MWANACHAMA na mjumbe wa kamati ya utendaji wa siku nyingi wa klabu ya Yanga, Mohamed Bhinda amekanusha kuchukua fedha za mapato za mechi ya Ligi ya Mabingwa ya Afrika kati ya timu yake na klabu ya Zamalek Spoting ya Misri.
Hivi karibuni kulikuwa na habari tofauti zikimuhusisha Bhinda kuwa amechukua baadhi ya fedha zilizotokana na kiingilio huku wengine wakidai kuwa mwanachama huyo anatarajiwa kuhojiwa hivi karibuni na kamati ya utendaji ya klabu hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Bhinda alisema kuwa mbali ya kufanya kazi kama kiongozi wa Yanga, pia alipewa jukumu la kutafuta wauzaji tiketi ambao aliwasisimia yeye ili kufanikisha zoezi hilo gumu kwa maeneo ya Kariakoo na Temeke.
Alisema kuwa alipewa kazi hiyo na kampuni ya Prime Time Promotions ambao walikuwa wasimamizi wakuu wa mechi hiyo. Alifafanua kuwa kutokana na utaratibu mpya wa tiketi za ki-elotroniki, zpezi la kuhakiki tiketi lilikuwa gumu sana kwani uwanja wa Taifa unaingiza watu 60,000.
“Kutokana na zoezi la kuhakiki tiketi kuwa gumu, uuzaji ukachelewa, hivi mimi nilipewa tiketi kwa ajili ya wauzaji wa Temeke na nilichukua dhamana yao baada ya kuwapa najira ya uuzaji huo,” alisema Bhinda.
Alisema kuwa anashangazwa na taarifa kuwa ameingia mitini na fedha za malipo ya tiketi wakati malipo yote alikabidhi Prime Time Promotion chini ya uangalizi wa kampuni ya ulinzi ya Ultimate Security. “Sina deni Prime Time wala Yanga, sasa haya majungu yanatoka wapi, naamini kuna watu ambao hawataki sisi kufanya kazi hizi, baada ya kupongeza wanatoa tuhuma ambazo si za msingi,” alisema.
Alisema kuwa Wanayanga wanatikiwa kuipongeza kampuni ya Prime Time kwa kufanikisha zoezi hilo na kuipatia mapato Yanga ya kihistoria. Mara ya mwisho Yanga ilipata jumla ya Shs milioni 100.5 baada ya kucheza mechi na timu ya Al Ahly ya Misri.
Alisema kuwa hamasa ya mchezo huo ilikuwa kubwa sana na Prime Time imefanya kazi ya kupongezwa katika kufanikisha hayo. Yanga ilipata mgawo wa zaidi ya shs milioni 170 baada ya mechi hiyo.
No comments:
Post a Comment