Mabingwa wa Tanzania bara na Afrika mashariki na kati klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, imezima uvumi kwamba imemtema kocha wake raia wa Uganda, Sam Timbe, kwa kile kilichodaiwa kutoridhishwa na mwenendo wa timu hiyo kwenye mechi za Ligi Kuu nchini, na badala yake imemrejesha kocha wake wa zamani Costadin Papic.
Uvumi huo uliongezwa nguvu zaidi hasa baada ya Timbe kutokuwepo kwenye benchi la la Yanga katika mechi ya ya ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Toto African iliyochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam juzi.
Kufuatia ujio wa Papic, uvumi ulienea kwamba kocha huyo amerudi kuchukua nafasi ya Timbe.
Lakini Katibu mkuu wa Yanga, Selestin Mwesigwa alisema klabu yake haijawahi kuwa na mpango kama huo, na kwamba wanamtambua Timbe kama kocha wao mkuu mpaka sasa.
Mwesigwa alisema, si kweli kwamba kutokuwepo kwa Timbe kwenye benchi wakati wa mechi dhidi ya Toto, kulikuwa na maana ya kwamba ametimuliwa.
"Hakuna kweli wa taarifa hizi, Timbe bado ni kocha wetu isipokuwa tu alishindwa kutokea katika mechi hiyo kutokana na matatizo ya kiafya," alisema Mwasigwa.
Kuhusiana na ujio wa Papic aliyetua nchini Jumatano iliyopita Mwesigwa alisema kuwa kocha huyo amekuja nchini kwa shughuli zake binafsi.
Alisema kuonekana uwanjani Papic katika mechi yao dhidi ya Toto ni moja ya mapenzi yake kwa Yanga kwa sababu alishawai kuifundisha kwa mafanikio makubwa.
Search This Blog
Saturday, October 22, 2011
YANGA: HATUNA MPANGO NA PAPIC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment