Kwanza nitumie nafasi hii kuipongeza Taifa Stars kwa kumaliza salama mchezo dhidi Msumbiji na kulazimisha sare ya bao 1:1, Tumepata sare matokeo ambayo hayakuwa ya kuridhisha sana,lakini niwapongeze kwa hilo.
Nilikua miongoni mwa watanzania tuliokuja Uwanja wa Taifa kuangalia mpambano huo lakini tukiwa na mahitaji tofauti. Mimi sikuja kuishangilia timu bali nilikuja kuwaangalia vijana wetu wanaochipukia kama vile Salum Abubakari ‘ Sureboy ’wanafanya nini. Kama nilivyowahi kusema huko nyuma ya kwamba timu yetu ya taifa ilivyo kufuzu kwa mashindano makubwa ni miujiza tu inayohitajika.
Mechi ya jana iliendelea kuchochea zaidi hoja yangu ya kuutumia mwanya huu ambao tunajua fika hatuna uwezo wa kwenda mbele kujenga timu mpya ya taifa.
Mechi ya jana iliendelea kuchochea zaidi hoja yangu ya kuutumia mwanya huu ambao tunajua fika hatuna uwezo wa kwenda mbele kujenga timu mpya ya taifa.
Naombeni sana tufanye utafiti wa haraka haraka ni watanzania wangapi wenye matumaini ya timu yetu ya taifa kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwakani au Kombe la Dunia mwaka 2014 kule nchini Brazil,naamini huo utafiti utasaidia kuilinda hoja yangu ya kuachana na ndoto za alnacha za stars kufuzu mashindano makubwa pasipokuepo maandalizi ya dhati.
Tuwashukuru sana kina Nizar,Henry na Mrwanda pia tuwashukuru sana wachezaji wazoefu waliopo kwenye kikosi cha Stars cha sasa.
Tuna takribani mechi 6 za kucheza kwa ajili ya kufuzu kombe la dunia,miongoni mwa timu tutakazocheza nazo ni Ivory Coast na Morocco.
Atakachojifunza leo hii Nadir Haroub kumkaba Didier Drogba hakitatusaidia hata kidogo huko mbeleni kwasababu asilimia kubwa ya wachezaji wa kikosi cha sasa cha Stars viwango vyao vinaelekea ukingoni.
Lakini tukiwatumia makinda wenye umri chini ya miaka 24 wakaburuzwa na kina Drogba litakua fundisho kwao hatimae litatusaidia kwa miaka mingine mingi tu ya mbeleni. Kwahiyo mimi nashauri tuwape nafasi vijana wetu wakapambane na kina Drogba na Chamakh ili wapate uzoefu ili waje kutusaidia mbeleni. Hapa matokeo siyo kipaumbele acha wafungwe ili wapate kitu kitakachokuja kuwasaidia huko mbeleni.
Sidhani kama huu ni muda wa mjadala wa Timu ya taifa inatakiwa iundweje,nadhani huu ni mjadala wa namna gani mpira wa nchi yetu utapatiwa ufumbuzi kwa siku za usoni,kwa maana ya kutengeneza miundo mbinu pamoja na program endelevu za namna ya kuibua na kuviendeleza vipaji vipya maana kwasasa hakuna njia ya kujikomboa hapa tulipo.
Tunahitaji kujitoa mhanga na pa kuanzia ni kuivunjilia mbali hii timu iliyopo ya Taifa na hii itasaidia kutoa changamoto kubwa kwa kizazi kijacho.
TFF msikubali kuyaburuza mashindano ya Copa CocaCola pasipokuwepo mikakati endelevu,yatumieni kama msingi wa kuibua na kupata vipaji vipya kila mwaka na rasilimali za Airtel Rising Stars zitumike ku-maintain vipaji vinavyotokana na Copa Cocacola,ni kweli tunahitaji wafadhili lakini lazima TFF tuwabane hao hao wafadhili waliopo ili program zetu za muda mrefu zilindwe. TFF, mlinufaika sana na vipaji vilivyotokana na mashindano ya UMISETA miaka ya nyuma na hapo hamkuwa na hela. Inakuwaje sasa hivi hampeleki pesa huko kwenye UMISETA wakati wadhamini mnao? …itaendelea
sawa shaffih uko sahihi kabisa lakin changamoto kubwa ni consistency ya hao makinda,unaweza kumuona anachipukia ukajua sasa anaelekea kuzuri lakini msimu unaofuata anapotea mpaka haeleweki anafanya nini na ndo mwanzo wa kwenda kwa mikopo timu dhaifu,TFF wanawajibu wa kurekebisha sera na mipango yao kwa kushirikiana na wizara ya michezo na wawasilishe hiyo programe serikalini na kwa wadhamini na wadau ili wajue wanafanya nini,hiyo progame iwe ya kuibua na kukuza vipaji hapo ndo tutatoka,kwasasa sidhani kama kuna kitu cha maana wanafanya TFF zaidi ya kuratibu mashindano na kusumbuana na wambura
ReplyDeletechela wa dom
tushawazoea na maneno hayo kila siku,wacha tuamini hakuna tunachokijua watanzania labda big brother.
ReplyDelete