Search This Blog

Thursday, August 25, 2011

VICTOR COSTA AREJESHWA STARS


Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen leo (Agosti 25 mwaka huu) ametangaza kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya mechi ya mchujo dhidi ya Algeria ‘Desert Warriors’ kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Equatorial Guinea na Gabon.
Wachezaji walioitwa ni makipa Shabani Dihile (JKT Ruvu Stars), Juma Kaseja (Simba) na Shabani Kado (Yanga). Mabeki wa pembeni ni nahodha Shadrack Nsajigwa (Yanga), Idrissa Rajab (Sofapaka, Kenya) na Amir Maftah (Simba). Mabeki wa kati ni Aggrey Morris (Azam), Juma Nyoso (Simba) na Victor Costa (Simba).

Viungo wakabaji ni Henry Joseph (Kongsvinger IL, Norway), Nurdin Bakari (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Juma Seif (Yanga) na Jabir Aziz (Azam). Viungo washambuliaji ni Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada), Mrisho Ngassa (Azam) na Salum Machaku (Simba).

Washambuliaji ni Abdi Kassim (DT Long An, Vietnam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Ramadhan Chombo (Azam), Dan Mrwanda (DT Long An, Vietnam), Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden) na John Bocco (Azam).

Timu itaingia kambini Jumapili (Agosti 28 mwaka huu) mchana na jioni itaanza mazoezi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume. Mechi dhidi ya Algeria itachezwa Septemba 3 mwaka huu kuanzia saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment