Search This Blog

Friday, March 2, 2012

SAKATA LA MBWANA SAMATTA KUACHWA TIMU YA TAIFA LACHUKUA SURA MPYA,WADAU WAENDELEA KUTOA MAONI YAO!

mawazo/maoni yaliyotolewa na wadau hapo juu si mabaya sababu kila mtu anamtazamo wake kwenye kila jambo anapolitazama au kulifikiri. Ila mimi nataka kupingana na Bw. GEORGE [Mchangiaji wa kwanza kama ilivyoorodheshwa hapo juu] kwa hoja zifuatazo.

1. Timu yoyote ile ambayo ina uhai hapa duniani hata kama ikicheza team work 100 percent ni lazima pawepo na mtu angalau mmoja au wawili ambao watatumia uwezo binafsi na umakini wao kuleta ushindi kwenye timu, hilo huwezi kulipinga kutokana na mpira wa sasa ulivyo. Kwa mfano: Man United bila ROONEY utaona wanapata tabu sana kushinda, au ARSENAL ya leo bila ROBIN Van PERSIE pale mbele na pale kati akikosekana SONG BILLONG utata huonekana kwenye perfomance ya team. Hiyo ni mifano michache tu ingawa ipo mingi na yenye mantiki. Tazama mabingwa wapya wa Africa [ZAMBIA] pale kati walikuwepo watu wawili muhimu sana ISACK CHANSA na KALABA kukosekana kwa hawa watu zambia ingekuwa na wakati mgumu sana...pia pale mbele alikuwepo captain mwenye CHRISTOPHER KATONGO huyu mtu balaa bana we acha tu.

2. Napenda kukukumbusha tu kuwa NAPOLI ni timu moja nzuri yenye kucheza ki-team work huku ikiwa na wachezaji muhimu inaowategemea kufanya matokeo yawe mazuri kwao, utaizungumziaje NAPOLI bila EDINSON CAVANI na EZEQUIEL LAVEZZI pale mbele, au MAREK HAMSIK pale kati!!??? kama ni mpenzi wa mpira na unafuatilia serie A kwa karibu na si kusubiri uione NAPOLI kwenye UCL hapo utakuwa unakosea sana kaka

MWISHO, napenda kusema kuwa SAMATTA ni muhimu sana kwenye timu ya Taifa [TAIFA STARS] na kukosekana kwake ni tatizo kubwa sana, kuna kitu ambacho Kocha POULSEN anashindwa kufanya uamuzi wa maana, kuwa mfungaji bora wa league haimaanishi hata ukiperfom vibaya then watu wakae kimya eti kisa kwenye VPL unafunga magori. Huyu JOHN BOCCO hawezi kutufikisha kokote kule kwenye hii safari yetu, hebu jiulize kwanza tangu aanze kuvaa jezi ya timu ta taifa kafunga goli ngapi? then ukipata jibu ndo utajua kwanini wadau tunalia na uwepo wa SAMATTA pale mbele
NASHUKURU SANA KWA MJADALA HUU

17 comments:

  1. Kw hyo laiti Poulsen angekuwa Argentina angemuacha Messi kisa anacheza kibnafsi?

    ReplyDelete
  2. Inamaana Poulsen angekuwa anafundisha Argentina angemuacha Messi au Neymar kw Brazil?

    ReplyDelete
  3. ongereni kwa mitazamo tofauti,mi nachopenda kusema tumwache kocha yeye ndio anajua majukumu ya wachezaji wake kwani sisi tumezoea kukosoa sana,kocha kamuona samata hafai itakuaje mlazimishe kitu tujaribu kuwa watulivu watafanya vizuri,tatizo tunapenda mafanikio ya haraka na lawama nyingi hasa kwa watu wale wanaojiita wachambuzi.

    ReplyDelete
  4. Acheni ushabiki usio na maana! Hao wachezaji wote mliowataja wanacheza kwa kujituma lakini si samatta! Tatizo la samatta ni kujiona superstar hivyo anashindwa ku perform katika kiwango nakuonekana hana mapenzi na STARS! BIG UP POULSEN!

    ReplyDelete
  5. shafii unamlaumu bure tu poulsen,samata hajafikia hatua ya kuidharau national team,ni kweli hajitumi,huyo John boko labda una bifu nae tu.anajituma sana,tatizo mpaka sasa Timu ya taifa stars haina mtu ambae kweli akikosekana timu haichezi vizuri,huyo samata kaitwa mara ngapi na hajafanya lolote ? Mwacheni kocha afanye kazi yake.

    ReplyDelete
  6. kama huyo john bocco anajituma then kaisaidia timu ya taifa kupata ushindi mara ngapi?

    ReplyDelete
  7. Hebu muacheni mzee afanye kazi yake, hilo pia ni fundisho kwa Mbwana Samatta, sometimes you need to agree with coach, labda alishamuambia mara kadhaa acheze anavyotaka hakufanya. Sometimes you need to be a team player not too much individual. ukitolea mfano rooney sio sawa. anajituma sana na si individual kabisa. Pia mwalimu anatakiwa aweke kitu fulani (i mean to instil something for players to feel commited to the team).

    ReplyDelete
  8. Tanzania bado haijawa na bahati na mchezaji ambae unaweza kumuita roho ya timu.Huyo Samata,hatukatai kuwa ni mchezaji mzuri kwa kiwango cha soka la bongo lakini bado hajafikia hadhi ya kwamba lazima awepo kwenye ya taifa.
    Tuache visingizio,tujichunguze ili kuweza kusonga mbele.

    ReplyDelete
  9. MI NATAMANI SIKU MOJA TFF IWAPE KAZI WACHAMBUZI WAIFUNDISHE TAIFA STARS KWA MIAKA MIWILI TU,KOCHA MKUU AWE SHAFII,MSAIDIZI WAKE EDO KUMWEMBE TUONE UWEZO WENU.

    ReplyDelete
  10. salam,

    mimi mdau wa soka mdogo tu mbele ya magwiji mbali mbali waliochangia.

    kwanza nianze na samata.jamani bado wengi hatujui kawaida ya makocha. makocha ni watu ambao wanataka wawe huru sana kufanya maamuzi. yuko tayari kulaumiwa na atabeba msalaba wake.

    leo tunasema kuhusu paulsen kumuacha samata. tumesahau marcio maximo alifanya nini kwa kaseja na wachezaji wengine. tujue hivi ndio makocha dunia nzima walivyo.

    pili, mchezaji kuwachwa na kuchukuliwa timu ya taifa ni jambo la kawaida. tuzoea kuona kuwa mchezaji anapewa nafasi iwapo kiwango kiko juu na kiwango kikishuka tukubali pia, kama ambavyo nakubaliana na kocha kuhusu canavaro kwa sasa na hata henry joseph lakini sikubaliani na kocha kumchezesha nsajigwa mbele ya cholo.

    kama paulsen anaona lazima amchezeshe nsajigwa kwa kuwa ni nahodha, basi amvue unahodha na aanze kumpadisha kijana yasije kuwa ya kufia timu ya taifa kama ya maxine na ivo mapunda..

    halafu kila kocha anadai asilimia 100 ya mchezaji akiwa uwanjani. na ni yeye anaejua mchezaji ametimiza maagizo yake au la. kuwa nyota uwanjani si shani muhimu kufuata maelekezo ya kocha.

    wachezaji wangapi wakubwa wameachwa na makocha kwa sababu katika picha ya timu kama hayumo anakaa upande tu hata awe mkubwa kama mbuyu na tunakumbuka brazil nzima ilivyolia lakini nyota wao romario alikataliwa na kocha.

    samata ndio kwanza chipukizi. ni lazima afunzwe adabu kwa vitendo. ajue kwenye timu ya taifa na popote pale ni team work. matokeo ya juzi si kwa kuwa samata hakucheza la, ni kwa sababu boko hakutumia nafasi alizozipata.

    pili, boko angecheza vyema kama ngasa angeanza nae kwa sababu partnership yao katika klabu ni nzuri sana. lakini kocha hakuona hivyo.

    na sio kama angecheza samata basi tungeshinda, la. kwani mechi zote alizocheza samata tumeshinda? la hatujashinda.

    tusianze kum glorify samata. ni kijana mdogo na kwa kweli ni chipukizi ambaye anataka kuongozwa. tukianza kumjengea mazingira ya kumuona samata ni super stary kesho hivi atapanda kichwa na tutampoteza kabisa kwa faida ya baadae.

    tatizo ni kuwa tanzania hatujapata MAJEMBE YA KWELI. nafasi ya striker wa juu imekuwa ngumu sana nchini tanzania. sijui yule kijana wa coastal vipi, lakini naona na yeye kuna kazi kubwa mpaka kum tune kufikia level nzuri.

    tumpigieni debe sana ali badru ali. huyu yuko misri ambako akiwa na canal suez saa hizi ana magoli 12. sikupata maelezo yake kwa nini hakuja kwenye timu ya taifa.

    ama kuhusu poulsen mwenyewe mimi najua uwezo wake si mkubwa sana. baada ya kuondoka maximo kwenye mchakato nilimleta kocha ambaye amefundisha sweden national team akiwa msaidizi kocha, amefundisha klabu ambayo imekuwa bingwa wa sweden, amefundisha akina mariga...lakini naona pengine alikuwa ghali kwa tff...

    lakini na sisi wapenzi wa soka tuna kasumba kubwa ambayo inapaswa irekebishwe...tunalaumu kilele wakati shina tunaliwacha....iko wapi taifa stars B ambayo itatoa matunda kwa taifa stars A?

    mbona hatuulizi vipaji vyote vya coca cola vinaenda wapi? amekiri juzi poulsen kuwa zanzibar kuna vipaji zaidi basi mbona haendi huko akaviibua vipaji hivyo?

    ally saleh

    ReplyDelete
  11. Samatta siyo muarobaini wa matatizo ya football Tanzania,nildhan ninyi waandishi na wananchi kwa jumla kuwa na agenda moja juu ya mustakabali wa soccer letu.

    ReplyDelete
  12. Kuhusu suala la Samatta mie naona tunamuonea bure kocha. Huyuhuyu kocha ambaye hata TFF inaonekana inamtenga. Matokeo yake tunamtimua tutaanza upya na kurudisha nyuma maendeloeo ya nchi.

    Sidhani kama kwa Samatta kufunga bao hivi karibuni ni kumtumia salamu Paulsen. Maana huyu Dogo bado hatuwezi kumuita 'tegemeo' kwenye timu ya Taifa. Nakubali kuwa ni mchezaji mzuri lakini ni lazima hata yeye aelewe kuwa Maamuzi ya kocha ndo ya mwisho. Na kama ni mwelewa basi afanyie kazi tasarifa zilizotolewa na kosha badala ya kujibiozana naye.

    Wote tulimuona alivyocheza kwenye chalenji na tunakubali alionekana kutokuwa na moyo wa kujituma. Hii mara nyingi inatokea kwa wachezaji wa Africa wanaolipwa sana kwenye club zao.

    Pia sidhani kama ni wakati mwafaka wa kudai kocha anatumia mfumo mgumu. Wachezaji ndo kazi yao inabidi wakomae washinde. Kama mfumo ni mgumu kwani walitengeneza nafasi ngapi dhidi ya Msumbuji?

    ReplyDelete
  13. Kuhusu suala la samatta tumuachie kocha afanye kazi ya kitaalam,kocha ndiyo anayechagua mfumo wa uchezaji wa timu na aina ya wachezaji wanao"fiti" kwenye mfumo huo,labda niwarudishe nyuma mwaka 2002,kocha wa Brazil alikua Phil Scolari,katika kikosi chake kilichoenda kombe la dunia alimuacha mchezaji maarufu enzi hizo Romario na kuzua malalamiko mengi kutoka kwa mashabiki akiwamo Raisi wa nchi hiyo,lakini Scolari aliendelea na msimamo wake na kikosi chake ndicho kilichochukua kombe la dunia bila Romario.

    ReplyDelete
  14. Habari wadau wa soka,

    Hongereni kwa kutumia japo dakika 5 kujadili swala hili, nawapongeza sana.

    Hebu tujiulize maswali ya msingi yafuatayo:
    1)Tanzania(wizara husika) inajua kuwa soka ni taaluma(profession)na ni ajira?.
    2)TFF wanajua kama soka ni taaluma na ajira?.
    3)Vijana wetu wanajua kuwa soka ni taaluma na ajira?.
    4)Watanzania tunajua kuwa soka ni taaluma na ajira?
    5) Kuna haja ya kuwa na wahezaji wataalam?

    Kama majibu ni hapana, basi haina maana kumlaumu Paulsen wala Boko wala Samatta wala nani.

    Kama jibu ni ndiyo tujiulize:
    1)Je ni mfumo gani ambao upo wa jinsi ya kuwapata hawa wachezi wataalamu(professionals)?
    2)Kama huo mfumo upo je, unafanya kazi vizuri kama mifumo mingine duniani?

    Nimalizie tu kwa kutoa mtazamo wangu tukitaka kusonga mbele kisoka:

    1)Tz vipaji vya soka vipo tena balaa

    2) Tuamue sasa kwamba tunataka mpira wa kitalaamu(professional)

    3) Tuunde mfumo rasimi na sahihi wa kutengeneza wachezaji wa soka

    4) Twende popote Tz penye vipaji(from 12yrs) tuviibue na kuvinoa the way we want

    5) Tuweke mikakati ya muda na kudumu katika mfumo wetu


    6) Tuingie gharama kwa kuwekeza(tufanye kama soka ni biashara)


    Nawasilisha

    ReplyDelete
  15. Habari wadau,
    naona sakata zima la mada hii ndgu ally kaongelea vyema suala lote na kaka shafii chukua pindi hilo. Ni kweli Samata akichezea timu ya taifa hajitumi kabisa na huwa anarelax sana akiwa uwanjani, ofcoz it does matter kuwa na individuality kwenye timu haswa kwa striker, ila kama mfano wa rooney ulivyotumika hapo juu, ni kweli ana individuality na pia anajituma mbaya to ensure success ya timu kwenye mechi tofauti na Samata ambaye hana hiyo,sasa nashndwa kuelewa kuwa kaka Shafii huwa tunamuangalia Samata huyu huyu wa TP Mazembe au pengine unamuongelea mwingine?.

    Poulsen ni kocha which means he knows better na ndicho anacholipiwa kufanya, wadau mwacheni apige kazi..Mwacheni pia Dogo afunzwe, hapo tu bado kinda mnataka kumvimbisha kichwa, samaki mkunje angali mbichi bana ili next time akiitwa atafanya bidii na kwa uzalendo zaidi ili kuprove people wrong.

    ReplyDelete