoa woga na kuacha kutafuta sababu mapema kabla hata mpira haujaanza.Go go go go go Yanga Afrika.
Shaffih kuna mchezaji 1 hapo ananichanganya kidogo, kutoka kushoto walioinama ni Wasso, Mwakingwe, Kaseja, Machupa, Pawasa,Kulia waliosimama, Matola, Costa, Alex masawe,....,Macho,Gabriel.huyo aliyesimama katikati ya Macho na batgoal ni nani mkuu: moja ya vikosi bora kabisa vya timu ya simba nilivyowahi kuviona.Aksante kwa kutukumbusha Shaffih
Mike.
Germany.