Search This Blog

Tuesday, July 26, 2011

PODOLSKI AVULIWA UNAHODHA COLOGNE



Mshambuliaji wa Ujerumani Lukas Podolski amevuliwa unahodha timu ya FC Cologne na beki wa kibrazil Pedro Geromel ameteuliwa kama mrithi wake, kocha Stale Solbakken amesema jana Jumatatu.

Kocha huyo Mnorway, ambaye bado hajaanza kuiongonza timu hiyo katika mechi za ushindani tangu ajiunge na klabu hiyo mwezi uliopita, amechukua uamuzi huo ikiwa ni wiki mbili kabla ya kuanza kwa ligi ya Bundesliga.

“Naelewa uamuzi niliouchukua utakuwa na athari zipi, na nitakubaliana kabisa na baadhi ya malalmiko ya mashabiki,” kocha huyo aliwaambia waandishi wa habari.

“Lakini nataka mashabiki wauamini uamuzi wangu kuwa ni mzuri na una manufaa kwa timu, Pedro Geromel atakuwa ndio nahodha mpya katika kuhakikisha naleta utaratibu na utamaduni mpya ndani ya timu ninayoingoza.

“Nimeongea na Lukas, na amenielezea masikitiko yake lakini pia ameamua kuuheshimu uamuzi huu kwa sababu ameelewa maana na dhamira yangu.”

Podolski, 26, alirudi Cologne mwaka 2009 baada ya misimu 3 ndani ya Bayern Munich na amekuwa kipenzi cha mashabiki wa timu, amefunga mabao 13 kwenye Bundesliga msimu uliopita na kuisaidia klabu kumaliza ligi wakiwa kwenye top 10.

Geromel alijiunga na Cologne mwaka 2008 akitokea Vitoria Guimaraes ya Ureno.

No comments:

Post a Comment