Search This Blog

Thursday, April 25, 2013

BENDERA: IKIWA MFUMO WA SOKA UTAENDELEA KUWA HIVI - SOKA LETU LINA SAFARI NDEFU KUENDELEA MBELE


KOCHA wa zamani wa timu ya taifa Taifa Stars ambaye aliwahi pia kuwa naibu waziri wa vijana,
Utamaduni na Michezo, Joel Bendera, amesema kuwa soka la Tanzania bado linasafari ndefu kufikia mafanikio ikiwa mfumo wa uendeshaji mchezo huo hautabadilika.

Bendera ambaye mwaka 1980 aliweka rekodi ambayo haijavunjwa hadi leo ya kuiwezesha Tanzania kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya kuifunga timu ya taifa ya Zambia
(Chipolopolo) katika uwanja wa Independence mjini Lusaka, Zambia huku mechi hiyo ikishuhudiwa na aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Dk Kenneth Kaunda, alisema nilazima Tanzania kurudi kwenye mfumo wa awali.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Bendera ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Morogoro alisema kuwa katika kipindi ambacho yeye alikuwa kocha wa Taifa Stars alipata wachezaji wa timu hiyo
kwa kuzunguka mikoani wakati wa mashindano ya UMITASHUMITA, UMISETA, Taifa CUP na SHIMIWI na kuweza kukusanya wachezaji wenyevipaji na wanaojituma.

“Leo hii timu yetu ya taifa inashindwa kufanya vizuri kwa sababu ya wanaohusika kushindwa kufanya selection (uchaguzi) unaofaa kwa kuelekeza nguvu zaidi katika kuchagua wachezaji kutoka timu zinazoshiriki ligi kuu pekee,” alisema Bendera.

Pia, alisema kuwa mbali ya mfumo mbovu wa kuchagua wachezaji uliopo kwa sasa, lakini bado Tanzania inachangamoto kuwa ya kukosa viwanja vya michezo, vifaa na walimu wanaofundisha
michezo mashuleni.

Alisema kuwa hali hiyo imewafanya wachezaji wengi wanaoingia katika timu ya taifa na hata vilabu vinavyoshiriki ligi kuu kukosa vitu vitatu muhimu katika mpira ambavyo ni uzalendo, ari na nidhamu.

Kuhusu matumizia ya lugha ya kiingereza inayotumiwa na makocha wengi wa kigeni kuwafundishia wachezaji wa timu za tanzania ikiwa ni pamoja na taifa staa, kocha huyo wa zamani alisema kuwa lugha za mpira zinafanana kote duniani kufundishwa kwa kishwahili au kiingereza hakubadilishi lugha hiyo.

Kama ilivyo kwa mataifa mengine ya Afrika, Tanzania imeingia katika mkumbo wa kuwatumia
makocha wa kigeni ambao hutumia lugha ya kiingeza kufundishia, lugha ambayo huzungumzwa na
wachezaji wachche wa timu ya taifa.

No comments:

Post a Comment