Search This Blog
Friday, February 15, 2013
Zawadi nono kutolewa kwa wanariadha Kilimanjaro Marathon
Waandaaji wa Kilimanjaro Marathon 2013 wametangaza kutoa zawadi nono kwa wanariadha watakaoshiriki mbio za Kilimanjaro Marathon 2013.
George Kavishe, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager alisema katika taarifa kwa vyombo vyua habari jana kuwa“Kilimanjaro Premium Lager inaendelea kutambua mchango wa wanariadha kwa kuwazawadia kwa mara nyingine na mara hii ikiwa ni zawadi nono pamoja na motisha nyingine’’.
Alisema fedha kwa ajili ya zawadi kwa mshindi wa kwanza hadi wa tatu pande zote mbili wanaume na wanawake kwenye Kilimanjaro Marathon kilometa 42 ni zaidi ya shilingi milioni ishirini.
Washindi wa kwanza wa Kilimanjaro Marathon kilometa 42 upande wa wanaume na wanawake watajishindia Tsh Milioni 3 kila mmoja, lengo likiwa kuvutia wanariadha wa hadhi ya juu duniani, kuhamasisha uwekaji wa rekodi mpya na pia kusheherekea miaka kumi na moja ya Kilimanjaro Marathon.
Aliongeza kuwa ‘‘Kipaumbele cha Kilimanjaro Premium lager ni kuwapa motisha wanariadha wa Tanzania zaidi, na kwa sababu hiyo Kilimanjaro Premium Lager wametenga kiasi cha pembeni cha Tsh milioni 6 kwa wanariadha watanzania ambao watamaliza wa kwanza katika pande zote mbili wanaume na wanawake katika mbio ya Kilimanjaro Marathon kilometa 42 kila mmoja akijipatia milioni 3.
Kiasi hicho cha fedha kitakabidhiwa kwa wanariadha Watanzania kama nyongeza ya kile watakachopata kwenye ushindi wa mbio walizoshiriki na kushinda. “Tunaamini kuwa hii itawahamasisha wanariadha watanzania kuongeza juhudi na kumaliza mbio kwa muda mzuri”.
Washindi wa pili watajipatia shilingi milioni 1.5 kila mmoja na wa washindi wa tatu watajipatia shilingi 850,000 kila mmoja kwa wanawake na wanaume.
John Addison, Mkurugenzi Mtendaji wa Wild Frontiers ambao ni waandaaji wa tukio hilo alisema Mshindi wa nusu Marathon kwa wanaume na wanawake atajishindia Tsh 1,500,000 kila mmoja, mshindi wa pili Tsh 750,000 na mshindi wa tatu Tsh 375,000.
Washindi wa mbio za GAPCO Nusu Marathon kwa walemavu watajipatia zawadi nono pia, ambapo mbio hizi zinajumuisha sehemu tatu yaani kiti cha matairi, hand cycle na walemavu wengine na kila mshindi kwenye kipengele chake atapata zawadi kama ifuatavyo;
Mshindi wa kwanza Tsh 300,000, mshindi wa pili kwa wanaume na wanawake Tsh 200,000, na mwisho mshindi wa tatu atajinyakulia Tsh 50,000.
Kwa upande wa mbio za kujifurahisha za Vodacom 5km Fun Run washiriki wote watakaomaliza mbio hawataondoka mikono mitupu bali watajipatia t-shirts na zawadi nyingine nono kama simu na muda wa maongezi pia zitatolewa kupitia bahati nasibu. Mbio hizi ndio zinazotoa fursa kwa watu wa rika zote kuwa sehemu ya Kilimanjaro Marathon.
Mbio hizo zinaratibiwa na Executive Solutions na kudhaminiwa na Kilimanjaro PremiumLager, huku wadhamini wengine wa tukio hilo ni pamoja na Vodacom Tanzania (5km Fun Run), GAPCO (Nusu Marathon Walemavu), Tanga Cement, CFAO Motors, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, TanzaniteOne, New Arusha Hoteli, Kilimanjaro Water, FastJet na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment