Search This Blog

Wednesday, April 24, 2013

CHELSEA NDIO TIMU YA MWISHO KUIFUNGA BARCA MABAO 4 KWENYE CHAMPIONS LEAGUE: MESSI ANA NUKSI NA MULLER

* Mara ya mwisho mshambuliaji Lionel Messi kuichezea timu iliyofungwa mabao 4-0 ilikuwa dhidi ya wajerumani. Argentina ilipofungwa kwenye robo fainali ya kombe la dunia 2010. Pia siku hiyo kama ilivyokuwa leo Thomas Mueller, alifunga mabao mawili tena. 

 * Barcelona wameruhusu wavu wao kuguswa mara nne katika mechi ya Champions League kwa mara ya kwanza tangu walipofungwa 4-2 na Chelsea katika hatua ya 16 bora March 2005.

* Timu ya kwanza kuifunga Barcelona 4-0 katika michuano ya ulaya ilikuwa ni Dynamo Kiev katika hatua ya makundi mnamo November 1997.

* Hakuna timu iliyofungwa kwenye raundi ya kwanza ya hatua ya mtoano ya Champions League/European Cup kwa mabao manne kwa bila au zaidi iliyoweza kufuzu kuendelea raundi ya pili. 

* Barcelona walipiga shuti moja tu liloenga goli la Bayern leo, idadi ndogo zaidi katika Champions League msimu huu. 

* Katika mashindano yote - Barcelona hawajafungwa 4-0 tangu walipoonyoshwa na Getafe katika kombe la mfalme May 2007. Miaka sita iliyopita.

3 comments:

  1. Shaffih wewe ni mwandishi mzuri wa habari za michezo lakini kuwa makini na unacho kiripoti.. si kweli kwamba Dynamo Kiev ni timu ya kwanza kuifunga Barcelona 4-0 mwaka 1997 la hasha... Je, unafahamu kwamba mwaka 1994 AC Milan iliifunga Barcelona 4-0 kwenye fainali ya Champions League???
    Kuwa makini na takwimu zako.. ni hayo tu

    ReplyDelete
  2. Mwendo wa kusuasua, ligi yenyewe inayoshiriki ndio rahisi zaidi ulaya!! Ligi ya timu 2.Lakini mmeijazia sifa kibao!! Barca kiko wapi? Messi anabebwa na wanahabari akihamia EPL hamna kitu hapo afadhali hata Chuji pale kati atazungusha!!!

    ReplyDelete