PIA VIONGOZI WA VILABU WAALIKWA KUJA KUPIGWA MSASA NAMNA YA KUUENDESHA KISASA MCHEZO WA SOKA.
Mtendaji mkuu na mmiliki wa timu ya SEATTLE SOUNDERS Mr ADRIAN Hanauer ameahidi kuwapatia wachezaji 3 wa kitanzania kila mwaka nafasi ya kuja kufanya majaribio ya kujiunga na timu ya Seattle Sounders, lakini mmoja kati ya hao wachezaji lazima awe ni kijana mwenye umri chini ya miaka 17.
Adrian amesema sera nzuri za Mweshimiwa Raisi JAKAYA MRISHO KIKWETE kutaka kuinua michezo nchini ndizo zimemsukuma kutoa hiyo nafasi adimu kwa watanzania.
" Ligi yetu inazidi kupata umaarufu mkubwa kadri siku zinavyokwenda mbele na timu yetu kama unavyoiona inafanya vizuri na wachezaji wengi sasa wanataka kuja kuichezea,na hii ni kwasababu ya mipango madhubuti tuliyojiwekea kwa ajili ya kuindeleza timu yetu"
ADRIAN pia amesema SOUNDERS itawatumia mialiko baadhi ya viongozi wa timu zinazoshiliki ligi kuu ya VODACOM kuja nchini Marekani kujifunza namna mpira unavyoendeshwa kisasa.
" Hapa Marekani michezo ni moja kati ya sekta zinazotengeneza sana pesa,kwa miaka mingi michezo kama Basketball,American Football na Baseball imekuwa ikitengeneza sana pesa na hii ni kutokana na michezo hiyo kuwa na umaarufu mkubwa hapa, lakini tangu mchezo wa soka nao uanze ku-promotiwa vilivyo basi nao umeanza kuwa maarufu na sasa pesa nyingi zinatengenezwa,
kwahiyo nafikiri tutatoa fursa kwa viongozi wa vilabu vyenu kuja hapa wapigwe msasa kidogo ili wakaongoze mpira kisasa, mpira wa miguu ni bidhaa hadimu sana si ulaya au marekani pekee, bali mahala popote pale kama wahusika wanajua maana na umuhimu wa kuuendesha kisasa basi pesa zitatengenezwa "
No comments:
Post a Comment