Search This Blog

Friday, July 20, 2012

MPINZANI WA SEPP BLATTER FIFA - BIN HAMMAM ASHINDA RUFAA YA KUFUNGIWA MAISHA

Mgombea wa zamani wa nafasi ya uraisi wa FIFA Mohamed bin Hammam ameshinda kesi yake iliyomfanya aadhibiwe kufungiwa kujihusisha na soka maisha kutokana kutuhumiwa kutoa rushwa kwa wapiga kura wakati akikabiliana na Sepp Blatter.

Uamuzi huu utakuwa sio mzuri kwa Blatter, ambaye kwa sasa anakabiliana na vita kubwa ya rushwa kwenye soka huku akitaka kulimaliza tatioz hilo na kujipa sura safi mbele ya wapenda soka ulimwenguni.

Kwa bahati nzuri sasa kwa raisi huyo wa FIFA, Bin Hammam sasa amesimamishwa na shirikisho la soka barani A    sia - hivyo uwezekano wa kupishana na Blatter kwenye korido za FIFA itabidi kusubiri.

Habari nzuri kwa FIFA ni kwamba wakati wa usikilizwaji wa kesi ya Bin Hamman huko CAS - hakuonekana kutokuwa na makosa ju ya tuhuma za kutoa kiasi cha $40,000, ambazo zilichukuliwa na mjumbe wa kamati kuu ya FIFA Jack Warner ili kupeleka kwa wajumbe wa Caribbean Football Union.

Kwenye kesi ya CAS wajumbe watatu walipiga kura na zikipatikana 2-1, huku 2 zikiwa upande wa utetezi wa Bin Hammam kwa madai kwamba hakuna uthibitish kwamba zile fedha zilitoka kwa Hammam, hivyo kwa maana hiyo raia huyo wa Qatar anaweza asiwe amekiuka sheria za maadili ya kuweza kuongoza chombo cha kuongoza soka.

Kufuatia maamuzi ya CAS, FIFA wametoa taarifa haraka kutoa ahadi kwamba watafungua uchunguzi mpya dhidi ya Bin Hammam. Wakisisitiza "Mohamed Bin Hammam bado hajasafishwa - hajaonekana hana kosa." FIFA wamehaidi kutoa vielelezo vyote na mafaili ya kesi ya Bin Hammam kwa kamati mpya inayosimamia maadili, kuamua kama kuna hatua yoyote kinahitajika kuchukuliwa dhidi ya Bin Hammam.

No comments:

Post a Comment