Chelsea striker Didier Drogba maeanza mbio za kutaka kusaini mkataba mpya huku akivuta mshahara wa paundi million 6 kwa mwaka.
Mazungumzo juu ya deal mpya at Stamford Bridge yamesimama na Drogba sasa ameanza kuangalia sehemu nyingine.
Ivory coast captain amebakiza miezi mitano ya mkataba wake, hivyo anaweza kuanza kufanya mazungumzo na klabu kutoka nje ya England kwa ajili ya kuhamia mkataba wake utakapoishia.
Upatikanaji wa Drogba umezusha vita ya kumgombea kupata saini yake.
Huku washauri wake wa masuala ya kifedha wakimsisitiza kukubali kujiunga na timu ambayo itatoa ofa ya paundi million 6 kwa mwaka baada ya kodi.
Lakini pamoja na kwamba fedha hiyo ni kubwa lakini kumekuwa na timu nyingi zinazohitaji saini yake.
Drigba tayari amekataa ofay a paundi million 4 kutoka klabu ya Qatar Al Saad.
Drogba pia yupo katika listi ya Anzhi Makhachkala inayofundishwa na Guus Hiddink, na chanzo kutoka ndani ya klabu hiyo kinasema warusi hao wapo tayari kulipa kati ya paundi million 8 au 10ili kuweza kumsaini Didier.
Pia kuna ofa kutoka Marekani kwa Chicago Fire. Wakala wa Drogba Thierno Seydi alisema “Atajiunga na timu itakayompa fedha nyingi”
No comments:
Post a Comment