Imefahamika Roman Abramovich alitaka maelezo ya kutosha kwanini Andre Villas-Boas aliwapiga benchi Ashley Cole, Frank Lampard na Micheal Essien.
AVB aliwaacha watatu hao katika kikosi kilichoanza katika mechi waliyofungwa 3-1 na Napoli in Champions league jumanne iliyopita.
Kutokana na hali ya hiyo mmiliki wa timu hiyo Abramovich alisisitiza kupewa maelezo ya kutosha kuhusu sakata la kutemwa wachezaji hao ambao siku mbili kabla waliponda mbinu za ufundishaji wa mreno huyo hadharani.
Mkurugenzi wa ufundi wa Chelsea Micheal Emenalo alimbana Villas-Boas kuhusu uchaguzi wake wa kikosi siku na akapeleka majibu kwa aliyemtuma, Roman Abramovich.
AVB alikiri: “Sikuongea na mmiliki mwenyewe badala yake nilipeleka taarifa kwa watu wa karibu yake kama vile Emenalo na wengine ili kupeleka majibu kwa mwenyewe Roman.
“Walitumwa kuniuliza. Hii ndio njia ya kawaida kuwasiliana na mmiliki. Naona kawaida tu. Alikuwa anataka kujua mawazo yangu juu ya uchaguzi wa kikosi ninaoufanya.
“Mmiliki alikasirishwa na matokeo na aliuliza maswali kuhusu timu na mimi nikapeleka majibu.”
Lampard na Cole pamoja na Essien walimtolea uvivu manager wao walipopigwa benchi nchini Italy.
Pamoja na kufungwa na Napoli lakini AVB anasema alichagua kikosi sahihi.
“Ilikuwa ndio timu sahihi kucheza, japo tulifungwa lakini sina majuto. Uchaguzi wa kikosi ulikuwa sahihi.
“Nina mahusiano mazuri na Cole na Lampard lakini muda pekee unaokuwa ukisapotiwa na wachezaji ni pale na wenyewe wanapokuwa kwenye kikosi cha kwanza.
“Kitu muhimu kwa Chelsea ni kanuni na taratibu. Klabu ni muhimu kuliko mtu yoyote binafsi.”
“Nitafanya kila kitu ninavyoona mimi, na mtu yoyote hatakiwi kuwalaumu wachezaji kwa chochote.” Alimaliza AVB.
No comments:
Post a Comment