Baraka Mbolembole
WAAMUZI, hivi sasa wamekuwa kero kubwa kwa wapenzi wa soka nchini kutokana na kuboronga kwao katika michezo mbalimbali ya ligi kuu inayoendelea nchini. Abdallah Kambuzi, mwamuzi huyu alichezesha mchezo kati ya Yanga SC na Mbeya City, jumamosi iliyopita alionekana kushindwa kufanya maamuzi sahihi. Si yeye tu kumeibuka malalamiko zaidi kutoka kwa timu nyingine kuhusu uchezeshaji mbaya wa waamuzi wengi nchi.
Nao ni binadamu, hivyo kufanya makosa ni jambo la kawaida. Kama mchezaji hufanya makosa na kuadhibiwa, hivyo mwamuzi nae anaweza kufanya makosa. Ila pamoja na adhabu mbalimbali ambazo wamekuwa wakipata bado hali si nzuri. Wamekuwa wakifanya makosa kwenye mechi za Yanga, Simba na Azam FC, tena ni makosa ya makusudi kabisa. Mfano, ni kadi nyekundu ambayo alipewa kiungo wa City, Steven Mazanda wiki iliyopita katika mchezo dhidi ya Yanga, na matukio ambayo yalifanywa na Haruna Niyonzima, baada ya kiungo huyo wa Yanga kuwa na kadi ya njano, baadae alitakiwa kuondoshwa uwanjani kwa kadi ya pili ya njano ila haikuwa hivyo, mwamuzi akaamua kukataa bao lililokuwa halali la Hamis Kizza kama njia ya kusahihisha makosa yake.
WANAPANGA MATOKEO?
Bado hakuna ushahidi wa moja kwa moja kuhusu hilo, ila timu nyingi zimekuwa zikiandaa 'fungu' la marefa ili wapate upendelo. Katika mchezo wa Ntibwa Sugar na Simba, kocha wa Mtibwa, Mecky Mexime alionekana kuwa na jabza kuhusu uamuzi wa mwamuzi , Deonisia Kyura ambaye alimtoa nje kiungo na nahodha wa timu yake Shaaban Nditti. Awali Nditti alikuwa na kadi ya njano ila aliamua kumchapa kofi Amis Tambwe ambaye alimbana na miguu walipokuwa wameanguka wote chini.
Nditti,
inadaiwa alitoa lugha chafu kwa mwamuzi huyo ndiyo maana akaadhibiwa,
ila muda mwingi alionekana kushindwa kuendana na ukubwa wa mechi. Kwa
nini alipangwa? Tafakari....
Bahati
mbaya ni kuwa waamuzi hao wamekuwa wakilalamikiwa zaidi katika michezo
dhidi ya timu kubwa tu, huku wanapokuwa wakichezesha michezo dhidi ya
timu nyingine nje ya Yanga, Simba na Azam wamekuwa wakifanya vizuri.
WANACHEZESHA KWA KUFUATA MAELEKEZO...
Ndiyo
ukweli ulivyo, ila ni vigumu mtu wa Yanga, Simba au Azam kusema kuwa
wanakuwa wakipata ' mbereko' kutoka kwa waamuzi. Tatizo hili
linajulikana na wahusika ni viongozi wa klabu, waamuzi na wasimamizi
wao. Klabu ndiyo zimekuwa zikihusika moja kwa moja kwa nia ya kupata
matokeo ya ushindi tu. Mambo haya yanakera. Waamuzi nao ni binadamu
hivyo ni rahisi kuingia katika ushawishi wa kuchukua pesa zinazowekwa
mezani na viongozi wa klabu.
Mambo
haya naamini yanafahimika kwa wahusika hivyo wanatakiwa kuchukua hatua
ya haraka ya kuachana na mambo hayo ili kufanya timu zetu zishinde kwa
uwezo wao, na mwisho tupate mabingwa sahihi. Siku zaidi ya 100 za rais
wa TFF, Jamal Malinzi, soka la Tanzania bado lipo majaribuni. Waamuzi ni
changamoto nyingine kubwa kwake. Awakataze kuchezesha kwa maagizo
kutoka nje ya uwanja.
Umeangalia upande mmoja tu ambao mara nyingi ni hisia na ni mgumu kuuthibitisha.Ukweli ni kwamba pamoja na kuwepo uwezekano wa waamuzi kupindisha sheria kwa makusudi ili kuzibeba baadhi ya timu,lakini tatizo kubwa ni uwezo mdogo wa waamuzi wetu katika uchezeshaji na dndio maana hawapati nafasi nyingi za kuchezesha mashindano makubwa kama vile fainali za klabu bingwa afrika au kombe la dunia.Makosa unayoyazungumzia hayatokei kwenye mechi za simba na yanga tu bali hata kwenye mechi zinazohusisha timu nyingine isipokuwa tu macho yetu wengi tumeelekeza kwenye mechi zinazohusisha simba au yanga.Ukiangalia mechi ya nani mtani jembe ambayo mwamuzi alitoka Zanzibar, kadi ya kwanza ya njano aliyompa Yondani kwa kucheza rafu utaona kwamba licha ya Yondani kucheza rafu na kumnyang;anya mpira mchezaji wa simba, lakini refa aliruhusu mpira uendelee kuchezwa na wachezaji wa yanga kwa sekunde kadhaa huku mchezaji wa simba akiwa bado amelala chini hadi pale mchezaji mwingine wa simba alipomfanyia rafu mchezaji wa Yanga katika move hiyo ndipo refa aliposimamisha mchezo na kutoa kadi kwa faulo ya kwanza ya Yondani badala ya rafu iliyosababisha asimamishe mchezo
ReplyDeleteOya we mwandshi utajiju,hivi hujui km tff wanatoa adhabu kwa yeyote ataewasema vibaya waamuzi?? Utaingia matatani bure!!
ReplyDelete