Search This Blog

Tuesday, May 10, 2011

CECAFA YAHAIRISHA DRAW YA KAGAME CUP


Chama cha soka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) kimeharisha upangaji wa ratiba wa kombe la Kagame Cup iliyopangwa kufanyika jumapili.
Hali hiyo ilijitokeza ili kuweza kusubiri uthibitisho wa ushiriki wa timu za Al-Ahly kutoka Egypt na Liberty Professionals kutoka Ghana.
"Kutokea mwanzo timu za Al-Ahly na Liberty zilionyesha kuvutiwa na kushiriki katika mashindano haya, lakini mpaka sasa bado hawajathibitisha ushiriki wao"-alisema Nicholas Musonye, Katibu Mkuu wa CECAFA.
Mashindano hayo ambayo mwaka huu yatafanyika jijini Khartoum-Sudan kuanzia tarehe 5 July yatajumuisha timu za Bunnamwaya-Uganda, Ulinzi-Kenya, St.George-Ethiopia, El-Merreikh and Al Hilal-Sudan, Ocean View-Zanzibar, Vital'O-Burundi, Port Of Djibouti, Red Sea-Eritrea, Elman-Somalia, Etincelles and APR-Rwanda.
Ikiwa tofauti na miaka iliyopita mwaka huu mashindano hayo yatakuwa co-sponsored na Rwandan President Paul Kagame atakayetoa $60,000 na El Muriate Group watatoa $40,000.
APR ya Rwanda ndio mabingwa watetezi wa kombe baada ya mwaka jana kuwafunga St.George ya Ethiopia kwa mabao 2-0.

No comments:

Post a Comment