Matumaini ya Fernando Torres kucheza at Euro 2012 yameanza kushuka baada ya kutemwa katika kikosi cha Spain kwa ajili ya mechi ya wiki ijayo dhidi ya Venezuela.
Spain, ambao watatea ubingwa wao wa ulaya baadae mwaka huu, wanakutana na wasouth America mjini Malaga wiki ijayo Jumatano huku Del Bosque akisema kunaweza kuwa na mabadiliko katika kikosi kabla ya michuano ya ulaya nchini Ukraine na Poland, na Torres anaonekana yupo mbali katika kuipata nafasi ya kuwemo ndani ya kikosi cha watu 23.
Del Bosque anasema anataka kuwazadia wachezaji ambao wamekuwa wakifanya vizuri. Torres amekuwa hafanyi chochote kwa zaidi ya mwaka sasa.
“Torres ni mchezaji ambao ninaheshimu sana mchango wake na inaniuma kumuacha nje ya kikosi lakini nataka kuwa fair,” Del Bosque aliwaambia waandishi.
Torres amekuwa na wakati mbaya kuliko wowote katika maisha yake ya soka tangu ajiunge na Chelsea kutoka Liverpool na ada iliyoweka rekodi £50million mwanzoni mwa mwaka uliopita. Amefunga goli tu katika mechi 18 msimu uliopita huku msimu huu katika mechi 29 akiwa amefunga magoli 5, na sasa hajafunga goli tangu October 19 alipofunga dhidi ya Genk katika UCL.
Enzi Hizo Torres akifunga goli la ushindi dhidi ya Ujerumani in Euro 2008 final. |
Mara ya mwisho kufunga katika premier league ilikuwa dhidi ya Swansea mwezi September last year.
Pia mara ya mwisho kuifungia Spain ilikuwa katika kufuzu kmbe la euro dhidi ya Liechtenstein waliposhinda 4-0 in septmber 2010.
No comments:
Post a Comment